Pendekezo: Mbinu Mpya Ya Kumbana Mkapa

S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,138
82
Kwa sababu sioni Mtanzania mwandishi au mtu wa kawaida aweze kufanya la zaidi....napendekeza yafuatayo.

Maoni yangu; kwa nini tusikusanye makala zote za magazeti ya Thisday na mengine yaliyoaandika mtitiriko wa Skendo za Mkapa then tuzitume kwenda kwenye Media zote zinazojulikana duniani ikiwamo BBC. Mtazamo wangu ni kuwa huenda kuna mwandishi wa habari au mwana documentary atayekubali kufanya story ya uraisi wake. Naamini kwa UK hii ina nafasi nzuri ya kufanikiwa kwani Mkapa alikuwa mmoja wa wajumbe kwenye Africa Comm chini ya Tony Blair, iliyochunguza na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondoa umaskini barani Africa.

Iwapo hakutatokea mwandishi atayekubali kutoa TV documentary au kuandika makala ndefu kwenye media za hawa wafadhili wa bajeti zetu. Kwa kiwango cha chini kabisa angalau tutakuwa tumejaribu na yeye atakosa usingizi kama watanzania wenzetu wanavyokosa usingizi kwa ugumu wa maisha.

Natoa hoja...
 
Nadhani hakuna muda tena wa kutoa hoja na kuijadili, kwa kuwa nakala zote za THISDAY na mengineyo kuhusu Mkapa yako humu JF katika ile thread ya JF Special kuhusu Mkapa, basi kwa kuanzia Yebo Yebo, zitume moja kwa moja kokote unakoamini wanaweza kuzisambaza katika vyombo vyao, na mwingine yeyote afanye vivyo hivyo, naamini ujumbe utafika tu kama haujafika
 
Tukishindwa yote nadhani ipo haja ya kucheza sinema kama ile ya Idd Amin ama Darwin's Nightmare labda ndio dunia itaweza kutusikia. Mkimtaka mtu anayefanana na Mkapa kama pacha wake yupo tayari na namjua vizuri. hapo labda Mkapa ataweka madai yake mahakamani kupinga shutuma hizo na kisheria ( za kimataifa) atakuwa kavua hiyo immunity yake. Ni lazima yeye aonyeshe kuwa habari hizo ni za Uongo!.

No jamani huu ubabe umefika mbali sana tena kwa kuulizia tu yule mwandishi wa habari na Mlinzi walikuwa wamesongwa na sol la Darwin's nightmare.. nini hatima yao?... nachofahamu mimi kwa uhakika ni kwamba yule mhindi mwenye kiwanda cha samaki ndio kesha kuwa mufilisi baada ya kufungiwa. Kosa lake ni kukubali kuhojiwa ktk sinema ambayo pamoja na kwamba ilikuwa na ukweli.. serikali haikutaka utoke nje!..Yametokea wakati wa Mkapa na JK alikuwa mbele kufunika kombe!.. yote haya tunayasahau hata kama yaliwekwa ktk picha ya documentary!

Kizuri kilichotokana na sinema hiyo ni kwamba hakuna tena mapanki kama chakula cha wananchi wa Mwanza.

Sasa hivi mapanki yanatengeneza chakula cha kuku.
 
Nadhani hii imekaa vizuri,hili likifanikiwa lazima ajitokeze ajibu.
 
Mnanipa furaha sana Watanzania wenzangu katika kumbana huyu fisadi, mjilimbikizia mali na kama sikosei mla rushwa anayejificha nyuma ya kibanda cha NIACHENI NIMESHASTAAFU na KATIBA BOMU inayowalinda watenda maovu.

Alishawahi kututukana kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikiri tunawaonea gere wale wenye mafanikio.

Sasa, tumuonyeshe huyu kwamba Watanzania si wavivu wa kufikiri na siku zote tunayafurahia mafanikio ya Mtanzania yeyote yule kama yamepatikana katika njia za halali na sio ufisadi, ula rushwa na kutumia madaraka kujilimbikizia mali.
 
Huyu mkuu lazima anaishi maisha ya taabu sana sasa hivi, maana wwe kila mahali nwananchi wanakuandama tu, hivi ni hela gani duniani inaweza kukupa usingizi na mashambulizi yote yanayoendelea bongo, against huyu Mkapa?

Kisheria na kisiasa, he isin big trouble regardless ya katiba yetu inavyosema, maana sasa hivi politically immunity yake inategemea Muungwana, kwa hiyo anaweza kum-sacrifice kwa sheria ili kuzima kelele za mafisadi, kwenye siasa hakuna guarantees, kama anafikiri yataisha hivi hivi tu basi anajidanganya sana, yeye cha muhimu ni kwenda mahakamani tu, ili akaseme ukweli maana huenda anasingiziwa tu!

Otherwise, tutaendelea tu kupiga filimbi mpaka kieleweke!
 
Whatever Nche Nkapa display ni Image ya majorityleadres wa nchi za Dunia ya tatu.

Leaders are for gaining their economic muscles. wanachoshindana ni yupi katafuna nyingi. Na yupi kajilimbikizia nyingi. Tena Good enough Mkapa yupo katika kinyang'anyiro cha Mapeza ya Celetel Mo Bilions. Ila si Uuungwana hata kidogo kutojisafisha jina lako unapotuhumiwa kuwa mfisadi.

Je Poor JK, what lesson is he going to learn? atakubali aondoke kapuku? si unaona anavyohangaik ana ziara nje, do you think 100% ni taifa? Who knows? Labda anatengeneza nia zake vilevile maana Usiri ni mwingi katika sirikali zetu. Mawaziri mikoani Rais Ulaya, amarika na Asia. Mhh ndiyo mtaji huo.

I want at thge end of the financial yr wananci waelezwe Ziara za Rais zilicost kiwasi gani na mawaziri kueleza bajeti zilicost kiasi gani. na je nchi ilinufaika vipi na matembezi hayo. Good luck
 
Maarifa,
Shukran sana kwa mchango wako na hii ndio maana halisi ya madai ya wananchi.
Kitu kinachotushtua zaidi ni future ya nchi yetu ikiwa mwanzo wenyewe ndio huo. Leo Mkapa kachukua mifedha na kaachiwa huru kwa sababu alikuwa rais , kesho JK na wengine watafuata kugombea urais kwa malengo hayo hayo wakifahamu kwamba wanalindwa na katiba.
Marehemu baba wa Taifa Mwl. JKN alifahamu mapungufu haya ya katiba na hata kudiriki kusema katiba inampa nguvu kubwa sana kiasi kwamba anaweza kuwa dikteta..
Kwa bahati yeye Mwl. aliweza kuwa dikteta wa kisiasa lakini hakufahamu kwamba mabadiliko ya mfumo wetu wa kisiasa yamebeba bado nguvu za Udikteta toka ktk Ujamaa na kuwa ktk Uchumi.
 
Nadhani hili wazo ni zuri sana la kumbana huyu nguchiro anayeitwa Mkapa na ambaye Watanzania walipata bahati mbaya ya kuongozwa naye. And what about kumuomba gwiji la kesi Tanzania i.e mchungaji Mtikila kuangalia uwezekano wa kuwatuma mawakili wake wavurumishe kesi dhidi hili dubwana? Hilo linaweza lisifanikishe kumfikisha kizimbani, lakini the fact kwamba mahakama kuu itafungua jalada la kesi dhidi ya Mkapa, that alone will be something to celebrate for.
 
Kuact movie kama ya darwins nightmare, mnadhani kutasaidia chochote ? kuna watu wapo mbele kwa kuzima moto cheche kabla hazijawa skendo kubwa, mfano mzuri ni hiyo dokyumentari ya darwin ilikuja kwa kishindo, then what was next ? samahani to be the bearer of the bad news, tanzania sasa hivi huwezi kufanya movie yoyote bila kupewa ruhusa/kibali then ikakubaliwa na serikali which was a mandate done after the documentary of darwin nightmare was introduced, sasa mnadhani mnaweza kitu hapo ???????????????
 
Mkuu Kada,

Unaona kuna namna nyingine inayoweza kutumika...nia kubwa iwe kufikisha ujumbe huu wa ufisadi wa Mkapa kwa watu wengi Tanzania na duniani kwa ujumla...yaani mpaka kule Davos alikokuwa akiongea kwa badaha kama kiongozi bora nao wajue kuwa huyu mtu ana tuhuma za kuwajibu Watanzania. Hebu mwaga maono yako na wewe kama unaona hiyo documentary itapigwa stop. Ila mimi naona hata kusambaza zile article za magazeti ni silaha nzuri tu pia ni sawa na kupanda mbegu huwezi jua kama unavuna au zitaliwa na wadudu.
 
Tukishindwa yote nadhani ipo haja ya kucheza sinema kama ile ya Idd Amin ama Darwin's Nightmare labda ndio dunia itaweza kutusikia. Mkimtaka mtu anayefanana na Mkapa kama pacha wake yupo tayari na namjua vizuri. hapo labda Mkapa ataweka madai yake mahakamani kupinga shutuma hizo na kisheria ( za kimataifa) atakuwa kavua hiyo immunity yake. Ni lazima yeye aonyeshe kuwa habari hizo ni za Uongo!.
No jamani huu ubabe umefika mbali sana tena kwa kuulizia tu yule mwandishi wa habari na Mlinzi walikuwa wamesongwa na sol la Darwin's nightmare.. nini hatima yao?... nachofahamu mimi kwa uhakika ni kwamba yule mhindi mwenye kiwanda cha samaki ndio kesha kuwa mufilisi baada ya kufungiwa. Kosa lake ni kukubali kuhojiwa ktk sinema ambayo pamoja na kwamba ilikuwa na ukweli.. serikali haikutaka utoke nje!..Yametokea wakati wa Mkapa na JK alikuwa mbele kufunika kombe!.. yote haya tunayasahau hata kama yaliwekwa ktk picha ya documentary!
Kizuri kilichotokana na sinema hiyo ni kwamba hakuna tena mapanki kama chakula cha wananchi wa Mwanza.
Sasa hivi mapanki yanatengeneza chakula cha kuku.

Mkandara
Japo suala hili si mchezo lakini hilo la kumuigiza Mkapa kwa picha za sinema umenivunja mbavu ile mbaya. Ila ukweli ni kwamba meseji itafika vizuri na itabidi watu waelewe nini maana ya slogani yake ya "Ukweli na Uwazi". Mimi nilikuja nikagundua kuwa ilikuwa ni uwazi kupitia kioo chenye tinted si mwanga halisi, tulikuwa tunafichwa mambo mengi sana, sasa kwanini "Ukweli na Uwazi" hataki kuusemea eti kastaafu, je sisi wananchi ambao tulistafu siasa kabla ya kuzaliwa kwetu alikuwa anatuhubiria itusaidie nini? Hakuna rudi utujibu.
 
Kwanza Mkapa kafanya nini cha ajabu sana? Hao THISDAY hizo data wanazipata wapi? Hizo ni mbinu za serikali ya awamu ya nne kuwasahaulisha mazuri japo machache ya Mkapa! Pia kupoza makali ya serikali ya awamu ya nne kushambuliwa kwa kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa, kushindwa kutekeleza ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania, kuandamwa na kashfa za kila siku ndani ya miaka miwili tu na kadhalika!

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo! Mbona Balali kaongea na vyombo vya habari, akasema hajiuzulu, basi yakaisha. Karamagi hali kadhalika....Sasa kabaki Mkapa...Je naye mnataka aongee na vyombo vya habari tu ili yaishe? Au watu wataendelea kuchonga ili wauze magazeti?

Nahisi ni njama za wana mtandao tu, kupunguza mashambulizi kwa serikali yao ya sasa ambayo imejaa watalii...Kila siku Ulaya na Marekani, Uchina na Asia.... Wakiwa Tanzania utawasikia wako Kigoma na Tarime...Hebu niambieni, ni mafaili mangapi yapo mezani kwao yanasubiri sahihi zao ili kazi za maendeleo zianze? Fungueni macho, huu ni mchezo mchafu tu, kama ule wa akina Salim na Sumaye walivyopakwa matope mpaka wakaonekana hawafai, kisha mwenzao akaonekana kama malaika wa Nuru, tena wengine wakadiriki kumfananisha na masia...ambaye angeleta Tanzania yenye neema, yenye kumiminika maziwa na asali, yenye maisha bora kwa kila Mtanzania..Yako wapi? Au tuendelee kusubiri?
 
Masaki, ulichosema nakubaliana na wewe, lakini nadhani pia hapa watu wamefunguka macho kiasi cha kutosha kuweza kujua kuwa Mkapa pamoja na mazuri yake kuna madudu kafanya, na ana haki aueleze uma ilikuwaje kuwaje kwa mfano akainajisi Ikulu kwa 'kufanya biashara' mle? ukiachilia mbali mambo mengine

Kuhusu JK nadhani unaona upepo unavoenda bado anabanwa na safari hii inaonekana sasa upepo umehamia ndani kabisa kabisa kwake, sasa sijui atakuwa anaona moshi sebuleni halafu azidi kukaa kimya kwa vile moto haujamfikia ama vipi....
 
Back
Top Bottom