beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mshauri mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo Salim Bimani wameripoti katika Kituo cha Polisi Wete Pemba asubuhi ya leo.
Viongozi hao wa ACT Wazalendo wameitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jinai (RCO) Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Wananchi na Wanachama wa ACT - Wazalendo wamekuwa nje ya maeneo ya karibu ya jengo la Polisi la Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa lengo la kujua hatma ya viongozi wao wanaohojiwa na inadaiwa wamejiandaa na kuwachukulia dhamana ikibidi.
Mshauri Mkuu wa ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Salim Bimani wameshutumiwa kufanya mkutano bila kibali mwezi Desemba 2019 huko Micheweni Zanzibar.
Hata hivyo, Viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kupitia Mtandao wa Twitter Chama chao kimedai kuwa walifanya mkutano wa ndani usiohitaji kibali.