Nyaraka kaama hizo si ngeni kutoka toka kuanza chaguzi za vyama vingi. Lakini hii yaonekana yaonekana kukilenga chama tawala kwa muono wa Serikali ambayo i sawa na kusema CCM kwa sasa hivi. Kwa baadhi wameenda mbali zaidi na kuona kuwa, waraka huo si tu unailenga CCM, bali ni Rais Kikwete na washabiki wake serikalini kwa kuonekana kutolisikiliza kanisa katoliki kama ilivyokuwepo kwa akina Nyerere na Mkapa.
Wataalamu wa mambo ya siasa, wameeleza kuwa nguvu au ushawishi wa kanisa katoliki ndani ya serikali umepungua sana. Na hii imetokana na Kikwete kutaka kutenganisha kabisa dini na serikali kwa vitendo kitu ambacho kitakuwa kipya kabisa toka tukiwa Tanganyika na hatimaye Tanzania. Kwa maana hali hiyo ilirithiwa toka kwa wakoloni na kupewa baraka zote na mataifa ya magharibi.
Kikwete aliweza kuwashinda kidiplomasia akina Pengo na wafuasi wake, na ndio maana wakathubutu kutamka kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu. Rais Kikwete alijua wazi kuwa kuna gharama kubwa ya kulipa kwa kuungwa mkono na makanisa yote. Ni vipi alijiandaa na hilo, hakuna ajuaye isipokuwa waliyekaribu naye tu. Kwa vile yeye ni mkongwe wa siasa wa muda mrefu, ninahakika kabisa anaelewa Nguvu na ushawishi wa kanisa Katoliki duniani. Tena liko tayari hata kuleta vita pale ambapo linaona kuwa linapoteza umaarufu, kwa nia ya kujipanga upya.
Haya mambo yanahitaji tafakuri ya hali ya juu sana ili kuyaelewa.Yawezekana wengi hatujausoma huo waraka na tunajibizana kutokana na jinsi vyombo vya habari vinavyoandika au wanasiasa wanasemaje na mbaya zaidi kila mtu anatoa hoja akitokea upande anaodhani yeye uko sahihi. Kwa kuusoma na kuujadili waraka huo kwa pamoja tunaweza kujibu Maswali mengi bila hata kuhitaji msaada wa mtu mwingine.Ninasisitiza ili tuwe analytical tuusome waraka huo kwa makini tujue Wakatoliki (AU WAKRISTO in general kama wengine wanavyosema) wana hoja gani ndani yake.
Hebu fikiria sisi tuliosogeza madarasa mbele kidogo tunashindwa kuutafsiri je wale ndugu zetu wengine tuliwaacha madarasa ya nyuma kidogo itakuwaje?Tuusome na tuwasaidie wengine kuujua vizuri kama utatusaidia tuudumishe na kama utatutgawa basi wakatoliki/Wakristo tutawauliza kwa nini wanataka kutugawa.
Mungu awe nanyi Daima
Kweli kabisa wewe ni DOGMA!Kati ya hao walioandika huo waraka na huyo Mwanya(PENGO) ni nani kila kukicha anausemea huo waraka?
Nimeamini unaweza ukamaliza madarasa hata mwalimu kufa darasani bila ya kuelimika!Maskini wee,yaani unatia aibu kutetea utumbo!Huko katoliki hakuna demokrasia leo anayetetea hiyo demokrasia atokee katoliki!Maajabu,mbona askofu Malasusa tumemchagua wenyewe hapa bongo?Na ndio maana utagundua viongozi wote wa kidini wanaoteuliwa au kuchaguliwa nje ya nchi yao ni watumwa wa mabeberu hao wa nje kwa ajili ya utashi wao binafsi.Hata ufanye vipi hutaweza kujitakasa na maji ya ******.
Umetaka ndio hivyo hukutaka ndio hivyo,huko hakuna kitu toka njoo huku lutheran au nenda anglican kwani demokrasia inapatikana na si kuletewa mamluki toka roma
Kwa juhudi kubwa umejaribu kujadili mtu badala ya ujumbe anaouleta. Kuishiwa hoja kwako kwa namna hii kunaitwa ad hominem.
Pili unasahau kuwa msingi wa hoja zote hizi ni waraka wa wakatoliki kuelekea uchaguzi wa 2010. Waraka huu umeandaliwa na wataalamu wakatoliki, na sio maaskofu kama kichwa chako kidogo kinavyoshindwa ku-grasp, hivyo wote mnaoushambulia waraka na kuuhusisha na Pengo au yeyote kwa namna moja mnadhihirisha mlivyo na vichwa vigumu na mlivyo mahodari wa kudandia matreni kwa mbele, ila sisi wenye busara tunawaangalia tu mkipiga makasia pasipo na maji.
Ni kweli kanisa katoliki lilitaharuki baada ya kugundua Kikwete na serekali yake walikuwa na mpango kuwaifanya Tanzania kuwa Jamhuri ya Kiislam kupitia OIC na kuanzishwa mahakama ya Kadhi.Tusisahau wakristo kwa ujumla wao [walutheri,wasabato,waanglicana na wapentecoste]hawakujua ujanja wa serekali ya kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ingawa ilikuwa ni sehemu ya ilani ya CCM.
Serekali inaweza ikafikiri inapambana na kanisa katoliki pekee lakini ukweli wa mambo itakuwa ikipambana na wakristo wa madhehebu yote na pengine inaweza kuitumbukiza Tanzania katika mgogoro mkubwa kuliko tunavyofikiri.Kikwete anajua hili ndiyo maana hawezi kumwona Pengo mwenyewe kwa kuwa anajua dhambi na hila za serekali yake dhidi ya kanisa.Kikwete alilitumia kanisa kufika hapo alipo,ni huyu huyu Pengo na maaskofu wa madhehebu karibu yote walikuwa wakituambia muungwana ni chaguo la Mungu.
Kikwete kwa maoni yangu anayo karata moja ya kucheza nayo ni kumtumia Mizengo Pinda ambaye ni mkatoliki safi kutuliza mambo kabla hayajaaribika kabisa.Tatizo hapa je Pinda atakubali kutumika kama daraja au naye atataka kutumia fursa hii adimu kama mtaji wake wa siasa hasa kupewa nafasi na chama kugombea urais baada ya muungwana mwaka 2015.
Mkuu Zawadi imekuwa nongwa katoliki kutoa waraka mbona waislam wametoa wakwao tena kwa mbwembwe kubwa pale mnazi moja.Waraka wa kanisa katoliki hauwezi kuzuiwa na wanasiasa wanaowafuga na kuwalelea mafisadi,waraka wa kanisa katoliki ni jibu sahihi kwa serekali iliyokuwa tayari kuvunja katiba ili kuanzisha mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC.
Ni kweli kanisa katoliki lilitaharuki baada ya kugundua Kikwete na serekali yake walikuwa na mpango kuwaifanya Tanzania kuwa Jamhuri ya Kiislam kupitia OIC na kuanzishwa mahakama ya Kadhi.Tusisahau wakristo kwa ujumla wao [walutheri,wasabato,waanglicana na wapentecoste]hawakujua ujanja wa serekali ya kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ingawa ilikuwa ni sehemu ya ilani ya CCM.
Kweli tunaoelekea ni kubaya....kwa mawazo kama haya!!!!
Serekali inaweza ikafikiri inapambana na kanisa katoliki pekee lakini ukweli wa mambo itakuwa ikipambana na wakristo wa madhehebu yote na pengine inaweza kuitumbukiza Tanzania katika mgogoro mkubwa kuliko tunavyofikiri.
Mkuki kwa Mwislamu kwa Mkristo mchungu....wakati Serikali inapambana na "uchochezi" wa waislamu ilikuwa sawa na wala hakujaweza kuitumbukiza Tanzania katika migogoro lakini sasa imeshwakuwa hivi...Yaani akifanya uchochezi Sheikh PONDA serikali ina haki ya kuchukua hatua, akifanya Kadinali Pengo serikali haina haki wala wajibu wa kulishughulikia na zaidi inataka kuitumbukiza Tanzania katika migogoro..
Kikwete anajua hili ndiyo maana hawezi kumwona Pengo mwenyewe kwa kuwa anajua dhambi na hila za serekali yake dhidi ya kanisa.Kikwete alilitumia kanisa kufika hapo alipo,ni huyu huyu Pengo na maaskofu wa madhehebu karibu yote walikuwa wakituambia muungwana ni chaguo la Mungu.
Nakubaliana nawe 100%
Kikwete kwa maoni yangu anayo karata moja ya kucheza nayo ni kumtumia Mizengo Pinda ambaye ni mkatoliki safi kutuliza mambo kabla hayajaaribika kabisa.
Ni kweli PINDA ni mkatoliki mnyenyekevu lakini hili la UKATAOLIKI SAFI sijui ni vigezo gani unavitumia....unaweza kutuhabarisha zaidi?
Tatizo hapa je Pinda atakubali kutumika kama daraja au naye atataka kutumia fursa hii adimu kama mtaji wake wa siasa hasa kupewa nafasi na chama kugombea urais baada ya muungwana mwaka 2015.
Pinda kuongelea suala hili kama alivyofanya bungeni na hakuna aliyeaanz kumtukana na kumkejeli kama wanavyofanyiwa wasio wakatoliki ni jukumu lake kwa serikali na taifa lake. Kama ulivyosema, ni Pinda ndiye anaeweza kulishughulikia hili suala kwa mafanikio zaidi kuliko wengine lakini hilo ni jukumu lake kama waziri mkuu tuache kuanza kuspin mambo kufurahisha misimamo yetu iliyojaa USISI na UWAO....
omarilyas
Fumbo mfumbie mjinga mwenye akili huling'amua!! Wakristo siyo wavivu wa kufikiri kama unavyotaka kutusadikisha.Kujiunga na OIC au kuwa na Mahakama ya Kadhi sio kuwa ndo nchi imeshakua ya kiislam! hapa nyie wakristo ndo mna-mis point. lakini wakiristo wenye akili wanaelewa tafauti hizi. Kuna nchi nyingi duniani zimejiunga na OIC na zina Kadhi court na bado ziko secular sasa nyie wakiristo wa Bongo mkiondoa uvivu wa kufikiri mtaelewa
Pamoja na hayo yote juhudi za mara kwa mara za marais waislamu kutaka kuisilimisha nchi zitafikia mwisho hasa pale wakristo watakapoungana wote dhidi ya islamization! Waislamu kwa upande wao huwa wakishindwa kwa hoja huwa wanatafuta njia ya mapigano! All in all viongozi wa kiislamu wasipoacha islamic agenda wakati wa uchaguzi watatufikisha pabaya: kama Lebanon alivyodai kikongwe Kingunge!
Yawezekana usemavyo i kweli, lakini ujumbe alioutoa Kingunge safari hii umewafikia wengi. Nahii haitokani eti kwa vile aliyesema ni Kingunge, bali ni kutokana na utata wa waraka wenyewe. Yabidi uhudhurie j'pili kanisani ili uusikilize waraka huo, sasa hii ni nchi gani?
Na ndio maana waislamu nao wakatoa wao. Siamini kama waislam huko nyuma walikuwa na nia ya kutoa waraka kama huo, ila hii ilikuwa ishara ya ushindani au uamsho kwa kundi jingine la imani.
Ni kweli kanisa katoliki lilitaharuki baada ya kugundua Kikwete na serekali yake walikuwa na mpango kuwaifanya Tanzania kuwa Jamhuri ya Kiislam kupitia OIC na kuanzishwa mahakama ya Kadhi.Tusisahau wakristo kwa ujumla wao [walutheri,wasabato,waanglicana na wapentecoste]hawakujua ujanja wa serekali ya kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ingawa ilikuwa ni sehemu ya ilani ya CCM.
Serekali inaweza ikafikiri inapambana na kanisa katoliki pekee lakini ukweli wa mambo itakuwa ikipambana na wakristo wa madhehebu yote na pengine inaweza kuitumbukiza Tanzania katika mgogoro mkubwa kuliko tunavyofikiri.Kikwete anajua hili ndiyo maana hawezi kumwona Pengo mwenyewe kwa kuwa anajua dhambi na hila za serekali yake dhidi ya kanisa.Kikwete alilitumia kanisa kufika hapo alipo,ni huyu huyu Pengo na maaskofu wa madhehebu karibu yote walikuwa wakituambia muungwana ni chaguo la Mungu.
Kikwete kwa maoni yangu anayo karata moja ya kucheza nayo ni kumtumia Mizengo Pinda ambaye ni mkatoliki safi kutuliza mambo kabla hayajaaribika kabisa.Tatizo hapa je Pinda atakubali kutumika kama daraja au naye atataka kutumia fursa hii adimu kama mtaji wake wa siasa hasa kupewa nafasi na chama kugombea urais baada ya muungwana mwaka 2015.
Mimi nsons hii sio issue ya kuzungumzia watu wenye uweleo wenu. MIMI NAONA PENGO NA WENZAKE NI WANAFIKI SANA. NA KAMA WAO WAWAZI BASI WAJITOSE DHAHIRI KUGOMBEA UONGOZI WA SIASA KAMA ALIVYOFANYA DR SLAA NA MCHUNGAJI RWEKATARE AU HATA ALIVYOFANYA KAKOBE KUMPIGIA WAZI DEBE MGOMBEA MMOJA WA SIASA AWE KIONGOZI.
Ukumbuke kuwa hao unaowaita viongozi wa waislamu bila ya kutaja makundi yao nao pia wapo wenye fikira punguwani kama zako kuwa Nyerere na viongozi wengine wakriso wamekuwa wakichristianize Tanzania lakini hadi sasa bado hatujafika kama walipo hao wa Lebanon. Kitu ambacho kitawezekana kabisa kufikiwa hivi karibuni kama tutaendelea na huu ujinga wa hao tunaowaona kuwa wapo sawa kutua hizo Waraka na Miongozo yao na matamshi ya kinafiki kama yanayoendelea.
Tusipoangalia kuna kila uwezekano watanzania wakapiga kura kufuata makundi yao ya kidini katika uchaguzi ujao kama ambavyo wabunge wao wameshaanza kuonyesha mifano....
omarilyas
Huu ni unafiki na uzushi usio mfano! Jee, Tanzania kujiunga na OIC na kuwa na Mahakama ya Kadhi ndio imeshageuka kuwa Jamhuri ya Kiislam? huo ni upumbavu wa hali ya juu.
Nchi ngapi duniani zina hizo Mahakama za Kadhi na wamejiunga na OIC mbona hazijawa Jamhuri za KiIslam?
Jirani zetu, Uganda na Msumbiji ni memba wa OIC na Kenya kuna Mahakama ya Kadhi, Jee ni lini ulizisikia zikawa Jamhuri za kiIslam?
Wacha upumbavu!