Pendekezo: Wale wote waliodhulumiwa chochote na Serikali ya Tanzania ya awamu ya 5 Wajitokeze hadharani Tufunge mjadala

Ainisheni mateso yenu hapa tuwasaidie
Tumedhulumiwa na kuporwa mabilioni kwenye ujambazi unaoitwa "tozo" .Tumefilisika mitaji kwa kufunga saluni na biashara zetu wengine wauza samaki zimeozea kwenye mafriji kwa migao ya umeme.

Watu wamekufa kwa huduma mbovu za afya wengine wamekufa umeme ulipokatika ICU, Watu wamepoteza maisha kwa ajali kisa miundombinu mibovu.

Watu wana njaa,kiu, bei ya bidhaa zimepanda n.k wakati huo Rais yuko busy na hafla, semina za pongezi,Birthday party, ziara zisizo na tija na ulambaji asali ukishamiri.Laana hii haitawaacha salama.
 
Erythrocyte
20230319_155222.jpg
 
Sasa ni dhahiri kwamba Wimbi la watu kudhulumiwa mali zao wakati wa Utawala wa John Magufuli liko bayana na ni kubwa kuliko tulivyodhani...
Mimi nilidhurumiwa kutokupiga madili yaliyokuwa yanatufanya tunatamba vilabuni na kupola Mali za uma na kunyanganya viwanja vya masikini na kuwatishia. Pia nilidhurumiwa kuwatishia watu
 
Kwahy kumbe ukipata kura 2m+ ndo unapata posho zaidi ya 800m+ kumbe siasa ina pesa hv ndo mana kuna watu hawataki kuiacha.
Hv hy posho wanakuwa wanapewa kila baada ya muda gani.?
Je hiyo posho ni ya miezi mingapi ?
 
Sasa ni dhahiri kwamba Wimbi la watu kudhulumiwa mali zao wakati wa Utawala wa John Magufuli liko bayana na ni kubwa kuliko tulivyodhani .

Watu wameporwa karibu kila kitu , wako walioporwa hela zao , humu wamo walioguswa kwenye akaunti zao ( bila kujali kama wanadaiwa au hawadaiwi ) , wako pia wale wa Plea bargain akiwemo Habhinder Seth na wamo pia wenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ( Bureau De Change ) , wako walioporwa Mashamba yao akiwemo Sumaye , wako walioporwa Viwanja na nyumba , akiwemo GSM , Wako walioporwa magari na kesi zingali Mahakamani , Bila shaka wako walioporwa Wake ama Waume zao kwa utaratibu ule ule wa kishamba wa " Unanijua mimi nani " , Wako wengine walioporwa Uhai wao akiwemo Lwajabe , mnyororo wa walioporwa ni mrefu sana , hatutaweza kuumaliza .

Kwa vile serikali ya awamu ya 6 imetambua uporaji huu na imeanza kuwarejeshea pesa zao baadhi ya wahanga , basi Natoa Wito kwa watu wote waliodhulumiwa chochote kile na serikali ya kikatili ya awamu ya 5 , wajitokeze hadharani tuwafahamu na kufahamu njia zilizotumika kuwapora mali zao ili tuangalie namna ya kuwasaidia , hakuna haja ya kuficha ficha mambo , hakuna haja ya kuogopa kufichua maovu ili kuanika kila uchafu uliofanywa kwenye awamu ile .

Jambo hili ni muhimu kufanyika kwa sababu si wote walioporwa ni maarufu , si wote walioporwa wana ujasiri wa kuyatoa mambo yao hadharani wao wenyewe bila kulindwa , watu waliowatisha na kuwapora wengine bado wako hai na wengine bado wamekalia vitengo .

View attachment 2559592
Watu wengi waliumizwa kwa namna mbalimbali, kuna waliouawa, waliovunjiwa nyumba zao, walioharibiwa mashamba yao, kuna walifukuzwa kazi, kuna waliporwa fedha na zingine nyingi tu. Maridhiano ni muhimu katika sehemu zote maana watu wana maumivu mioyoni mwao.
 
Back
Top Bottom