Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,730
- 218,304
Tunaendelea na mada zetu za mwezi huu ambao ni mwezi wa Mungu .
Kwenye uongozi wa awamu ya 5, haki za kikatiba, ikiwemo haki ya faragha ilipuuzwa , viongozi wote wa sasa na wastaafu , wakiwemo hata raia wa kawaida waliotiliwa shaka, hasa wale wanaotumia mawasiliano ya Kitanzania walidukuliwa, Taarifa zinaeleza kwamba hawa akina Nape, Membe, Kinana na Makamba ni wachache katika wengi waliodukuliwa, faragha za watu zilianikwa na wadukuaji waliotumwa, simu zote za familia za viongozi na wajukuu zao zilidukuliwa, unaambiwa ilikuwa aibu, maana udukuzi huo ulikuwa wa kishamba sana, kiasi cha kudukua hata waliokuwa wanaongea mambo yao na mahawara zao au michepuko yao, hivi unamdukua mtu anayeongea na hawaraake ili upate nini?
Ukitaka kuthibitisha hilo fuatilia nyuzi za Cheusi Mangala, ambayo tunadhani ilikuwa ID ya wadukuzi wenyewe au mtu wa karibu na wadukuzi ama labda msamaria mwema, huyu ndiye aliyeanika udukuzi wote hapa JF
Udukuzi ule zaidi ya kudhalilisha viongozi waliotajwa haukuwa na tija yoyote kwenye Taifa , hakuna hata mmoja kati ya waliodukuliwa aliyeonyesha uhaini wowote. Hoja zao nyingi walizodukuliwa nazo zilikuwa ni za mshangao tu wa namna nchi inavyoendeshwa kishamba, badala ya kuwadhalilisha wadukuliwa, hoja zao zilipaswa kutumia kujisahihisha.
NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO