PCCB: Tuna manufaa nayo?

PCCB: Tuna manufaa nayo?

Mkuu,

Sasa umeanza kuiita TAKUKURU kimbilio la mafisadi kwa facts zipi?

badala ya kuwashauri watanzania wenye ushahidi kuwasiliana na polisi au TAKUKURU wewe unaanza kutumia jambo la RA kwenda TAKUKURU kuifanya taasisi yote ionekane ya kifisadi?

Inaelekea hapa JF tumechanganyikiwa hata hatujui nini tunataka, hatuna msimamo mmoja unaoeleweka, tunayumba, tunatapatapa kwa kuangalia mhusika ni nani.

RA katumia haki yake kama Mtanzania mwingine, muhimu ni kuwashauri wengine wenye habari kuhusu uhalifu kuweza kuzifikisha kwenye vyombo vyetu vya usalama.

Huwezi kumlazimisha mtu aende sehemu unayotaka wewe, mtu anaweza kwenda polisi, anaweza kwenda vyombo vya habari ili viandike, anaweza kwenda mahakamani, anaweza kwenda TAKUKURU.

Kitu ambacho hutakiwi kufanya ni kuilamu taasisi yote kama TAKUKURU kwamba ni kimbilio la mafisadi. Je wale walioko mahakani baada ya kupelekwa na TAKUKURU sio mafisadi?

Ndio TAKUKURU wana matatizo na wanatakiwa kuongeza ufanisi na kupunguza kuwa tegemezi sana kwa serikali, lakini hiyo sio sababu ya kuwaita TAKUKURU kimbilio la mafisadi.

Sio kila case unaweza kupeleka mahakamani. RA anaweza kwenda mahakamani kumshitaki Mengi kwa kumkashifu lakini hawezi kwenda mahakani kumshitaki Mengi kwa kuiibia NICO au mabank. Hiyo ni kazi ya serikali kama sikosei.

Hawa jamaa watoe ushahidi walio nao ili tuwajue vizuri hawa papa na Nyangumi bila kujali ni Mengi au RA.

Tatizo la watu wengi hapa ni double standards, kama Mengi amekosea sio fisadi, kama RA ni fisadi. Hawa wote mapapa na Nyangumi ni mzigo kwa Tanzania. List haiishii hapo, wako wengi mno. Wakiumbuana ndio faida kwa sisi wananchi.
Ni kweli TAKUKURU ni kimbilio la mafisadi kwani ndio wanaoficha siri za mafisadi na kuuwa upelelezi pale fisadi anapotakiwa kupelekwa mahakamani.
Niambie ni lini walimhoji Rostam kuhusiana na kagoda na waligundua nini??
Niambie si hao waliomsafisha mwizi Richmond kwa kumwita ni safi na mwakyembe akasema sio.
Niambie ni nani takukuru imesha toa ushahahidi dhidi yake.
je ni kweli TAKUKURU hawajui kwamba chenge alituibia baada ya SFO KUHAKIKI.
Au hawajui kwamba Chenge alikuwa na marehemu kabla hajawauwa. come on now.
takukuru ina nia ya kumsafisha RA na hii ni plan move.
 
mahakamani akafanye nini ? Kwani yeye ni bwana mashtaka ???? Aidha anaweza kwenda police au takukuru....wao sasa ndio kazi yao kuchunguza.....
Amefanya jambo jema sana....watu majungu sana......fisadi ni fisadi tu..kama ni papa au nyangumi.....anachosema mengi ..ni tuhuuma na alichosema rostam ni tuhuma.....lakini kwa uchache alichotuhumiwa rostam ni marejeo ya akina dakitari slaa...lakini alichotuhumiwa mengi ni mapya...nani alijua kama nico chini ya mengi katumia hela za walalahoi za nico 2.5 billioni kazikaanga kwenye kiwanda chake??// na tena kimefilisika....kwa mtindo ule ule kopa tumia kidogo kwa kulisha pilau kwa albino...nyengine tumbua mwenyewe.....halafu ua kiwanda kilichokopa kifilisiwe...ndio utajiri wake.....kule usa kulikua na vitendo kama hivi....mnakumbuka kampuni iitwayo enron walikua na mtindo huu wa kukopa sana bank kwa kutuo mahesabu ya uongo kwamba company inafanya vizuri..then company vuuuu inafilisika....bank hawajui waanzie wapi kupata hela zao....hatimae wakurugenzi wake wako jela wanakula ugali....huwezi kuua company tu....ili usidaiwe na banks...ni wizi wakiaina....hatukujua..haya.....kuna lile la account ya billion 40 ya account ya ukimwi..rostam hakuitaja hii lakini.....inashangaza kidogo.......kweli mtu ataenda kufungua account kwa jina la mengi na kuingiza kiasi chote hicho cha pesa then mengi meza aseme yeye haijui account hio????? Kawaida banki zetu wanakupigia simu...wakati zikitolewa...hakuna bank isiyomjua mengi meza....huyu yumo ni nyangumi tu..kama mnampnda labda kwa kuwa hii forum ni ya wa moshi basi mapenzi yenu kwake ni haki yake....lakini ni fisadi kama wenzake...mimi nasema kama angekua vita hiii kaianzisha dt shein ama pinda basi hawa ndio safi tuliobakiwa nao tz yote..lakini sio mengi.....yeye ni mmoja wao
 
Watanzania bana mnanichosha sana sijui uvivu wa kufikiri na kung'amua mambo? Huyu papa katumia haki ya msingi na ya kikatiba amepeleka vielelezo vyake vya kumtuhumu Mengi sasa na Mengi nae ana haki ya kutumia haki ya msingi kupeleka ushahidi wake kama anao wa kumtuhumu RA apeleke mahala husika kama alivyo fanya huyu papa.
Mkuu wewe ulitaka apeleke wapi?


Mkuu Fidel80,
RA alimpa masaa 48 RM amuombe radhi kwa kumchafulia jina kwa kumhusisha na ufisadi. RA alitakiwa kwenda mahakamani maana RM hakumwomba radhi. Huko ndio angesafishwa jina. Kupeleka vielelezo vya ufisadi wa RM hakumaanishi RA siyo fisadi na wala hakumsafishi jina. TUKUKURU nani asiyeijua. wizi mtupu
 
You seem to be out of Tanzania tunayoijua Pamoja na TAKUKURU ambayo tukiweka post zako hapa ulizowahi kuilalamikia TAKUKURU na HOSEA utatia aibu !!! na Ndicho kinachowafanya Watanzania wasiopenda UFISADI wahoji kwa nini RA apeleke huko na kwa nini asiende mahakamani kumshitaki Mengi !!! ???? Ili Mengi aje na ushaidi huko mahakamani!!! mahakamani ni openly na wananchi wanaruhusiwa kusikiliza lakini huko alikopeleka wanafanya ni siri na mwisho wa siku wanaibuka na report za kuwashafisha Mafisadi kama walivyofanya kwenye Richmond na sehemu nyingi tu. Hapo ndipo hoja ilipo, elewa kuwa hakuna anayepinga Mengi asipeleke ushaidi, kinachopingwa ni wapi pa kupeleka .

Thanks man! "The fact will always be the fact never will it be an opinion"
 
Wanamkimbilia mwokozi wao Hosea na ndio maana wanamlinda kwa gharama yoyote asiondolewe TAKUKURU.
hivi tatizo ni HOSEA AU MUUNDO WA TAKUKURU...???

Jamani tuwefocused kwamba ili takukuru ifanye kazi yake kwa uwazi na haki basi iondolewe chini ya IKULU!!! Period...

hili ndilo la msingi sanaaaa....
 
. Una hisa New Habari Cooperation? Mbona unaelezwa lakini huelewi? Usiwe kama Jackton Manyerere, unaambiwa Takukuru ndiyo iliyosafisha mafisadi wa Richmond na kwamba bila ya jitihada za Kamati ya Bunge ufisadi huu ungepeta, iweje leo Takukuru hiyohiyo iwachunguze tena wahusika walewale iliyokwishawasafisha?
Wajinga kama wewe ndio wanawafanya Watanzania waendelee kuwa wajinga, washindwe kuhoji hata mambo ya maana kwa kuhofia kupachikwa maneno.

Ni kukosa hoja kuanza kutuhumu watu bila ushahidi wowote.

Kikubwa zaidi ni ujinga uliokithiri kutumia lugha za kipumbavu kama hizo bila kujaribu hata kutoa ushahidi wowote.

Kama nina hisa Newhabari onyesha hizo hisa nimenunua wapi?
 
Mkuu umesahau tamko la Hosea lililo jaa mbwembwe kwamba RICHMONDI safiiiiiiiiii... ???

Hivi imani itoke wapi?na fact zipi unazitaka zaidi ya uumbukaji wa taasisi ile? baada ya kamati ya bunge kuanika kila kitu?

Kwa taarifa yako, toka wakati ule ile TAKUKURU ilipoteza kabisa credibility machoni petu wananchi, na Kibaya zaidi huyo bosi wao Hosea ndo kabisaaaaa anazidi kuifanya ionekane haifai kabisa,kwanza ni mtuhumia mkubwa, pili utendaji wake unaonekana wazi ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya mafisadi period!

lakini pia haijakushanganza, Fisadi papa Rostamu Azizi kwenda Takukuru kupinga tuhuma dhidi yake? yaani huko kweli ndiko alipaswa kwenda tena kwa mbwembwe na picha mnato na muondosheo juu? kama siyo, hivi mtu waweza jisafisha tuhuma kwa kumtuhumu mtu mwingine?

Hivi serikali nayo mwanzoni si ilesema hivyo hivyo? Bunge nalo mwanzoni si lilisema hivyo? Je huko nako ni kimbilio la mafisadi?
 
Iweje Takukuru iwe kimbilio la mafisadi...

Inavyoonekana wote (Takukuru na mafisadi hawajui) hawajui majukumu yao...

Mafisadi wanatakiwa kwenda mahakamani ili ukweli ujulikane...

Takukuru hawakutakiwa kukubali Makablasha ya RA maana kwa kufanya hivyo watakuwa wanaingilia uhuru wa mahakama wa kutafuta haki ili hali wao si kazi yao...Utaratibu huu wa kukimibilia Takukuru inabidi ulaaniwe sana na kila mtu vinginevyo ukiendelezwa mahakama zitakuwa hazina hadhi au kazi tena...

Ni hayo wakuu...
 
Watanzania bana mnanichosha sana sijui uvivu wa kufikiri na kung'amua mambo? Huyu papa katumia haki ya msingi na ya kikatiba amepeleka vielelezo vyake vya kumtuhumu Mengi sasa na Mengi nae ana haki ya kutumia haki ya msingi kupeleka ushahidi wake kama anao wa kumtuhumu RA apeleke mahala husika kama alivyo fanya huyu papa.
Mkuu wewe ulitaka apeleke wapi?

APELEKE MAHAKAMINI. Takukuru iliisafisha Richmond ya RA, ndio maana anakimbilia huko. Mahakamani kuna uwazi, ndio the best option kwa haki. Takukuru toka iwasafishe Richmond/Dowans haiwezi kuwa na credibility kushughulikia issues kama hizo.
Ni jitihada zilizile za watuhumiwa wa uchafu/ufisadi kutaka kujisafisha toka EL ajiuzulu.
 
Sawa Kamende,

Ila nina ushauri. Hoja yako ni nzuri ila sisi wanaJF ni wachache. Kama kuna uwezekano kuweka kwenye magazeti kama Mwananchi, Tanzania Daima e.t.c

Kama vile tunavyocopy na kupaste kutoka kwenye magazeti na kuleta JF.

JF kuna hoja nzuri sana ila hazipati mwanga. Nashauri baadhi ya hoja pamoja na majadiliano yachapishwe kwenye Magazeti au vijarida.

Lets try
 
Na pia tukumbuke RA alimpa masaa 48 aombe radhi la sivyo atamchukulia hatua. Nilitegemea angeenda mahakamani kumshitaki RM kamchafulai jina na amtake mengi alete uthibitisho wa aliyosema. Badala yake kaenda kusema ufisadi wa Mengi. Mengi yeye alikanusha aliyotuhumiwa na akiitwa PCB atapeleka defence yake ila rostam hakukanusha kwa vithibitisho.Hivyo maana yake kwa wenye akili madai ya Mengi kwa rostam kwamba ni fisadi papa yamesimama pale pale


We vipi?

Mbona kisha mchukulia hatua??
Kesha peleka ushahidi wake Takukuru na vyombo vyote vya habari vilishuhudia. Kwenda Mahakamni na Takukuru ni kitu kilekile.
Wewe unajifanya unajua sheria kuliko MH Rostam Aziz Mbunge wa Igunga Yote?
EeH!
Unadhani kupeleka ushahidi wake Takukuru ni mchezo siyo?

Mengi atakiona cha mtema kuni wakati wowote Takukuru wakimaliza kupitia ushahidi watamvaa pale nyumbani kwake wanamtia pingu anawekwa ndani, kesi inapigwa kalenda, Mengi anaozea Keko Rostam anapeta.
 
Mkuu,

Sasa umeanza kuiita TAKUKURU kimbilio la mafisadi kwa facts zipi?

badala ya kuwashauri watanzania wenye ushahidi kuwasiliana na polisi au TAKUKURU wewe unaanza kutumia jambo la RA kwenda TAKUKURU kuifanya taasisi yote ionekane ya kifisadi?

Inaelekea hapa JF tumechanganyikiwa hata hatujui nini tunataka, hatuna msimamo mmoja unaoeleweka, tunayumba, tunatapatapa kwa kuangalia mhusika ni nani.

RA katumia haki yake kama Mtanzania mwingine, muhimu ni kuwashauri wengine wenye habari kuhusu uhalifu kuweza kuzifikisha kwenye vyombo vyetu vya usalama.

Huwezi kumlazimisha mtu aende sehemu unayotaka wewe, mtu anaweza kwenda polisi, anaweza kwenda vyombo vya habari ili viandike, anaweza kwenda mahakamani, anaweza kwenda TAKUKURU.

Kitu ambacho hutakiwi kufanya ni kuilamu taasisi yote kama TAKUKURU kwamba ni kimbilio la mafisadi. Je wale walioko mahakani baada ya kupelekwa na TAKUKURU sio mafisadi?

Ndio TAKUKURU wana matatizo na wanatakiwa kuongeza ufanisi na kupunguza kuwa tegemezi sana kwa serikali, lakini hiyo sio sababu ya kuwaita TAKUKURU kimbilio la mafisadi.

Sio kila case unaweza kupeleka mahakamani. RA anaweza kwenda mahakamani kumshitaki Mengi kwa kumkashifu lakini hawezi kwenda mahakani kumshitaki Mengi kwa kuiibia NICO au mabank. Hiyo ni kazi ya serikali kama sikosei.

Hawa jamaa watoe ushahidi walio nao ili tuwajue vizuri hawa papa na Nyangumi bila kujali ni Mengi au RA.

Tatizo la watu wengi hapa ni double standards, kama Mengi amekosea sio fisadi, kama RA ni fisadi. Hawa wote mapapa na Nyangumi ni mzigo kwa Tanzania. List haiishii hapo, wako wengi mno. Wakiumbuana ndio faida kwa sisi wananchi.

Hebu Fikiria kwamba Kampuni inaingia Tanzania kinyemela ina sign mkataba wa fedha nyingi na serikali, serikali inaliipa mabilioni kampuni hiyo. baadaye inabainika wazi kwamba mkataba huo kati ya serikali na kampuni ni batili.
Takukuru inapewa kazi ya kuchunguza, inakijkanyaga na kushindwa kutoa majibu yenye kubeba maana.

Kikubwa zaidi mpaka leo inashindwa kutuambia Nani yupo nyuma ya Richmond na Dowans wakati trail kadhaa zinaonyesha mtu mmoja mashuhuri miongoni mwa Makada wa CCM anahusika kwa namna moja au nyingine na ushenzi huu.

Takukururu imeshindwa kutoa majibu ya maswali hata baada ya kupewa leads!
Je Takukururu bado ni chombo cha kuaminiwa na wananchi?


NBC ilikuwa mali ya serikali kwa 100%?

Serikali inaijua NBC na inajua zaidi ya mtu yeyote what happened in NBC.

Rostamu anapeleka ushahidi serikalini wa madai ya mikopo isiyo rudishwa na Mengi NBC kama nani?
Kuna jinai hapo?
Kukopa na kushindwa kulipa ni ufisadi?
Swala la madai ni kati ya Mdai na Mdaiwa?

Mdaiwa ni Mengi mdai ni Serikali ambaye ni alikuwa mmilikiwa halali wa Marehemu NBC.
Je Rostam ni Mdai? Rostam ni serikali?

NBC haikufilisika. Tulikuwepo ilipokua hai mpaka kifo chake.

NBC ilipigwa Roba na serikali yenyewe ili Ife itoe mwanya kwa Mabenki binafsi ya ndani na ya kigeni kuingia nchini Tanzania na serikali kujitoa kwa kiwango kikubwa katika biashara ya Mabenki.

Rostam inawezekana kanizidi uwingi wa Fedha isiyo halali, lakini kuhusu kilicho ipata NBC hadi kufa kwake Rostam hana kitu ni mtupu.
Habari za kufilisika kwa NBC alizipata kijiweni, sasa anataka ziwe ushahidi wa kumfunga Mengi. Anachekesha kweli.
 
mahakamani akafanye nini ? Kwani yeye ni bwana mashtaka ???? Aidha anaweza kwenda police au takukuru....wao sasa ndio kazi yao kuchunguza.....

Wanasema eti aende mahakamani akashtaki kwamba ametukanwa ... tehetehe ... hata ningekuwa mimi ningeenda, nisingevumilia mtu mzima kutiwa aibu hivyo tehe tehe

Halafu wanasema eti kesi za defamation hazihitaji police au takukuru kuchunguza ... tehe tehe ...
 
7th May 2009b-pepeChapaMaoniKwa mara ya kwanza katika historia ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini, umma umeonyeshwa maofisa wake vielelezo vya madai kutoka kwa `msamaria mwema`.

‘Msamaria mwema’ huyu ni Rostam Aziz ambaye ametuhumiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, kwamba ni fisadi papa naye akajitokeza na kuunganisha madai na kusema Mwenyekiti huyo naye ni fisadi nyangumi.

Kama alivyokuwa ameahidi, Rostam, amewasilisha madai hayo kwenye ofisi za Takukuru. Tunafikiri ana haki ya kufanya atakalo kuhusu madai yake, iwe ni Takukuru, polisi au kwingine kokote.

Hiyo ni mbinu yake ya kujisafisha na kujilinda na hatuna sababu ya kulumbana naye kwani mwisho wa siku ukweli utajulikana tu. Kinachotusumbua leo ni taratibu mpya za Takukuru.

Kwamba siku hizi msamaria mwema akiwasilisha taarifa za kumtuhumu mtu au raia mwingine, Takukuru wanaita waandishi wa habari na wapiga picha. Picha zinapigwa kana kwamba ni makabidhiano ya chakula cha msaada kwa mkuu wa mkoa kwa ajili ya watu waliokumbwa na janga la mlipuko wa mabomu.

Kwamba Takukuru siku hizi wamebadilika kiasi kwamba sasa wanafanya kazi sambamba na vyombo vya habari katika kupokea taarifa mbalimbali za malalamiko ya wananchi!

Bila shaka huu ni utaratibu mpya, na umebuniwa mahususi kwa ajili ya Rostam. Tunajiuliza tena na tena, vyombo vya serikali vimeingiliwa na nini kiasi cha kuanza kukiuka taratibu zake za kutenda kazi ili kuwafurahisha watu wenye tuhuma nzito katika jamii yetu?

Juzi hapa, tuliona kituo cha televisheni cha Shirika la Utangaza la Tanzania (TBC) kikirusha matangazo ya Rostam.

Kwamba kilikuwa ni kipindi maalum kilicholipiwa hakuna anayebisha, lakini TBC ikiwa inatambuliwa kama chombo cha habari cha umma, kinatoa tangazo lolote tu hata kama halina maslahi kwa umma kwa sababu wamepewa fedha?

Tunajiuliza tena na tena, inakuwaje mwehu yeyote atakaye taka kuweka tangazo lake TBC kwa kuwa analipa fedha, Je, atakataliwa na akataliwe kwa sababu gani alimradi analipia muda wa kwenda hewani?

Tulikwisha kusema huko nyuma, kwamba nchi hii kuna dalili kwamba ipo mifumo tofauti ya sheria, taratibu na kanuni katika kushughulikia watuhumiwa.

Mwizi wa kuku au kibaka wa vidani vya akina mama mitaani anashughulikiwa kwa hasira ya umma, anapigwa na kuchomwa moto, anakufa. Umma unachukua sheria mkononi.

Watuhumiwa wa uhalifu mkubwa mkubwa, wanaundiwa tume, kamati, vikosi kazi na kila aina ya uchunguzi. Majina yao yanahifadhiwa, wanaogopwa na kwa kuweli hadi watawala wanasema kuwa kwa kuwa ni watu wenye fedha, bila kujali usafi wa fedha hizo, ni lazima watazamwe kwa tahadhari.

Ugonjwa ule ule wa kulinda na kuficha waovu, kuwasadia kupoteza ushahidi kwa kuwa tu ama kuna njia ambazo baadhi ya watu waliokabidhiwa ofisi za umma wananufaika na uchafu wa watuhumiwa hawa, zinapigiwa debe ili kuwalinda.

Ni kwa msingi huo, umma umepigwa mshangao wa ajabu kusikia na kuona kwamba watu ambao sasa hivi wangestahili kuwa Keko wakila dona, wako mitaani wakitamba na kutisha wale wanaohoji usafi wao kutokana na kuhusika kwao na vitendo vingi vinavyotiliwa shaka.

Takukuru bila kujali kama inacho chombocha kuchunguza juu ya mlolongo wa madai ya kutunga yaliyowasilishwa na Rostam kwao, imejikuta ikijipanga kusaidia kampeni chafu zinazoendeshwa na baadhi ya watu wenye tuhuma za kuifilisi nchi.

Kwamba Takukuru walipokea nyaraka za kutengeneza za Rostam mbele ya vyombo vya habari ni jambo la kuumiza kichwa. Je, Rostam aliwakodisha na kwenda nao, na wao Takukuru wakakubali kufanya tendo hilo la kushirikisha vyombo vya habari?

Tunabaki na bumbuwazi kwamba sasa vita dhidi ya ufisadi inakabiliwa na upinzani mkali. Watu wanataka kujisafisha kwa gharama yoyote lakini bila kuzungumzia mambo ya msingi yanayowakabili.

Hapa ndipo shida kubwa ilipo, kwamba vyombo kama Takukuru vinafahamu tuhuma zote zilizoelekezwa kwa mabingwa wote wa ufisadi nchini, kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, rada, Ndege ya Rais, zana za jeshi, uwindaji haramu wa kitalii na mikataba mingine mingi ya kilaghai, lakini havionekani vikichukua hatua na kusema nini kinafanyika, ila wanakubali kuwa sabuni ya kuwatakasa watu kama Rostam kwa kuwapa fursa ya kupiga nao picha wakati akiendeleza juhudi za kughilibu umma. Kweli kazi bado pevu mbele ya safari.

CHANZO: NIPASHE
 
TAKUKURU inawajibika kwa ofisi ya Rais, haiwezi kufanya kazi kwa ufanisi mpaka itakapokuwa taasisi huru.
 
TAKUKURU inawajibika kwa ofisi ya Rais, haiwezi kufanya kazi kwa ufanisi mpaka itakapokuwa taasisi huru.

Kwanza mi sioni inafanya kazi gani hasa, Tangu ilipo kuja na blah blah za RICHMONDI safiiii mi nilisha tamani kwanini wasiifute tu?
 
Hadi siku itakapovunjwa na kuundwa taasisi huru.....na watendaji wapya na mfumo mpya....vinginevyo...makida tu hata miaka 200 hakuna lolote
 
Ufisadi mkubwa kuanikwa
Imeandikwa na Basil Msongo; Tarehe: 10th May 2009

Habari Leo

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Julai mwaka huu itatoa taarifa kuhusu uchunguzi unaoendelea wa rushwa kubwa, na imeagiza maofisa wake katika kila mkoa na wilaya wachunguze rushwa kubwa 12 kila mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea alisema jana kuwa, mwaka jana taasisi hiyo ilichunguza rushwa kubwa 10, lakini mwaka huu hawatafikia idadi hiyo kwa kuwa uchunguzi unaoendelea unazihusisha pia mamlaka za nje ya nchi.

Dk. Hosea aliyasema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa nne wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kwa nchi za Mashariki ya Afrika uliomalizika Dar es Salaam. Alisema, licha ya kutoa ripoti hiyo kwa wananchi, itakapoanzishwa tovuti ya Takukuru, taarifa zote kuhusu rushwa zikiwamo za uchunguzi zitawekwa kwenye tovuti ili wananchi wazisome lakini watakaokuwa wanachunguzwa hawatatajwa kwa sababu wana haki ya kulindwa.

Kwa mujibu wa Hosea, kati ya tuhuma kubwa 10 zilizochunguzwa mwaka jana, uchunguzi wa tuhuma saba umekamilika, kesi zinaendelea mahakamani. Alisema, Takukuru inashughulikia ipasavyo suala la rushwa kubwa na inastahili kupongezwa badala ya kushutuhumiwa kwamba haitimizi wajibu wake ipasavyo.

Hosea aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo wakiwamo wabunge wa kamati tatu za Bunge la Tanzania, Kamati ya Hesabu za Serikali, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, kwamba Takukuru inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na si malalamiko ya wananchi.

Alisema, Takukuru haiwezi kuikiuka sheria iliyoianzisha, hivyo hata kama wananchi wanalalamika lakini kama sheria hairuhusu kuchukua hatua, taasisi hiyo haitapingana nayo. Alitoa mfano kwamba, Takukuru haikuwachukulia hatua watuhumiwa katika kashfa ya zabuni ya ukodishaji mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Kampuni ya Richmond kutokana na kuepuka kukiuka sheria.

Alifafanua kuwa sheria iliyopo ina kipengele cha kuzuia rushwa lakini haizungumzii suala la jinai hivyo hata maelezo yake (Hosea) kuhusu sakata hilo yalizingatia sheria na si kuisafisha kampuni hiyo. “Msiseme hapana, someni sheria,” alisema Hosea alipokuwa akiwaeleza wajumbe wa mkutano huo ambao baadhi yao ni wabunge ambao walionekana kwamba hawakuelewa hoja yake kuhusu Richmond.

Aliwaeleza kuwa, kwa mujibu wa sheria iliyopo, hata kama sakata la Richmond lingefikishwa mahakamani kusingekuwa na kesi na kwamba, ili mtuhumiwa apandishwe kizimbani lazima kuwe na ushahidi wa maneno, nyaraka, na kidhibiti.

Alisema katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Jaji Mkuu, Augustino Ramadhani na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, na kutoa mfano kwamba mtu akiiba gari halafu akalirudisha kwa mmiliki na akampa na funguo, hataweza kumshitaki kwa kuwa hatakuwa na ushahidi dhidi ya mtuhumiwa.

Alishukuru mchango wa vyombo vya habari na Bunge katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa unaiwezesha Takukuru kutokuwa na kazi ya kuwasaka watuhumiwa wa rushwa. Aliliomba Bunge liisaidie taasisi hiyo itekeleze majukumu yake na Spika Sitta, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo alisema Bunge litafanya hivyo ila jambo la msingi ni dhamira ya mamlaka hizo kutimiza wajibu wao.

Hosea alisema, rushwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika eneo la Mashariki ya Afrika, ni ajenda kwenye makundi yote kwenye jamii, inaharibu mshikamano wa watu, inasababisha umasikini, inawatisha wawekezaji, na inaathiri sera na msingi wa kodi kwenye nchi.

Wakati huo huo, Jaji Ramadhani alisema ingawa Bunge lilikataa kuwapo kwa wagombea binafsi, lakini suala hilo ni la lazima kwa kuwa hata kwenye uchaguzi, mara nyingi wapiga kura wanachagua mtu na si chama. Aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali kuwa, mgombea binafsi ni suluhisho la mizengwe inayofanywa katika vyama vya siasa wakati wa uchaguzi.

Alieleza pia umuhimu wa kuongezwa kwa kiwango cha fedha kinachotengwa kwenye bajeti ya serikali kwa ajili ya Idara ya Mahakama kwa kuwa mahitaji ni makubwa hivyo kuwe na kiasi maalumu kitakachotengwa kila mwaka bila kujali ukubwa au udogo wa bajeti husika. Katika bajeti ya serikali ya mwaka huu wa fedha, mahakama imetengewa Sh bilioni 21, Bunge limetengewa takribani Sh bilioni 50.

Jaji Mkuu alisema, Idara ya Mahakama pia inakabiliwa na uhaba wa watumishi wakiwamo majaji kwa kuwa kuna majaji 16 tu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania hivyo analazimika kwenda mikoani kusikiliza kesi wakati alipaswa kubaki Dar es Salaam kushughulikia mambo ya utawala. Katika mkutano huo ulioanza Alhamisi wiki hii, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma, Dk. Ramadhani Mlinga alisema, kuna umuhimu wa kuboresha mfumo wa ununuzi nchini kwa kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004.
[/B]
 
Back
Top Bottom