Mkuu internet banking ya crdb ni huduma nyingine tofauti kabisa na mtoa hoja alivyoainisha. Hapa kwenye hii mada inazungumziwa tatizo la ku-link paypal account na kadi ya crdb(visa/master). Kama ambavyo mdau mmoja hapo juu alivyoeleza,ukishafungua account ya paypal, hatua inayofuata ni ku-link kadi yako na paypal account. Paypal watacharge kama usd 1 au 2 toka kwenye account yako, na watakwambia uende bank yako ukaombe statement ambayo itaonyesha reference ya hiyo transaction. Mwishoni mwa hiyo reference utaona code(4 digits) ambazo hizi ndio muhimu kwako, kwani utakapokuja kulogin kwenye paypal ukienda sehemu ya kuverify card yako watakutaka uingize hizo code.
Changamoto iliyopo hapa ni kwamba transaction hii huchukua siku kama 3 kuonekana kwenye akaunti yako. Ingawa ukienda bank(crdb) hata kabla ya siku hizo 3, kuna namna ambayo wenyewe wanaweza kuona hiyo transaction reference. Na vilevile si wafanyakazi wote wa bank(crdb) wanaoelewa mambo ya paypal kwani hamna mkataba au mahusiano ya moja kwa moja kati ya bank(crdb) na paypal.