DAWA YA SIKIO
JF-Expert Member
- Dec 8, 2011
- 979
- 180
Narudia,Mkuu,
Pamoja na hayo mapungufu ya kucheleweshwa kwa fedha lakini tatizo ni MSD. Wafanyabiashara wengi hawalipwi kwa wakati lakini wameendelea ku-survive.
Kinachonishangaza ni kwamba leo hii utasikia MSD haina hela lakini leo hiihii utasikia mkurugenzi wa MSD kanda ya mashariki akabidhi kitita cha milioni kadhaa kuisaidia timu ya taifa ya wanawake. Are we serious?
Bado naendelea na ombi langu la kutaka MSD ipatiwe mshindani, ikiwa mi sehemu ya kuboresha huduma mahospitalini.
Kwa watoa huduma za afya tulio wengi kilio chetu ni kama chako mkuu. Kikubwa tukiamini MSD ni ya "wakubwa", ndo maana wana kiburi. Lakini kabla ya kuruhusu washindani serikali iandae mazingira mazuri. Huwezi kuendesha zahanati hata kwa 3m kwa robo mwaka achia mbali hiyo 1.2m ya Mbunge wangu Mponda na Dr Nkya. Tutaendelea kutukanwa na wananchi tunauza dawa zao hadi lini ?! Kumbe wakutukanwa ni Mponda, Mkullo na nani sijui. Zamani watu walikuwa wanapiga dili hizo, lakini siku hizi ukipokea mzigo wa miezi mi3 toka MSD unashika tama tu. Wiki 2 tu umeisha, unatamani ufunge kituo kwa aibu! Frustrations zinaanzia hapo.
....MSD kusaidia timu ni issue ndogo tu Mkuu. MSD haijafikia hata hatua za kushindwa kulipa mishahara wafanyakazi. MSD haishindwi kutoa 10m kusaidia timu lakini 200m ni upuuzi tu kuendesha shirika kama MSD.
Nimesoma post jamaa wanahitaji kulipwa 60 billions ili watafute uongo mwingine na sio huu wa madeni. Walipwe basi ili waje na single nyingine masikioni mwetu (kama).