Pengo amtolea uvivu Kikwete

jadilini hoja na sio imetolewa wakati gani na nani! Hilo ni jicho la udini.msiharibu mjadala.
 
Hatumchagui mtu kwa dini yake..ukatoliki na serikali wapi na wapi. Makanisa yote na misikiti husajiliwa na wizara tu ambayo ni home affairs. Unadhani ukitaja RC umetaja jambo kuuuubwa?! Ni NGO tu hiyo baba. Na sasa imekuwa civic and profitable organization...inakosa hata hadhi ya Religious NGO. Ombeeni Taifa siyo kulumbana kisiasa. Aliomba audience na Rais aseme linalomkwaza au analotaka kushauri akanyimwa appointment? Anatumia media apate publicity ili iweje?

MUENDE KULIA..KUSHOTO...MAGHARIBI...MASHARIKI...KUSINI...KASKAZINI...MTATAWALIKA TU. MNA ILA SANA NINYI
 
wakuu tunaomba sana tupunguze jazba kwani thread hii inaelekea kuongeza hisia za kidini , tunaipenda Tanzania tusingependa hisia hizi ziongezeke sana.


pls wana JF tusiingize udini kama hoja zijengwe kwenye utendaji na si udini wakuu
dawa ya moto ni moto
dawa ya mdini ni kumletea udini mara kibao.
 
tena katumwa huyu ni usalama kuendelea kumujibu tunapunguza umaarufu wetu ni bora kumuucha aendeleee kuonesha ujinga wake
Umenipa hadhi kubwa mno ya usalama. Inshallah mdomo wako uwe wa kheri ili taifa letu liwe salama zaidi nikinyaka ajira hiyo.
 
tatizo ni rais kuwafaham wahalifu na kukataa kutueleza kwa kututajia majina hao wahalifu.
kwa nini polisi isumbuke kwa kutumia rasilimali nyingi kupambana na madawa ya kulevya wakati mkuu wa nchi anaweza akawaweka ndani hao said maaskofu mara mmoja na kutuokolea taifa?
rais ana mafungamano gani na hao maaskofu mpaka akatae kuwataja?
rais anamwogopa nani?
urais hauna shareholders, yupo huru kimawazo so atusaidie mara mmoja kumaliza tatizo la madawa ya kulevya kama anaipenda tanzania
 

Nadhani tuna haja ya kupima akili na ubongo wa Pengo, katika watu wanafiki yeye ni 1 . Hili jambo liliisha fafanuliwa na ikulu na Bunge, anachokitaka ni kipi ? . Huwezi kuwataja watu wakati uchunguzi bado unaendelea na wana mtandao mrefu. Hili ni jambo la kushughulikia kimya kimya na kwa vile amelipigia kelele nadhani kuna watu wake wa karibu wamekamatwa pabaya.
 

Najitahidi kukuelewa lakini nimeshindwa. Si kwasababu nina uelewa mdogo la hasha bali umejichanganya sana. Mosi kumwambiia mtu ukweli si kutokumpenda hata kidogo. Pengo kasema wazi kama ni yeye anauza unga amtaje... bila shaka anamaanisha kama hata wapo walio chini yake wanafanya hiyo biashara watajwe ili waondolewe kwenye utumishi na sheria ichukue mkondo wake. Huo ndio ujumbe wake kwa Rais. Sasa kigugumizi chatoka wapi? Kama rais wa nchi anakuwa mlalamikaji kama alivyo waziri mkuu wake nani achukue hatua? Heshima unayoizungumzia itatoka wapi? Kama kweli hao watu wapo, CCT walishasema na wakampa masaa 48 awataje, Sasa Pengo kasema... Najua BAKWATA watasema in opposite way lakini ukweli kwa fikra sahihi unabakia kuwa ....... Rais amekosea na sisi wananchi tunamtaka ajitokeze awaseme hadharani hao anaowatuhumu. Anavyo vyombo vyote kwanini ajiume ume? Kama aliteleza si aseme tu wakuu utelezi? Tusitetee ujinga tuwe objective.
 

Wewe kweli ni mchicha mwiba , uliisha ona wapi wahalifu wanatajwa ? mbona hamsemi wahalifu wengine watajwe isipokuwa hawa wa madawa ya kulevya ? waache washughulikiwe kimya kimya. Na nimjuavyo Pengo lazima kuna watu wake wameshikwa pabaya, huyu mzee huwa sio msafi
 

Kama hivi ndivyo sasa wewe mwenye akili timamu huoni hata unamtusi aliyetoa hayo matamshi huku akijua uchunguzi unaendelea? Sio kihere here hicho? Kuna akili timamu hapo? Hata wanaochunguza si watamshangaa?
 
hapo blue: Uchunguzi unaendelea kivipi alisema hadharani maaskofu ni wauza misuba?
Ikiwa uchunguzi utaprove wrong atajitokeza hadharani na kusema maaskofu sio wauza misuba?
Maaskofu ni binadamu so ni possible kabisa baadhi wakawa wauza madawa ila kwa nini aligeneralize?

IF JK kwa moyo wa dhati anapambana na hii biashara ya kuuza misuba ni bora awataje hao maaskofu ili jamii iwaepuke na kuwaogopa kama ukoma
pili lazima sheria ichukue mkondo wake maana wameharibu maelfu ya vijana.

JK itakuwa alikuwa anatafuta namna ya kuwafunga mdomo maaskofu wanaohoji utendaji wake serikali
 
inawezekana hata pengo akawa mchafu as yeye pia ni binadamu.
Rais Obama alitaja majina (wawili ni wa kenya) ila hakusema wakenya ni wauza misuba
Ikiwa rais mtu mwenye madaraka makubwa kuliko yeyote nchini anashindwa kumtaja askofu flani na flani hii inatoa picha gani?
 

Huo ni ulofa na hatutegemei nchi iongozwe kiwoga namna hiyo! Sijawahi kuona nchi ya hovyo namna hiyo duniani isipokuwa Tanzania ya awamu ya 4 tu. Lakini haya yana mwisho! Wahalifu wote wanatakiuwa kutajwa jamii iwaelewe ijitenge nao kisha mkondo wa sheria uchukue hatamu. Kinyume cha hayo ni ulofa ni kujenga mazingira ya rushwa na ni kinyume cha kanuni za utawala bora za za openness & Transparency.
 
Ayawasilishe maoni yake ktk lugha za heshima. Unajua tafsiri ya neno msaliti?
 
be blessed!
rais anaogopa kutaja sasa mimi marytina nitaanzaje kutaja jina la afisa misitu mlaa rushwa hapa halmashauri ya IRAMBA?
 
Ayawasilishe maoni yake ktk lugha za heshima. Unajua tafsiri ya neno msaliti?
KUJUA MHALIFU NA KUKATAA KUMTAJA NI NINI KAMA SIO KUSALITI?
ulitaka atumie neno ghani?
JK akunjue makucha mara mmoja kwa askofi muuza misuba asipakazie baraza lote la maaskofu
 
Ukifikilia kwa umakini utagundua kazi ya mkuu wa nchi kwa sasa ni ufigure head rule hana impact yoyote.Yeye na serikali yake hawafikili hata wanavyoendesha nchi.Ina maana wakuu hampati hata muda wa kutafakari mtakachokisema,mnachotenda,unavyoishi,jamii inawachukuliaje,yanayoendelea nchi za jirani.Hivi wakuu huyu jamaa akiwa kwenye ndege muda wake mwingi unautumia kufanya nn au ndo kulala.Ofisini akai sasa utajuaje hata mwenendo wa kazi zake.
 
Kikwte sio kiongozi ila ni mjasiliamali ,haiwezekani kiongozi mkubwa kama rais wa nchi hawezi kuwa na kauli zenye masiliahi kwa nchi badala yake kauli zake nyingi hazina mashiko,penye tatizo la umeme mara utamsikia mimi ningekuwa mvua,ningenyesha ili umeme upatikane ona kauli hiyo ni ya kiongozi wa nchi anaetakiwa kutoa mwongozo ktk mambo sensitive ya nchi,leo anasimama na kutoa tamko kuwa viongozi wa dini wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya lkn huwataji ni sawa na baba anaewatuhumu watoto wake lakini hataki kuwataja anabaki tu kusema lkn sio nyie wakubwa ila ni hawa wadogo zenu,hivi huyu atakuwa baba anaelewa wajibu wake kweli? au ni mjasliamali tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…