Pendekezo: MSD wapate mshindani

Seriously speaking mkiongeleaga taasisi za serikali huwa najua they are always not serious yaani wote ni wale wale kama TANESCO tuu!
System yao ya uongozi imekaa kimagumashi alafu utarajie ufanisi.Watu wanapewa vyeo kama fadhila.
 
nadhani hospitali na mashirika ya kidini yameshajiundia ka-msd chao siku nyingi.ndio maana hatusikii ukosefu wa dawa ukiwasumbua.
 
Hivi kama mchele unapoisha nyumbani na mwenye nyumba akataarifiwa. Nani wa kulaumiwa? anayetoa hela ukanunuliwe au anayeenda kununua? Mtalaumu tu kuwa MSD utendaji mbovu lakini tatizo liko serikarilini. Hakuna ofisi inaweza kuendesha biashara kwa ufanisi wakati daily activities zake ni kukopesha tu bila kujua watalipwa lini. serikari inaweza kutenga bajeti ya mil 2 halafu ikatoa laki tano. Sasa MSD wakishindwa kufikia malengo utawalaumu. Muelewe mara nyingi MSD inabeba lawama za serikali.

Kama unabisha jiulize kwa nini wabunge walitulia baada ya kujue ukweli wa hali halisi ya ufanyaji kazi wa MSD.

Ni maoni yangu tu.
 
in general tatizo lipo serikalini kwa kushindwa kusimamia sera zake yenyewe, kuweza kusimamia financing ya dawa, na tatizo linaenda MSD kwa kushindwa kuwa efficient na kuwa innovative, labda tuongezee tu kwamba internal MSD processes could be improved

tukija kwenye watekelezaji wakuu wa public health supply system, the local government through district health management, hawa ndio wanaoharibu kabisa mfumo mzima, hawako makini kwenye usimamizi, hawana ujuzi, hawako accountable, wako corrupt - anaglia ma DT wanavyopenda emergency purchase kwa local suppliers wanaouza dawa zilizoibiwa humohumo mahospitali nk

We can go on and on and on.... ila kufupisha tu naweza kusema; matatizo ni

  • rushwa
  • governance
  • accountability
  • uelewa
  • sabotage ya system
  • wizi wa kupindukia wa pesa na dawa (hapa ntajadili pesa za NHIF badae)
  • wizara ya afya makao makuu kukumbatia wasiyoweza kwa ajili tu ya 10%
  • ujinga wa wanachi kutokujua haki zao za msingi

MSD bado haina structure ya kibiashara
 
Tatizo si MSD bali ni serikali yenyewe. Ni kweli kuwa hospitali zetu na zahanati pamoja na vituo vya afya havina dawa muda mwingi na vifaa tiba, au havipati kwa wakati, lakini tatizo ni serikali kutokulipa madeni kwa wakati.

Kama mtakumbuka bunge lililopita, wabunge walicharuka na kutaka msd ivunjwe au iwepo mbadala, hii ilipelekea kamati ya huduma za jamii kutembelea msd. Wabunge waliambiwa ukweli kuwa MSD wakati mara nyingi wanapeleka dawa na vifaa tiba kwa mkopo, na wanaidai serikali zaidi ya bilioni 40-60, ndio maana wabunge waliporudi bungeni waliishia kuiomba serikali kupiti wizara ya afya ilipe madeni yake ili kuongeza ufanisi. Kwa sasa baadhi ya mikoa MSD wanapeleka dawa mpaka vituoni, gharama zimeongezeka kwa MSD.

Lakini tatizo lingine ni la watendaji hasa wakurugenzi na DMOs kwa ujumla, unakuta kituo au hospitali haiagizi dawa kwa wakati au dawa zinapelekwa kwa DMO, lakini hazifiki vituoni kwa wakati sababu hakuna usafiri, hivyo kuwaumiza wananchi. Sehemu ambazo Dmos wanawajibika ipasavyo, hata pale ambapo dawa za MSD hazijafika, wamekuwa wakinunua dawa na vifaa tiba kwa pesa za mifuko ya bima kama CHF na NHIF, lakini kwa wakurugenzi na DMOs walafi hakuna wanachofanya. Mifano ipo pia, ukitembelea zahanati za wilaya za mbeya kama rungwe ni tofauti na ukitembelea zahanati na vituo vya afya vya Morogoro vijijini na kwingineko.

Kwa Dar es Salaam ni vioja, maana hospitali za Amana, Temeke na Mwananyamala wanategemea sana MSD, na pesa za mifuko ya bima ya afya zinakusanywa na kupelekwa manispaa, ili hospitali inunue dawa nje ya MSD inabidi wamwombe mkurugenzi na tenda itangazwe ndio dawa zikanunuliwe, ni ukiritimba mtupu.

Hivyo tatizo si MSD tu, ni serikali na the whole system need overhaul.

nakubaliana nawe kabisa kwa hili.ukiangalia juujuu unaweza ukafikiri wanaosababisha ukosefu wa wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu ni MSD wakati sio kweli kabisa.mfumo unaotumiwa na serikali katika kuagiza dawa na kufanya malipo huko MSD umesababisha madeni makubwa na matokeo yake imepelekea MSD kushindwa kufanya kazi yake vizuri kutokana na ukosefu wa fedha ya kutosha.
 
Tatizo si MSD bali ni serikali yenyewe. Ni kweli kuwa hospitali zetu na zahanati pamoja na vituo vya afya havina dawa muda mwingi na vifaa tiba, au havipati kwa wakati, lakini tatizo ni serikali kutokulipa madeni kwa wakati.

Kama mtakumbuka bunge lililopita, wabunge walicharuka na kutaka msd ivunjwe au iwepo mbadala, hii ilipelekea kamati ya huduma za jamii kutembelea msd. Wabunge waliambiwa ukweli kuwa MSD wakati mara nyingi wanapeleka dawa na vifaa tiba kwa mkopo, na wanaidai serikali zaidi ya bilioni 40-60, ndio maana wabunge waliporudi bungeni waliishia kuiomba serikali kupiti wizara ya afya ilipe madeni yake ili kuongeza ufanisi. Kwa sasa baadhi ya mikoa MSD wanapeleka dawa mpaka vituoni, gharama zimeongezeka kwa MSD.
Pamoja na badhi ya ukweli hapo kwenye kuidai serikali bilioni 60 umedanganya sana!!! acha hizo aisee
 
nakubaliana nawe kabisa kwa hili.ukiangalia juujuu unaweza ukafikiri wanaosababisha ukosefu wa wa dawa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu ni MSD wakati sio kweli kabisa.mfumo unaotumiwa na serikali katika kuagiza dawa na kufanya malipo huko MSD umesababisha madeni makubwa na matokeo yake imepelekea MSD kushindwa kufanya kazi yake vizuri kutokana na ukosefu wa fedha ya kutosha.

chanzo si msd, chanzo ni serikali na ulaji wa local government, peas ya NHIF tu inaweza kabisa kumaliza shida ya medical supplies nchini ila wanaiba sana

ila aliposema bil 60 kadanganya
 
Kwa kiasi kikubwa tatizo sio MSD, ni mfumo mzima wa wizara, mds ilaanzishwa kwa sheria ya bunge, na ikumbukwe kuwa MSD haiuzi madawa kama retail sales yani kwa yeyote tu, no bali inauza dawa kwa wateja ambao wizara ya afya imeelekeza na sehemu kubwa ya wateja hao wanalipiwa na serikali.

Sasa kama serikali anakuwa hawalipi msd hayo madeni makubwa hivyo unategemea msd afanyeje kwa ufanisi, maana serikali hiyo hiyo ndio imemwekea msd masharti ya kutokuwa na wateja wa rejareja mpaka apewe kibali na wizara.

Solution hapa ni serikali kulipia madeni yake MSD ili waweze ku plan ununuzi wa madawa ipasavyo, kwa sababu MSD na serikali waingia mkataba yani MSD nunua madawa, hifadhi, tawanya kwenye vitua, yeye serikali atalipa. Sasa shida inakuja huyu serikali anafunja utaratibu wa kutolipa, automatically MSD watacollapse
 
chanzo si msd, chanzo ni serikali na ulaji wa local government, peas ya NHIF tu inaweza kabisa kumaliza shida ya medical supplies nchini ila wanaiba sana

ila aliposema bil 60 kadanganya
MTM, nilipotoa figure hiyo nilisema ni 40-60 billioni, nakubaliana na wewe yawezekana ikawa si 60bilioni. Nimesahau figure exactly, lakini nilikuwepo wakati mkurugenzi wa MSD alipokuwa anawapa maelezo wabunge kamati ya huduma za jamii, na deni wanalodai MSD ni range hiyo.

Nikirudi kwa Meningitis,nadhani hujafanya utafiti wa kutosha. Huwezi ukaringanisha upatikanaji wa dawa hospitali binafsi na zile za serikali, mfumo wa utendaji ni tofauti sana. Wakati hospitali nyingi za serikali na zahanati zake, wananchi wanaokwenda kupata huduma wengi wana "exemptions" hospitali za binafsi hawaruhusu hili, unalipia na pesa wanayopata wanairudisha tena kwenda kununua dawa hata private famasi maana pesa wanayo, wakti hospitali za serikali na vituo vyake 60% to 80% wagonjwa hawajiwezi na wanapata dawa free, unategemea dawa ziwepo?

Pia huwezi kuwapa sifa NHIF, maana pesa zao ni makato moja kwa moja toka kwa wafanyakazi wa serikali, wapende wasipende wanakatwa tu, lakini hawana cha kuwasifia, ni mfumo tu umewasaidia. Utawasifia vipi NHIF wakati unakwenda hospitali unaambiwa dawa hakuna, unakwenda famasi pia hakuna? Tatizo unaangalia NHIF ukiwa dar na si vijijini au wilayani huko ambako walimu na kada nyingine, hawana mbadala wa Famasi za hospitali.
 
asilimia sitini ya mapato yanayotokana na NHIF hutakiwa kununuliwa dawa.tatizo local goverments haziwezi kununua dawa bila kupata list ya Out of stock kutoka msd.
Kuna wakati serikali inakuwa haijaweka fedha msd lakini local goverment inaweza kuchota sehemu ya mapato yake na kuamua kununulia dawa,tatizo ukienda huko msd watakwambia kwa kuwa una deni (ambalo kimsingi sio lako
)hawawezi kukupa dawa!kwa hiyo hapa halmashauri hata kama ilitaka kuspend cash ya sh milioni 5 inaweza kushindwa kufanya hivyo kwa kosa la serikali kutopeleka hela msd.
 
Tatizo ni MSD tu!

We mtu uunaagiza kopo 20 za amoxcilline kwa mfano wao wanakuletea kopo sita katika kituo cha afya wanakujazia BBE tin ambazo wewe uliagiza kwa uchache au pengine hukuagiza kabisa ili kufidia pesa yako kwa robo kwa vile vituo vinavyotumia mfumo wa indent system? Sasa huu ni wizi kabisa, kwanini wakuletee dawa ambazo wewe hukuagiza kabisa na huna wagonjwa watakaotumia kwa wingi? Hayo ma BBE nani atatumia? Yanaishia tu kuexpire pharmancy!

Kwahiyo, aje mshindani wa MSD, sasa hivi kila kitu cha afya kinatengewa shiling tatu milioni kwa robo mwaka; hizi ni fedha ndogo sana kwa kununulia vifaa vya tiba. Serikali iongeze bajeti zake! Halafu tunashindwa kuelewa hizi fedha za cost sharing na bima ya afya zinatumika vipi. Kulikuwa na umuhimu wa kuzitumia pale dawa zina pokwisha kabla ya MSD hawajaleta.
 
mkuu kama tatizo ni upatikanaji wa dawa
basi hapo ndipo tunapohitaji washindani wengi zaidi ili mmoja anapokosa mwungine awe nazo.

tuna vitu vitatu vya kuangalia,
  1. central governance - wizara/serikali
  2. operations - MSD
  3. clients understanding and usage of the system - halmashauris etc

unataka nifocus wapi??? maana hoja yako imechanganya vyote, ntakusaida tu
 
Tatizo ni MSD tu!

We mtu uunaagiza kopo 20 za amoxcilline kwa mfano wao wanakuletea kopo sita katika kituo cha afya wanakujazia BBE tin ambazo wewe uliagiza kwa uchache au pengine hukuagiza kabisa ili kufidia pesa yako kwa robo kwa vile vituo vinavyotumia mfumo wa indent system? Sasa huu ni wizi kabisa, kwanini wakuletee dawa ambazo wewe hukuagiza kabisa na huna wagonjwa watakaotumia kwa wingi? Hayo ma BBE nani atatumia? Yanaishia tu kuexpire pharmancy!

Kwahiyo, aje mshindani wa MSD, sasa hivi kila kitu cha afya kinatengewa shiling tatu milioni kwa robo mwaka; hizi ni fedha ndogo sana kwa kununulia vifaa vya tiba. Serikali iongeze bajeti zake! Halafu tunashindwa kuelewa hizi fedha za cost sharing na bima ya afya zinatumika vipi. Kulikuwa na umuhimu wa kuzitumia pale dawa zina pokwisha kabla ya MSD hawajaleta.

mkuu unajua kwamba 80% ya wanaoagiza hawajui their monthly consumption ya any commodity??? study zipo nizaonyesha over 95% ya hospitali zinaover order antibiotics?? fore reasons known to all health professionals ??

na unajua kuna right of rejection of anything brought by MSD na utalindwa na sheria?
 
MTM, nilipotoa figure hiyo nilisema ni 40-60 billioni, nakubaliana na wewe yawezekana ikawa si 60bilioni. Nimesahau figure exactly, lakini nilikuwepo wakati mkurugenzi wa MSD alipokuwa anawapa maelezo wabunge kamati ya huduma za jamii, na deni wanalodai MSD ni range hiyo.

Nikirudi kwa Meningitis,nadhani hujafanya utafiti wa kutosha. Huwezi ukaringanisha upatikanaji wa dawa hospitali binafsi na zile za serikali, mfumo wa utendaji ni tofauti sana. Wakati hospitali nyingi za serikali na zahanati zake, wananchi wanaokwenda kupata huduma wengi wana "exemptions" hospitali za binafsi hawaruhusu hili, unalipia na pesa wanayopata wanairudisha tena kwenda kununua dawa hata private famasi maana pesa wanayo, wakti hospitali za serikali na vituo vyake 60% to 80% wagonjwa hawajiwezi na wanapata dawa free, unategemea dawa ziwepo?

Pia huwezi kuwapa sifa NHIF, maana pesa zao ni makato moja kwa moja toka kwa wafanyakazi wa serikali, wapende wasipende wanakatwa tu, lakini hawana cha kuwasifia, ni mfumo tu umewasaidia. Utawasifia vipi NHIF wakati unakwenda hospitali unaambiwa dawa hakuna, unakwenda famasi pia hakuna? Tatizo unaangalia NHIF ukiwa dar na si vijijini au wilayani huko ambako walimu na kada nyingine, hawana mbadala wa Famasi za hospitali.

Thanks

now kwenye issue ya NHIF, ninazungumzia zile pesa kuwa allocated kwenye medical insurance; labda niweke hivi
  • NHIF wanalipa vituo vya afya kwa huduma, na kusema ukweli ile pesa inge-cover over 80% ya basic clinical and commodity needs [kinachotakiwa sasa ni kusimamia hizi pesa katika level ya health facility, NHIF na wilayani]
  • sijawasifia kwa kukata pesa, ile ni kazi, huwezi kusifiwa kwa kutimiza wajibu, nimesema pesa yao inaweza.... just FYI, kuna bad ring kati ya NHIF na watendaji wa mahospitali na wilaya inayoiba pesa kwa ku-over report cases na dawa (nyingine hutoka kwenye miradi mingine na zile zinazonunuliwa na mfuko wa wilaya)...
  • pia kusema 60-80% wanapata dawa free ni other misinformation - check your facts

MSD have to blamed pia kwani ukiangalia ni zaidi ya miaka kumi sasa hawajabadili chochote kwenye utendaji kuaddress recurrent challenges kwenye supply system; hawajui nini kipo kwenye godowns zao, hawana wataalam wa dawa wala vifaa tiba wa kutosha, hawaangalii mteja, wanaangalia walivyofundishwa shule nk

it is complicated, but we cant rely on lies made by MSD reps kuwatetea
 
Nikirudi kwa Meningitis, nadhani hujafanya utafiti wa kutosha. Huwezi ukaringanisha upatikanaji wa dawa hospitali binafsi na zile za serikali, mfumo wa utendaji ni tofauti sana. Wakati hospitali nyingi za serikali na zahanati zake, wananchi wanaokwenda kupata huduma wengi wana "exemptions" hospitali za binafsi hawaruhusu hili, unalipia na pesa wanayopata wanairudisha tena kwenda kununua dawa hata private famasi maana pesa wanayo, wakti hospitali za serikali na vituo vyake 60% to 80% wagonjwa hawajiwezi na wanapata dawa free, unategemea dawa ziwepo?
Exemptions ni mzigo mwingine uliokaa kisiasa.

Ilipoanzishwa hii kitu tukaambiwa serikali itakuwa inatoa fungu vituoni kufidia.

...IKAWA UTANI MWINGINE WA WANASIASA WETU.
 
  • NHIF wanalipa vituo vya afya kwa huduma, na kusema ukweli ile pesa inge-cover over 80% ya basic clinical and commodity needs [kinachotakiwa sasa ni kusimamia hizi pesa katika level ya health facility, NHIF na wilayani]
  • sijawasifia kwa kukata pesa, ile ni kazi, huwezi kusifiwa kwa kutimiza wajibu, nimesema pesa yao inaweza.... just FYI, kuna bad ring kati ya NHIF na watendaji wa mahospitali na wilaya inayoiba pesa kwa ku-over report cases na dawa (nyingine hutoka kwenye miradi mingine na zile zinazonunuliwa na mfuko wa wilaya)...
  • pia kusema 60-80% wanapata dawa free ni other misinformation - check your facts
Mkuu achana na data za huko kwenu mijini. Unajua Sagara - Makopo kuna wanachama wangapi wa NHIF ? Unajua Sagara Makopo kuna wazee wangapi na watoto wangapi wanaougua kila siku?

Kaka huku vijijini hakuna uzazi wa mpango,hakuna institutes za kutuletea NHIF members, zaidi ya walimu wa 5 wa pri skuli na wawili wa sec skuli. Sasa hiyo 80% through NHIF itatoka wapi?!
 
mkuu dawa ya sikio

labda niombe uwe unasoma na kuelewa kidogo tu.... context ya NHIF itabaki kuwa ya NHIF na target itakua ya wateja wake. i have worked in a rural program kwahiyo najua kwamba walio vijijini kabisa hawana NHIF lakini pia si vibaya kujua kwamba thier health seeking behavior ikoje na uwezo wao ukoje, na kwa ujumla ni dawa gani au medical supplies zipi zinatumika huko periphery, in short kuna ile pareto theory ya 80/20.... waweza wakawa 80% vijijini lakini matumizi yao yakawa madogo hivyo kuweza kufidiwa kirahisi na walio mjini: how? the policy ya nchi inarestrict aina fulani ya dawa au supplies kwenda chiya ya health center level, nk

tukija kwenye financing ya commodities, tuna NHIF, cnetral funds, council funds (combined kwenye basket au vertical) tuna donor funds, tuna other community financing na hata donations, hizi zote zaweza kuchangia kewnye mfumo

now back to MSD; kuna vitu viwili vikubwa tuangalie... kwa kwenda juu, je anapata pesa stahili kutokana na huduma yake?? hii ni ngumu kujua mojakwamoja kutokana na mfumo wa usiri wa nchi yetu hadi shida itokee na wanasias waingilie, ingawa inapingana na good governance

tukienda kwa chini, je anajua wateja wanataka nini??? kipimo ni kidogo tu... fanyeni test ya service level tena mawilayani; unachotaka vs. ulichopata, halafu categorize priority commoditeis na ujua anafikia wapi... linganisha na takwimu wanazotoa wao, mara nyingi zinatofautiana... maana yake nini?? its either hawajui wateja wanataka nini?? au wanaamua kupima utendaji wao kwa kigezo watakacho, all in all ni kosa kubwa sana.

tukirudi kenye NHIF, ni vigumu kujenga hoja iwapo hatujui kama wana direct agrement na MSD on certain supplies (they should know by now the category A and B of the health commodities used, because wanarudishiwa ripoti za matumizi ya dawa) ili kusaidia kuboresha.... binafsi naamini kabisa halmashauri zinakula tu pesa za NHIF ni kiasi kidogo labda 50% ndio inafanya kazi stahiki

there is a book to write about MSD coz similar problems zipo kwa over 10 years pamoja na mabadiliko mbalimbali ya sera, structure na watendaji..... lets have a structured discussion kwenye hii, na tuchague pa kuanzia
 
***
Sasa nimekuelewa vizuri Mkuu! Thanx.
 
wafamasia na baadhi ya wafanyakazi wa msd ni mafisadi.kuna ka mchezo cha kuandika bidhaa fulani ni out of stock wakati bidhaa hiyo ipo.hii hupelekea manunuzi kufanyika nje ya msd kwa bei za juu sana.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
nasikitika kuona kamati za bunge zikipoozwa na maneno ya ulaghai kutoka msd
 
Back
Top Bottom