mimi naikubali mikakati yenu na nawapongeza kwa ubunifu kama nilivyowapongeza na kuwaunga mkono mlipoolewa na cuf na kukubali kwa hiari yenu kipindi cha ndoa yenu kumsimamisha na kumpigia kura Lipumba,mlionyesha uungwana sana japo sijui ni kwanini mlijitoe baade naamini mgedumu sasa hivi mngekuwa mbali sana.Lakini pamoja na hayo kiti cha ARUMERU kinataka HEAVY WEIGHT wa aina ya SLAA!Hii tusiisahau.
nakubaliana na ww kabisa, japo mashaka yangu yapo kwenye hiyo nguvu ya EL ambapo nasikia mwenyekiti wa tume ni shemeji yake, so bado inaweza ikawa shida kulinganisha nguvu ya Dr. na EL kwenye kampain.
So far hakuna hoja iliyobaki zote ulizoweka mezani nimezipoteza.
Kama kuna nyengine ilete, nimekwambia i'm here to stay!
akiambiwa yeye ni antichadema anadai eti kaambiwa yeye ni CDM.Kweli Mkuu Mwita Maranya uliona mbali. Hapo kwenye red ndipo anaonesha rangi zake halisi! Eti kaanzisha thread "kuishauri Chadema". Chadema haishauriwi na wana wa Shetani - the gambaz et al. Uzuri, hila zenu hujionesha mapemaaaaa kabla hamjapiga hata hatua moja katika "hoja" ya kipuuzi mnayotaka kuijenga.
kwa uchaguzi upi mzee au alirithi toka kwa mzee wake?Mnafiki utamjua tu. we kwa mapenzi gani kwa CDM mpaka utushauri kwa dhati? hizo trick zako za kitoto warudishie masaburi wenzako huko magambani. DR SLAA NDO RAIS WA TANGANYIKA.
KIM!tatizo kubwa sana,mzee hivi unajua process ya uchaguzi na nafasi ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi lakini?tatizo hii chadema yenu wengi mnaifanyia hapa jf tu,hebu siku moja muombe nafasi mkawe ma agent wa chama chenu huko site mkaone kura zinavyohesabiwa na kujumlishwa kituo kwa kituo,yani hata wewe ukiwa na baiskeli yako ukaamua ku take trouble ya kuzunguka kituo hadi kituo na daftari lako then ukakaa chini ya mwembe na kujumlisha utayapata matokeo hata kabla mwenyekiti hajayatangaza na ikakusaidia kuacha kukariri mambo wanayosema wanasiasa baada ya kushindwa
ni ngumu sana kuwaelimisha watu type ya kina makamba na shekhe yahya (R.I.P)
mkuu utaenda msibani Arumeru kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele mzee wetu?Lakini ni rahisi sana kwa watu type ya SHekh SAID ARFI, ZUBERI KABWE ZITTO,PROF SAFARI n.k. sio?
Mkuu merekebisho kidogo kwenye red: Chadema kufuata ushauri wa magamba na anti-Chademas ni sawa na Adam kukubali ushauri wa Hawa (CCM) aliyekubali ushauri wa Nyoka (mafisadi; the real gambaz) kula tunda la mti wa kati! Mola apishe mbali hilo lisitokee asilani.
Frankly speaking, ni mwendawazimu tu anyeweza kutegemea lolote la maana, hata ushauri tu, kutoka kwa CCM hii ya sasa. Imefika mahali kwamba whatever is coming out of CCM ni rubbish.
Hiyo ya kushindwa mimi siiamini sana,ok pengine labda tunatofautina,mimi ni mpiganaji huwa siamini katka kushindwa bali kushinda tu.Na hii haitakua mara ya kwanza kwa heavy weight wa aina ya slaa ambae ni national figure kwenda jimbo lingine na kushinda,alifanya hivyo mrema,licha ya serikali nzima kuhamia temeke kumhami sisco mtiro lakini kwa kuwa kura ni siri mrema alishinda,achaneni na maneno ya kitoto ya wizi wa kura,wananchi wakiamua ushinde utashinda tu.Rejea uchaguzi wa tarime kumrithi chacha.
Kwa nini naamini slaa atakua bora zaidi ya mbowe bungeni?jibu lake ni tofauti wa ELIMU na ufahamu wa wawili hawa,katika hivyo viwili mboe na dr ni sawa sawa na kulinganisha kifo na usingizi,mboe ni kama usingizi tu kwa kifo(slaa),na elimu ni jambo muhimu sana nadhani wote hapa tunakubaliana ya kwamba mwenye elimu zaidi ana maarifa zaidi.Sitaki kusema sana hapa namstahi mwenyekiti.Nadhani naeleweka,watu wazima nyie.
Kijana joshua kama yuko kwa ajili ya chama ataitwa na wazee kina makani watamuelewesaha ataelewa tu kama alielewa zitto na ukaidi wake wote tunaojua akamuachia mbowe uenyekiti itakua joshua!ndio mana kuna wazee,wazee ni grisi kazi yao ni kulainisha chuma kinapopata moto.kumsimamisha mtu kama joshua kwa nyingi lenye interest za mafisadi kama arumeru is a disaster!
sasa mkuu nyufa za kuvuana gamba kwenye chama chenu chanzo chake ni nani?
hoja yako ya Dr. kwenda kuongeza nguvu bungeni sijaisoma vzr, je atawashika wabunge wa CCM mikono kuunga mkono hoja zenye tija kwa maslahi ya umma? au lengo lenu mnataka aende bungeni mseme Dr.kafuata posho bungnei baada ya posho kuongezwa? aisee kuna maswali mengi sana ninayojiuliza ni kwann magamba mnataka Dr. agombee alumeru? ni kwann magamba mnataka Dr. asalimiane na JK?
sasa kwann kwenye hoja zako juu umepinga kuwa CCM hamna nyufa?
Nadhani hivi ni viroja vya kufungulia mwaka 2012, kwamba mtu amekanusha kuwa yeye si mwanaChadema lakini anasimama dede kuishauri chadema nini cha kufanya katika uchaguzi mdogo wa arumeru.
Mtu huyo kila anavyozidi kuandika anaonekana ana nia mbaya kabisa, hata katika threads nyengine ameonekana ni antiChadema.
Kinachofanyika hapa kwa maneno machache sana naweza kukiita ni sawa na upendo wa shetani!
Nimekua kimya nikijaribu kufuatilia hoja zenu waungwana,mnaodai ukatibu mkuu wa slaa ni mkubwa kuliko ubunge,hoja yenu dhaifu sana,umaarufu wa slaa hautokani na ukatibu mkuu wake bali ulitokana na ubunge sasa kwa nini asirudi bungeni akamalizie kazi aliyoianzisha?au mnataka asubiri nafasi ya ubunge wa kuteuliwa na rais mwaka 2013 mwishoni kufuatia muafaka wa haya mazungumzo ya upenuni kati ya jk na mbowe?kama hamjui ndio tunakoelekea!
Na nyie mnaodai eti slaa ni rais mnamdanganya pamoja na kujidanganya nyie!na pia mnaosema eti sijui ataibiwa kura na kufirisika kisiasa pia ni uongo!hivi kura huwa zinaibiwaje?ndugu zanguni amkeni msikubali kudanganywa na wanasiasa,tatizo wanasiasa wetu wa africa huwa hawasemi ukweli kwa kuogopa kuwajibika kutokana na kushindwa chaguzi ndio huwa wanakuja na kisingizio cha kuibiwa kura wakishindwa,hivi hamjiulizi kama wizi wa kura upo kwanini cuf inairesa ccm pemba?au kwanini Ndesambura anaitesa kila wakati ccm moshi mjini?au kwanini Mzee Said Arfi makamu mwenyekiti wa cdm amekua kwa muda mrefu hata wakati slaa hajulikani amekua akiitesa ccm huko mpanda kwake?au zitto kwa nini anitesa ccm?Huwezi kuiba kura,huwa mnakua mmeshindwa tu,msidanganyike na watu kujaa kwenye mikutano yenu ya kampeni au hapa jf watu wengi kuonekana wanaipenda chadema,wengi sio wapiga kura!