Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

Kama kuna wilaya ambayo UKABILA na UKOO ni kigezo namba moja katika kuchagua na kuchaguliwa ni hii ya ARUMERU. Msimdanganye Dr Slaa kwamba umaarufu wake unatosha kumpatia Ubunge jimbo hili. Halafu, mbona tayari anafanya kazi nzuri tu ya Ukatibu Mkuu wa CHADEMA jukwaa pana zaidi kuliko Ubunge wa Jimbo?
Tuliambiwa humu kuwa analipwa vizuri tu na chama chake kama Eto'o kule Urusi au Anelka kule China. Siasa za Arumeru ziacheni hivohivo kwani hata ULUTHERI ni kigezo muhimu sana.

Hata temeke tuliwahi kuaminishwa ni wilaya yenye uislam na undengereko mwingi lakini mrema alitoka kwa kiraracha akamshinda mndengereko,muislam na mzawa wa temeke bwana cisco mtiro,wakati mwingine hizi zinakua ni hofu za kupikwa tu
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru. Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile, kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.

Binafsi sijaona km mbowe kapwaya,kiongozi wa upinzani bungeni ni nafasi kubwa ambayo sio tu inahitaji mpwayukaji ila pia busara na hekima. Mbowe anakidhi na anaitendea haki nafasi ile bungeni. Hata juzi hapa bungen ni busara na hekima yake ilofanya wafikie muafaka kwenye kuwaingiza DC na Mkurugenzi. Binafsi siungi mkono slaa kujiingiza ktk siasa za ubunge atajipunguzia hadhi yake,pia km atashindwa atakua amejitoa kutogombea urais ktk uchaguzi ujao 2015.
 
hawa wametumwa dr keshasema hagombei na hatoki huko sasa wao wanalazimisha nini? nia yao wanataka agombee ili wakamuibie kura na kujifanya hakubaliki ili kummaliza kisisasa hili tunalijua sana hawa ccm sio watu

Hii gia hata mimi nimeistukia mkuu.
 
Hata temeke tuliwahi kuaminishwa ni wilaya yenye uislam na undengereko mwingi lakini mrema alitoka kwa kiraracha akamshinda mndengereko,muislam na mzawa wa temeke bwana cisco mtiro,wakati mwingine hizi zinakua ni hofu za kupikwa tu
Majimbo ya Dar ni "No man's land", kama hicho ni kiingereza sahihi. ARUMERU ni ngazi nyingine kabisa. Hata wilaya na majimbo yenyewe unaona majina yake. Tusifichane bwana. Nchi hii Ubunge na Udiwani vigezo hivi ni muhimu sana ukiondoa majimbo ya miji mikubwa ya Dar, Mwanza na Arusha. Narudia, vigezo vizito vya Ubunge wa Arumeru Mashariki ni:
-Uwe Mmeru wa koo kama Kaaya, Ndosi, Pallangyo...
-Uwe Mlutheri. Ukatoliki kama wa Dr Slaa ni kikwazo tosha.
-Lowasa anakufahamu?
Acheni Dr Slaa aendelee na kazi yake ya kukiimarisha chama chake. Hana wabunge waasi kama alookuwa nao Mrema mwaka 1995 kule NCCR-M.
 
People, Msiumize Vichwa sana..Nassari is still strong to shake Magamba's, He will have enough support from Chadema Head Officers, So we believe, Alone he managed to fight with x minister and he collected unbelievable numbers, Front line with, Mbowe, Slaa, Zitto, Lema, Mnyika, Kiwia, Msigwa, Kidume Mbeya Presidaaaa Sugu, What do you think here?? I am sorry for CCM...SEGEREA ANGEANGUSHWA FISADI MAHANGA..SASA KIDUME SLAA ANGETINGA NA SAMAKI BAHARINI WANGEJUA.
 
Majimbo ya Dar ni "No man's land", kama hicho ni kiingereza sahihi. ARUMERU ni ngazi nyingine kabisa. Hata wilaya na majimbo yenyewe unaona majina yake. Tusifichane bwana. Nchi hii Ubunge na Udiwani vigezo hivi ni muhimu sana ukiondoa majimbo ya miji mikubwa ya Dar, Mwanza na Arusha. Narudia, vigezo vizito vya Ubunge wa Arumeru Mashariki ni:
-Uwe Mmeru wa koo kama Kaaya, Ndosi, Pallangyo...
-Uwe Mlutheri. Ukatoliki kama wa Dr Slaa ni kikwazo tosha.
-Lowasa anakufahamu?
Acheni Dr Slaa aendelee na kazi yake ya kukiimarisha chama chake. Hana wabunge waasi kama alookuwa nao Mrema mwaka 1995 kule NCCR-M.

Hata mbeya mjini tuliwahi kuamishwa hivyo hivyo kwamba pale ni kina mwa... tu lakini leo tunae mbilinyi pale,hoja zako hazina mashiko kubali nimekushika pabaya,lete sababu nyingine kuhusu slaa kutogombea pale sio ukabila,leo tuna wahindi na wazungu wabunge wetu hapa itakua slaa mtanzania mweusi mwenzetu abaguliwe kwa kabila na dini yake?hapana.
 
Ni khatari sana kumsimamisha Slaa kwa mustakabali wa chama chake. Kwani akishindwa itakuwa ni aibu kubwa si kwa chama chake bali hata yeye binafsi.

Someni alama za nyakati kabla kufanya maamuzi.
 
Hii ishu ya Dr, Slaa kugombea Arumeru siyo jambo la kupotezea muda tena kujadili, yeye mwenyewe Dr. Slaa ameshaweka wazi msimamo wake kuwa hataki kugombea ubunge tena, na pia yeye si mkazi wa Arumeru, na zaidi ya hayo Mbowe amesema wanaheshimu uamuzi wake huo.Mimi naona wanaochombeza Dr. Slaa agombee ni CCM ili wachakachue matokeo kwa nia ya kumdhalilisha.
 
Binafsi sijaona km mbowe kapwaya,kiongozi wa upinzani bungeni ni nafasi kubwa ambayo sio tu inahitaji mpwayukaji ila pia busara na hekima. Mbowe anakidhi na anaitendea haki nafasi ile bungeni. Hata juzi hapa bungen ni busara na hekima yake ilofanya wafikie muafaka kwenye kuwaingiza DC na Mkurugenzi. Binafsi siungi mkono slaa kujiingiza ktk siasa za ubunge atajipunguzia hadhi yake,pia km atashindwa atakua amejitoa kutogombea urais ktk uchaguzi ujao 2015.

kwanza kama nilivyoshauri chadema kiachane na ndoto za urais,kijikite katika kujiiimarisha bungeni kwani muhimu ni kuunda serikali sio kutoa rais,unaweza ukaunda serikali bila kutoa rais.

Pili kwani chadema kimemtangaza slaa kuwa mgombea wke wa kudumu wa urais?mimi taarifa hizo sina na nikizipata nitaanzisha thread mara moja ya kujadili ubakaji huo wa demokrasi mchana kweupe,hii ina maana hakuna ruhuusa kwa mtu mwingine huko cdm kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama kugombea urais kwa kuwa ni nafasi ya slaa ya maisha?

halafu hiyo picha badilisha kuna member maarufu tayari anaitumia hata nilipokuwa najibu nilidhani ni yeye kumbe wewe ni mpya!hiyo ni picha maarufu ya NITONYE!
 
Hii ishu ya Dr, Slaa kugombea Arumeru siyo jambo la kupotezea muda tena kujadili, yeye mwenyewe Dr. Slaa ameshaweka wazi msimamo wake kuwa hataki kugombea ubunge tena, na pia yeye si mkazi wa Arumeru, na zaidi ya hayo Mbowe amesema wanaheshimu uamuzi wake huo.Mimi naona wanaochombeza Dr. Slaa agombee ni CCM ili wachakachue matokeo kwa nia ya kumdhalilisha.
Ni kweli kabisa kaka..!But Kitu kikiwa kinasemwa semwa sana..,maya be msimamo wa Dr Slaa haujatolewa kupitia vyombo vya habari thats y magazeti still yanaandika sana kuhusu hilo..
 
Hata mbeya mjini tuliwahi kuamishwa hivyo hivyo kwamba pale ni kina mwa... tu lakini leo tunae mbilinyi pale,hoja zako hazina mashiko kubali nimekushika pabaya,lete sababu nyingine kuhusu slaa kutogombea pale sio ukabila,leo tuna wahindi na wazungu wabunge wetu hapa itakua slaa mtanzania mweusi mwenzetu abaguliwe kwa kabila na dini yake?hapana.
Hauifahamu Mbeya. Mbeya sio ya WANYAKYUSA. Kabila ya bwana Sugu ndio wenyewe Mbeya. Nakueleza kwa kurudia, Ukabila una-play role kubwa sana kuupata UBUNGE nchi hii na sehemu kama Arumeru, Kilimanjaro yote, Kagera yote, Mbeya yote,... hauwambii kitu bila kuzingatia kigezo hiki.
 
KWAKO DR. SLAA.
Heshima yako Mkuu pamoja na wana Jf.
Mkuu pamoja na hoja zote zinazotolewa hapa jamvini, binafsi sikubaliani na pendekezo la wewe kugombea Ubunge kwa sasa. Ninazo sababu nyingi ila kwa uchache tu ni kwamba
* unahitajika zaidi ktk kuimarisha chama.
* wewe ni zaidi ya Ubunge.
* wewe si m-Arumelu.
* kugombea kwako Arumelu utaoneka ni uchu wa madaraka na posho na hii itakuwa ni kete ya ******* kukumaliza ki siasa.
*kugombea kwako Arumelu utatunyima nafasi ya kuongeza idadi ya wapiganaji wapya.
@ Nitahoji kwanini uende Arumeru? Inamaana mnawadharau wameru kwamba hawawezi kujitetea hadi msaada utoke ng'ambo!!??

Dr. Nakuomba kwa dhati baki na msimamo wako, bado tuna kazi ngumu kufikisha ujumbe vijijini tunahitaji uhuru wako wa majukum kufikia ukombozi wa Taifa!
Dr. Hizi ni Pre-campain za ******* usikubali wanakuogopa kwa nafasi unayocheza, wanajua wakikuvunja mguu team haifiki final!!
CDM hata isimamishe mti Arumelu itashinda!!
PEOPLEEEEEESSS...!!
 
Ni khatari sana kumsimamisha Slaa kwa mustakabali wa chama chake. Kwani akishindwa itakuwa ni aibu kubwa si kwa chama chake bali hata yeye binafsi.

Someni alama za nyakati kabla kufanya maamuzi.
Kweli kabisa, inabidi ajikite katika kukijenga chama.
 
Dr Slaa for Presidency 2015, nafasi hiyo ya Arumeru iwe kwa vijana...
 
KWAKO DR. SLAA.
Heshima yako Mkuu pamoja na wana Jf.
Mkuu pamoja na hoja zote zinazotolewa hapa jamvini, binafsi sikubaliani na pendekezo la wewe kugombea Ubunge kwa sasa. Ninazo sababu nyingi ila kwa uchache tu ni kwamba
* unahitajika zaidi ktk kuimarisha chama.
* wewe ni zaidi ya Ubunge.
* wewe si m-Arumelu.
* kugombea kwako Arumelu utaoneka ni uchu wa madaraka na posho na hii itakuwa ni kete ya ******* kukumaliza ki siasa.
*kugombea kwako Arumelu utatunyima nafasi ya kuongeza idadi ya wapiganaji wapya.
@ Nitahoji kwanini uende Arumeru? Inamaana mnawadharau wameru kwamba hawawezi kujitetea hadi msaada utoke ng'ambo!!??

Dr. Nakuomba kwa dhati baki na msimamo wako, bado tuna kazi ngumu kufikisha ujumbe vijijini tunahitaji uhuru wako wa majukum kufikia ukombozi wa Taifa!
Dr. Hizi ni Pre-campain za ******* usikubali wanakuogopa kwa nafasi unayocheza, wanajua wakikuvunja mguu team haifiki final!!
CDM hata isimamishe mti Arumelu itashinda!!
PEOPLEEEEEESSS...!!

Acha urongo wewe unataka kusema chadema ni a one man team?mbona unakitusi chama chako na wanachama wake wote kasoro slaa.
 
kwanza kama nilivyoshauri chadema kiachane na ndoto za urais,kijikite katika kujiiimarisha bungeni kwani muhimu ni kuunda serikali sio kutoa rais,unaweza ukaunda serikali bila kutoa rais.

Pili kwani chadema kimemtangaza slaa kuwa mgombea wke wa kudumu wa urais?mimi taarifa hizo sina na nikizipata nitaanzisha thread mara moja ya kujadili ubakaji huo wa demokrasi mchana kweupe,hii ina maana hakuna ruhuusa kwa mtu mwingine huko cdm kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama kugombea urais kwa kuwa ni nafasi ya slaa ya maisha?

halafu hiyo picha badilisha kuna member maarufu tayari anaitumia hata nilipokuwa najibu nilidhani ni yeye kumbe wewe ni mpya!hiyo ni picha maarufu ya NITONYE!
Chama cha siasa kisipokuwa na ndoto ya URAIS hakipaswi kuendelea kuwepo. Hakifai. Wakigeuze kiwe NGO kama TAMWA ya Mama Nkya.
Dr Slaa tayari ana kazi kubwa na nzuri tu. Arumeru haijapungukiwa vichwa vya UBUNGE. Ubunge hauhitaji watu wa kukodi. Uliona Mrema hakumaliza kipindi chake cha Ubunge pale Temeke. Hakujali waliompigia kura. Aliondoka kihuni tu. Hawezi kufanya hivo kwao Vunjo.
 
Hauifahamu Mbeya. Mbeya sio ya WANYAKYUSA. Kabila ya bwana Sugu ndio wenyewe Mbeya. Nakueleza kwa kurudia, Ukabila una-play role kubwa sana kuupata UBUNGE nchi hii na sehemu kama Arumeru, Kilimanjaro yote, Kagera yote, Mbeya yote,... hauwambii kitu bila kuzingatia kigezo hiki.

wewe unaeifahamu mbeya sawa sawa hebu nitajie mbunge mwingine ukiacha sugu ambae kabila lake sio la pale mbeya na amewahi kushinda ubunge pale kutoka chama chochote unachokijua wewe..
 
Back
Top Bottom