KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,150
- Thread starter
-
- #121
ok, nilikuwa sijamuelewa, kumbe antichadema ni CDM? hahahahahahahahaha
kim kardash says;
hata wewe wapo waliokutangulia kuijua chadema,lakini haikuzuii kutoa maoni yako na pia kama ni mwanachama una hadhi sawa na wanachama wengine huko cdm,acha ushamba wa mambo!
by Mwita maranya
Katika wakati huu tulionao sitegemei kuona mwanachama hai wa Chadema mwenye mawazo kama yako.
Labda utakuwa ni mshabiki tu ama ni gamba linalohadaa watu kwamba ni chadema.
Mkuu yule kijana Joshua nilimuona kwenye mchakato majimboni enzi zile za kampeni, kwakweli alionyesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na upeo mkubwa wa uelewa wa mambo,...wazo zuri lakini litajenga kutoaminika kwa dr. Kuna vijana wengi wanaoweza kuwakilisha maeneo yao vizuri na wanakubalika pia. Joshua asimamishwe kama mgombea.
Kumbe sikio la kufa halisikii dawa! usijisumbue kupost hoja kabla ya kusoma political pogress ya tanzania.ccm ni wezi wa kura,majambazi wa haki.hivi hukumbuki hata mh.alivyokimbia na sanduku la kura.cdm haina nafasi ya kujadili hoja mufilisi kama yako,sugu keshakwambia slaa sio wa ubunge tena,kama unabisha kamulize anayeitwa Dr.kikwete.
mkuu hapo kwenye bold mwenzako anaelewa kivingine.
siungi nkono hoja.Nassari apewe haki yake.Slaa ana kazi kubwa ya kuimarisha chadema nchi nzima akijiandaa kukamata dola 2015
jibu wapi nilipoandika au kuonyesha nina nasaba na hicho chama chenu cha kususa na kuandamana?mbona unaikwepa hii,sema tu ulikurupuka usione haya!Nikuonyeshe nini wakati una macho lakini huoni. Unasoma lakini huelewi.
Hoja zimekuishia, hakuna jipya hapa ngoja nisepe, ukikumbuka ulichosahau unifahamishe nitakuja kujibu.
Mzee kutokana na uvivu wako wa kusoma na kukimbilia kudandia treni kwa mbele nimelazimika kurudi page ya 2 ambako ndiko kwenye chanzo la hiko unachoking'ang'ania,sasa soma jamaa yako alichokisema na mimi nilichokisema,unadhani mimi ni mtu wa kukurupuka?
kwani hamkuwahi kuwa na ndoa na cuf?waulize wazoefu huko cdm nyie si mmeingia cdm baada ya slaa kugombea urais...this may be too big for you guyz but ndoa tena rasmi ilikuwepo kati yenu na cuf!mkuu kweli una viroja.
Acha kumkashifu mkuu wa nchi aliyenyang'anywa ushindi.Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru. Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.
Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile, kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....
Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.
Nikuhadharishe ndugu yangu,
kwenye Siasa hakuna cha heavy weight! Nijuavyo mimi hata akigombea hatashinda kwani hakuna atakae kuwakilishwa na wale wenye sifa ya kuwaletea vurugu na maandamano ya kila mara yasiyo na tija. Majimbo yote kwa sasa yanayoongozwa na wenye kupenda vurugu wananchi wamechka na wana waasa wanachi wengine wasiingie kwenye kubahatisha kwa kukichagua chama chenye maslahi na vurugu!
Kweli Mkuu Mwita Maranya uliona mbali. Hapo kwenye red ndipo anaonesha rangi zake halisi! Eti kaanzisha thread "kuishauri Chadema". Chadema haishauriwi na wana wa Shetani - the gambaz et al. Uzuri, hila zenu hujionesha mapemaaaaa kabla hamjapiga hata hatua moja katika "hoja" ya kipuuzi mnayotaka kuijenga.
KIM!
nilikuwa miongoni mwa walinzi wa kura wa john mnyika pale ubungo, kura zilizohesabiwa na kutangazwa majimboni ni tofauti na kura zilizotajwa na tume ya uchaguzi? upo hapo?
mkuu utaenda msibani Arumeru kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele mzee wetu?
La hasha,ila kilombero nilikuwako!una lingine au ni hilo hilo tu?lakini cdm wakimsimamisha slaa ntakwenda kwa nauli yangu na gharama zangu arumeru kushiriki kampeni za kumpeleka bungeni kwa kishindo akafanye kazi za watanzania cuz mr slaa is a very honest men na anaipenda sana nchi yake kuliko mfanyabishara mbowe ambae ni rafiki wa mwenyekiti wa ccm,unaona unafiki wa wanasiasa,huyu hashikani mkono na mwenyekiti wa ccm huyu anakunywa nae chai ikulu!mzee wangu slaa ana kazi sana lakini kwa kuwa ni muaminifu kwa taifa atashinda tu
Mkuu post zako unataja kuwa CDM imeshindwa kihalali na mifano yako lukuki lakini hapo hapo huamini katika kushindwa
Mkuu watu makini hawafanyi mambo kwasababu fulani alifanya akaweza, unatakiwa kufanya tathmini yakinifu na kuzingatia factor mbali mbali, kila jimbo lina tabia zake,
Ok umetoa mfano wa Tarime nikweli yule bwana alimrithi vizuri Chacha lakini unajua sababu za kuja kupoteza jimbo kwa CCM uchaguzi mkuu, simply ni kwa sababu CDM walisimamisha mtu kwa matakwa ya chama.
Unapozungumzia swala la elimu hivi elimu gani unazungumzia hiza za Havard za kina Chenge au? hivi unaweza kulinganisha michango ya wasomi wangapi bungeni ukaweza kulinganisha na michango ya watu kama akina Kafulila na Mnyika wasio na degree.
Sitaki kuamini kama mapendekezo yako yote hayo ya Dr Slaa dhidi ya Mbowe kigezo ni elimu. you better think than that dude
Kumuita Joshua mbele ya chama si kuita wapigara kura mbele ya chama, ndio yale yale ya kusimamisha mgombea kwa matakwa ya chama badala ya wapiga kura.
Nimekuuliza mambo ya msingi lakini umekimbila mepesi kwa sababu tu eti Mrema aliweza temeke basi Slaa ataweza Arumeru mashariki, nyakati zimebadila sana mkuu watu wamepata mwamko na uelewa mkubwa wa nini wanataka wao, Temeke leo hii haina mzawa ni full wahamiaji toka bara unapo zungumzia Arumeru yaani kule ni wenyewe watupu mkuu, unahitaji uhakika wa kutosha kama watakubali mgeni kuja kuwawakilisha na si kwasababu Mrema sijui alifanya nini, NOPE
Mwisho kwenye red, maandiko yangu yamejaribu sana kuangalia factor hiyo, tuna maanagani tunaposema "wananchi wakitaka utashinda tu" je ni kwa kuwapelekea mtu au kwa wao kuamua mtu wampedae na kuona ni mwenzao
Rejea bandiko langu la kwanza pitia risk za Dr kugombea ndio utajua je wakati unakwenda kwenye uchaguzi wananchi wanataka?
basi mkuu yaishe, japo sijaona mahali popote aliposema ww CDM zaidi yakuhoji. (''Katika wakati huu tulionao sitegemei kuona mwanachama hai wa Chadema mwenye mawazo kama yako.
Labda utakuwa ni mshabiki tu ama ni gamba linalohadaa watu kwamba ni chadema'')
alipokuwa akiwatumikia wana karatu uliukosa utumishi wake?ndio mana nikakwambie yule ni heavy weight kwanini sikusema mbowe ni heavy weight?sasa mkuu huoni akianza kuwatumikia wana arumeru sisi wa huku mabwepande tutakosa utumishi wake?
mbona hamkuandamana..Acha kumkashifu mkuu wa nchi aliyenyang'anywa ushindi.