Penzi lenye Maumivu

Penzi lenye Maumivu

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,177
Reaction score
34,444
PENZI LENYE MAUMIVU-01
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Katika maisha yangu yote ya ndoa sikuwa ni miongoni kati ya wale wanaume waliyotulia. Licha ya kuwa mke wangu, Lillian alinionyesha mapenzi ya dhati, alinijali pamoja na kunithamini lakini hilo sikuonekana kujali, isipokuwa nilikuwa bize kuwatongoza wasichana ambao mwisho wa siku nilitembea nao.
Kwa kuwa nilikuwa nikifanya biashara nyingi hapa mjini ambazo zilikuwa zikiniingizia kiasi kikubwa cha pesa, hivyo sikuona ugumu wowote kumfuata msichana mrembo niliyemtamani na kumtongoza.
Katika maisha yangu ya ndoa na Lillian nilibahatika kuzaa naye mtoto mmoja wa kiume ambaye tulimpa jina la Brighton. Kama ilivyozoeleka katika maisha ya ndoa nyingi pindi mtoto anapozaliwa basi furaha na upendo huongezeka ndani ya nyumba lakini hali hiyo haikuwa kwangu. Sijui niseme nilirogwa maana siamini kile kilichotokea. Kwanza nakumbuka kipindi nilipofunga ndoa na Lillian na rasmi kuutangazia umma kuwa mwili mmoja kama vitabu vya dini vilivyoandikwa, nilikuwa nina wivu sana, wala sidhani kama kuna mwanaume ambaye alikuwa na wivu kama niliyokuwa nao kwa mke wangu.
Sikutaka awe na ukaribu wowote na kiumbe kiitwacho mwanaume, yaani neno lolote la utani aliloambiwa hata na ndugu yake wa damu ambaye alinitambulisha kama kaka yake au mjomba wake mimi kwangu lilinikwaza na kusababisha ugomvi mkubwa kati yetu.
Wivu wangu wa kimapenzi ndiyo uliyosababisha nikamkataza Lillian asifanye biashara yoyote ile, sio kwamba sikuwa nina uwezo la, kama nilivyotoka kukisimulia kuwa nilikuwa nikifanya biashara nyingi tena zilizokuwa zikiniingizia kiasi kikubwa cha pesa lakini hofu yangu kubwa ilikuwa ni kama ningekubali kumfungulia biashara mke wangu aifanye basi nilikuwa nikijitengenezea mazingira ya kuja kumwaga machozi ya kusalitiwa baadae.
Hapo kabla niliwahi kuwashuhudia baadhi ya marafiki zangu waliyowahi kuoa kabla yangu wakisalitiwa na kuumizwa vibaya mno na mapenzi. Hilo sikutaka litokee kwangu na ndiyo sababu kitu nilichokiamini ni sahihi kukifanya ni kumkataza Lillian asifanye biashara yoyote. Nilikuwa nipo radhi kumuhudumia kila kitu alichokuwa akikihitaji lakini sio kuona akitoka nje na kwenda kufanya biashara.
Baada ya Lillian kubeba ujauzito wangu ndipo hapo mambo yalipoanza kubadilika. Ghalfa! nilianza kumdharau, nilimuona kuwa mwanamke wa kawaida mno, hakunivutia kwa chochote wala kwa lolote lile, kipindi hicho cha ujauzito kilikuwa ni kipindi ambacho nilimuona kuwa kama mwanaume mwenzangu.
*****
Siku moja majira ya saa 12:30 jioni nilipokuwa nikitoka Milimani City nikirudi nyumbani kwangu Mbezi Beach Africana, nilikuwa ndani ya gari langu aina ya Toyota Mark X lenye rangi nyeusi, nilikuwa nikitembelea mwendo wa kawaida sana kiasi kwamba kwa wakati huo niliweza kuona kila kitu kwa upande wa nje, japokuwa nilikuwa nimefunga vioo vyote kwani gari lilikuwa na kiyoyozi.
Nilipofika kituo cha Mwenge ilibidi nisimamishe gari, sio kwamba nilipata tatizo la isipokuwa nilimuona msichana mrembo akiwa amesimama kituoni hapo.
Siku hiyo usafiri ulikuwa ni wa shida sana, abiria wengi walionekana kusubiria usafiri kwa muda mrefu huku wengine wakionekana kukata tamaa.
Nilishusha kioo cha upande wa kushoto kisha nikapiga honi, halafu nikanyoosha kidole kuashiria nilikuwa nikimuita huyo msichana. Kijana mmoja ambaye na yeye alikuwa amesimama eneo hilo akamgusa na kumpa ishara kuwa nilimuita.
Haikuchukua sekunde nyingi baada ya kuguswa na kijana huyo nikamuona akinifuata.
"Samahani kaka angu nimeambiwa unaniita, sijui una shida gani?" aliniuliza huku akionekana kuwa mwenye wasiwasi.
"Ndiyo nimekuita, nataka nikupe lift kama hutojali, sijui unaelekea wapi nikupeleke mrembo," nilimjibu kisha nikatoa tabasamu pana, akaonekana kuogopa zaidi.
"Hapana kaka angu usijali asante nashukuru sana," aliniambia huku akijing'atang'ata.
"Kwahiyo umeona ukiniambia unaelekea wapi nitanenepa au?"
"Hapana."
"Kwani unaishi wapi?"
"Hapo Tank bovu."
"Kumbe hapo tu panda nikusogeze usiogope."
"Hapana asante nashukuru."
"Sikia embu jaribu kuukunjua moyo wako halafu niamini just a few minutes okay! I'm good man so don't be afraid," nilimwambia.
Japokuwa nilitumia zaidi ya dakika tano kuzungumza naye lakini mwisho wa siku alikubali nimpe lift, hapa ni baada ya kuona muda unazidi kwenda na daladala zilikuwa ni za tabu siku hiyo.
Kitendo cha msichana huyo kukubali nimpe lift kilinifanya nijisikie mwenye furaha kubwa mno moyoni mwangu.
Alionekana kuwa msichana mrembo wa sura, umbo matata, kwa kifupi nilipomtazama kwa mara ya kwanza nikajikuta nikimtamani.
"Unaitwa nani?" nilimuuliza, wakati huo nilikuwa nimefika Makongo, nikapunguza mwendo kwa makusudi, lengo langu lilikuwa ni maongezi yazidi kuwa mengi.
"Naitwa Coletha," alijitambulisha.
"Oooh! Una jina zuri sana mrembo," nilimwambia huku nikitabasamu.
"Asante sana na wewe unaitwa nani?"
"Naitwa Kelvin."
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kufahamiana na Coletha, kwenye gari tulizungumza mambo mengi mpaka kufikia hatua nikafahamu alikuwa ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto watatu katika familia yao (Mtoto wa kwanza ni Dada yake ambaye alinitambulisha kwa jina la Caren na wa mwisho ni mdogo wake wa kiume ambaye alikuwa akiitwa Samwel) lakini pia alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu.
Ndani ya muda mfupi niliyokutana na Coletha mpaka nikafikia hatua ya kumpa lift, sikutaka mawasiliano yetu yaishie Tank bovu kituoni, nilichoamua kukifanya ni kubadilishana naye namba za simu na huo ndiyo ulikuwa muendelezo wa kuwasiliana.
Kila siku nilihakikisha namtumia meseji Coletha, nampigia simu na hata kumjali kushinda mke wangu ambaye alikuwa ni mjamzito.
Mawasiliano yangu na Coletha mwisho wa siku yalizaa penzi. Katika kipindi hicho sikujali kuhusu mke wangu Lillian ambaye nilikuwa nikimsaliti. Nilijiona kuwa sahihi kwa kila kitu nilichokuwa nikikifanya katika maisha yangu.
*
 
PENZI LENYE MAUMIVU-02
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Nilimdharau sana Lillian, japokuwa mwanzoni nilimuona kuwa mwanamke mrembo lakini wakati huo macho yangu yalimuona kuwa mwanamke m'baya sana, kuna wakati nilimfananisha na wale viumbe wa sayari nyingine.
Katika kipindi hicho akili yangu ilikuwa ikimfikiria Coletha tu! Alikuwa ni mwanamke mrembo mwenye sura ya kuvutia, macho ya kuita, kifua kilichosimama, umbo matata, yaani kwa kifupi alivutia mno.
Sikuona ajabu kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kwenda kufanya starehe na Coletha. Niliutumia muda wangu mwingi kwake kuliko kwa mke wangu Lillian ambaye alinihitaji usiku na mchana.
Ndani ya mwezi mmoja tangu alipopata ujauzito tayari aligundua mabadiliko yangu. Nilipunguza mapenzi kwake kwa asilimia themanini 80% jambo ambalo lilikuwa ni rahisi kuyaona mabadiliko yangu.
Hakutaka kubaki kimya, aliniuliza tatizo lililokuwa limetokea mpaka likanibadilisha kiasi hicho lakini sikuwa tayari kumueleza ukweli, nilimdanganya kuwa ubize wa biashara zangu ndiyo uliyosababisha yote hayo.
Wakati yote hayo yakiendelea nyuma ya pazia niliendelea kumsaliti mke wangu. Coletha na yeye sikumueleza ukweli, nilimficha huku akiamini katika maisha yangu sikuwa na mke.
****
Siku moja majira ya mchana nilipokuwa nyumbani Coletha alinipigia simu, akaniambia kuwa alihitahi kuniona kwa wakati huo kwani alikuwa akiumwa sana.
"Saa ngapi?" nilimuuliza.
"Hata sasa hivi ikiwezekana naumwa sana mpenzi," alinijibu kwa sauti ya kulalamika.
"Kwani uko wapi?" nilimuuliza.
"Nipo chuo," alinijibu.
"Sawa nakuja," nilimwambia kisha nikakata simu.
Sikutaka kupoteza muda, nikaanza kujiandaa harakaharaka, nilipomaliza nikamuaga Lillian ambaye muda wote huo alibaki akinishangaa kwani nilionekana kama mtu niliyechanganyikiwa hivi.
"Kuna nini na unaenda wapi?" aliniuliza Lillian.
"Nimepigiwa simu na mfanyabiashara mwenzangu kaniambia kuna mzigo umeingia bandarini sasa hivi hivyo natakiwa niende huko, yeye hayupo mjini ndiyo sababu amenipigia mimi," nilimjibu huku nikionyesha msisitizo wa hali ya juu.
"Sawa mume wangu, leo utarudi mapema?" aliniuliza.
"Sijajua ila nitakupigia simu," nilimjibu kisha nikamuaga na kuondoka.
Nilipokuwa ndani ya gari, niliendesha kama mwendawazimu, sikutaka kupoteza muda mpaka pale nilipofika eneo hilo la chuo kikuu cha Daresalaam.
Nilimpigia simu Coletha na kumwambia kuwa tayari nilikuwa nilifika eneo hilo la chuo, akaniambia nisubiri, nikasubiri.
Ndani ya dakika tatu au nne hivi nikamuona Coletha akiwa anakuja huku akiongozana na wasichana wawili. Kwa jinsi nilivyokuwa nikimuangalia hakuonekana kuwa mgonjwa kama alivyoniambia kwani nilimuona akizungumza na kucheka pamoja na wale wasichana aliyoongozana nao.
Walipofika nikawaruhusu waingie ndani ya gari, wale wasichana wawili walikaa siti za nyuma, Coletha akakaa siti ya mbele nikawa natazamana naye.
Hakutaka kuificha furaha alivyokuwa nayo baada ya kuniona, akanikumbatia huku akinipiga mabusu mfululizo. Wale wasichana wakabaki wakitutazama kama muvi.
"Baby hawa ni marafiki zangu, huyu anaitwa Loveness na huyu anaitwa Getrude. Hey Getrude and Loveness this is my future husband," alinitambulisha Coletha, macho yangu yakatua kwa Getrude, huyu alionekana kuwa msichana mrembo kuliko wote, alimzidi mpaka Coletha.
"Nashukuru kukufahamu Shem," aliniambia Loveness kisha akanipa mkono.
"Okay mimi pia," nilimwambia kisha nikatoa tabasamu pana.
"Nice to meet you Shem," aliniambia Getrude kisha na yeye akanipa mkono.
"Me too," nilimwambia huku na mimi nikitoa tabasamu.
Mpaka kufikia muda huo sikuelewa nini kilichokuwa kikiendelea, maana Coletha alionekana kuwa mwenye furaha kiasi kwamba nikaanza kushangaa.
"Nini baby?" aliniuliza.
"Huyo mgonjwa yuko wapi?" nilimuuliza.
"Jamani baby hata siumwi, nilikumis tu, nilitaka kukuona halafu pia nilitaka nikutambulishe marafiki zangu," aliniambia kwa sauti ya kudeka.
"Hilo tu?" nilimuuliza.
"Ndiyo," alinijibu kisha akacheka, Getrude na Loveness na wao pia wakacheka.
Nilijikuta na mimi nikicheka, basi furaha ikawa imetawala, muda wote Coletha alikuwa akijibebisha.
Macho yangu yalikuwa yakimuangalia Getrude ambaye alionekana kuwa mwenye aibu mno.
"Kwahiyo mnaratiba gani sasa hivi?" niliwauliza.
"Now tuko free, hatuna kipindi mpaka kesho tena," alijibu Coletha huku akiwaangalia wenzake, wote wakaitikia.
Wazo lililonijia kwa wakati huo ni kuwapeleka Mlimani City ambapo huko ningewafanyia shopping ya maana, sikutaka kuwauliza walitaka nini au walipanga kwenda wapi.
Nilichokifanya nilitembeza gari mpaka Mlimani City. Tulipofika niliwaambia wafanye shopping wanayoitaka wote watatu. Wakaonekana kufurahi.
Hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee niliyoitumia kuwateka marafiki zake, nilifahamu siku moja ningetembea nao kila mmoja kwa muda wake hivyo kwanza nilitaka wafahamu kuwa mimi ni nani? na nilikuwa nina pesa kiasi gani.
Shopping ambayo waliifanya siku hiyo iligharimu kiasi cha shilingi laki saba 700,000, nikalipa huku nikiwalaumu kuwa hawakuijua kutumia pesa, yaani kitendo cha kufanya shopping ya laki saba nilikifananisha na shilingi elfu saba 7,000.
Siku hiyo nilipanga kuwaonyeshea jeuri ya pesa, tulipotoka Mlimani City niliwapeleka Posta pale Serena hotel, huko nikawaambia waagize kila kitu wanachojisikia kuagiza kisha ningelipia. Kama nilivyowaambia ndivyo walivyofanya na ndicho kilichotokea.
Baada ya kumaliza kula na kunywa huku tukiwa tumeongea mengi hatimaye bili ilikuja, nikalipa huku nikionekana kutokuwa na wasiwasi wowote.
Kila kitu nilichokuwa nikikifanya siku hiyo niliamini nilikuwa nikiweka kumbukumbu katika vichwa vyao.
Coletha alizidi kupagawa, hakuamini kama katika maisha yake aliweza kukutana na mwanaume mwenye pesa kama mimi. Yaani kila kitu alichokuwa akikihitaji nilimtimizia tena kwa haraka kama risasi inavyofyatuliwa.
Siku ziliendelea kukatika, katika hali ya kushangaza nilianza kuonyesha chuki za waziwazi kwa Lilian. Nilimchukia kiasi kwamba kuna kipindi kilifikia akawa akikosea kidogo namfokea na kumpiga bila kujali hali aliyokuwa nayo.
Hicho kilikuwa ni kipindi cha kilio na maumivu kwa mke wangu. Sikujali lolote, niliendelea kula starehe na Coletha
 
PENZI LENYE MAUMIVU-03
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Kila nililokuwa nikilifanya lilimliza mke wangu na kumpa maumivu makali mno, sikujali lolote lile kwani mapenzi yangu kwa wakati huo yalihamia kwa mwanamke mwingine ambaye ndiye alikuwa akikidhi haja zangu. Nilimgharamia Coletha, nilimpa matunzo yote, ilipofika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (Birthday party) sikuona tabu kumnunulia gari show room aina ya Harrier yenye gharama ya shilingi milioni 30.
Coletha alizidi kunipenda mno, nilikuwa huru kimapenzi chochote ambacho nilitaka kukifanya kwake nilikifanya tena bila kuomba samahani.
Kipindi hicho tayari alinitambulisha kwa ndugu zake, wakawa wananifahamu. Hata pale siku za wikiendi nilipoamua kumchukua na kwenda naye sehemu kama Zanzibar, Mombasa au mbuga za wanyama kutalii nilikuwa huru naye. Nilifanya kila aina ya starehe na Coletha.
"Baby unakwendaga klabu?" aliniuliza Coletha siku moja, nilikuwa nikizungumza kwenye simu.
"Ndiyo lakini mara moja moja," nilimjibu.
"Basi nataka wikiendi hii twende wote klabu," aliniambia kwa sauti fulani hivi ya kumtoa nyoka pangoni, mwili wangu wote ukasisimka, nikajikuta nikimkubalia.
Wikiendi ilipofika kama alivyoniomba kweli tukaenda klabu, huko hakukuwa na kitu kingine kilichoendelea zaidi ya kunywa pombe na kucheza muziki kwenda mbele.
Nilikuwa ni mwenye furaha mno kuwa na Coletha msichana ambaye alijua nini maana ya kuishi mjini, kama ni starehe zote alizifahamu hivyo sikupata shida kabisa.
Nilipomfananisha Coletha na Lillian mke wangu niliwaona wasichana wawili tofauti, macho yangu yalimuona Coletha kuwa bora zaidi kuliko Lillian ambaye kwanza katika kipindi hicho alikuwa na tumbo kubwa, mimba yake ilitosha kuwa mzigo kwangu, nilifahamu huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kufanya naye mapenzi.
Kipindi hicho kilikuwa ni kipindi ambacho matumizi yangu ya pesa yalikuwa ni makubwa, nilitaka kuwaonyesha watu ni jinsi gani nilivyokuwa na pesa nyingi, nilianza tabia ya kubadilisha magari, yaani kama leo ukinikuta natembelea Land Cruiser Prado kesho utanikuta natembelea BMW X6. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu, waliyonifahamu walipenda kuniita Billionea Kelvin, nilikuwa nikitabasamu muda wote, jina hilo nililiona likinifaa kabisa.
Wakati nikiyafanya yote hayo mke wangu Lilian alikuwa akidondokwa na machozi, japokuwa nilimtafutia dada wa kazi ambaye alimsaidia kazi za nyumbani lakini sikutaka kumjali, kwa macho ya harakaharaka kama ungenitazama maisha nilizokuwa nayo ungeamini kabisa hata mke wangu alikuwa ni mwenye furaha kwani hakukuwa kitu alichokikosa, huo ndiyo ukweli ambao ungeuamini lakini nyuma ya pazia kuna siri kubwa imejificha. Nilikuwa ni mtu wa kumliza mke wangu kila siku, nilimnyanyasa na kumfanya ajutie kubeba ujauzito wangu.
"If I'm wrong please forgive me," (Kama nimekukosea tafadhali nisamehe) aliniambia Lillian huku machozi yakimdondoka.
Sikuyaangalia machozi yake wala sikutaka kumjibu lolote, nilichokifanya kwa kuwa siku hiyo nilipanga kuonana na Coletha niliamua kuondoka lakini ghafla! nikashangaa akinishika mkono, hakutaka kuona nikiondoka bila kumjibu lolote, hilo ndilo lililokuwa kosa kubwa alilolifanya, yaani nililifananisha na traffic kusimamisha gari lililokuwa katika msafara wa raisi.
Bila hata kuuliza hapohapo nikampiga kofi moja lililomuacha na alama shavuni, akaanza kulia kwa sauti ya kwikwi.
"Usije ukarudia kunishika mkono tena, nitakuua," nilimwambia kwa sauti ya hasira kisha nikaondoka zangu, nikamuacha akilia kwa kuugulia maumivu ya kofi.
****
Japokuwa nilikuwa nikitembea na Coletha lakini moyo wangu ulianza kuingiwa na tamaa, nilimtamani rafiki yake Getrude na ni hapo ambapo moyo wangu ulianza kuishi kwake.
Kosa kubwa la jinai ambalo alilifanya Coletha ni kukubali kunipa namba ya simu ya Getrude na Loveness siku ile ya Birthday party. Hapo ndipo moyo wangu ulipohama kwake, ukahamia kwa Getrude ambaye na yeye alionekana kutamani kuwa na mimi kupita maelezo. Njia zote alinionyesha, milango yote aliifungua, kilichobaki ilikuwa ni mimi kupita katika njia hizo na mwisho wa siku kuingia katika milango ambayo ilikuwa wazi.
Hakutaka kuniita jina la shemeji tena, akabadilisha akawa ananiita jina la My. Awali nilichukulia kawaida lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga nilianza kuona tofauti.
"Kama sio rafiki ningehakikisha nakupata," aliniambia Getrude siku moja nilipompigia simu, sauti yake ilikuwa ni ya utulivu kitu ambacho kilionyesha alikuwa akimaanisha kile ambacho alikizungumza.
"Kwanini na ungewezaje kunipata wakati hata hunifahamu?" nilimuuliza kisha nikaanza kucheka.
"Ningejua tu pakukupata my unajua wewe na Coletha hata hamuendani sema kwa kuwa sisi ni marafiki zake tunamsifia kwa kumpaka mafuta," aliniambia Getrude.
"Kivipi siendani naye?"
"My kwa muonekano wako jinsi ulivyo unatakiwa uwe na msichana mrembo, Coletha hakufai," alinijibu.
Maneno ya Getrude yalitosha kunipa maana na dhamira yake, nilifahamu kuwa alinipenda, alitamani kuwa na mimi na ndiyo sababu akazungumza yote yale.
Kwa kuwa na mimi nilimpenda tangu siku ya kwanza nilipomuona, nilijisemea kimoyomoyo kuwa lazima nitembee naye, yaani ilikuwa ni lazima Coletha nimsaliti kwa kutembea na rafiki yake.
****
Usaliti haukuanzia kwa mke wangu Lilian tu, uliendelea mpaka kwa Coletha. Kipindi ambacho aliamini nilimpenda na kumuhitaji kupita maelezo ndicho kipindi hicho hicho ambacho nilimzunguka na kutembea na rafiki yake.

Je, nini kitaendelea?
 
PENZI LENYE MAUMIVU-04
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Kama ilivyokuwa kwa Coletha na kwa Getrude pia nilifanya hivyohivyo. Nilikuwa nikimtoa out nyingi zilizogharimu kiasi kikubwa cha pesa. Kwangu sikuona tatizo hata kidogo, kama kwa mwezi nilikuwa nikiingiza kiasi cha shilingi milioni kumi, kitendo cha kutumia milioni tatu au nne kwa mtoko mmoja hakikunishtua chochote.
Getrude alizidi kuchanganyikiwa kila aliponiona, hakuacha kunisifia, kwake nilionekana kuwa mwanaume mwenye pesa ambaye nilikuwa kama mkombozi wa shida zake.
Mpaka tunafanikiwa kuwa katika mapenzi yeye ndiye aliyenitongoza, aliniambia mengi kuhusu hisia zake kwa wakati huo ambazo zilinihitaji kupita maelezo. Niliitumia nafasi hiyo kufanya naye starehe huku Coletha akiwa hafahamu lolote.
Licha ya mambo yote niliyokuwa nikiyafanya bado niliendelea kumliza mke wangu, nilikuwa sababu ya kumpa maumivu kila kukicha. Hakukuwa na furaha ndani ya nyumba, matusi, kipigo na hata kumkaripia ilikuwa ni sehemu ya maisha yangu.
Sikujali machozi na maumivu yake kwa wakati huo, niliyafananisha na machozi ya waigizaji wa bongo muvi.
"Kwanini unanichukia kiasi hiki, nimekukosea nini mume wangu?" aliniuliza Lillian, machozi yalikuwa yakimtoka, nilimkazia macho, hasira zilikuwa zimenitawala. Sikumjibu kitu.
"Mume wangu," aliniita.
"Sema," nilimjibu kwa kumfokea.
"Huyu mtoto anakuhitaji sana, wewe ndiyo baba yake lakini umebadilika, hunipendi, hukipendi hata hiki kiumbe kilichokuwa tumboni, sijui kimekukosea nini?" aliniuliza Lillian, machozi yaliendelea kumtoka.
"Sikia sina muda wa kuzungumzia huo upuuzi kwa sasa, nipo bize na mambo yangu, halafu nashangaa unaniambia nakuchukia hivi unajua maana ya kuchukiwa wewe... eeeh?" nilimuuliza kwa ukali swali ambalo alishindwa kulijibu, akabaki akitikisa kichwa chake kuashiria hakufahamu lolote.
Sikuwa na huruma na mke wangu, nilimchukia bila sababu, hata pale nilipoanzisha mahusiano na wasichana wengine sikuhofia jambo lolote.
Kuna kipindi kilifika nikawa mpaka namtajia majina na kumuonyesha picha za wanawake ambao nilikuwa nikitembea nao, kitendo hicho kilimuumiza mno.
Nilifanya yote hayo huku nikiamini kwa asilimia mia moja ilikuwa ni vigumu kwa Lillian kunishtaki au kunipeleka katika vyombo vya sheria. Hii ni kwasababu nilimtoa katika familia yenye dhiki kubwa, nilimsaidia mengi, niliwasaidia wazazi wake ambao walikuwa katika hali ngumu. Kutokana na dhiki iliyoikumba familia yao kitendo cha mimi kumuoa kilionekana kuwa neema katika familia yao.
Nguvu ya pesa niliyokuwa nayo ilinifanya niwe na jeuri wa kufanya lolote katika maisha yangu ya ndoa.
Wakati ambao Lillian alikuwa akitokwa na machozi, moyo wake ukipata maumivu ya mapenzi kwa upande wa pili nilikuwa nikitembea na Getrude pamoja na Coletha. Nilitumia matumizi makubwa ya pesa. Kwao sikutaka kuonekana jeuri au katili kama nilivyokuwa kwa Lillian, nilionekana kuwa mwanaume mpole, mwenye mapenzi tena niliyehodari wa kusifia na kubembeleza.
Ndani ya muda mfupi tayari Coletha nilimnunulia gari, nilimpa kila kitu alichokuwa akikitaka, nilikuwa katika mpango ya kumnunulia nyumba kwani huo ndiyo ulikuwa mwaka wake wa mwisho chuoni. Alifurahi sana, kutokana na imani kubwa aliyoniwekea akanitambulisha kwa ndugu zake, wakanifahamu lakini sikuwa tayari kuwaeleza ukweli kuwa mimi ni mume wa mtu.
Huwezi kuamini, nilifanya yote hayo lakini akili yangu iliniambia ni lazima siku moja ningeachana na Coletha kwani kulikuwa kuna wasichana warembo zaidi yake, kila siku walikuwa wakizaliwa Muhimbili.
Hivi ndivyo nguvu ya pesa ilivyonipa jeuri na kiburi, kila nililolifanya lilikuwa likimliza na kumuumiza Lillian.
"Lazima nikuoe Coletha, nakwambia lazima nikuoe," nilimwambia maneno haya Coletha nilipokuwa nikizungumza naye kwenye simu majira ya usiku, nilikuwa nimelala na Lillian, aliponisikia akashtuka.
"Who is Coletha?" (Coletha ni nani?) aliniuliza.
"She is my girl," (Ni mwanamke wangu) nilimjibu kisha akaonekana kushikwa na bumbuwazi. Hakuamini kile nilichomwambia.
Jibu langu likamfanya atokwe na chozi, nikaonekana kutojali kitu, kama haitoshi nikampigia simu Getrude na kuanza kuzungumza naye. Kiukweli niliendelea kumuweka Lillian katika wakati wa maumivu.
Hakujua ni kosa gani alilonikosea katika maisha yangu kiasi kwamba liliniudhi na kunibadilisha kuwa mbogo. Licha ya vituko na mambo yote niliyokuwa nikimfanyia Lillian, katika hali ya kushangaza bado akawa ananiomba msamaha kwa kosa ambalo hakulifanya yeye, sikuwa tayari kumsamehe, niliendelea kumtesa japokuwa nilifahamu fika kuwa mimi ndiye nilikuwa mwenye makosa.
****
Baada ya kupita miezi tisa hatimaye Lillian alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume ambaye tulimuita jina la Brighton, alikuwa ni mtoto mwenye afya nzuri.
Nilipokea sifa nyingi kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walikuja kumuona mwanangu. Maisha yalibadilika kwa kiasi fulani, nikaonekana kujirudi na kuanza kumjali mke wangu, japokuwa tabia yangu ya kumsaliti sikuiacha lakini niliamua kumuomba msamaha na maisha yetu yakaendelea kama kawaida. Lillian akafurahi mno, hatimaye maisha ya furaha yakatutawala huku mtoto wetu Brighton akiendelea kukua. Katika maisha ya ukuaji wa Brighton nilianza kuiona tofauti katika mwili wake, mwanzoni sikuitilia maanani lakini kadri siku zilivyokuwa zikikatika ndivyo ambavyo tofauti hiyo ilizidi kuonekana. Na ni katika tofauti hiyo ya Brighton ikanifanya niingiwe na chuki nyingine tena, safari hii ilikuwa ni tofauti na ile ya mwanzo.

Je, nini kitaendelea?
Ni tofauti gani hiyo iliyoonekana katika mwili wa Brighton?
Na ni nini hatma ya Lillian?
 
PENZI LENYE MAUMIVU-05
Mtunzi:Juma Hiza
0712988278

Ndani ya kipindi cha miaka miwili niliishi na mke wangu maisha ya raha mustarehe, kilikuwa ni kipindi alichojivunia mno kuwa mimi. Ndoa iliyoonekana kuingia doa hapo mwanzo ikawa imefutika, kikawa ni kipindi cha furaha muda wote.
Mtoto wetu Brighton aliendelea kukua vyema huku akiwa ni mwenye afya nzuri. Kila aliyekuja kumuona mwanangu alivutiwa naye jambo ambalo lilifanya akapendwa na kila mtu.
Katika kipindi hicho cha miaka miwili, nilianza kuiona tofauti katika mwili wa mwanangu. Hakuwa kama watoto wengine ambao walikuwa katika ukuaji wao. Yeye alichukua muda mrefu sana kutambaa, sio kutambaa tu bali hata kwenye kuzungumza mdomo wake ulikuwa mzito. Kwa kumuangalia alionekana kuwa kama bubu.
Hilo sikutaka kukubaliana nalo, ikabidi nimpeleke hospitalini ili aweze kupimwa igundulike nini tatizo lililokuwa likimsumbua. Mke wangu Lilian tayari alianza kupatwa na wasiwasi, hakujua ni nini kilichokuwa kinakwenda kutokea katika maisha ya mtoto wetu.
Baada ya kufanyiwa vipimo majibu ya daktari yalionyesha kuwa mwanangu Brighton alipata ulemavu wa miguu hivyo ndiyo ilikuwa sababu iliyosababisha kushindwa kutambaa na hata kutembea kama watoto wengine. Daktari hakuishia hapo, aliendelea kuzungumza, majibu yake ya mwisho yalinisononesha kiasi kwamba nikahisi kuishiwa nguvu za mwili. Wakati huo Lillian machozi yalikuwa yakimtoka.
"Pia tumejaribu kuchukua baadhi vipimo, tumegundua mtoto wenu ana kifafa," alisema daktari majibu yaliyoendelea kuniumiza.
"Unasemaje dokta?" aliuliza Lillian kwa mshangao mkubwa, machozi yaliendelea kumtoka.
"Jamani hayo ndiyo majibu ya mtoto wenu na kama mnavyojua ugonjwa huu wa kifafa hauna tiba hivyo kuna dawa tumemuandikia za kupunguza makali lakini kupona hatoweza," alijibu dokta.
Nilishikwa na bumbuwazi, nikabaki namtazama daktari ambaye alinipa majibu ambayo nilihisi hayakuwa ni ya mwanangu, niliamini labda alichanganya mafaili, nikamuuliza tena swali ambalo mke wangu Lillian alitoka kuliuliza muda huohuo na majibu yake yakawa ni mtoto wetu asingeweza kupona tena na kwa ulemavu wa miguu aliyokuwa nao ungebakia kuwa ni wa hivyohivyo milele mpaka siku ya kufa kwake.
"Ninauhakika na hiki ninachowaeleza wala sijachanganya mafaili, mtoto wenu anaitwa Brighton Kelvin na haya ndiyo majibu yake," alisema dokta kwa msisitizo.
Ugonjwa huu wa kifafa ni ugonjwa unaosababishwa na seli za mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutia umeme (Impulse) mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu nyingine za mwili.
Dalili za kifafa ni kuanguka chini na kupoteza fahamu, kukakamaa, mapovu kutoka mdomoni, kichwa kuuma, kushindwa kuona vizuri, kutetemeka mwili.
Chanzo cha ugonjwa huu wa kifafa ni ugonjwa wa kurithi, kuumia sehemu za kichwani, ulaji wa nyama ya nguruwe, homa ya uti wa mgongo, uvimbe kwenye ubongo, kiharusi, matatizo wakati wa kuzaliwa, magonjwa ya uzeeni, matatizo ya utengenezaji mtoto tumboni na kukosa usingizi kwa muda mrefu.
Jinsi ya kumsaidia mtu mwenye tatizo hili la kifafa, ondoa vitu vya ncha kali karibu yake, kumuweka juu ya kitu laini kama vile godoro, usimpe chochote mdomoni, usimshike kuzuia mizunguko yake. Weka kichwa chake kilale ubavu mmoja.
Vipimo vya kimahabara ni maji ya uti wa mgongo, picha ya ubongo (Scan), x ray ya kifua, uwezo wa kazi ya maini na uwezo wa kazi ya figo.
Tiba ya ugonjwa wa kifafa, kiukweli ugonjwa huu hauna tiba na mpaka sasa hivi haijagundulika lakini kuna dawa ya kutuliza ambapo mgonjwa atahitajika kumeza siku zote za maisha yake.
Miongoni kati ya dawa hizo ni Carbamizapine na Phenorbabiton ambapo utameza moja kwa moja kutokana na ushauri wa daktari.
****
Nilifahamu mwanangu Brighton asingeweza kupona tena, yaani maisha yake yote yangekuwa ni ya kuteseka na ulemavu wa miguu aliyokuwa nao pamoja na ugonjwa wa kifafa.
Nilimuhurumia sana Brighton, kila nilipokuwa nikimtazama niliona ninasababu milioni mia moja za kumsaidia, ni hapa ambapo nilianza kuhangaika usiku na mchana katika kuyapigania maisha yake.
Kwa kuwa nilikuwa ninapesa hakukuwa kuna ugumu uliyojitokeza mbele yangu. Tulianza kuhangika kwenda hospitali mbali mbali na mke wangu, hitaji kubwa la moyo wangu kwa wakati huo lilikuwa ni kuona mwanangu akipona.
Hilo lilikuwa ni jambo gumu mno kutokea, kila hospitali niliyompeleka majibu yalikuwa ni yaleyale kuwa mwanangu Brighton asingeweza kupona.
"Ni nini hiki kimetokea katika maisha yangu, Mungu uko wapi, mwanangu anateseka kiasi hiki," alisema Lillian huku huzuni ikiwa imemtawala, hakukuwa kuna wakati wa furaha tena, machozi ndiyo yalikuwa yametawala. Kuna kipindi tulipokuwa tukiteseka na Brighton hospitalini, mke wangu Lillian alianza kukata tamaa maana kila hospitali tuliyokuwa tukienda majibu yalikuwa ni yaleyale.
Japokuwa nilikuwa katika kipindi cha kuuguliwa na mwanangu Brighton lakini bado niliendelea kuishi maisha yaliyojaa dhambi. Nilikuwa nikimsaliti Lillian.
****
Katika kipindi hicho nakumbuka Coletha alikuwa tayari amemaliza chuo lakini hatukuwa na maelewano mazuri. Kwa kifupi nilikuwa nimegombana naye, hapa ni baada ya kugundua kuwa nilitembea na dada yake Caren pamoja na rafiki yake Getrude. Kitendo hicho kilizua ugomvi mkubwa sana. Japokuwa nilikuwa nimemnunulia gari pamoja na nyumba ya kifahari maeneo ya Mbezi ya kimara lakini sikuona kesi, niliamua kuachana naye, nikaendelea kutembea na Getrude japo hakukuwa na mawasiliano mazuri kati yake na Coletha.

Je, ni nini kitaendelea?
 
PENZI LENYE MAUMIVU-06
Juma Hiza
0712988278

Nilitumia pesa nyingi mno katika matibabu ya mwanangu Brighton, mwisho wa siku niliona kama nilikuwa nikitupa hela zangu katika shimo la choo kwani ugonjwa wa Brighton haukuwa na tiba.
Nilishakata tamaa kabisa moyoni mwangu.
Nilichokuwa nikikiona mbele yangu ni usaliti mkubwa kwa mke wangu, niliamini Brighton hakuwa ni mwanangu wa damu isipokuwa Lillian alinichezea mchezo mchafu nyuma ya pazia. Nikaanza kumshutumu mke wangu kutokana na usaliti huo ambapo kwake ilikuwa ni habari ngeni tena iliyomshtua mno.
"Nimekusaliti?" aliniuliza kwa mshangao mkubwa sana.
"Ndiyo haiwezekani huyu mtoto sio damu yangu utakuwa umenisaliti tu Lillian," nilimjibu huku nikionyesha msisitizo katika hilo.
Nilienda mbali zaidi nikaanza kumwambia Lillian kuwa katika ukoo wetu hakukuwa kuna mtu ambaye aliwahi kuugua ugonjwa wa kifafa, historia ya mababu zangu sikuwahi kusikia kama waliugua ugonjwa huu, sasa iweje mwanangu Brighton augue ugonjwa wa kifafa?
Kiukweli sikutaka kumuamini Lillian, hata machozi yake aliyokuwa akiyatoa mbele yangu na kuniambia kuwa Brighton ni mwanangu bado sikumuamini.
Wazo lililonijia kichwani mwangu lilikuwa ni la kwenda kupima DNA ili kuthibitisha kama kweli Brighton alikuwa ni mwanangu au la.
Hakukuwa kuna muda wa kupoteza, haraka nilifanya mipango ya kwenda hospitali kupima, majibu yaliyotoka huko yalionyesha kuwa Brighton ni mwanangu.
"No! Haiwezekani huyu mtoto sio wangu," nilisema wakati nikiyapokea majibu kwa mkemia.
"Majibu yanaonyesha kuwa huyu mtoto ni damu yako sasa unataka kubishana nayo?" Aliniuliza.
Kiukweli sikutaka kuyaamini majibu hayo, niliendelea kuyakataa mpaka ikabidi vipimo virudiwe kwa mara ya pili. Majibu yaliyotoka bado yalionyesha Brighton ni mwanangu.
Nikazidi kupagawa, nikamuangalia Lillian usoni, machozi yalikuwa yakimtoka mfululizo.
Japokuwa nilipewa majibu yaliyothibitisha kuwa Brighton ni mwanangu lakini sikutaka kukubaliana nayo. Niliamini vipimo vilidanganya.
"Sina mbegu za kuzaa mtoto kilema wala mwenye kifafa nakwambia utamtafuta baba wa huyu mtoto malaya wa kukubuhu wewe," nilimwambia Lillian maneno yaliyozidi kumuumiza mno, muda wote machozi yalikuwa yakimdondoka.
Nilipokuwa nikimuangalia Brighton kiukweli nilimfananisha na sokwe mtu, hakuwa na muonekano mzuri hata kidogo, hakufanana na mimi kabisa. Ulemavu wake na kifafa alichokuwa nacho kikanifanya nizidi kumchukia yeye pamoja na mama yake.
Sikuwa na mapenzi tena, chuki ilikuwa tayari imeshaniingia. Hakukuwa kuna mwanamke niliyemchukia katika maisha yangu kama mke wangu.
****
Yale yote yaliyokuwa yakiendelea katika maisha yangu Getrude hakuyafahamu. Alichoamini ni mimi nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na yeye.
Pamoja na kuishi maisha yaliyojaa dhambi lakini Getrude ndiyo msichana wangu ambaye alitokea kuniteka. Alikuwa na uzuri wa sura, umbo matata, mwendo wa maringo. Yaani alinichanganya mno kiasi kwamba nikaanza kumsahau Lillian.
Niliona ni bora nitoe pesa ATM nimnunulie nyumba Getrude aliyokuwa akiitaka pamoja na gari la kifahari lakini sio kuona nikitoa pesa zangu zitumike kumtibia Brighton ambaye alifanana na sokwe, kilema mwenye kifafa.
Kila alichokuwa akikihitaji Getrude nilimtimizia na hii ndiyo ilikuwa kama desturi yangu, kila msichana niliyetembea naye nilimtimizia kila kitu alichokuwa akikihitaji, nilikuwa miongoni kati ya wanaume ambao kazi yao ni kuwahonga hela wanawake wa nje na kusahau familia zao ambazo zilikuwa zikiteseka ilihali uwezo wa kuwasaidia ulikuwa mikononi mwetu.
Baada ya kupita kipindi cha mwaka mmoja nilikuwa tayari nimeshamnunulia nyumba Getrude pamoja na gari aina ya Murano. Sikuishia hapo tu pia nilimfungulia duka kubwa la nguo maeneo ya kinondoni.
Getrude hakutaka kuamini kile nilichokuwa nimekifanya katika maisha yake, alinishukuru mno. Hilo sikupendezewa nalo, nilimwambia asijali lolote kwani kuna mengi mazuri nilipanga kumfanyia katika maisha yake ukiachana na tukio la kumnunulia nyumba, gari pamoja na kumfungulia duka la nguo.
****
Katika kipindi chote hicho Lillian alianza kuhangaika kumpeleka Brighton kanisani ili aweze kuombewa na kupona, alikuwa akihudhuria makongamano mbalimbali lakini kila alipokuwa akienda kwa ajili ya maombi hakukuwa kuna mabadiliko yoyote yaliyoweza kutokea.
"Huu msukule wako siwezi kuulea hapa nilipofikia nimechoka," nilimwambia Lillian.
"Kelvin," aliniita Lillian.
"Serious nimechoka kupoteza pesa zangu yaani nakuwa kama natupa hela kwenye shimo la choo, hospitali zote tumehangaika, kwenye maombi napo lakini hakuna kilichobadilika huyu mtoto wako ataniletea gundu tu," nilimwambia.
"Kumbuka Kelvin hii ni damu yako lakini?"
"Sina damu ya walemavu na wenye kifafa."
"Kelvin unasemaje?"
"Huu msukule wako tafuta pa kuupeleka lakini hapa nyumbani kwangu sitaki kuuona."
Maneno yangu yalizidi kuwa mwiba kwa Lillian uliyomuumiza mno. Alihangaika, aliteseka sana, alifanya kila lililokuwa ndani ya uwezo wake kupigania maisha ya Brighton lakini hilo sikuliona. Ndani ya miaka miwili nilikuwa ni mtu wa kumuumiza na kumliza mke wangu.
****
Nilichomwambia Getrude ni kuwa nilitaka kuzaa naye katika kipindi hicho kwani ndilo ambalo lilikuwa hitaji langu kubwa. Kutokana na uzuri aliyokuwa nao kushinda mke wangu niliamini angeweza kunizalia malaika au mapacha.
Baada ya kupita miezi miwili hatimaye Getrude alipata ujauzito, nilifurahi sana, tofauti na mke wangu nikazidi kuongeza mapenzi kwake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom