Penzi letu la zamani

Tamu3

Member
Feb 17, 2023
25
16
1710779530473.jpg

Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati,
Tulikutana mtoni, kuipanga mikakati,
Halikuwa la kihuni, lisilo la kisaliti,
Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati.

Tulikutana porini, tunapookota kuni,
Ugumu tulipateni, mpenzi kuweka ndani,
Mahari ng'ombe sitini, mwari wamtoleeni,
Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati.

Kukuta binti bikra, ilikuwa kawaida,
Nani yake mashaara, haijaguswa na rada,
Binti mweupe wa sura, dau lilikuwa zida,
Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati.

Michepuko Kama sasa, haikuwepo zamani,
Ilikuwa kubwa kosa, watozwa hiyo faini,
Ilikuwa si ruhusa, kuidhinisha uhuni,
Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati.

Heshima ndani ya ndoa, ilikuwa namba wani,
Ndoa za kimazoea, likuwa mwiko nyumbani,
Mme na mkewe pia, pamoja lifurahini,
Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati.

Penzi letu la zamani, lilikuwa tamu tamu,
Bila woga lifanyeni, ukimwi bado lakini,
Mipira ya kuvaeni, haikuwepo zamani,
Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati.

Wapenzi walipendana, huba lao likanoga,
Wote liheshimiana, jioni kipiga soga,
Alifundwa msichana, siha njema ya kuoga,
Penzi letu la zamani, lilikuwa ni la dhati.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa Mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi TANZANIA
 
Hata sasa kumkuta bikra ni Kawaida ila shida nyie wa kisasa mnatoboa na kumwacha akiwa singlemom
 
Back
Top Bottom