Penzi la Chuo Kikuu

Penzi la Chuo Kikuu

Penzi la Chuo Kikuu 02

Mtunzi: Michaelray22.

Mambo yalikuwa tafrani. Hofu na mashaka viliota katika mioyo ya abiria. Nyuso za Abiria zilishaonyesha alama ya kuzimu. Mara nikasikimshindo mkubwa na fahamu zikanipotea.

*******************

Habari iliyokuwa ikitangazwa karibu kila chombo cha habari ilikuwa habari ya kupinduka kwa Basi. Magazeti yote katika kurasa za mbele yalipambwa na vichwa mbalimbali kuhusu Habari ya ajali ya Basi.
" BASI LAUA WATU 30"
Yalikuwa maneno ya gazeti moja yaliyoandikwa kwa herufi kubwa huku likionesha picha ya Basi lililopinduka likiwa nyang'anyang'a.

Kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na what's app habari za kuanguka kwa basi zilipamba moto. Kila kona mwa nchi taarifa zilienea. Ilikuwa habari mbaya sana kwa ndugu wa waliopata ajali.

Fahamu zilirejea nikajikuta nipo katika chumba chenye mashuka meupe. Moja kwa moja nilijua pale ni hospitali japo sikujua ni hospitali gani. Nilijaribu kujigeuza lakini nikashindwa ndipo nilipogundua nina jeraha kubwa mgongoni ambapo maumivu nilianza kuyasikia baada ya kutonesha kidonda nilipokuwa nikijaribu kujigeuza.

Usoni nilikuwa nimefungwa plasta na mkono wa kulia nimefungwa ndripu la maji wakati mkono wa kushoto ukiwa umetundikiwa dripu la damu.

Nilianza kukumbuka tukio zima la ajali hadi nilipopoteza fahamu. Sikujua nimefikaje fikaje pale hospitali.
Nikiwa katika kukumbuka punde nikasikia kifaa kimoja kama computer kilichopo kwenye meza kikilia huku kikionyesha Grafu zilizokuwa zikipanda na kushuka taratibu.

Mara mlango ukafungulia akatokea mdada mmoja aliyevaa koti jeupe bila shaka alikuwa daktari.
Aliingia na kunitazama bila kunisemesha kisha kwa haraka akaenda kukiminya kile kifaa kilichokuwa kinalia. Bila shaka kilisetiwa kuwa nikiamka kitoa sauti.

"Unaendeleaje mkaka mzuri"
Yule dada aliongea kwa sauti iliyotulia yenye ukarimu mwingi. Aliongea akiwa ametabasamu akinisogelea na kukaa pembeni ya kitanda. Sikumjibu kitu.
"Naitwa Dakta Devotha, nipo nawe hii wiki ya tatu"
Aliongea Dakta Devota huku akiniangalia kwa upendo.
"Wiki ya tatu!?"
Niliukiza kwa kushtuka.
"Ndio. Hii ni wiki ya tatu sasa"
Kimya kidogo.
"Sasa umepona, tulikuwa na wasi wasi kuwa huenda hutaamka. Tumekufanyia operesheni ndogo ya mgongo"
Aliendelea kuongea.

Nilikaa hospitali wiki nyngne moja Dakta Devotha akiwa ananiangalia na kunihudumia kwa kila kitu.
Sasa nilikuwa nimepata nafuu. Niliweza hata kutembea mita kumi na kurudi. Dakta Devotha ndiye aliyelipia gharama za matibabu.
Kutokana na hali yangu kuzidi kutenngemaa Dakta Devotha alinichukua nyumbani kwake kwa ajili ya kunihudumia vizuri.

Nyumba ya Dakta Devotha ni kubwa kiasi nje ikiwa na Bwawa dogo la kuogelea. Maisha mapya yalianza nikiwa kwa Devotha. Nilimueleza Dakta Devotha kuhusu kwenda chuo akanambia ataenda kufuatilia na kutoa taarifa.

Wiki mbili zilipita nikiwa nipo kwa Dakta Devotha. Mara kwa Mara alikuwa akija kunitazama japokuwa kulikuwa na mfanyakazi wa ndani. Niliona anavyojua kujali na kukarimu.
Nikiwa nimepona kabisa nilikumbuka nyumbani. Kilichonishinda ni kuwa sikuwa na kumbukumbu za namba za mama. Kwa bahati nilikumbuka habari za Facebook ambapo mama yangu anaakaunti. Niliandika jina lake na kukuta taarifa za kushtusha na kusikitisha.
Niliona picha ya jeneza langu na kaburi langu ambalo Mama alikuwa amezituma FB.
Mapigo ya moyo yalinikimbia huku nafsi yangu ikiyakimbiza.

Niliangalia Comments na kukuta R.I.P nyingi sana. Nilihisi joti mwilini.
"Inamaana nimekufa"
Niliongea kwa sauti ndogo nikiwa nimeacha kuangalia picha.

Niliona picha ya Msalaba ulioandikwa kwa herufu kubwa
MICHAELRAY22
ALIZALIWA. 25/03/199
AMEFARIKI. 20/09/ 2014

Sasa nilihisi kichwa kinajaa.

Nikiwa katika kuchanganyikiwa Mara Dakta Devotha akaingia akiwa amebeba Mfuko wenye vitu vitu. Alikuja na kunihagi lakin sikuonyesha kujali sana.

Alitambua ninashida
"Michaelray kuna nini?"
Aliniuliza ila sikumjibua.
"Michael nini shida?"
Aliuliza tena akiniangalia kwa udadisi. Mara macho yake yakaangalia kunaposimu yangu aliyonipa na kuona picha ya msalaba. Aliichukua simu na kuanza kuperuzi.
Aliliona jeneza ambalo kwa mbele limewekwa picha yangu.

"Haiwezekani Michael"
Dakta aliongea akiwa na yeye sasa anaanza kuchanganyikiwa.

"Michael ni kweli au?"
"Ni kweli hiyo ni Akaunti ya Mama yangu"
Nilimjibu.
"Ngoja tumpigie"
Aliongea na kuchukua namba za Mama kwenye Facebook.
Simu iliita na Mara sauti ya mwanamke upande wa pili ilisikika ambayo ni liitambua yakuwa ni mama.

"Hallo!"
"Hallow shikamoo mama!"
Niliitikia na kumsalimia nikionyesha kufurahi.
" Marhaba! Nani?"
Mama aliongea huku akisikiliza kwa umakini
"Mimi Dapshan Mama"
Nilitaja jina alilozoea kuniita Mama yangu.
"Dapshan...."

Itaendela...
 
Taaaaamuuuu itabidi nikutafute unihadithie tukiwa wawili... Tunanunua miwa yetu ya bukuuu aka stor mwanzo mwishoo
 
Back
Top Bottom