SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,953
- 2,044
Wakuu nachukua nafasi hii kuwapongeza TANESCO kwa kuweza kupiga hatua ya ukuaji kwa kuhakikisha licha ya ukame na vipindi tunavyopita bado wamekuwa wakitupa umeme pasipo kukatika masaa 24/7.
Muda huu wana Dar tungekuwa huku tunalia na maji huku tunalia na TANESCO. Wote tunakumbuka vipindi vya jua kali hapa kungekuwa na watu wanatupiwa lawama kuwa wanafanya biashara ya majenereta wakati vyanzo vya uhakika vya umeme tunavyo.
Hongereni TANESCO kwa huduma bora. Yaani natamani huyo mkurugenzi wenu wa sasa aongezewe na idara ya maji safi aisimamie kwa muda au aende akatoe darasa huko DAWASA, maana ni aibu sisi wana Dar kupitia adha hii kubwa ya maji. Tena saa nyingine maji yenyewe yakitoka yana chumvi, wakati vyanzo vya maji tunavyo na serikali inatoa hela nyingi tu kufadhili miradi ya maji.
Hongereni sana TANESCO, maana muda huu nanyi mngekuwa kwenye maneno ya kashfa kibao lakini dhamira yenu ya kumaliza changamoto na kero tumeiona.