PENZI LILILOTAZWA.. (Based on A True Story)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Na. M. M. Mwanakijiji


Moyo ulianza kunienda kwa kasi, viganja vilianza kulowa jasho, na koo lilinikauka nilipokuwa nikikata kona kuingia katika eneo la Hospitali ya Bombo, mjini Tanga. Moyo wangu ulikuwa umegubikwa na ubaridi utadhani alfajiri katika mji wa Makambako kule Iringa. Nilishikwa na huzuni, hofu, na nilihisi kuchanganyikiwa. Akili yangu ilikuwa ikinizunguka utadhani mkokoteni wa kisambaa. Nikifikiri mara milioni ni kitu gani ningekifanya tofauti kukwepa ukweli ambao ulikuwa unanikabili. Nilikuwa natembea kama akili zimeniruka nilipoingia katika geti za hospitali hiyo na hatimaye kwenye wodi ya kina mama. Nilikaribishwa hospitalini hapo na Nesi aliyevalia sare nyeupe na kikofia cheupe chenye mistari ya rangi ya hudhurungi.

“Tafadhali nifuate” Aliniambia Nesi Fatma Ally, ambaye alikuwa amevaa beji yenye jina lake. Walikuwa wananitarajia kwani Nesi Fatma aliniambia walikuta namba yangu ya simu na jina langu kwenye pochi ya mgonjwa.

Bila kufanya ajizi au kuuliza maswali nilimfuata kwa haraka huku miguu yangu nikiihisi kunitetema utadhani miti ya mianzi ipagwapo na upepo. Tuliingia katika Wodi namba tatu ambayo madirisha yake yaliangalia bahari ya ya Hindi. Vitanda vya wagonjwa vilipangwa kinadhifu na wodi nzima ilikuwa inang’ara kufuatia matengenezo ya hivi karibuni kutoka msaada wa serikali ya Ujerumani. Toka mbali niliweza kuona ngalawa na mitumbwi ikipita, wavuvi wakiendelea na uvuviw, na upeo wa mbali wa bahari hiyo niliweza kuona meli iliyotia nanga katika Gati ya Ras Kazone.

Sista Fatma (kama manesi wanavyoitwa) alinielekeza hadi kitanda namba 11 kilichokuwa kwenye kona. Nilisogea na moyo wangu nusura unitoke kwani mpenzi wangu wa moyoni, wa ubani wangu na aliyekuwa nuru ya maisha yangu alikuwa amelala chali akizungukwa na mipira na machine za kila aina zilizomsaidia kunusuru maisha yake.


SOMA ZAIDI HAPA (USIMWAMBIE MTU - NO UNDER 18)
 
Mwanakijiji unatisha!khe! Kumbe utamu halisi umeweka chumbani hapa ni kionjo tu!nimeshasoma robo sisemi sana wacha niendelee nitarudi........:biggrin: :biggrin:
 
Mwanakijiji unatisha!khe! Kumbe utamu halisi umeweka chumbani hapa ni kionjo tu!nimeshasoma robo sisemi sana wacha niendelee nitarudi........:biggrin: :biggrin:

Utam????Gud mrng wise!!
 
man...u are indeed a writer! Unajenga maudhui vizuri sana, kiasi mtu anapata picha nzima ya eneo. Hiyo ndio sign ya mwandishi mzuri. Sijui kama umeandika vitabu na kuviuza mkuu? Ningependa kununua angalau kimoja nikipata nafasi.
 
Mwanakijiji WEWE NI NOMA! Hii story Ijazie matukio mengi zaidi, naimani ni synopsis uliyotupa then kuja na kijitapu. Mengine yote fine, Ukweli upo pale pale kuwa we mkali bro. Much salute!
 
Mwanakijiji WEWE NI NOMA! Nimependa arrangement yake zaid n hiyo flashback style yako. Hii story ipo poa chamsing Ijazie matukio mengi zaidi, naimani ni synopsis uliyotupa tu then kuja na kijitabu. Kwa jinsi ulivyotenga hoja sina shaka na kipaji chako, ur realy a story writer and you deserve to have more readers than in facebook and jamiiforums. Mengine yote fine, Ukweli upo pale pale kuwa we mkali bro. Much salute!
 
Badala ya kumalizia kusoma... nimeishia kupata shock niko facebook... NICE ONE...
 
umenikumbusha enzi zileeeeee za hadithi za chiku binti kachumbari!!!


ha hahaaaaaaa!! uko juuuuuu sana!!
 
Baada ya kusoma mpaka mwisho,,nimeamua kufuta comment yangu ya mwanzo. Duu!!inasikitisha.
 
Wewe ni creative writter,na kama hujasomea basi kipaj unacho,kanun zote za uandish wa riwaya umezizngatia,matumiz ya lugha,tamathal za semi,umeingza tanzu za fasihi simulizi kama nyimbo,mandhari umeijenga vzuri,wahusika umewajenga vizuri,NAHSI HII NI RIWAYA PENDWA,lakini sokoni ujue na watoto wataipata,
any way hongera mwanavillage
 
Mshikaji we ni bonge la novelist, chumbani nilisoma kitu hati nikanihi(pale hotelin) nikalia(ajal, na kifo) na kiukwel mwanakijiji mazee we ni mkareeeeeee!
 
l salute u kwa jinsi unavyoweza cheza na lugha,maana lugha unaifinyanga utakavyo kazi kwa wenye kutafsiri
 
Back
Top Bottom