nimesoma gazeti leo kuwa takukuru wameanza kumchunguza ceo wa tanroads, ephraim mrema kwa tuhuma kuwa alipata kazi kwa mlango wa nyuma na kama analipa kodi ya mapato yake inavyopaswa.
Mnaona double standards za serikali yetu na hasa vyombo vya dola na sheria?
Mrema katuhumiwa kuwa haieleweki alivyopata kazi na mshahara wake ni mkubwa, takukuru inaanza kumchunguza bila kimemo.
Lakini kwenye suala la richmond ambalo lowassa na msabaha walihusika na kutuhumiwa pamoja na wengine, takukuru ilisema mapema hakuna kosa na hata baada ya kamati ya bunge ya mwakyembe kubainisha kuwa mchakato mzima wa richmond ulikuwa na walakini mkubwa na kuegemea kuwa na vitendo vya uhalifu na rushwa, takukuru wamekaa kimya.
Njoo suala la karamagi na mkataba wa buzwagi. Mazingira yanaonyesha ama kuna hujuma au rushwa, lakini karamagi anapeta na takukuru wamekaa mguu pande.
Ingiza rada, chenge katuhumiwa, serikali na takukuru wanasema hawafanyi uchunguzi wa ndani, hawana sababu kwa kuwa serikali ya uingereza inaichunguza bae. Sasa kama afisa mwandamizi wa serikali yetu inasadikiwa alipokea rushwa ili nchi iingie mkataba mkenge, kwa nini serikali yetu isimchukulie huyu mtuhumiwa na badala yake kudai fidia kwa muuzaji na si afisa mwandamizi aliyefanya uzembu au uhujumu?
Epa, meremeta, tangold, cis. Sijasikia takukuru kuanza uchunguzi mara moja kwenye hili mpaka slaa alipopiga kelele ingawa tulishaanza kupiga kelele mwaka mmoja kabla ya siri kufichuka. Ni vipi takukuru ilipuuzia suala zima na kujifanya haina uwezo mpaka kulazimishwa na bunge huku uhujumu wa hali ya juu unaendelea bot kwa kisingizio cha usalama wa taifa?
Atcl! Tumeingia mkataba bomu, maafisa wa atcl wamejinunulia magarina kuingia mkataba mmbovu ambao unaigharmu serikali na taifa mamilioni ya fedha. Lakini si takukuru au polisi waliokwenda kwa haraka kuwachunguza kina mattaka kuhusiana na hili.
Ripoti ya cag. Utouh katoa ripoti mwaka jana inayoonyesha uzembe uliokithiri ambao una harufu ya ubadhirifu wa karibu shilingi trilioni 3! Lakini sijasikia takukuru wakichunguza hasa lile suala la mikataba na manunuzi yanayofanyika bila kufuata taratibu.
Cha maana takukuru walichofanya ni kukamata watu kwa tuhuma za rushwa ndogo ndogo na za uzandiki kama suala la kina mollel na laizer wa arusha na kugombea nafasi nec ccm na sasa hili la mrema wa tanroads.
Je kuna faida gani kuendelea kuwa na imani na serikali na vyombo vya dola na sheria ikiwa vinafanya mambo kwa upendeleo?
Imenishangaza kusikia kwamba sasa Rostam badala aende mahakamani alikoshauriwa kwenda kwa lengo la kujisafisha mbele ya jamii ya watanzaia, amekimbilia TAKUKURU.
Watanzania bana mnanichosha sana sijui uvivu wa kufikiri na kung'amua mambo? Huyu papa katumia haki ya msingi na ya kikatiba amepeleka vielelezo vyake vya kumtuhumu Mengi sasa na Mengi nae ana haki ya kutumia haki ya msingi kupeleka ushahidi wake kama anao wa kumtuhumu RA apeleke mahala husika kama alivyo fanya huyu papa.
Mkuu wewe ulitaka apeleke wapi?
Sasa wewe unaonyesha wazi kuwa hutaki RA ashutumiwe. Basi tukutake radhi!
Watanzania bana mnanichosha sana sijui uvivu wa kufikiri na kung'amua mambo? Huyu papa katumia haki ya msingi na ya kikatiba amepeleka vielelezo vyake vya kumtuhumu Mengi sasa na Mengi nae ana haki ya kutumia haki ya msingi kupeleka ushahidi wake kama anao wa kumtuhumu RA apeleke mahala husika kama alivyo fanya huyu papa.
Mkuu wewe ulitaka apeleke wapi?
Imenishangaza kusikia kwamba sasa Rostam badala aende mahakamani alikoshauriwa kwenda kwa lengo la kujisafisha mbele ya jamii ya watanzaia, amekimbilia TAKUKURU.
Lakini ni vema tuangalie kwa nini anakimbilia huko. Je kuna nini huko?
Huko TAKUKURU ndo kule shauri la Richmond lilipopelekwa lilisafishwa kabisa.
Ndo huko huko ambako mkurugenzi wake hashikiki ingawaje amekwishashutumiwa kwa mambo kadhaa.
TAKUKURU ilikuwepo Dr. Slaa alipotaja majina ya mafisadi lakini ilikaa kimya hadi moto ulipozidi ndo wale walaji wa EPA walipopekwa Kisutu.
TAKUKURU isiyo na meno, ambayo RA anaijua vizuri kwamba haina mpango wa kuwabana makada wa CCM na hasa maswahiba wa rais ndo sasa RA anapeleka malalamiko na uthibitisho kwamba Mengi ni mkwepa kodi na madeni ya mabenki.
RA anajua wazi kuwa kufanya hivyo TAKUKURU haitahangaika na ukweli ulioko katika madai kwamba yeye ni fisadi papa na ya kwamba amewahujumu watanzania yeye binafsi.
RA anajua wazi kuwa anaiweka TAKUKURU busy kushughulika na eti madai dhidi ya Mengi na lazima ofisi hiyo yetu tunayoigharamikia kwa kodi nyingi itajifanya blind dhidi ya uozo wa RA na kupoteza muda mwingi kumchunguza Mengi halafu wanaamini kuwa temperature ya madai dhidi ya mafisadi papa itapoa tu yenyewe.
Ninasubiri kuona TAKUKURU itampa tafu gani RA.
Watanzania bana mnanichosha sana sijui uvivu wa kufikiri na kung'amua mambo? Huyu papa katumia haki ya msingi na ya kikatiba amepeleka vielelezo vyake vya kumtuhumu Mengi sasa na Mengi nae ana haki ya kutumia haki ya msingi kupeleka ushahidi wake kama anao wa kumtuhumu RA apeleke mahala husika kama alivyo fanya huyu papa.
Mkuu wewe ulitaka apeleke wapi?
Mkuu,
Sasa umeanza kuiita TAKUKURU kimbilio la mafisadi kwa facts zipi?
badala ya kuwashauri watanzania wenye ushahidi kuwasiliana na polisi au TAKUKURU wewe unaanza kutumia jambo la RA kwenda TAKUKURU kuifanya taasisi yote ionekane ya kifisadi?
Inaelekea hapa JF tumechanganyikiwa hata hatujui nini tunataka, hatuna msimamo mmoja unaoeleweka, tunayumba, tunatapatapa kwa kuangalia mhusika ni nani.
RA katumia haki yake kama Mtanzania mwingine, muhimu ni kuwashauri wengine wenye habari kuhusu uhalifu kuweza kuzifikisha kwenye vyombo vyetu vya usalama.
Huwezi kumlazimisha mtu aende sehemu unayotaka wewe, mtu anaweza kwenda polisi, anaweza kwenda vyombo vya habari ili viandike, anaweza kwenda mahakamani, anaweza kwenda TAKUKURU.
Kitu ambacho hutakiwi kufanya ni kuilamu taasisi yote kama TAKUKURU kwamba ni kimbilio la mafisadi. Je wale walioko mahakani baada ya kupelekwa na TAKUKURU sio mafisadi?
Ndio TAKUKURU wana matatizo na wanatakiwa kuongeza ufanisi na kupunguza kuwa tegemezi sana kwa serikali, lakini hiyo sio sababu ya kuwaita TAKUKURU kimbilio la mafisadi.
Sio kila case unaweza kupeleka mahakamani. RA anaweza kwenda mahakamani kumshitaki Mengi kwa kumkashifu lakini hawezi kwenda mahakani kumshitaki Mengi kwa kuiibia NICO au mabank. Hiyo ni kazi ya serikali kama sikosei.
Hawa jamaa watoe ushahidi walio nao ili tuwajue vizuri hawa papa na Nyangumi bila kujali ni Mengi au RA.
Tatizo la watu wengi hapa ni double standards, kama Mengi amekosea sio fisadi, kama RA ni fisadi. Hawa wote mapapa na Nyangumi ni mzigo kwa Tanzania. List haiishii hapo, wako wengi mno. Wakiumbuana ndio faida kwa sisi wananchi.
. Una hisa New Habari Cooperation? Mbona unaelezwa lakini huelewi? Usiwe kama Jackton Manyerere, unaambiwa Takukuru ndiyo iliyosafisha mafisadi wa Richmond na kwamba bila ya jitihada za Kamati ya Bunge ufisadi huu ungepeta, iweje leo Takukuru hiyohiyo iwachunguze tena wahusika walewale iliyokwishawasafisha?TAKUKURU kimbilio la mafisadi kwa facts zipi?
. Una hisa New Habari Cooperation? Mbona unaelezwa lakini huelewi? Usiwe kama Jackton Manyerere, unaambiwa Takukuru ndiyo iliyosafisha mafisadi wa Richmond na kwamba bila ya jitihada za Kamati ya Bunge ufisadi huu ungepeta, iweje leo Takukuru hiyohiyo iwachunguze tena wahusika walewale iliyokwishawasafisha?