Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,367
- 2,407
Kimsingi mimi sitaki Taasisi, Jumuiya, mtu binafsi au NGO yeyote ile kutoa waraka au Muongozo juu ya kuwaelimisha wananchi kupiga kura. Nikifahamu wazi kuwa suala hili lipo very sensitive, bila ya kuangalia maudhui yaliyomo kwenye waraka au muongozo.Huu waraka sio mara ya kwanza kutolewa, ule wa mwanzo haukuleta matatizo kama inavyosemekana yatakuja kusababishwa nao. Zawadi kama ungetaka kubalance story ungezungumzia hatari ya MWONGOZO wa waislamu hata kama umekuja baada ya waraka wa wakatoliki. MWONGOZO huo umeji-isolate zaidi kwamba wafuasi wake watapiga "kura maslahi." Sasa linganisha na waraka ambao unataka watu wachague viongozi waadilifu! Usipobalance story hata kama una pointi nzuri namna gani huna tofauti na wale ambao unawalaumu kimakosa kwenye thread hii huku na wewe unayafanya yaleyale, kwa maana hiyo unajihukumu mwenyewe!
Uko sahihi kabisa, na hii ndio hatari ambayo wanaopinga waraka wa wakatoliki waliiona. Nafikiri wenzengu hapa JF mtamuelewa huyu mtoa hoja.hata kama waraka wao ungekuwa mzuri kiasi gani nitaupinga mbaka kufa,wao ni watu wa dini hivyo wanatakiwa kuwaandaa watu kiroho,wawaelimishe waumini wao namna ya kuishi ili wafike mbinguni na si vinginevyo ndio maana hata yesu alikataa kushugulikia mambo ya duniani hata kama utawala wa kiyahudi ulikuwa mbovu ingawa watu walijua yeye ndiye mfalme lakini yeye alisema hana shida ya ufalme wa duniani yeye ni mfalme wa mbinguni,sasa nyie mnaohangaika na mambo ya dunia ndo biblia ya wazungu ilivyowaagiza hivyo?
Kimsingi mimi sitaki Taasisi, Jumuiya, mtu binafsi au NGO yeyote ile kutoa waraka au Muongozo juu ya kuwaelimisha wananchi kupiga kura. Nikifahamu wazi kuwa suala hili lipo very sensitive, bila ya kuangalia maudhui yaliyomo kwenye waraka au muongozo.
Katika hili suala la kwanza linalojitokeza ni nani kautoa huo waraka au muongozo. Lazima tufahamu kuwa kama Katoliki na waislam wanaweza kutoa waraka basi hata mtu binafsi akiwa na pesa zake anaweza kufanya hivyo. Hali kadhalika kwa NGO.
Hapa ni lazima ikumbukwe kuwa kila mmoja ana mawazo yake juu ya nani ni kiongozi mzuri. Kama waraka ungeandikwa na Mchungaji Mtikila angeandika waraka wake, basi ni wazi kuwa kigezo No 1 angeseama kuwa MAGABACHORI msiwachague kuwa viongozi. Tusingeweza kumkataza kwa sababu hivyo ndivyo afikiriavyo.
Ukiliona tatizo hili utakubaliana nami kuwa jukumu la kuwaelimisha wananchi kuwachagua wagombea waadilifu ni la serikali. Lazima tukumbuke kuwa hili ni jambo la kudumu na inabidi liwafikie wananchi wote kwa fedha ya walipa kodi.
Pamoja tuaendelea, tusikimbilie utatuzi wa harakaharaka. Dalili ya mvua ni mawingu.
Hamukujibu hoja yangu.
Nimesema wapi ndani ya vitabu vyake 73 ameamrishwa kukemea maovu na munakimbilia logic, common sense, haki kama Raia. Nimedai reference ya kitabu nikiamini kwamba anaongozwa na Kitabu chake kwa kuwa yeye amezungumza kama kiongozi wa dini.
Kukwepa hoja yangu nadhani ni ushahidi kwamba hakuna linalomwarisha akemee uovu, kama lingekuwepo lingeletwa.
Kama majibu na misimamo ya viongozi wa dini yanatokana na common sense sasa muongozo wa vitabu una faida gani?
Kesho akija mwingine na common sense ikimwambia jibu ni kupindua Serikali kwa mtutu wa bunduki itakuwaje?
Umeuliza swali zuri. Kuna maxim inasema: "He who alleges must prove." Sasa wapi imeandikwa kwamba maovu yasikemewe? Kwa kuuliza swali lako, una maana kwamba kwenye hivyo vitabu 73 ulivyotaja hakuna sehemu hata moja inayosema maovu yakemewe na ndio maana unahoji kwa nini kakemea hayo maovu. Sasa lete mstari au aya kwa aya kwenye hivyo vitabu ututhibitishie kuwa maovu hayapaswi kukemewa!
- CCM wanapaswa kuukumbatia waraka, kwanza ni mzuri sana kwao kama wakiutimiza kama unavyoshauri, kama ni kushindana viongozi wao wangetumia muda huu wanaoupoteza kushidana na huu waraka kushindana na matatizo mengine sugu kwa taifa, kama usalama kwa wananchi.
- yaani sasa Tanzania imekua ni nchi ambayo huwezi tena kutembea usiku kama zamani utaishia kukabwa na majambazi, mimi ninakumbuka enzi zetu tulikuwa tunatoka Msasani Beach Disco kwa Ma-DJ John Peter Pantalakis na Choggy Sly usiku kwa mguu kurudi majumbani mwetu baada ya Disco, sasa haiwezekani tena maana utaishia kukabwa tu,
- Sasa hawa viongozi badala ya kuelewa kwamba taifa lenye wananchi wanaoishi maisha ya wasi wasi na productivity yao kwa taifa itakuwa ni ya wasi wasi pia, wao wako busy kushindana na waraka wa kanisa na huku wakiwa hawana hoja kabisaa, labda tuwakumbushe tu hawa viongozi wetu, ni kwamba kukosekana kwa uongozi imara wa taifa siku zote hupelekea hata makanisa kuingilia kati kujaribu kurekebisha udhaifu,
Sasa kama tuna viongozi wasiotaka kukosolewa basi watoke sasa wawaaachie wengine, maana haiwezekani wakaziba midomo ya kila mwanachi, wameanza kule NEC, na sasa wanajaribu tena kuyaziba midomo makanisa, sasa nani atakaye waongelea wananchi, nasema hivi viongozi wote waliochoka na wasiofaa wakumbushwe na kanisa au hata misikiti, kama hawataki kusikia watoke sio lazima tuongozwe nao wao tu, get out of there now waachieni wengine, au just shut up! we had enough already na serikali dhaifu!
- And yes I said it, serikali dhaifu!
Ahsante.
William.
Hamukujibu hoja yangu.
Nimesema wapi ndani ya vitabu vyake 73 ameamrishwa kukemea maovu na munakimbilia logic, common sense, haki kama Raia. Nimedai reference ya kitabu nikiamini kwamba anaongozwa na Kitabu chake kwa kuwa yeye amezungumza kama kiongozi wa dini.
Kukwepa hoja yangu nadhani ni ushahidi kwamba hakuna linalomwarisha akemee uovu, kama lingekuwepo lingeletwa.
Kama majibu na misimamo ya viongozi wa dini yanatokana na common sense sasa muongozo wa vitabu una faida gani?
Kesho akija mwingine na common sense ikimwambia jibu ni kupindua Serikali kwa mtutu wa bunduki itakuwaje?
Wakuu, Dini ya kweli daima itahubiri binadamu kuwa mwema na kutotenda dhambi (uovu). Dini yatufundisha, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda nafsi yako". Ukimpenda jirani yako huwezi kumwibia, huwezi kumsingizia uwongo na huwezi kumfanyia lolote lile kinaloweza kumdhuru au kumletea mateso.
.
Mzanganyika. Mbona katika vitabu hivyo unavyosema hakuna sehemu inayosema viongozi hao wasijenge SHULE,HOSPITALI NK mambo mengine ya kijamii lakini wamejenga vitu kama hivyo. Sasa hujui kuwa swala la ufisadi linahusu jamii vile vile. Jalibu kuwa OBJECTIVE ndugu yangu
Wakuu, Dini ya kweli daima itahubiri binadamu kuwa mwema na kutotenda dhambi (uovu). Dini yatufundisha, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda nafsi yako". Ukimpenda jirani yako huwezi kumwibia, huwezi kumsingizia uwongo na huwezi kumfanyia lolote lile kinaloweza kumdhuru au kumletea mateso.
Dini ya kweli inahubiri upendo katika jamii na upendo ni mwanga na ukiwepo, giza (dhambi) hutokomea na hata siku moja huwezi kuvichanganya hivi vitu viwili. Dini inayokaa kimya uovu ukitendeka katika jamii ni dini ya giza na kwa kufumbia macho vitendo hivyo, yenyewe inakuwa mshirika na haiwezi tena kuwa safi mbele ya Mwenyezi Mungu - ni dini ya kishetani.
Wakuu, Dini ya kweli daima itahubiri binadamu kuwa mwema na kutotenda dhambi (uovu).
Swali kwako ndugu yangu, nitajie ni sehemu gani ya waraka inayotishia amani, au iliyovunja sheria ya nchi? Halafu sasa tutafahamishana tu kwa kiustaarabu pale tunapotufautiana kati yetu.
Asante mdau, nasubiri hoja yako!
Ndugu yangu mzanganyika mi nadhani unachanganya mambo. Wewe umeisoma biblia na hukuielewa vizuri. Biblia inakataza matendo mabovu. Inatuongoza ili tutende mema. Hivyo, kukemea mabaya si tu suala la aya za biblia, bali ni kazi ya kila binadamu, awe ni mkatoliki au la, mwislamu au la, mlokole au la. Sasa nikuulize swali, je biblia haipingi ufisadi? Naomba unijibu.
Serikali ni Watu, au Watanzania wote. Na ili kuwepo kwa utaratibu maalum wa watanzania wote kusikika kumewekwa utaratibu wa kuwachagua viongozi.Serikali ni nini? labda tuanzie hapo