Penzi bila maumivu

Penzi bila maumivu

SEHEMU YA 56...
Furaha ilikuwa kubwa katika Kijiji cha Chibe, watu hawakuamini kile walichokuwa wamekisikia kwamba msichana aliyeondoka kuelekea nchini Marekani kutokea katika kijiji hicho, Tatiana alikuwa amechukua ushindi kwa kuwa muimbaji bora katika shindano lile lililokuwa likiendelea nchini huko kwa miezi sita.

Wazazi wake, mzee Sangiwa na mkewe walizidiwa na furaha, kila walipokuwa wakifurahia, walionekana kama vichaa fulani. Hawakufikiria zaidi kuhusu fedha, kitu pekee walichokuwa wakikifurahia kwa wakati huo ni heshima tu kwa kujua kwamba nchi yao na kijiji chao, vyote hivyo vingetangazika mno.
Baada ya wiki moja ya furaha yao, Wazungu wanne wakafika kijijini hapo na kuwaambia kwamba mzee Sangiwa na mkewe walitakiwa kuondoka nao kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kumpongeza mtoto wao kwa kile kilichokuwa kimetokea.
Furaha zao zikaongezeka maradufu, taarifa ile walioletewa na Wazungu wale ikawapa furaha ya ajabu kiasi kwamba wakaenda kanisani kesho yake na kutoa sadaka ya shukrani.

“Kwa hiyo ndiyo tunakwenda kwa Wazungu, hukoooooo, kule alipotoka Michael Jackson,” alisema mzee Sangiwa huku akionekana kuwa na furaha tele.
Mipango ilishasukwa, baada ya wiki mbili, wazazi hao wakachukuliwa na safari ya kuelekea nchini Marekani kuanza mara moja. Njiani, ndani ya ndege hawakuamini, kuna wakati mwingine walihisi kwamba walikuwa ndotoni na muda wowote ule wangeamka na kujikuta wakiwa chumbani wamelala.

Safari hiyo ilikuwa ni kwenda Marekani kwa kuelekea Accra nchini Ghana ambapo huko walitakiwa kuwapitia wazazi wa Febby na kisha kuunganisha mpaka nchini Marekani kwani ni washirika wawili tu kutoka Afrika ndiyo waliokuwa wameingia kwenye tano bora.

“Ndiyo Ulaya hiyo tunakwenda, kumbe ndani ya ndege kuzuri sana,” alisema mzee Sangiwa huku meno yote thelathini na mbili yakiwa nje. Ndege iliendelea kukata mawingu tu.
 
SEHEMU YA 57...
Tatiana hakuamini kama waliosimama mbele yake walikuwa wazazi wake, japokuwa alikuwa kipofu lakini hisia zilimfanya kugundua kwamba watu waliokuwa wamesimama umbali mdogo kutoka alipokuwa walikuwa wazazi wake.
Uso wake ukajawa na tabasamu pana na kuanza kusogea kule mbele kwa lengo la kuwafuata huku akiwa na fimbo yake mkononi. Alipoona kwamba amewafikia, akaiachia fimbo na kuitanua mikono yake kama mtu aliyesubiri kuwakumbatia watu fulani, wakamsogelea na kumkumbatia kwa furaha.

Hawakuami kama binti yao mrembo alikuwa amefanikiwa kuchukua ushindi ule uliokuwa ukitamaniwa na kila mtu, huo, kwao ukaonekana kuwa muujiza mkubwa na walimshukuru sana Mungu kwa kila kilichotokea.
“Alichokifanya Tatiana ni kuwatambulisha wazazi wake kwa Smith, mbaya zaidi aliwatambulisha kama mpenzi wake ambaye alikuwa na mipango ya muda mrefu ya kufunga naye ndoa.
“Unasemaje?”

“Huyu ndiye atakayenioa mama, ninampenda na ananipenda,” alijibu Tatiana.
Wazazi walibaki na mshangao lakini hawakutaka kuzungumza kitu, walichokifanya ni kusubiri mpaka sherehe hiyo ifanyike na kumalizika. Hapo, hata ile furaha waliyokuwa wamekuja nayo ikapotea, mioyo yao ilimfikiria Peter tu ambaye alijitoa sana kwa ajili ya binti yao na alikuwa akimpenda Tatiana kwa penzi la dhati.

Siku ya sherehe ilipofika, kamakawaida ikatangazwa sana. Tatiana hakuwa yule wa kipindi cha nyuma, huyu wa sasa hivi alikuwa tajiri mkubwa, aliheshimika na kutangazwa sana kila kona. Umaarufu mkubwa duniani ulikuwa ukimnyemelea, alitafutwa sana na waandishi wa habari ambao walitamani kusikia mengi sana kutoka kwake.

Sherehe ilipokwisha, wazazi hao walitaka kuzungumza na binti yao, maneno aliyowaambia kwamba alikuwa amempata mwanaume mwingine ambaye alijitolea kumuoa, yaliwashtua kwani kitu walichokuwa wakikifahamu ni kwamba Peter bado alikuwa kwenye mapenzi ya dhati kwa binti yao.
“Hivi ulisemaje vile?” aliuliza mama yake.
“Nimempata mwanaume ambaye nahisi nina mapenzi naye ya dhati,” alijibu Tatiana.

“Hivi unajua unachokisema?”
“Ndiyo mama.”
“Na vipi kuhusu Peter?”
 
SEHEMEU YA 58...
“Mama! Kile kilikuwa kipindi cha nyuma, nilikuwa mtoto hivyo wakati mwingine sikuwa na maamuzi , sasa nimekua mama,” alisema Tatiana.
“Yaani miezi sita tu unasema ulikuwa mtoto, kweli?”

“Ndiyo mama. Ninampenda Smith,” alisema Tatiana kwa ujasiri mkubwa.
Mioyo yao ilichomwa na kitu kikali zaidi ya sindano, hawakuamini kile walichokisikia kutoka kwa binti yao. Mioyo yao ilikuwa kwa Peter tu, hawakutaka kusikia habari za mwanaume yeyote yule, kitu walichokitaka ni kuona binti yao akiwa na Peter tu.
“Hapana! Wala sikubaliani na wewe Tatiana.”

“Baba! Mkubaliane na mimi, msikubaliane nami, hilo wala sijali, ninachokisema ni kwamba ninampenda Smith,” alisema Tatiana huku akionekana kumaanisha alichokuwa akikisema.
Hawakuwa na jinsi, binti yao alikuwa ameamua kitu kilichokuwa kigumu kukubalika mioyoni mwao, hawakutaka kumuingilia sana zaidi ya kumsisitizia kwamba wao kama wazazi walitamani kumuona akiwa na Peter kwani ndiye mwanaume aliyeonyesha kuwa na mapenzi naye ya dhati na si kama ilivyokuwa kwa Smith.

Siku zikaendelea kukatika, baada ya wiki moja sherehe kumalizika, wazazi hao wakarudi zao nchini Tanzania huku wakimuacha Tatiana akijiandaa kwenda Colorado kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa macho kwa daktari mkubwa aliyekuwa akisifika nchini Marekani.
Hakuwa na shida ya hela, Tatiana alikuwa tajiri mkubwa tu na kwa matibabu yale uliotarajiwa kufanyiwa, asingetumia fedha zake, gharama zote zilikuwa kwa Smith tu.

Siku mbili baadae walikuwa ndani ya ndege binafsi ya Smith na safari ya kuelekea Colorado kuanza. Ndani ya ndege Tatiana alionekana kuwa na furaha tele, hakuamini kama ndani ya siku chache zijazo angeweza kuona kama walivyokuwa watu wengine.

Kila alipokuwa akiisikia sauti ya Smith, alimpenda mno, alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kumuona uso kwa uso ili awe huru zaidi wa kufanya mambo mengi na ikiwezekana hata kuoana.
 
SEHEMU YA 59...
Saa nane mchana walikuwa wakiingia katika Jimbo la Colorado, ndege yao ikaanza kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Denver na kisha kuingia ndani ya gari maalumu lililoandaliwa kwa ajili yao na safari ya kuelekea hotelini kuanza.

Kitendo cha kufika Denver tu tayari kikampa uhakika Tatiana kwamba ndani ya siku chache zijazo angeweza kuona kitu ambacho kingemfanya kuwa na furaha kuliko siku nyingine katika maisha yake.

Katika kipindi chote cha safari yao kuelekea hotelini, Smith alikuwa akitumia muda mwingi kumsifia Dk. Buffet tu kwamba alikuwa daktari mtaalamu wa magonjwa ya macho kitu kilichompa uhakika Tatiana wa kuweza kuona tena.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika Hoteli ya Everest ambapo wakateremka na kuchukua chumba hapo. Usiku mzima walilala huku wakiwa wamekumbatiana tu, walifanya vitu vyote ambavyo wapenzi wangeweza kufanya wawapo faragha.

Kwa Tatiana, hakumkumbuka kabisa Peter, alimsahau mwanaume huyo na hakutaka kukumbuka kama katika maisha yake aliwahi kukutana na mwanaume mwenye jina kama hilo. Smith alimteka, alimpenda na kumuona mwanaume wa kweli ambaye aliletwa duniani kwa ajili yake tu.

“Kesho ndiyo tunakwenda kumuona daktari, upo tayari?” aliuliza Smith huku wakiwa wamekumbatiana tu kitandani.
“Nipo tayari mpenzi.”
“Basi sawa. Nitafurahi kama ukiona jinsi dunia inavyokwenda. Nakupenda sana mpenzi,” alisema Smith huku akiachia tabasamu pana.
“Nakupenda pia.”

Asuhbuhi ilipofika, wawili hao wakaamka na kisha kujiandaa kwenda katika Hospitali ya Mount Sinai Medical Center iliyokuwa katikati ya Jiji la Denver ambapo huko wangekutana na daktari huyo wa magonjwa ya macho na kuanza kumtibu Tatiana ugonjwa huo ili aweze kupona.

Wakachukua gari na kuanza kuelekea huko ambapo baada ya dakika ishirini, walikuwa wamekwishaingia ndani ya jengo la hospitali hiyo nakuelekea ilipokuwa ofisi ya daktari huyo.
“Karibuni sana,” aliwakaribisha Dk. Buffet.
“Asante sana. Ndiyo tumekuja,” alisema Smith huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.
 
SEHEMU YA 60...
Walikuwa wamekwishazungumza simuni juu ya kitu gani kilichotakiwa kufanywa mahali hapo hivyo hawakuwa na sababu ya kujielezea sana. Alichokifanya Dk. Buffet ni kumchukua Tatiana na kuelekea naye katika chumba cha uchunguzi kilichokuwa na mashine nyingi kwa ajili ya kuwapima wagonjwa uwezo wao wa kuona na hata wale waliokuwa vipofu kabisa.

“Mkalishe hapo,” alisema Dk. Buffet na kisha Smith kumkalisha Tatiana katika kiti kilichokuwa pembeni kabisa ya chumba kile.
Alichokifanya Dk. Buffet ni kutayarisha vifaa vyake kwa ajili ya kuanza kazi. Hatua ya kwanza kabia aliyoifanya ni kuyaangalia macho ya Tatiana huku akiyamulika kwa tochi. Hayakuonekana kuwa na tatizo lolote lile zaidi kitu kilichomfanya kugundua kwamba inawezekana tatizo kubwa likawa kwenye mishipa inayoyafanya macho hayo yawe na nguvu ya kuona.

“Ana tatizo kubwa la mishipa, kuna uwezekano ikawa imelegea, ni tatizo kubwa lakini pia linatibika endapo nitapewa muda zaidi wa kufanya hivyo,” alisema Dk. Buffet.
“Hakuna tatizo, ninachotaka ni kumuona akiona tu, hakuna jingine.”
“Basi hakuna tatizo. Kazi ni kubwa na itachukua mwezi mzima.”
“Hata kama mwaka, ninachohitaji ni kumuona akiona tena.”
“Basi sawa.”

“Kwa hiyo kazi inaanza lini?”
“Leoleo, tena sasa hivi.”
“Nashukuru sana,” alisema Smith, akamwangalia Tatiana usoni kisha kumbusu shavuni.
“Nakupenda mpenzi,” alimwambia.
“Nakupenda pia.”
“Unakwenda kuona, ninamwamini sana daktari huyu, hautakiwi kuhofia chochote kile,” alisema Smith.

“Asante mpenzi, hata mimi naamini hilo.”
Alizungumza naye kwa mara ya mwisho kabla ya kazi ile kuanza rasmi. Dk. Buffet aliwapa nusu saa kuzungumza na kisha kumuomba Smith atoke chumbani na yeye kubaki na mgonjwa ambapo mara moja kazi ikaanza.
*
*
 
SEHEMU YA 61...
Peter hakuwa na furaha tena, akili yake ilichanganyikiwa na hata aliporudi shuleni hakuwa akisoma kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma. Kichwa chake kilimfikiria zaidi Tatiana ambaye aliamua kulitupa pezi lake na kumchukua mwanaume mwingine.

Kila alipokuwa akilikumbuka tukio lile lililofanyika ukumbini, moyo wake ulimuuma mno na kujikuta akimchukia msichana huyo. Muda mwingi Peter alikuwa na mawazo tele, wakati mwingine kila alipokuwa akikaa peke yake, alikuwa akibubujikwa na machozi tu, moyo wake ulijaza maumivu makali yasiyokuwa na mfano.

Hali ya kuwa na mawazo mengi yakamfanya kutokusoma kabisa, muda mwingi alikuwa akimfikiria msichana huyo ambaye aliweka doa kubwa moyoni mwake.
Siku zikaendelea kukatika zaidi, hakusoma tena kwani kila alipokuwa akishika daftari kwa ajili ya kusoma, hakuwa akielewa chochote kile zaidi ya kutumia muda mwingi akimfikiria Tatiana.

“Peter...” aliita rafiki yake.
“Naaam!”
“Una nini rafiki yangu?”
“Kwani kuna nini?”
“Unaonekana kuwa na mawazo sana, halafu hata kusoma husomi, kila siku unalala tu bwenini, tatizo nini?” aliuliza rafiki yake huyo.

“Hakuna kitu, muda mwingi najisikia uchovu tu.”
“Hapana! Nahisi kuna kitu. Hebu niambie rafiki yangu naweza kukusaidia,” alisema rafiki huyo.
“Usijali. Hakuna kitu.”

Hakutaka kumshirikishamtu yeyote juu ya kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake. Kila siku maumivu yale aliyachukulia kama yake na hakutakiwa kumshirikisha mtu yeyote yule. Siku ziliendelea kukatika, mpaka muda wa kufanya mitihani ya mwisho ulipofika, wakafanya na Peter kuelekea Shinyanga kabla ya Mwanza, alitaka kuonana na wazazi wa msichana huyo tu.

Kama kawaida safari ilikuwa ndefu lakini baada ya masaa kadhaa akafika katika Kijiji cha Chibe na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwa mzee Sangiwa. Kijiji kilikuwa kimebadilika, hakikuwa kijiji kilichokuwa na nyumba nyingi za nyasi, kulianza ujenzi wa kujenga nyumba kubwa za matofali ambazo zilitolewa kwa ajili ya wanakijiji tu.
 
SEHEMU YA 62...
Mbali na hiyo, kulikuwa na bomba kubwa lililopitishwa chini, shida ya kuchota maji haikuwepo tena. Hakukuwa na haja ya kwenda kuchota maji kisimani, wanakijiji waliwekewa mabomba ya maji huku umeme ukiwa umeletwa kwa wingi kijijini hapo. Kwa kifupi, Tatiana alikuwa akikibadilisha kijiji hicho.

Kitendo cha kumuona mvulana huyo akiingia ndani ya nyumba yao, mioyo yao ikawa kwenye maumivu makali, walijua ni kwa jinsi gani alikuwa na maumivu moyoni kutokana na kile kilichokuwa kikiendelea.
“Mama! Kweli Tatiana hatorudi?” aliuliza Peter huku akilengwa na machozi.
“Hatujajua. Ngoja tusubiri, tutajua hivi karibuni. Amekuwa akituma fedha kwa ajili ya maendeleo ya kijiji na familia, kuhusu kurudi, bado hatujajua,” alijibu bi Frida.

Peter akajikuta akianza kububujikwa na machozi yaliyokuwa yamemlenga kwa kipindi kirefu, bado hakuwa akiamini kama huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kila kitu. Mapenzi yalipotoea, msichana aliyekuwa akimpenda sana alikuwa ameruka.

Siku iliyofuata akaamua kurudi jijini Mwanza huku moyoni akiwa na maumivu makali ya moyo. Alipofika Mwanza Mjini, magazeti mengi yalikuwa na habari ya Tatiana. Alikuwa msichana maarufu aliyeiwakilisha Tanzania kuliko mtu yeyote yule.

Aliifanya Tanzania kuzungumzwa na watu wengi waliokuwa barani Ulaya na nchini Marekani, katika nchi zote zilizokuwa na maendeleo, mtu aliyekuwa akizungumzwa kwa kipindi hicho alikuwa Tatiana tu.
Kipindi cha nyuma alikuwa na upofu, ila kwa kipindi hiki, hakuwa kipofu tena, alikuwa mzima na aliona vizuri kabisa.
“Tatiana, sitokuacha kukupenda, najua kuna siku utarudi tu,” alijisemea Peter huku akionekana kuumia moyoni mwake.
*****

Uwezo wa Dk. Buffet ulikuwa mkubwa mno, alipoliangalia tatizo la Tatiana, alijua kwamba kulikuwa na mishipa kadhaa ambayo ilikuwa imelegea hivyo kuanza kazi ya kuirudisha katika hali yake ya kawaida.
Ilikuwa kazi kubwa lakini hakutaka kulala kwa kipindi kirefu kama zamani, kitu pekee alichokuwa akishughulika nacho kwa kipindi hicho ni mgonjwa huyo aliyekuwa ameletwa hospitalini kwake.
 
SEHEMU YA 63...
Magazeti na vyombo vingine vya habari viliendelea kuripoti kila hatua aliyokuwa akipitia Tatiana, kila mtu alitamani kuona msichana huyo akipata nguvu ya kuona ili ajue ni kwa jinsi gani ulimwengu ulikuwa ukiendelea.

Baada ya matibabu kufanyika kwa mwezi mzima, hatimaye Tatiana akaanza kuona vivulivivuli. Mtu alipokuwa akipita mbele yake, hakuwa akimuona vizuri kitu kilichomfanya kuhisi kwamba alikuwa akienda kupona.

“Vipi?” aliuliza Dk. Buffet.
“Naona vivulivivuli,” alijibu.
“Haya ni maendeleo makubwa sana, amini kwamba utakwenda kupona kabisa,” alisema Dk. Buffet.
Maendeleo yake yalimfurahisha kila mmoja, baada ya wiki mbili kukatika, Tatiana akafanikiwa kuona kabisa, upofu aliokuwa nao tangu alipozaliwa, ukakoma na mishipa yake kukaza na kuwa kama mtu ambaye hakuwahi kuumwa macho maishani mwake.

“Dokta! Naona,” alisema Tatiana huku akionekana kutokuamini.
“Unasemaje?”
“Naona dokta! Naona,” alisema Tatiana.
“Hebu subiri, hivi vidole vingapi?” aliuliza Dr. Buffet.
“Vinne.”
“Na hivi?”

“Viwili, naona dokta,” alisema Tatiana huku akipiga kelele kwa furaha.
Hiyo ilikuwa taarifa njema kwa kila mtu, hakukuwa na aliyekuwa akiamini kile kilichokuwa kimetokea, hapohapo alichokifanya Dk. Buffet ni kuchukua simu yake na kumpigia Smith akimtaka afike hospitalini hapo kwani mpenzi wake alifanikiwa kupona ugonjwa ule.
“Nakuja,” alisikika Smith na kukata simu.
Tatiana hakulala tena, akasimama na kuanza kuzunguka chumbani mule, kila alichokuwa akikifanya, madaktari walikuwa wakimwangalia, huku nyuso zao zikiwa na furaha tele, hawakuamini kama msichana huyo alifanikiwa kuona kama watu wengine.

Kila wakati Tatiana alikuwa akimshukuru Mungu kwa kumpa uwezo wa kuona. Kuna wakati alikuwa akirukaruka kwa furaha, wakati mwingine alikuwa akikimbia humohumo chumbani, yaani vyote hivyo alikuwa akivifanya huku akiwa kwenye furaha tele.
Ndani ya nusu saa tu Smith akafika hospitalini hapo, moyo wake ulikuwa na furaha tele, hakuamini kile alichokuwa amekisikia kwamba mpenzi wake alikuwa amepona na kuona kama kawaida. “Nimekuja...”
“Kufanya nini?”

“Kumuona mpenzi wangu! Kumbe amepona,” alisema Smith, alikuwa akizungumza na dada wa mapokezi.
 
SEHEMU YA 64...
“Karibu sana,” alisema dada yule kwani alichokijua ni kwamba mtu pekee aliyeuwa akifanyiwa matibabu ya macho alikuwa Tatiana tu. Hapohapo akaelekezwa chumbaalichokuwemo muda huo kwani kile chumba cha siku zote alikuwa amehamishiwa na kupelekwa kwingine.

Smith hakutaka kutembea kwa mwendo wa taratibu, alikuwa akitembea kwa kasi kubwa kuelekea katika chumba hicho, msichana ambaye alikuwa amepewa kwa ajili ya kumpeleka chumbani huko alikuwa amemuacha nyuma kana kwamba yeye ndiye alikuwa akimpeleka msichana huyo.
“Ni huku,” alisema msichana huyo mara baada ya kuona Smith ameelekea njia nyingine.
“Tangulia wewe basi, tena kwa mwendo wa kasi kidogo,” alisema Smith na dada yule kufanya hivyo.

Walipofika ndani ya chumba hicho, Smith hakuamini kumuona mpenzi wake akitembeatembea chumbani mule huku wakati mwingine akiviruka vyombo vya kuweka uchafu (dust bin) ili kuwaonyeshea watu wote kwamba alikuwa amepona.

“Tattie,” alimuita Tatiana huku akionekana kutokuamini.
“Smith...” aliita Tatiana huku akionekana kuanza kunywea, furaha kubwa aliyokuwa nayo ikaanza kupungua. Hivyohivyo, tena kwa kujivuta akaanza kumsogelea Smith na kisha kumkumbatia.

“Hatimaye umepona,” alisema Smith huku akiwa na furaha tele.
“Nashukuru kwa msaada wako Smith, nimepona,” alisema Tatiana.
Smith hakujisikia vizuri, alimfahamu Tatiana, hakuwa mtu wa kupenda kulita jina lake, kila alipokuwa akizungumza naye, alimuita jina la mpenzi, kitendo cha kuitwa Smith na kule kunywea kwa Tatiana kukaonekana kumtia mashaka makubwa.

Hakutaka kujiuliza sana, kwa kuwa lengolake la kila siku lilikuwa ni kumuona mpenzi wake huyo akipona, kwake ilikuwa ni furaha tu.

“Nashukuru sana Buffet, umekuwa msaada mkubwa kwangu,” alisema Smith huku akiachia tabasamu.
“Nashukuru sana. Hii ni kazi yangu, nafurahi sana kumuona Tatiana akiwa amepona,” alisema Buffet.
Tatiana hakutakiwa kuondoka siku hiyo, alihitajika kukaa kwa siku mbili kwani alitakiwa kufanyiwa baadhi ya mambo ili hali itengemae kabisa.
 
SEHEMU YA 65...
Taarifa zikaanza kusambaa kwamba Tatiana alikuwa amepona macho yake na alikuwa akiona kama kawaida. Hiyo ndiyo ikawa habari kwa kipindi hicho, taarifa hizo zilisambaa kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba ndani ya nusu saa, kila mtu aliyekuwa akitumia mitandao ya kijamii alilifahamu hilo.

Nchini Tanzania, watu wengi walimshukuru Mungu kwa kuwapa mtu kama Tatiana ambaye aliipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania na kuifanya nchi hiyo ijulikane zaidi. “Amepona bwana...” alisikika jamaa mmoja.
“Ndiyo hivyo! Daah! Kweli Mungu mkubwa. Ila nao hawa Wazungu nuksi sana,” alisema jama mwingine.
Jina la Dk. Buffet likaanza kujulikana, kazi kubwa aliyokuwa ameifanya ilimfanya kupata sifa kubwa duniani kiasi kwamba kila mtu alisema kwamba hakukuwa na daktari aliyekuwa na uwezo mkubwa kama yeye.

Watu wengi hasa marafiki zake walikuwa wakimpigia simu Dk. Buffet na kumpa pongezi juu ya kile alichokuwa amekifanya. Kwake ilikuwa sifa kubwa, jina lake na hospitali hiyo vikatangazika sana kiasi kwamba wengi wakashauri kwamba apokee tuzo maalumu ya heshima kutokana na kile alichokuwa amekifanya jambo lililoungwa mkono na kila mtu.
 
SEHEMU YA 66...
Mtu wa kwanza kabisakumuona mbele yake alikuwa Dk. Buffet. Alivalia koti refu jeupe huku shingoni mwake akiwa ameipitisha mashine ya kusikilizia mapigo ya moyo. Kwa kumwangalia tu, alikuwa mwanaume mzuri wa sura ambaye kila alipokuwa akitabasamu, uzuri wake uliongezeka zaidi.

Tatiana alipomuona Dk. Buffet, akausikia moyo wake ukimripuka kwa furaha, hakuamini kama duniani kulikuwa na watu wenye sura nzuri kama alivyokuwa daktari huyo. Hapohapo, akauhisi moyo wake ukimuingiza daktari huyo na kumpenda kwa mapenzi ya dhati.
Hakujua Smith alionekanaje, hakujua sura yake ilikuwa vipi lakini kitu alichokuwa akikiamini ni kwamba mwanaume huyo hakuwa na sura nzuri kama aliyokuwa nayo Smith. Dk. Buffet alipokuwa akitabasamu, Tatiana alijiona kama anamwangalia malaika.

Kuna wakati alitamani kumvutia kwake, ambusu kwani hakukuwa na kitu alichokuwa na hamu kukifanya kwa daktari huyo kama hicho. Kila wakati alipokuwa akimwangalia, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda tu huku akihisi damu yake ikizunguka kwa kasi kubwa mishipani mwake.
“Vipi?” aliuliza Dk. Buffet kwani hata macho aliyokuwa akimwangalia yalionekana tofauti.

“Poa, nafurahi kuona,” alisema Tatina kwa sauti iliyojaza mahaba tele, sauti ndogo ambayo hakutaka manesi waliokuwa chumbani humo kuisikia.
Huo ndiyo ulikuwa wakati wake wa kuangukia katika penzi la mtu mwingine kabisa ambaye hakuwa amemtegemea kabisa maishani mwake. Hata Smith alipokuja hospitalini hapo na kumwangalia, hakuvutiwa naye kama alivyokuwa Dk. Buffet ambaye kila alipokuwa akitabasamu tu, moyo wake ulikuwa hoi.

Siku hiyo ambayo alitakiwa kubaki hospitalini hapo alitaka kuitumia vilivyo, hakutaka kuona akiendelea kuteseka mapenzini na wakati mtu ambaye alimuweka katika hali hiyo alikuwa na uwezekano mkubwa wa kumpata.
Alichokifanya usiku alipokuwa kitandani akichati na Smith ni kumuomba nesi amuitie Dk. Buffet ambaye pasipo kuhisi chochote kile alifika haraka chumbani hapo.

“Naomba manesi watoke, kuna kitu nataka kukwambia,” alisema Tatiana kwa sauti ndogo, hilo halikuwa tatizo, Dk. Buffet akafanya hivyo na kubaki wawili chumbani.
 
SEHEMU YA 67...
“Naomba uniguse hapa,” alisema Tatiana, alitaka kuguswa kifuani upande wa moyo.
“Kuna nini?”
“Nahisi kuna kitu, hebu niguse,” alisema Tatiana huku akiushika mkono wa daktari huyo na kuupelaka kifuani mwake.
“Unahisi nini?” aliuliza dokta.
“Hebu shuka chini kdogo.
“Mmmh! Tatiana.”

“Naomba ushuke jamani, shuka kidogo,” alisema Tatiana kwa sauti ndogo, sauti iliyomfanya Dk. Buffet kujua kilichokuwa kikifuatia. Akafanya hivyo.
“Nahisi matiti yangu yanawasha sana,” alisema Tatiana.
“Kivipi?”
“Yaani kama kansa inanianza.”
“Kansa?”
“Ndiyo! Hebu jaribu kuyashikashika,” alisema Tatiana.
Lilikuwa jambo gumu lakini hakuwa na jinsi, kwa maneno ya Tatiana kwamba alihisi kuwa anaanza kuwa na ugonjwa wa kansa yakamtia wasiwasi kwa kuhisi kwamba ni kweli kwani dalili moja ya wanawake waliokuwa wakianza kuumwa kansa ya matiti, yalianza kuwasha.
Alichokifanya Tatiana ni kulala chali kitandani, akaivua blauzi yake na kuyaacha matiti wazi hali iliyomfanya Dk. Buffet apigwe na mshangao.
“Nitakufa dokta, naogopa sana kansa, naomba uyashikeshike,” alisema Tatiana huku akionekana kuzidiwa.

“Ngoja nikamuite dokta wa magonjwa ya wakinamama.”
“Hapana! Nataka uanze kuyashika wewe jamani, au unataka nife?”
“Hapana.”
“Basi yashike.”
Hakuwa na jinsi, kila alipokuwa akikiangalia kifua cha msichana yule, yeye mwenyewe alichanganyikiwa. Mbali na kifua hicho, Tatiana alikuwa na sura nzuri ambayo hata yeye mwenye ilimpagawisha mno.

Kabla ya kuyashikla, alichokifanya ni kuufunga mlango na kushusha pazia la kisasa ili wasiweze kukutwa kisha kumrudia msichna huyo kitandani pale. Alichokuwa akikitaka ni kufanya kile alichokuwa ameambiwa hivyo kuanza kufanya hivyo.
Kila aliposhikwa, Tatiana alikuwa akitoa sauti ya kimahaba tu, alichanganyikiwa mno, alipoona akizidi kuchanganyikiwa, akaanza kuvua sketi yake jambo lililomfanya Dk. Buffet kuacha.
“Unataka kufanya nini?”
“Nimezidiwa doka.”

“Hapana! Siwezi. Namheshimu sana Smith. Siwezi kufanya hivyo,” alisema Dk. Buffet huku akimaanisha kile alichokuwa akikisema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom