Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 116,490
- 215,332
Sasa ni dhahiri kwamba Wimbi la watu kudhulumiwa mali zao wakati wa Utawala wa John Magufuli liko bayana na ni kubwa kuliko tulivyodhani.
Watu wameporwa karibu kila kitu, wako walioporwa hela zao , humu wamo walioguswa kwenye akaunti zao (bila kujali kama wanadaiwa au hawadaiwi yaani ukiwa na hela nyingi tu hata kama uliuza mahindi yako unaporwa ), wako pia wale wa Plea bargain akiwemo Habhinder Seth na wamo pia wenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni (Bureau De Change), wako walioporwa Mashamba yao akiwemo Sumaye , Wamo wengi walioporwa mifugo yao kwa kisingizio cha kuchunga kwenye hifadhi , yaani ngedere walionekana bora kuliko ng'ombe , Wavuvi waliporwa kila kitu , zikiwemo samaki walizovua , nyavu , mitumbwi , boti na vifaa vyao vyote , wako walioporwa Viwanja na nyumba , akiwemo GSM , Wako walioporwa magari na kesi zingali Mahakamani , Bila shaka wako walioporwa Wake ama Waume zao kwa utaratibu ule ule wa kishamba wa " Unanijua mimi nani " , Wako wengine walioporwa Uhai wao akiwemo Lwajabe , mnyororo wa walioporwa ni mrefu sana , hatutaweza kuumaliza .
Kwa vile serikali ya awamu ya 6 imetambua uporaji huu na imeanza kuwarejeshea pesa zao baadhi ya wahanga , basi Natoa Wito kwa watu wote waliodhulumiwa chochote kile na serikali ya kikatili ya awamu ya 5 , wajitokeze hadharani tuwafahamu na kufahamu njia zilizotumika kuwapora mali zao ili tuangalie namna ya kuwasaidia , hakuna haja ya kuficha ficha mambo, hakuna haja ya kuogopa kufichua maovu ili kuanika kila uchafu uliofanywa kwenye awamu ile .
Jambo hili ni muhimu kufanyika kwa sababu si wote walioporwa ni maarufu , si wote walioporwa wana ujasiri wa kuyatoa mambo yao hadharani wao wenyewe bila kulindwa , watu waliowatisha na kuwapora wengine bado wako hai na wengine bado wamekalia vitengo.