Pendekezo: MSD wapate mshindani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendekezo: MSD wapate mshindani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meningitis, Mar 17, 2012.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ni wiki kama moja hivi tumetoka kwenye mgomo wa kihistoria nchini,mgomo wa madaktari.kuna madai mengi yaliwasilishwa na madaktari ingawa kipropaganda tuliishia kuona madai mawili yakiongelewa sana,ni kuhusu maslahi na kuondolewa kwa mawaziri wa afya.

  Kwa sasa hali ni ''shwari'' ingawa sina uhakika na tija ya ufanyaji kazi huko mahospitalini.

  Kuna dai moja la msingi ambalo sikutegemea serikali au wananchi kulipuuzia kama kweli tunataka maendeleo. Dai hilo ni kuhusu kuboreshwa kwa mazingira ya kazi hasa hasa katika kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana mahospitalini.

  MSD ni chombo cha serikali kilichopewa dhamana ya kuhakikisha dawa na vifaa tiba muhimu na bora vinapatikana katika mahospitali yetu.

  Kumekuwepo na malalamiko mengi yanayoshutumu utendaji kazi wa MSD lakinu sijaona hatua stahiki iliyochukuliwa mpaka sasa.

  Kwa maoni yangu naona ni wakati muafaka wadau mbalimbali kuishinikiza serukali itoe fursa ya kumpata mshindani wa MSD. Hii ni njia muhimu ya kuhakikisha tunapata huduma nzuri hasa katika hospitali za serikali.
   
 2. m

  msafi Senior Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tatizo si MSD bali ni serikali yenyewe. Ni kweli kuwa hospitali zetu na zahanati pamoja na vituo vya afya havina dawa muda mwingi na vifaa tiba, au havipati kwa wakati, lakini tatizo ni serikali kutokulipa madeni kwa wakati.

  Kama mtakumbuka bunge lililopita, wabunge walicharuka na kutaka msd ivunjwe au iwepo mbadala, hii ilipelekea kamati ya huduma za jamii kutembelea msd. Wabunge waliambiwa ukweli kuwa MSD wakati mara nyingi wanapeleka dawa na vifaa tiba kwa mkopo, na wanaidai serikali zaidi ya bilioni 40-60, ndio maana wabunge waliporudi bungeni waliishia kuiomba serikali kupiti wizara ya afya ilipe madeni yake ili kuongeza ufanisi. Kwa sasa baadhi ya mikoa MSD wanapeleka dawa mpaka vituoni, gharama zimeongezeka kwa MSD.

  Lakini tatizo lingine ni la watendaji hasa wakurugenzi na DMOs kwa ujumla, unakuta kituo au hospitali haiagizi dawa kwa wakati au dawa zinapelekwa kwa DMO, lakini hazifiki vituoni kwa wakati sababu hakuna usafiri, hivyo kuwaumiza wananchi. Sehemu ambazo Dmos wanawajibika ipasavyo, hata pale ambapo dawa za MSD hazijafika, wamekuwa wakinunua dawa na vifaa tiba kwa pesa za mifuko ya bima kama CHF na NHIF, lakini kwa wakurugenzi na DMOs walafi hakuna wanachofanya. Mifano ipo pia, ukitembelea zahanati za wilaya za mbeya kama rungwe ni tofauti na ukitembelea zahanati na vituo vya afya vya Morogoro vijijini na kwingineko.

  Kwa Dar es Salaam ni vioja, maana hospitali za Amana, Temeke na Mwananyamala wanategemea sana MSD, na pesa za mifuko ya bima ya afya zinakusanywa na kupelekwa manispaa, ili hospitali inunue dawa nje ya MSD inabidi wamwombe mkurugenzi na tenda itangazwe ndio dawa zikanunuliwe, ni ukiritimba mtupu.

  Hivyo tatizo si MSD tu, ni serikali na the whole system need overhaul.
   
 3. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nitawatetea MSD kwa hili:

  Kwa miaka zaidi ya 6 kiwango kinachotengwa na serikali MSD kwa kila kituo kimekuwa kilekile. Hiyo haizingatii mfumko wa bei za dawa uliopo na ongezeko la watu.

  Km toka 2006 kila zahanati hupelekewa msd 1.2m kwa kila robo mwaka. Hiyo 2006 angalau kiasi zilitosha,lakini sio sasa. Mfano 2006 tabs Quinine 1000T ilikuwa 30,000/= hivi sasa ni zaidi ya 80,000/= (ongezeko la 267% ! ).

  Mwisho wa siku utakuta kituo kinadaiwa zaidi ya 10m msd. Hapo kitaendelewa kuletewa dawa kwa "huruma" ya MSD tu.

  All in all kwa hali hii hata akija mbadala wa MSD tatizo litabaki palepale endapo serikali haitalipa madeni na kuongeza fungu.
   
 4. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Umejitahidi kuwateta MSD ile mbaya lakini huu utetezi wako ndio wanaoutumia MSD kuhadaa watu.hayo uliyoyasema yana mchango kidogo katika suala la ukosefu wa dawa na vifaa tiba.

  Hivi ni kweli halmashauri zote pamoja na mahospitali ya dini zinakosa fedha za kununulia dawa? Jibu ni hapana.

  Tatizo la MSD ni ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika bohari zake. Serikali inaweza kutuma fedha nyingi sana msd lakini halmashauri zikienda kununua unakuta neno out ,pili unaweza kuambiwa in lakini haipo kwenye bohari ya zonal yako mfano in lakini sio Dar ni Moshi. Hili ni tatizo tusilikwepe, tuangalie hospitali binafsi zinavyokuwa na dawa sababu ni moja tu, wana uhuru wa kununua dawa kutoka maduka na sehemu mbalimbali.

  Hebu tujaribu kuweka washindani kama ilivyo kwenye kampuni za simu uone.
   
 5. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani MSD inafanya biashara na serikali pekee? Mbona hospitali au halmashauri zina uwezo wa kununua dawa kupitia vyanzo vyake wakati wanasubiri fedha kutoka serikalini, lakini kinachotokea ni kukosekana kwa dawa hapo MSD dawa ambazo ukienda maduka binafsi unazipata.
   
 6. K

  Kichoncho Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuwa hospitali za serikali zina upungufu mkubwa wa madawa na vifaa tiba.MSD inaweza kuwa na mapungufu yake ya kiutendaji, hata hivyo hali hii kwa kiasi kikubwa inachangiwa na matatizo yaliyomo katika mfumo mzima wa wizara ya afya, kama ifuatavyo:

  1. Bajeti kwa ajili ya kununulia madawa na vifaa tiba ni ndogo na haiendani na mahitaji halisi. Kwa mfano; mwaka 2007 MSD ilifanya zoezi la maoteo (demand forecasting and quantification) kwa utaratibu wa kufanya makadirio kwa kutumia bajeti ya hospitali moja moja(budget based ordering) ,lakini kilichotokea ni kwamba hayo mahitaji yalikuwa chini sana cha hali halisi.
  2. Hata hicho kiasi kidogo kilichotengwa na serikali kwa ajili ya mahitaji ya hospitali hakifiki MSD kwa wakati hivyo kuilazimisha MSD kuzikopesha hospital na kuzaa deni la karibu bilion 42 ambalo linatishia uhai wa MSD. Kuna tetesi kuwa pesa kwa ajili ya mwaka 2011/12 ndio zimepelekwa MSD mwezi march 2012 (badala ya july 2011) baada ya mgomo wa madaktari kuitikisa serikali, you can imagine this situation!
  3. Sehemu kubwa ya kiasi hicho kidogo cha madawa na vifaa tiba kutoka MSD kinaishia kufisadiwa na BAADHI ya watendaji (baadhi yawafamasia na manesi ) wasio waaminifu katika hospitali za serikali. Kwa hiyo, serikali inatakiwa ibuni utaratibu wa kuwabana watendaji wasio waaminifu badala ya kutegemea 'ledger' ambazo zinachakachuliwa.
   
 7. K

  Kichoncho Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Meningitis,

  Kumbuka MSD inategemea pesa hizo kutoka serikalini ili izizungushe (revolving fund) na kununulia madawa kwa wakati, vinginevyo supply system yake inakuwa destabilized.
   
 8. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,463
  Trophy Points: 280
  MSD ni wazembe kama TANESCO, EWURA, TTCL na Posta. Visingizio vingiii. ARV zinexpire wakati wagonjwa wanakufa.

  Nasikia MSD hawana kifaa hata kimoja kwa matibabu ya macho, kupata gloves na gauze ni ndoto ukienda hapo MSD; nashauri ifutwe.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 9. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Meningitis,

  Maoni yako ya kutaka MSD ipate mshindani ni dhahiri kwamba yamejikita katika mtazamo wa kibiashara ambapo msingi mkubwa ni Faida. Usichoelewa ni kwamba msingi wa MSD ni kutoa huduma na kujiendesha. Huyo mshindani unayemtaka unategemea atapata faida kwa kupeleka dawa na vifaa Tiba Nambendo au kwa kupiga panga pesa za dawa zinazotengwa na hazina Kwa mtindo Wa EPA? Fikiria hakuna aliyekatazwa kupeleka dawa na kuziuza Kokote nchini mbona sioni famasi Buhemba au Kiterere?

  Mkuu usiimbe wimbo wa wafanyabiashara ya dawa utaua watanzania walio maskini ambao huwaoni kwa kukaa mjini.

  "MSD might not be efficient but your visibility of a solution from your suggestion is Myopic big time" ipecacuanha
   
 10. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu ni kweli, ila bado nailaumu serikali, hivi hizo bilioni ngapi inazodaiwa ingezitupia pale MSD, kusingekuwa na mabadiliko ya hizo OS Items zinazozidi IN items kwa sasa?

  Hivi karibuni tulikuwa na kikao na Meneja wa kanda(MSD Central Zone). Alisema serikali ikiendelea kukacha madeni si ajabu nayo msd ika collapse. Msd iko kibiashara zaidi na mteja wake mkubwa ni serikali.

  Ok ! Halmashauri zina mafungu mengine lakini kwa mfumo uliopo uliojaa mambo ya kisiasa,ukiondoa bima nyingine, hivi viwango vya CHF vinakidhi nini kwa hali halisi ? Familia ya watu 9 hadi 10,wanalipia elfu 10 au 15 kwa mwaka! Au user fee,mtu analipa elfu 1 au 2 kwa huduma zote afikapo kituoni ! Nani anapaswa kufidia gharama ya ziada kama sio hii serikali legelege ?!

  Hivi karibuni Halmashauri yetu iliamua kununua dawa outside msd. Bajeti ya Mfamasia wa wilaya ilihitaji 120m,alipoipeleka bodi ya Afya (w),akapewa 50m tu!

  HAKUNA FEDHA.

  Naunga Mkono, MSD watafutiwe washindani. Hata sisi tulimwambia Mwakilishi wa Wizara siku ya kikao na MSD. LAKINI LAZIMA SERIKALI IFANYE KITU CHA MAANA.
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  MSD inafanya biashara na wala haitoi huduma tuache ujanjaujanja wa maneno.

  Watanzania tumeendelea kuwa wanafiki katika kitu kimoja, eti elimu na afya ni bure!? Kumbe tunategemea msaada, dunia ya leo inaendeshwa na uchumi wa soko na si vinginevyo Tanzania hatuwezi kuukata ukweli huu.

  Labda nikuulize; kuna huduma ngapi za msingi ambazo leo hii zinaendeshwa kibiashara? Fikiria kuhusu umeme, maji, sukari na nguo...jibu unalo.

  Ninachokitaka sio kuifuta MSD bali kumueka mshindani na hivyo kutoa fursa kwa wateja kuona wapi wana huduma nzuri. Kwa sasa MSD haiwezi kutoa huduma njema kwa sababu inajua iwe na dawa isiwe na dawa fedha yake ipo.

  Chukulia mfano wa bima ya afya (NHIF) imelazimishwa kuperform vizuri kwa kuwa kuna mifuko ya namna hii inashindana nayo mfano NSSF, AAR n.k

  Sasa, kama NHIF inaweza kufanikiwa katika eneo hilihili la afya ''huduma'' iweje MSD ishindwe?

  Kwanini MSD isiweke mpango wa kupeleka viduka vyake huko vijini kama kweli ni mtoaji huduma?

  Mtazamo wangu umeuona ni myopic kwa sababu na wewe umeuangalia kimyopic myopic. Tanua mawazo kidogo halafu fikiria sana siku wafadhili watakaponyanyua virago utafanyaje?
   
 12. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Pamoja na hayo mapungufu ya kucheleweshwa kwa fedha lakini tatizo ni MSD. Wafanyabiashara wengi hawalipwi kwa wakati lakini wameendelea ku-survive.

  Kinachonishangaza ni kwamba leo hii utasikia MSD haina hela lakini leo hiihii utasikia mkurugenzi wa MSD kanda ya mashariki akabidhi kitita cha milioni kadhaa kuisaidia timu ya taifa ya wanawake. Are we serious?

  Bado naendelea na ombi langu la kutaka MSD ipatiwe mshindani, ikiwa mi sehemu ya kuboresha huduma mahospitalini.
   
 13. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Katika bajeti ya mwaka huu, MSD ili waweze kuhudumia zahanati zote nchini, bajeti yao ilikuwa ni tshs. 60 bilioni. Kwa hiyo serikali ilipashwa kutoa tshs. Bil 60 kwa MSD ili MSD wapeleke dawa vijijini, but as of now serikali imewapa MSD tshs. Bilioni 6 tu.

  Labda, MSD wakaibe dawa ili waizagawe bure. Tatizo hapa ni mkulo hapeleki kabisa hela MSD.
   
 14. K

  Kichoncho Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  meningitis,

  Inaonekana hujafanya utafiti kwani ulipaswa kujua kuwa 'NHIF' ina enjoy monopoly market kwani wateja wake ambao wote wapo katika ajira za taasisi za serikali hawana option ya kuhamia katika bima zingine kama AAR n.k

  NHIF nayo katika huduma ina mapungufu yake kama vile doctors kulazimika ku prescribe dawa zile tu ambazo zipo kwenye list ya NHIF, hata kama siyo preference ya daktari husika.

  MSD haifanyi retail business hivyo haiwezi kufungua viduka vidogo vijijini.

  Ni kweli MSD inatoa huduma make mwaka jana katika baadhi ya mikoa ilianza kupeleka dawa moja kwa moja (direct delivery) vijijini badala ya kuishia wilayani kwa DMO's ambako kulikuwa na ucheleweshaji. Hata hivyo, inasemekana kuwa hiyo direct delivery siyo economically justifiable kutokana na uduni wa miundombinu vijijini na huenda serikali isifidie gharama hizo ipasavyo lakini MSD inalazimika kupeleka vijijini ili kutoa huduma.

  Je, ni wafanyabiashara wangapi wako tayari kufanya kazi ya hasara?
   
 15. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,463
  Trophy Points: 280
  Kwasababu tumeingia kwenye soko la pamoja la Jumuia ya Afrika Mashariki, basi ni wakati muafaka wa kuruhusu mashirika kama haya kutoka nchi wanachama kuleta ushindani na tija nchini.
   
 16. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kwanini NHIF ina-enjoy monopoly market in the presence of washindani kama hao niliowataja? NHIF bila washindani ingekuwa kama MSD. Hebu sasa tujaribu kuweka washindani kwa msd tuone. Hata NHIF hawapewi hela kwa wakati, kwanini wao wako vizuri?

  Kwa uzoefu wangu, halmashauri zina uwezo wa kusambaza hizo dawa ni isitoshe ni jambo ninaloliona likitokea sasa, kwa hiyo hiki hakiwezi kuwa kisingizio. Tatizo kubwa ni ukosefu wa dawa MSD hata kama serikali imeshatuma hela MSD na tatizo hili ni la siku nyingi sio miaka hii ambayo kumekuwa na upungufu wa fedha.

  MSD haikidhi mahitaji kwa sababu ya kukosa ushindani.
   
 17. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Kuna dawa au vifaa tiba havipatikani kabisa MSD. Havina code number kabisa, tatizo liko wapi? Kwanini watu binafsi waweze ku-supply hivi vifaa au dawa halafu MSD ishindwe?

  Hospitali nyingi za binafsi zinanunua dawa hizi nje ya nchi na vilevile hospitali za serikali zinanunua hizi dawa au vifaa kwa wauzaji binafsi. Kwanini MSD isiwe nazo? Ina maana MSD imemlenga mteja mmoja (serikali) pekee? Kwanini MSD inaachia hii fursa ya kujiongezea kipato?
   
 18. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Katika ushindani huu minaoupendekeza MSD itakuwa na advantage kadhaa, moja ni goverment subsidasation na nyingine ni wateja wengi kutoka serikalini.

  Tusiogope changamoto
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni serikali kwa kiasi kikubwa ila nadhani MSD nao wana some share of spoil
   
 20. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Serikali kuu ina tatizo katika kupeleka hela kwa wakati katika maeneo yote. Hata halmashauri hazipati ruzuku kwa wakati lakini kwa kutumia ubunifu zinaweza kutekeleza miradi mbalimbali. Sasa kwanini MSD ilalamikie jambo hilo kama ndio tatizo la wao kutoa huduma mbovu?

  Kwa maoni yangu taasisi za serikali zinatakiwa kupewa msaada wa kuanzia na baada ya hapo lazima zibuni mikakati ya sustainability kitu ambacho MSD wanalegalega kwa kuwa hawana mshindani.
   
Loading...