Personal attacks kwa Dr. Ulimboka zimeanza! Waziri mkuu kadhihirisha utendaji duni

Ma Dr walimuomba JK amuache awepo kwenye hilo kundi pamoja na kwamba yeye sio muajiriwa wa serikali na JK akakubali. Hii iko kwenye hotuba ya Rais.
 
Alijipenyezaje mpaka kuwa mbele ndio ninachotaka kujua na alikua na alikuwa ametumwa na nani kwa malipo kiasi gani maana ni wazi hakua anatumika bure
Alitumwa na professional calling deep down in him!
You dont have to be sick to treat the sick ! Please pray for his quick recovery
as Chinua Achebe said, and I quote "the chicken must be safe in the pen before its warned against wondering into the bush'
 
mpaka sasa naamini dk ulimboka alikua niu mchochezi tu wa kawaida kama wachochezi wengine,haiyumkiniki ajiingize kichwa kichwa kwenye jambo lisilomhusu wala kuwa na maslahi nalo,wale wenzake walikua na mgogoro na muajiri wao ambae wana mkataba nae,yeye alikurupuka na kujitumbukiza katikati kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe

Sasa wachochezi ndio wanaumizwa na kutaka kuuwawa vile? Kwani hii nchi haina sheria? What a failure in the system! Unaona tatizo hili lilivyokuzwa na kuwa kubwa sana bila sababu?
 
Tuache kudanganyana ajenda yao mama ni mshahara na malupulupu hivyo vitendea kazi ni kisingizio tu,na kisingizio chenyewe hakiapply kwa walioajiriwa kwenye private sector kama bwana Ulimboka,ninachojiuliza ni kwamba je ulimboka alijipa angalau muda wa kupitia mikataba ya aliyokuwa "amejitolea" kuwasemea na mwajiri wao?au alijitumbukiza tu matokeo yake yakampata yaliyompata akiwa kwenye mambo ya ulevi

Someni thread za huyu mtu,rangi yake inajionyesha.jambo moja tu ambalo sikulijua na nimelijua sasa,huyu bwana Romantic ni mpumbavu na bingwa wa ku divert mijadala humu kwa ID tofauti.mpumbavu hupuuzwa muachieni li thread lake!
 
Madaktari gani hawatii hata kauli ya mahakama? Ulimboka na wenzake ni genge la wahuni ambalo inabidi wananchi tulikemee vikali.

Mkuu, nchi hii ina sheria. Kwanini sheria hazikutumika kumdhibiti Dr. Ulimboka badala ya kumuumiza vile tena kwa nia ya kuona amekufa? Wananchi wana kiu na kuiona Tanzania inakuwa njema.

Ila two wrongs can't make a right...tatizo ndo limekuwa complicated zaidi sasa! Ukifikiria kwa makini, unaona kabisa ukosefu wa busara katika kushughulikia mambo yetu.

Nguvu ina kiasi....na zile siasa za kusambaza woga hazina tija tena kwenye hii dunia ya leo.

Tujifunze kufuata sheria ili tuheshimiwe. Ilivyo sasa, wewe unaona wananchi wana hisia gani na hayo aliyotendewa Ulimboka?
 
Dr Ulimboka si mwajiriwa wa serikali ni kweli, yeye ni mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari.

Kuhusika kwa dr ulimboka katika mgomo wa madaktari kunasababishwa na ukweli kuwa madai ya madaktari si katika nyongeza ya mshahara na maslahi yao tu. Hulo ni dai moja kati ya mengi ikiwamo kuboreshwa kwa huduma katika sekta ya afya.

Huenda haya madai mengine yakawa ni sababu tosha kwa Dr Ulimboka kuhusika katika kuinfluence mgomo lakini akaaminiwa na kupewa uongozi katika suala hilo.

Si afiki kuwepo kwa mgomo kwani watanzania wasio na hatia ambao walipaswa kupatiwa huduma za afya katika nchi yao wanaumia na kupoteza maisha lakini pia serikali haina budi kulitazama suala hili kwa jicho la tatu ili kuweza kulipatia ufumbuzi na madaktari warudi kazini.
 
Someni thread za huyu mtu,rangi yake inajionyesha.jambo moja tu ambalo sikulijua na nimelijua sasa,huyu bwana Romantic ni mpumbavu na bingwa wa ku divert mijadala humu kwa ID tofauti.mpumbavu hupuuzwa muachieni li thread lake!
Tatizo mmezoea kupigiana makofi hampendi kuwa challenged mnataka watu wote wafikiri na kuamini kama nyie ndio mana mnapata tabu,jaribuni kupima mambo na kupokea challenge,msikaririshwe,mtakua great thinker wa kweli siku moja
 
Kuna taarifa kwamba Dr.Ulimboka sio mtumishi wa serikali,je hili ni kweli?kama jibu ni ndio amewezaje kujipenyeza mpaka kuwa mtu mashuhuri zaidi kwenye mgogoro wa nyongeza za malupulupu ya watumishi wa serikali-madaktari waajiriwa wa serikali?alitumwa na nani na hao waliomtuma wamekuwa wakilimpa kiasi gani labda kwa mwezi.

MA DK. WAMEMWAMINI WW KINAKUWASHA KININI?
 
Mkuu, nchi hii ina sheria. Kwanini sheria hazikutumika kumdhibiti Dr. Ulimboka badala ya kumuumiza vile tena kwa nia ya kuona amekufa? Wananchi wana kiu na kuiona Tanzania inakuwa njema. Ila two wrongs can't make a right...tatizo ndo limekuwa complicated zaidi sasa! Ukifikiria kwa makini, unaona kabisa ukosefu wa busara katika kushughulikia mambo yetu. Nguvu ina kiasi....na zile siasa za kusambaza woga hazina tija tena kwenye hii dunia ya leo. Tujifunze kufuata sheria ili tuheshimiwe. Ilivyo sasa, wewe unaona wananchi wana hisia gani na hayo aliyotendewa Ulimboka?
Unajua ni ngumu sana kuzuia hisia ama speculations yanapotokea mambo kama haya hususan kwa watu maarufu kama dr ulimboka mzee,kuna watu mpaka leo wahisi na wanaamini mbowe ndio alipanga njama za mauaji ya marehemu Chacha wangwe na watu hao hata uwaeleze nini tofauti na hisia zao hawawezi kuamini lakini hiyo haihalalishi moja kwa moja kwamba freeman mbowe kweli anahusika in one way or another na kifo kile,kwa hiyo hisia za wananchi haziepukiki lakini kama great thinker tunatakiwa kuishi na facts kuliko hisia za wananchi ambazo hazizuiliki
 
Mkuu uzuri wa JF ni pamoja na kurekebisha kama ulivyofanya....nashukuru kwa hilo....hiyo heshima ya JF unayoiona sasa hivi ujue umeikuta na kuna watu wameifikisha hapo ulipoikuta...........however, lugha uliyotumia inaonyesha ni jinsi gani ulivyo mpumbavu!...........the bottomline ni kuwa kiongozi wenu Mkopi amekana kutohusika period!........sasa kama wewe unakuja na maneno ya kipuuzi.......eti MAT hakihusiki moja kwa moja na madai yenu........ndipo unapojidhihirisha zaidi kuwa wewe ni Mpumbavu..........

Ustaarabu ni jambo la msingi kwakweli; vinginevyo tunakiuka maana halisi ya majadiliano.
 
Alijipenyezaje mpaka kuwa mbele ndio ninachotaka kujua na alikua na alikuwa ametumwa na nani kwa malipo kiasi gani maana ni wazi hakua anatumika bure

Si ametumwa na hao madaktari?
Kama angekua hawajamtuma wasingemsikiliza kila analowaambia.

Historia inatukumbusha kua hata alieongoza mapinduzi Zanzibar Bw. Okello hakua Mzanzibar.

Che Guevara, mwanamapinduzi wa kweli mwenye heshima kubwa sana duniani alijituma kusaidia ukombozi wa nchi mbalimbali zikiwemo za Africa, je nae ilikua ni lazima awe na uraia wa nchi zote hizo??

Think greatly.
 
.......halafu Katibu wake Dr. Mkopi.....alikanusha kuwa hahusiki na mgomo..........hapo ndio ujue ni kitu gani hasa kinaendelea........

We vipi? No research, no right to speak! Chunguza kwanza ujue Dr. Mkopi ni wa chama gani na Ulimboka ni wa chama gani kati ya hivi: Jumuiya ya Madaktari Tanzania au Chama cha Madaktari (MAT).
 
Kuna taarifa kwamba Dr.Ulimboka sio mtumishi wa serikali,je hili ni kweli?kama jibu ni ndio amewezaje kujipenyeza mpaka kuwa mtu mashuhuri zaidi kwenye mgogoro wa nyongeza za malupulupu ya watumishi wa serikali-madaktari waajiriwa wa serikali?alitumwa na nani na hao waliomtuma wamekuwa wakilimpa kiasi gani labda kwa mwezi.

MA DK. WAMEMWAMINI WW KINAKUWASHA KININI?

Hakuna kinachoniwasha bali natafuta facts
 
Alitumwa na professional calling deep down in him!
You dont have to be sick to treat the sick ! Please pray for his quick recovery
as Chinua Achebe said, and I quote "the chicken must be safe in the pen before its warned against wondering into the bush'
na huko kwa muajiri wake ambako huduma yake ilikua inahitajika kuokoa maisha ya watu alimuachia nani wakati anadedicate muda wake mwingi kujihusisha na mgomo usiomuhusu?alikua analipwa kiasi gani kwa kusucrifice maisha ya wagonjwa wake huko kwa muajiri wake wakati yeye akicheza ngoma asiyoifahamu?
 
Yah alikua leaderz club akipata kinywaji
Hii inatofautiana na maelezo ya awali ya Dr Ulimboka. Umeiweka katika namna ambayo unataka tuamini kuwa yaliyompata, yamempata kwa sababu ya huko kuwa kwenye ulevi...mimi naona unajaribu ku-spin tu.

Suala la yeye kutokuwa mwajiriwa wa serikali halina mashiko na ndio maana hata wenyewe (serikali) hawakumkataa. Suala la muhimu ni hoja zinazotolewa kama zina msingi ama la. Ni dhana ya 'uwakilishi' tu, na sio jambo geni katika masuala ya majadiliano. Kama wanaowakilishwa wanamkubali mwakilishi wao, tatizo lipo wapi?
 
dr steve ulimboka alipoteza ajira ya serikali kwa kuongoza madaktari katika mgimo wa 2005.
Alipoteza kazi 2005 na sasa kamwaga damu

Kumbe ni dr..basi anayohaki ya kutetea maslahi ya fani yake..MBÖNA NYERERE ALIENDA KUPIGANA KUKOMBOA KUSINI YA AFRIKA NANI ALIKUWA NYUMA YAKE? (huwezi zuia uzalendo kwa vitisho)...jamani tukikusanya kodi na kudhibiti matumizi/wizi tunaweza walipa wataalamu wetu vizuri, tusibaki sifia wenzetu..tumelogwa na nani?
 
Mkuu, nchi hii ina sheria. Kwanini sheria hazikutumika kumdhibiti Dr. Ulimboka badala ya kumuumiza vile tena kwa nia ya kuona amekufa? Wananchi wana kiu na kuiona Tanzania inakuwa njema.

Ila two wrongs can't make a right...tatizo ndo limekuwa complicated zaidi sasa! Ukifikiria kwa makini, unaona kabisa ukosefu wa busara katika kushughulikia mambo yetu.

Nguvu ina kiasi....na zile siasa za kusambaza woga hazina tija tena kwenye hii dunia ya leo.

Tujifunze kufuata sheria ili tuheshimiwe. Ilivyo sasa, wewe unaona wananchi wana hisia gani na hayo aliyotendewa Ulimboka?

wananchi gani hao wenye kiu.mbona mitaani hii topic haipo na wala hata huyo ulimbaka hajulikani?
Au wananchi waliomo Jf?
 
Kama sio mwajiriwa wa serikali madaktari wakiongezewa huo mshahara yeye atafaidika nini??

Arvin sloane,

Whether Dr.Ulimboka ni mfanyakazi wa serikali au siyo is immaterial. Jambo la msingi hapa ni kwamba kuna serious and genuine issues to be discussed between Doctors and the Govt. Hii ya Dr.Uli cjui ni mfanyakazi wa serikali au siyo ni kushindwa kufikiri nje ya box. Always try to think deep.

Viongozi wa vyama vya WAFANYAKAZI MARA NYINGI SIYO LAZIMA WAWE WAFANYA KAZI KATIKA IDARA YA CHAMA HUSIKA. Vyama vya wafanyakazi mara nyingi huajiri mtu hata kutoka nje kabisa ya tasnia husika ingawa pia wanaweza kuwa na utalaamu katika tasnia husika ya vyama vya Wafanyakazi wanavyo viongoza.

Dr.Ulimboka anaweza kuwa hayuko kwenye Serikali lakini ni Daktari katika sekta binafsi au retired Doctor.Hiyo haimuondolei haki ya kuwa kiongozi wa Chama cha Madaktari wenzake. Kumbukeni kuna madaktari katika hospitali za serikali na wale wa hospitali za binafsi wote ni madaktari wana haki ya kuchagua kiongozi wao kutoka pande zote.
 
Back
Top Bottom