PENDEKEZO: Freeman Mbowe apewe heshima ya uongozi bora

Tujisahihishe Tz

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
3,050
Reaction score
1,359
Moja ya viongozi Tanzani ni huyu bwana Freeman Mbowe, namhusudu kwa 100%, nayasema haya kutokana na uongozi wake tangu awe Mwenyekiti wa Chadema taifa na kukipa chama hicho hadhi kubwa ndani na kimataifa kwa kung'ara bila misukosuko ya mara kwa mara, nadhani anastahili kutuzwa kwa hilo.

Naomba Nawasilisha.
 
Napinga hii hoja kwa sababu moja kubwa, Mbowe aliomba ridhaa ya kuongoza chama chake na akapewa. Kwa sasa anatekeleza majukumu yake kama wanavyofanya watu wengine i.e walimu, wafagia barabara etc etc. Tabia ya kupeana vi-heshima vya reja reja ya CCM na imeondoa kabisa maana ya utendaji kazi.
 
FJM
Naomba kutofautiana na wewe. Hivi wewe kazini/ofisini mwenu hamna annual awards? Hizi hutolewa kwa mfanyikazi bora, mbunifu, aliyekwenda extra mile, etc. etc. katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa hiyo kutambua na kuheshimu mchango wa mfanyikaz yeyote yule ni jambo zuri.
 
Kiongozi, CHADEMA wanatakiwa wafanye mambo tofauti na CCM. Zawadi anayotakiwa kuinyemelea huyu Freeman Mbowe ni kuifikisha CHADEMA Ikulu. Narudia mtindo wa kupongezana kwa reja reja ni wa CCM, na watu wanaikataa CCM na mambo yake yote. CHADEMA lazima watambue hilo na kukwepa mitego hii kizamani.
 
485150_222357234536389_100002863434879_331576_874608890_n.jpg
 
Kiongozi, CHADEMA wanatakiwa wafanye mambo tofauti na CCM. Zawadi anayotakiwa kuinyemelea huyu Freeman Mbowe ni kuifikisha CHADEMA Ikulu. Narudia mtindo wa kupongezana kwa reja reja ni wa CCM, na watu wanaikataa CCM na mambo yake yote. CHADEMA lazima watambue hilo na kukwepa mitego hii kizamani.

Ni kweli mkuu.Mbowe apate award akishaifikisha CDM Ikulu.
 
FJM
Naomba kutofautiana na wewe. Hivi wewe kazini/ofisini mwenu hamna annual awards? Hizi hutolewa kwa mfanyikazi bora, mbunifu, aliyekwenda extra mile, etc. etc. katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa hiyo kutambua na kuheshimu mchango wa mfanyikaz yeyote yule ni jambo zuri.

atakuwa amekuelewa
 
Kiongozi, CHADEMA wanatakiwa wafanye mambo tofauti na CCM. Zawadi anayotakiwa kuinyemelea huyu Freeman Mbowe ni kuifikisha CHADEMA Ikulu. Narudia mtindo wa kupongezana kwa reja reja ni wa CCM, na watu wanaikataa CCM na mambo yake yote. CHADEMA lazima watambue hilo na kukwepa mitego hii kizamani.
hapo umenena!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tuzo zipo sio kitu kigeni. Ni kuweka malengo na vigezo vya namna ya kuwapata washindi. Nadhani hapo ndio CDM inabidi itofautiane na magamba.

Kwamba CDM watoe tuzo kwa watu stahili NDIO. Njia gani itumike hapo tujadili
 
Mie binafsi namkubali Mbowe kwa kukijenga chama lakini kuna mambo mengine simkubali kwa kuwa kigeugeu alisema Chadema hatawachukuwa posho bungeni na akaita waandishi wa habari na kuwaambia anarudisha gari la kiongozi wa upinzani bungeni, lakini mwisho wa siku kalichukuwa tena kwa mlango wa nyuma na posho anachukuwa kama kawaida.
 
Napinga hii hoja kwa sababu moja kubwa, Mbowe aliomba ridhaa ya kuongoza chama chake na akapewa. Kwa sasa anatekeleza majukumu yake kama wanavyofanya watu wengine i.e walimu, wafagia barabara etc etc. Tabia ya kupeana vi-heshima vya reja reja ya CCM na imeondoa kabisa maana ya utendaji kazi.
Nakubaliana na hoja yako!kweli wewe ni GT
 
CHADEMA ni kama Barcelona, they always work as a team with one standard, one spirit, one product.

Mwisho heshima kwa kocha.
Mbowe deserves credit
 
FJM Naomba kutofautiana na wewe. Hivi wewe kazini/ofisini mwenu hamna annual awards? Hizi hutolewa kwa mfanyikazi bora, mbunifu, aliyekwenda extra mile, etc. etc. katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa hiyo kutambua na kuheshimu mchango wa mfanyikaz yeyote yule ni jambo zuri.
nadhani kwa sasa hakuna kitu cha kupongezana!Mpaka tutakaporiudisha rasilimali za watanzania mikononi mwwao,tuone haki ikitendeka bila kucheleweshwa,kikiwa na usawa kwa watanzania na maisha yakiwa bora kwa mtanzania ndio tutawapongeza hao waliokuwa viongozi wa mambo hayo mazuri!bado safari ni ndefu mno kuanza kutoa pongezi, mie nadhani ni muda wa kuhimizana!
 
Ni punguani tu ambaye hataona mchango wa Mbowe katika cdm.
Linganisheni Mbowe na Mbatia, Mrema, AU Dovutwa!..lol!
 
Hayo mambo ya kupeana tuzo na vyeo ni ugonjwa wa CCM.. Wanapeana mpaka majina ya mitaa.. Kuna Mtaa wa Makamba.. Shule ya Makamba.. Ukiuliza huyo Makamba ni nani au kaifanyia nini Tanzania hata mwenyewe Makamba hajui..!
 
full rispect mzee wa anga,unastahili kuliko maelezo.nyie ndio mashujaa wa ukweli sio haya majizi ya sisiemu
 
Mbowe,ni noma kiukweli.anastahili sifa kama huju mfuatilie utagungua.
 
Back
Top Bottom