Paul Makonda, jembe liliosahaulika pamoja na kuinyoosha Dar. Lilimpigia chapuo Samia Suluhu kupata Umakamu wa Rais

Sisi ndo tunaamini Cheo ni Hisani ya Mtawala na viongozi wapo wengi.

Wewe tuendelee kupiga jalamba tu hamna namna.

Nchi hii yetu sote kila mtu ana haki ya kuwa kiongozi ila hisani ya mtawala itamwangukia nani?

Hilo ndio zoezi
Right mkuu
 
Mkuu kabsaaa huyu Ni Bashite mwenyewe...huyu anatakiwa Lupango kujibu shutuma sio tuhuma. Huyu kwenye nchi zilizo na utawala bora alitakiwa kunyea kwenye debe mda huu!!
Kabisa MAKONDA ametesa sana watu na kawadharau sana wenye visomo na nafasi zao kisa kuliwa kiboga na Mwendazake. Jela hawezi kwepa
 
Kila mtu atakubali kuwa huyu jamaa aliionyoosha Dar. Maana vibaka, wazembe wa kila aina, wauza unga na matapeli walikiona cha moto.

Mbali ya hayo ni Makonda aliyempigia chapuo mama Samia awe makamu wa rais mwaka 2014 wakati bunge la katiba likiendelea mkoani Dodoma.

Cha ajabu amesahaulika kabisa kana kwamba sio jembe linalofaaa.
USED
 
Kabisa MAKONDA ametesa sana watu na kawadharau sana wenye visomo na nafasi zao kisa kuliwa kiboga na Mwendazake. Jela hawezi kwepa
We mse... Pumbavu mkubwa acha kutafuta mabwana.
 
Hata sisi tunatamani kuteuliwa.., mtu kama alishateuliwa akaacha mwenyewe saivi wa nini??
 
Nafasi ni chache watu ni wengi.
Waganga wa jadi na manabii uchwara wote wangelamba teuzi kwa mtindo huo wa kutabiria watu hali ingekuwaje?

Hata hivyo, alijiondoa mwenyewe baada ya kuona kala bata la kutosha na level aliyofikia hakustahili kuwa alipokuwa.

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
 
Nashauri tusiingilie mahesabu ya mama! Kuna mmoja anayeheshimika sana aliwahi kusema "usinipangie" na hatukuwahi kusikia watu wakimpangia!! Hali kadhalika tusimpangie mama!! As simple as that! Nashangaa watu wanajitoa ufahamu na wanataka kumpangia mama!! Uzuri wa kutokumpangia ni kwamba atajisikia kuwajibika vizuri kwa matokeo ya uchaguzi wake!! Vinginevyo atasema "haya sasa, mnalia nini si mlimtaka wenyewe?"
 
Back
Top Bottom