Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Hili tatizo la kupinga kila kitu sasa limegeuka sumu, Chadema ilianza kama Chama chenye mawazo mbadala, baadaye kama chama/serikali mbadala huku wakiwaainisha maadui wa nchi kwa uaminifu mkuu. Baadaye wakanunuliwa na wale waliowaita maadui wa nchi na hapa ndipo balaa likaanza. Tukashuhudia pepo la kupinga kila jema likiwavaa.
mambo mengi waliyowahi kuyapendekeza ikiwamo kufuta ushuru kwenye mazao,kutambuliwa kwa wamachinga na kudhibiti mapato na kodi kwenye madini pamoja na udhibiti wa matumizi sasa wamegeuka kuwa wapingaji wa mambo hayo na kibaya zaidi siku hizi hawaji na hoja mbadala,utasikia tu 'hakuna kitu', 'wanakosea', 'mpinzani hutakiwi kuunga mkono hoja' nk..nk..nk.
Niseme tu, kupinga mfululizo husababisha sumu mwilini na baadaye mpingaji hugeuka sumu, ni pepo..na ngumu kuaminika tena. Mfano mdogo ni jinsi ambavyo Tundu lissu alivyogeuka sumu kwa nchi yake na kila dalili zipo atakuwa sumu kali kwa chama chake. Kilichobaki ni kutafunana wenyewe kwa wenyewe.
Nawasilisha.