Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,869
- Thread starter
- #161
SEHEMU YA 68...
Hakutaka kuendelea kubaki chumbani mule, aliyaona majaribu yaliyokuwa yakiendelea, alichokifanya ni kuondoka zake huku akimuacha binti huyo akiwa kwenye muhemko mkubwa wa kufanya naye mapenzi.
Huo ukawa mwisho wa Dk.Buffet kuingia ndani ya chumba hicho usiku huo , hata Tatiana alipowaambia manesikwamba alitaka kumuona daktari huyo, alikataa kuonana naye kwa kujipa ubize na kwamba kama kumuona angemuona asubuhi.
Asubuhi ilipofika, Smith alikuwa hospitalini hapo, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumjulia hali mpenzi wake ambaye bado hakuonekana kuwa na furaha kabisa kwani mapenzi yake hayakuwa kwa mwanaume huyo hata kidogo, alianza kumpenda Dk. Buffet ambaye aliuteka moyo wake kwa kiwango kikubwa mno.
Smith alijaribu kujikesha kwa kumfanya mpenzi wake awe na furaha lakini hilo halikusaidia. Hakuingia hospitalini hapo mikono mitupu, alikuja na zawadi mbalimbali lakini bado Tatiana hakuonekana kuwa na furaha kabisa.
Baadae wakapokea maelekezo kwamba kila kitu kilikuwa tayari na Tatiana aliruhusiwa kuondoka hospitalini hapo. Hiyo haikuwa kawaida, mara zote mgonjwa anapotoka, mtu anayempa ruhusa kwa njia ya mdomo ni daktari mwenyewe ila siku hiyo, mtu aliyekuwa akiwapa taarifa alikuwa nesi ambaye aliagizwa na Dk. Buffet ambaye hakutaka kumuona kabisa Tatiana.
“Sawa, utamwambia kwamba ninashukuru sana,” alisema Simth.
“Hakuna tatizo, akija nitamwambia,” alisema nesi aliyetoa taarifa.
Walipoanza kutoka nje ya jengo la hospitali hiyo, tayari waandishi wa habari walikuwa wamekwishajikusanya na kuanza kuwapiga picha mfululizo. Jina la Tatiana lilikuwa kubwa na hatimaye hata Smith akaanza kujulikana sehemu mbalimbali duniani kupitia msichana huyo mrembo
Waandishi wengine walikuwa na vidaftari vidogo mikononi mwao, walitaka kumsikia Tatiana akizungumza kitu chochote kile kutokana na ule muujiza uliokuwa umetokea katika maisha yake. Hakuzungumza kitu, kwa kumwangalia tu alionekanakuwa na kitu kilichokuwa kikimtatiza moyoni mwake.