Penzi la Chuo Kikuu

Ryan The King

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,788
2,690
Wikiendi Hiyoooooooo!!!!!!

Baada ya kuishia hewani katika simulizi la "PENZI LA UTENAGE" sasa nimekuja na bonge la kichupa kingine.

Tahadhari: Soma ukiwa katika mazingira tulivu na uwe peke yako.

JIACHIE.......

" Nakupenda Michaelray, naomba unitunzie penzi langu. Huko chuo uendako tambua yupo mwanamke anayekupenda"
Neema alishusha pumzi na kunikumbatia baada ya kuniambia maneno hayo aliyoyatamka kwa hisia Kali sana. Uso wake ukiwa umejawa na huzuni huku mifereji midogo midogo ya machozi yakitiririka katika mashavu yake laini ya mviringo. Nilimuonea huruma sana. Nikitamani nibaki sema sikuwana jinsi zaidi ya kwenda chuo.

"Usijali Neema, nipo kwaajili yako. Maisha bila wewe ni sawa na dunia bila jua"
Niliongea Neema akiwa amenikumbatia bado. Nikisikia mapigo yake yakipiga akiwa yupo kifuani mwangu. Nilihisi mapigo yale yananiambia "wewe ndiwe shujaa wangu".

Tulikuwa bado tupo kituo cha mabasi. Neema alikuwa amenisindikiza. Wapiga debe, na baadhi ya Abiria walikuwa wakituangalia na hii ni kutokana na Neema kulia kwa kwikwi kila Mara.

Basi lilifika, nilimkumbatia tena Neema lakini wakati huu Kilio cha Neema kilikuwa dhahiri. Watu waliokuwa ndani ya gari kila nyuso zao zilionekana madirishani zikinichungulia Mimi na Neema.
"Nakupenda Michaelray"
Neema aliongea kwa tabu kutokana na Kwikwi iliyokuwa ikimtingisha.

Nilimuachia na kuanza kupanda ndani ya Basi. Nikiwa ndani ya Basi niligeuka nyuma kumwangalia Neema ambaye alikuwa ameweka mikono yote miwili kichwani huku machozi yakizidi kumtoka. Nilimuonea huruma sana.

Niliketi kwenye kiti cha Basi. Wakati basi linataka kuondoka Mara pakawa na kelele mlangoni. Nikaangalia. Alikuwa ni Neema aliyekuwa analazimisha aingie ndani wakati gari ipo kwenye mwendo wa polepole. Neema aliingia mpaka nikipokuwa nimekaa huku watu wakiwa wanamshanga. Kwa jinsi abiria walivyotoa macho ungeweza kusema wapo katika ukumbi wa sinema.

Neema alinikumbatia na kunipiga busu kisha akatoa bahasha na kunikabidhi.
Basi lilipiga honi na kondakta akaja kumtoa Neema. Safari ikaanza.

**********************

Basi lilienda kwa mwendo wa kawaida ukimya ukiwa umetawala. Abiria wengi walikuwa wakibinya binya simu zao huku wachache wakiwa kama wamelala.
Pembeni yangu alikuwa amekaa mrembo mmoja ambaye alikuwa ameweka Earphone masikioni huku akichati. Sikuongea naye tangu nilipoingia.

Kimya kilifukuzwa na Sauti ya Tv iliyomo ndani ya basi. Kondakta aliweka movies moja Kali ya Hollywood iitwayo "Attack from Mars". Hivyo macho mengi ya abiria yaliekezwa kunako TV.

Nilifungua ile bahasha na kukuta karatasi ya pinki. Niliifungua na kuanza kusoma;

" Michael Mpenzi!
Penzi lako ni zaidi ya maisha yangu. Wewe ni bawaba katika miimo ya moyo Wang. Nikupendavyo sina irabu za kuelezea. Wewe unajua Mme Wang.
Nakuombea kwa Mungu akulinde mme Wang.
Mwaaaa!!!!

Wako katika mahaba.
Neema Tarimo."

Ilikuwa barua iliyofanya kifua changu kijae pumzi nikaishusha taratibu kama mtu aliyechoka.

Ni kweli ninampenda Neema hilo nililijua. Si moyo tuu mpaka macho yalijua ninampenda Neema. Taswira ya Neema ilipita katika ubongo wangu. Mwili ulinisisimka mno. Moyo ulisinyaa.
Nilipitiwa na usingizi nikiwa namuwaza kipendi changu Neema.

" kelele zilisikika, moyo ulipasuka, nafsi ilikimbia kimbia. Utulivu ulikosekana. Sikuelewa nini kinaenda kutokea.
"Wami! Wami kweli unatuua!"
Nilimsikia mama mmoja akiongea huku abiria wengine wakipiga kelele.
Nilikumbuka hadithi za daraja la mto wami. Ilikuwa Mara yangu ya kwanza kusafiri kwenda Dar es salaam. Hivyo sikujua Daraja la wami likoje.
"Tunakufa!"
Kelele zilisikika. Muda wote gari lilikuwa likirudi nyuma baada ya kushindwa kupanda mlima. Mara Tukasikia kishindo cha Basi kama limegonga ukingo wa daraja na hapo hapo likadondoka kuelekea mtoni. Mabegi yalitudondokea yaliyokuwa juu sehemu ya kuwekea mabegi. Nilijua ndio mwisho wa maisha yangu.
"Pwaaaaaaaaa"
Kishindo cha Basi mtoni kilisikika. Maji yakaruka huku na huku kuachia nafasi Basi iliingie mtoni.
"Tunaliwa na mamba maamaa!""
Mama mmoja aliongea na kabla hajamaliza kioo cha dirisha kilichomoka na kumpasua kichwani. Maji yaliingia ndani ya Basi.
Nilihisi kama nipo kwenye sinema ya kutisha. Sikuwa na uhakika kuwa ni kweli au laa.
Nilimkumbuka Neema. Nililia sana lakini hakuna aliyeweza kumbembeleA mwenzake kwani kila mtu alikuwa anasubiri kifo.
Damu ya waliojeruhiwa ilizidi kuchangamana na maji. Maji yalizidi kujaa kwa kadiri muda ulivyokuwa unaenda.
Pumzi ilikuwa ndogo, maji yalikuwa ndiye hakimu aliyebakia kuhalalisha kifo chetu mule ndani. Masikini muda wetu uliisha na maji yajaa kabisa ndani pasiwe na sehemu ya kupumulia.

Picha ya maisha yangu ilipita kwa haraka haraka kama filamu ipelekwayo mbele.
Taswira ya Neema ilikuja mbele yangu ikiniambia;
"Usiende bado nakupenda. Usiende Michaelray"
Pumzi ilikata na Mara kukawa Giza kuu. Nikiwa sipo duniani wala akhera sipatikani likaja jitu la kutisha na kupanua midomo yake yenye harufu kali na meno yaliyochongoa.
Nilipiga makelele.
Mara nikazinduka kumbe nilikuwa naota."

"Wewe! Unashida gani?"
Mrembo aliyeketi na mimi aliniuliza akiwa anaogopa.
Bado sikuamini kama ilikuwa ndoto. Mawenge bado yaliniganda.
"Nimepiga kelele"
Nilimuuliza yule mrembo.
"Ndio"

Akiwa anajibu Mara sauti ya tairi la gari likalia kuashiria limepasuka. Gari ikaanza kuyumba hofu ndio ikatawala.

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom