PENDEKEZO: Freeman Mbowe apewe heshima ya uongozi bora

PENDEKEZO: Freeman Mbowe apewe heshima ya uongozi bora

Watanganyika kazi kweli kweli, yaani kashughuli kadogo wanatafuta sababu za kupeana posho kwa jina la zawadi.



Mawazo mengine jamani kama ya huyu member (Tume ya katiba) haifai isimame hapa juu!

Una mawazo isiyokustahili member km wewe!

Ama wee ndio wale wale nini?
Pole sana!
 
Mbowe na slaa ni makamanda wakuu wote kwa pamoja wanastahl pongez kwa kukijenga chama, bila wao kusimama imara hata wananchi tungeweza kubak legelege tu.
 
..mbona hao wa CCM waliomba wenyewe na wameshindwa kuongoza?!..Kwanui mfanyakazi bora anapopewa zawadi ya utendaji bora na bidii kazini ni kwa kuwa hakuomba kazi mwenyewe?..acha UMBUMBUMBU wa chuki za kipuuzi,kama mtu kafanya vizuri anastahili pongezi....kwa kweli hata mimi Mh.Mbowe nampongeza sana!
 
Napinga hii hoja kwa sababu moja kubwa, Mbowe aliomba ridhaa ya kuongoza chama chake na akapewa. Kwa sasa anatekeleza majukumu yake kama wanavyofanya watu wengine i.e walimu, wafagia barabara etc etc. Tabia ya kupeana vi-heshima vya reja reja ya CCM na imeondoa kabisa maana ya utendaji kazi.

.mbona hao wa CCM waliomba wenyewe na wameshindwa kuongoza?!..Kwani mfanyakazi bora anapopewa zawadi ya utendaji bora na bidii kazini ni kwa kuwa hakuomba kazi mwenyewe?..acha UMBUMBUMBU wa chuki za kipuuzi,kama mtu kafanya vizuri anastahili pongezi....kwa kweli hata mimi Mh.Mbowe nampongeza sana!
 
Stein
Nakubaliana na wewe Mbowe hana sababu ya kufisadi mali ya umma. Huyu ni kiongozi makini na amejitosheleza kiuchumi.
 
Moja ya viongozi Tanzani ni huyu bwana Freeman Mbowe, namhusudu kwa 100%, nayasema haya kutokana na uongozi wake tangu awe Mwenyekiti wa Chadema taifa na kukipa chama hicho hadhi kubwa ndani na kimataifa kwa kung'ara bila misukosuko ya mara kwa mara, nadhani anastahili kutuzwa kwa hilo.

Naomba Nawasilisha.
Mkuu Mweka,kwanza nikushukuru kwa mawazo yako mazuri uliyoyatoa.unastahili pongezi kwasababu hata biblia inasema kwamba,kwa asiye shukuru kwa machache hata mengi hawezi shukuru.
Wakuu wote ambao ni wapenda mageuzi na wapenda maendeleo hatuwezi kuongelea mafanikio yanayoanza kujitokeza nchini pasipo kuongelea chama cha CHADEMA.ni wazi kwamba kama sio CHADEMA ni kwamba hali iliyotokea kwa CCM kama chama na ufahamu wa mambo mengi ambayo sisi wananchi tulikuwa tumefichwa,kamwe yasingetokea.Tuneendelea kuwa gizani na nchi ingeendelea kuliwa na watu wachache.
Sasa tunapogundua kwamba CHADEMA kama chama ndio waliochangia kwa kiasi kikubwa kutufumbua macho sisi wananchi kuhusu yanayojiri serekalini basi lazima tuwape pongezi na shukrani kwa hilo.Tunapoongelea CHADEMA lazima pia tuongelee viongozi ambao wamekuwa madhubuti na imara kuhakikisha kwamba CHADEMA hakitayumbishwa kwa njia yeyote ile.Tumekuwa na vyama vingi vya upinzani ambavyo tumeona ni jinsi gani vimeshindwa kuendelea mpaka leo,matokeo yake vimekuwa vipo kama havipo.kwamba vingi vimekuwa vikipoteza umaarufu au imani kwa wananchi na mashabiki wao kwasababu baadhi ya viongozi wamekuwa wakinunuliwa na CCM.hivyo wamekuwa wakianzisha migogoro isiyo na tija au maslahi yoyote kwa wananchi mpaka kufikia hatua ya kuua chama.tumeshuhudia mambo yaliyotokea NCCR,TLP,CUF na kwingineko.Sasa kwanini nachangia kwa asilimia 100 kuhusu hii hoja ya kumpa Mh Mbowe heshima ya uongozi bora.
Kwamba Mbowe ni kweli amefanya juhudi kubwa sana mpaka chadema kufikia hapa kilipo.ni kiongozi strong ambaye
amekuwa makini kuhakikisha chama hakipotezi mwelekeo.kwamba hata kwa kutumia ubabe hamna pandikizi ambaye ameweza kupenyeza chadema mpaka kufikia kukimaliza chama.lazima tukubali kwamba kwa chama kama chadema kwasasa lazima CCM imekuwa inajaribu kutumia kila njia ili kukiua kama ilivyofanya kwa vyama vingine.kama sio kuwa na kiongozi imara kama Mbowe chadema isingefika hapa ilipo leo hii wala isingeweza kufika 2015.Mapandikizi walioko chadema wengine wanaeleweka,mpaka wamekuwa wanajaribu kutafuta vyanzo vya ugomvi ili wapate sababu wanazo zitaka lakini chama kimekuwa makini sana kuepuka mitego yao.kuna viongozi wengine ambao kwao kuhama chama kimoja kwenda kingine sio issue ilimradi wanajaribu kutafuta maslahi zaidi.kwahiyo leo anaweza kuharibu chadema akijua kesho atakimbilia CCM au chama kingine.kwamba kwao ni suala la maslahi zaidi.
Nakumbuka Mh Kingwangwala(Mp wa Nzega amewahi kuzungumzia suala la umuhimu wa Raisi kuteua mawaziri ambao ni makada wa chama.kwamba waziri ambaye ni kada wa chama chake atleast angeweza kuwa na uchungu pale anapoona chama chake kinakufa,hivyo angejitahidi kufanya kazi vizuri ili asiue chama.kwa mawaziri ambao hawana uchungu wowote na chama chao ni kwamba wanajua kwamba kesho chama kikifa watahamia chama kingine.
Sasa kwanini Mbowe.??????kutokana na historia ya chama ambacho anakiongoza CHADEMA ni wazi sio rahisi kwa Mbowe kukiuza chama.kwamba kwasababu kile chama aliachiwa na mkwe wake(MTEI) ni wazi kuwa Mbowe hawezi kuona kile chama kinakufa hata kwa gharama yoyote.kwamba anakisimamia kama anavyosimamia shughuli zake nyingine,kwamba anauchungu nacho.nadhani hii hali ya kukijali chama ndio inayomfanya apiganie maendeleo yake.kwamba CHADEMA hakiendelei kwa maneno tu,au kwa vijana ambao walikaribishwa ndani ya chama ili kukijenga chama lakini baada ya kupata umaarufu wanajiona ni bora zaidi.
chama cha upinzani kuendelea sio kazi ndogo,inahitaji kuwa na viongozi imara ambao wana uchungu na chama.ambao sio wakununuliwa,ambao kesho utasikia wako CCM kesho kutwa wako CUF au vyama vingine.Mbowe sio mtu wa kuhama chama.hayuko CHADEMA kwasababu ya kutengeneza pesa.ndio maana watu wenye nia mbaya wanashindwa kuimaliza chadema.tumeona viongozi ndani ya chadema ambao Mbowe ndio aliowapa nafasi ya kukua kisiasa na matokeo yake wamekuwa wanajaribu kupingana nae kwa kusingizia DEMOKRASIA.Kwanini wamekuwa wanatumia neno demokrasia pale tu wanapokuwa wana taka kugombea uenyekiti?tumeona yaliyomfika kafulila NCCR pale alipojidai yeye ni bora kuliko mwenyekiti wake.kwamba yeye ndiye anayestahili kuwa mwenyekiti.wakati akijua wazi kwamba alichaguliwa na wananchi wa jimboni kwake ili kuwasilisha na kutatua matatizo mengi waliyonayo waliomchagua na hawakumchagua ili akapambane na mwenyekiti wake au kujilinganisha nani zaidi.matokeo yake yamemfika yaliomfika.kimyaaaaaa!!!
Ndani ya chadema watu kama kina kafulila au hamad rashid wako wengi tuu lakini wameshindwa kutekeleza malengo yao kutokana na uimara wa chama chini ya uenyekiti wa Mh Mbowe.
Tutakuwa wachowo wa shukrani kama kweli tutashindwa kutambua au kuubeza mchango wa Mh Mbowe ndani ya CHADEMA.Anastahili atunukiwe nishani ya uongozi bora.Kwa yoyote mwenye mapenzi mema naomba tuzidi kumuombea kwa Mungu Mh Mbowe ili azidi kumpa moyo wa kuendelea kupigania,kutetea na kulinda maslahi ya watanzania wote.Tukijua kwamba yeye mbowe na chama anachokiongoza wanajitolea na kuweka maisha yao rehani ili kututetea sisi.basi tuwasupport na kuwaunga mkono ili mipango ya Mungu itimie.Mungu azidi kutubariki zaidi sisi watanzania ili tuwe na uwezo wa kufungua macho na kutambua pale anapotuma mtumishi wake kutukomboa.tusidharau na kubeza.Mungu anafanya kazi kwa njia za ajabu
 
Napinga hii hoja kwa sababu moja kubwa, Mbowe aliomba ridhaa ya kuongoza chama chake na akapewa. Kwa sasa anatekeleza majukumu yake kama wanavyofanya watu wengine i.e walimu, wafagia barabara etc etc. Tabia ya kupeana vi-heshima vya reja reja ya CCM na imeondoa kabisa maana ya utendaji kazi.

kaka kubali ukweli Jamaa ni Kichwa na amejenga na kukiongoza chama vizuri na si mnafiki. Na can be trusted, not easy to buy. Tena sio mbabaishaji.

Kamanda Mboe anastahili pongezi za dhati
 
Back
Top Bottom