Askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polcarp Kadinali Pengo amesema amemsamehe mchungaji Gwajima(hakuumtaja) na wote walioguswa ,ameyesema hayo wakati wa Misa Takatifu ya Jumapili ya matawi tarehe 29th March 2015 katika kanisa kuu la ST Joseph Cathedral .
"Naomba niseme kutokana na hali iliyopo kuwa kutoka moyoni kabisa nimesamehe yote yaliyosemwa na naomba tumuombee na kuwaombea wote walioguswa sina kinyongo chochote"
Waumini walilipuka kwa makofi baada ya kusikia kauli ya mwadhama.
Mytake:
Ushauri kwa Jamhuri, maadam Mwadhama ametamka tena huku akiwa amekalia kiti cha kiaskofu kwa sisi wakatoliki nadhani tunajua maana ya tamko linapotolewa huku Askofu akiwa amekalia kiti chake basi na wao wasikie mtukanwa kasemehe na wao watumie hekima kuachana na Gwajima ili kuipa uzito maana ya msamaha unless kama Jamhuri inataka kuendelea kwa mahojiano ya mambo mengine sio la kutukanwa,maana mtukanwa akitoa msahama huku mambo yanaendelea itaonekana hakuna msahama wa kweli kutoka kwa Mungu.
Chanzo mimi mwenyewe.
Kama ni kweli amemsamehe, akamtembelee basi hospitali, akiiga mfano wa Pope John Paul II!
Papa John Paul II alimsamehe Mehmet Ali aliyetaka kumwua kwa risasi, na hata kumtembelea gerezani alikokuwa amefungwa!