Paul Makonda hatafika mbali na atakuwa sababu ya CCM kupoteza mvuto kanda ya ziwa na maeneo mengine

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Mike Tyson alipozidiwa ujanja na Evander Holyfield, Tyson alimng’ata Evander sikio na ilikuwa aibu kwelikweli siku hizo na pia ulikuwa mwisho wa umaarufu wa Tyson.

Je watanzania mnajua kwanini nchi nyingi barani Africa ukabila ni tatizo kubwa? Na ni akina nani walianzisha ukabila huo na kwa madhumuni gani?

CCM wameshatumia mbinu zote chafu kushinda chaguzi nyingi na wasichokijua ni kwamba mtu huishiwa mbinu mwishoni na kuanguka.

Hii mbinu Makonda wanayotumia CCM sasa ili kuwini lile kundi Sukuma ni mbinu itakayoweza kuwalipukia CCM na kuwafanya wakataliwe maeneo mengine nchini. Tumeona pia mbinu Biteko ilivyotumika kwa kuunda cheo cha naibu waziri mkuu ambacho kikatiba hakipo,

Kuelekea 2025 wataunda mbinu Masanja na hata mbinu Maganga na bila kujua watajikuta wanabaki na kabila flani na kuchukiwa na wengine wote.

Kuwatenga watu kikabila ni strategy mbovu sana Tanzania na ina laana kubwa! Mkumbuke hata Magufuli alicheza rafu zote kuwahi kuchezwa katika historia ya chaguzi za Tanzania pamoja na kuwa Msukuma wa Geita na kumwaga miundombinu kibao huko! Sasa mtu wa Mkunazini anafikiri atakubalika kanda ya ziwa kwa mbinu hizi?

Mbinu Makonda inaipasua nchi na CCM pia. Lakini kwanini CCM imefika pahali pa kutumia mbinu hizi ili kushinda na bado hawashindi kihalali? Ni dadili za kuufikia mwisho wa safari yao?
 
Mbinu Makonda inaipasua nchi na CCM pia. Lakini kwanini CCM imefika pahali pa kutumia mbinu hizi ili kushinda na bado hawashindi kihalali? Ni dadili za kuufikia mwisho wa safari.
“ KARMA “ Law of the Universe !
Fimbo ya mnyonge hulipwa na Mungu !
What goes around comes around !!
Wengine tupo pembeni tunatumbua macho na kuugulia maumivu waliyotusababishia kwa kiburi cha nguvu na mapesa yao !!
Ngoja Tusubiri tuone !!
 
Kwa ujumla ni ubaguzi unamaanisha let’s wait and see japo style ya mwenezi ni hivyo kabisa
 
Nilikuwa napita safarini naona watu dancing in the rain wanamsubiri Makonda.
Tulipofika Maswa tukaona kigari.mkokoteni wa punda. Yule dreva wetu akasema,"Hawa wanamsubiri Makonda,akifika hapa atapanda huu mkokoteni".
 
Bila hofu nina imani Samia anajuta huko alipo kama kuna mtu alimdanganya kumrejesha Makonda hapo alipo anajuta. Makonda anakivuruga chama hasa.
 
Muda ni mwalimu mzuri sana, the way nilivyoona akimpandishia mwandishi aliyekuwa akimhoji nimeziadi kuamini kuwa huyu mtu sio kabisa na hafai bado!
 
Bila hofu nina imani Samia anajuta huko alipo kama kuna mtu alimdanganya kumrejesha Makonda hapo alipo anajuta. Makonda anakivuruga chama hasa.
Makonda anafanya yale ambayo yatawadhibiti wale ambao wanakimezea mate kiti cha Maza kutoka Chamani 2025 !!
Makonda yupo pale kwa mkakati maalum wa kudhibiti mahasidi wa Mkuu !
Ngoja tuone. 😅🙏🙏
 
Wewe upo chama gan mkuu, tuanzia kwanza hapo. Ili tujue kama unaongea kwa facts au kwa mihemko ya chama.
 
Matarajio yetu wapinzani wa Makonda, Samia na CCM mngeshangilia.
Ajabu nyote mnahaha, mnaweweseka na kuumia!
Hili linanishanigaza sana, wapinzani ndio wanaionea huruma na kumshauri Mwenyekiti wa CCM abadilishe uteuzi wake, badala ya kufurahia.

Screenshot_20231116-133654_1.png
 
Nilikuwa napita safarini naona watu dancing in the rain wanamsubiri Makonda.
Tulipofika Maswa tukaona kigari.mkokoteni wa punda. Yule dreva wetu akasema,"Hawa wanamsubiri Makonda,akifika hapa atapanda huu mkokoteni".
20231117_130809.jpg
Unazunguka na V8 40 halafu mita chache karibia na kituo unapanda punda, trekta, mkokoteni, baiskeli, bodaboda ili kuonesha wewe ni mwenzao. Ukisikia wajinga ndio waliwao ndio hii✍️

🔷 CCM wanatuona mafala sana✍️
 
Mike Tyson alipozidiwa ujanja na Evander Holyfield, Tyson alimng’ata Evander sikio na ilikuwa aibu kwelikweli siku hizo na pia ulikuwa mwisho wa umaarufu wa Tyson.

Je watanzania mnajua kwanini nchi nyingi barani Africa ukabila ni tatizo kubwa? Na ni akina nani walianzisha ukabila huo na kwa madhumuni gani?

CCM wameshatumia mbinu zote chafu kushinda chaguzi nyingi na wasichokijua ni kwamba mtu huishiwa mbinu mwishoni na kuanguka.

Hii mbinu Makonda wanayotumia CCM sasa ili kuwini lile kundi Sukuma ni mbinu itakayoweza kuwalipukia CCM na kuwafanya wakataliwe maeneo mengine nchini. Tumeona pia mbinu Biteko ilivyotumika kwa kuunda cheo cha naibu waziri mkuu ambacho kikatiba hakipo,

Kuelekea 2025 wataunda mbinu Masanja na hata mbinu Maganga na bila kujua watajikuta wanabaki na kabila flani na kuchukiwa na wengine wote.

Kuwatenga watu kikabila ni strategy mbovu sana Tanzania na ina laana kubwa! Mkumbuke hata Magufuli alicheza rafu zote kuwahi kuchezwa katika historia ya chaguzi za Tanzania pamoja na kuwa Msukuma wa Geita na kumwaga miundombinu kibao huko! Sasa mtu wa Mkunazini anafikiri atakubalika kanda ya ziwa kwa mbinu hizi?

Mbinu Makonda inaipasua nchi na CCM pia. Lakini kwanini CCM imefika pahali pa kutumia mbinu hizi ili kushinda na bado hawashindi kihalali? Ni dadili za kuufikia mwisho wa safari yao?
sijawahi kuamini kwamba makonda ana akili timamu nipo tayari kukosolewa. yaani asiende kumzika dictata magufuli akazulu kaburi lake? how
 
Back
Top Bottom