Ngisibara
JF-Expert Member
- Jan 2, 2009
- 3,306
- 2,083
Tanzania mpya
Tanzania mpya, Uongozi mpya, Maisha mapya
Jambo muhimu ni kuelimisha watu mpaka ngazi ya kijijini ambako watu wengi ndipo walipo na ndiko mahala ambapo hakuna usimamizi mzuri wa kura kama ambavyo tumejionea jinsi kura za mijini zilivyoweza kulindwa vizuri na vijana wa "Peoples Power" jambo muhimu ni zile percent alizoongelea JK kuwa 70% hufuata upepo basi hapo ndipo pakujikita hasa katika kundi la vijana ambao makali ya maisha wanayapata kwa kilele kikubwa, na mwisho CDM anzisheni mfuko maalumu wa kuchangia gharama za kampeni kuanzia hivi sasa na sio kusubiri dakika za majeruhi au kuwasubiri wasamaria wema kama mzee Sabodo kwani kazi hii ni kubwa kuliko uwezo wa watu wachache wenye upendo na mabadiliko