Paul Makonda awekewe ulinzi mkali sana kumzunguka kwa sababu ni hazina kwa Taifa

Ndugu zangu Watanzania,

Kupata viongozi aina ya Mheshimiwa Paul Makonda Wenye ujasiri wa kiwango cha juu kama alicho nacho katika kuwatetea, kuwapigania, kuwasemea, kuwakingia kifua wanyonge ni ngumu sana. Ni kazi inayohitaji kujitoa na kujitolea, ni kazi ambayo haihitaji kumuangalia mtu usoni katika kufanya uamuzi, ni kazi inayohitaji moyo wa chuma, moyo wa ujasiri, moyo wa kujitoa ,moyo wakusema acha nikosane na mapapa lakini niwaokoe na kuwafuta machozi wanyonge.

Paul Makonda ni aina ya kiongozi kijana ambaye Taifa letu linapaswa kumlinda kwa wivu mkubwa sana kama mboni ya jicho. Kwa kuwa ujasiri alio nao ndani ya moyo na kifua chake anatufaa sana huko mbele ya safari . Ni mwanadamu wa kipekee sana aliye zaliwa katika ardhi ya Tanzania. Ndio maana unaona kwa sasa namna watu na wananchi wanyonge wanavyo miminika na kufurika kwa wingi katika mikutano yake ili kufikisha kero zao.ndio maana wananchi wanapigana vikumbo huku wakibubujikwa machozi ili wasaidiwe na kuponywa majeraha ya mioyo yao.

Paul Makonda alindwe kwa nguvu zote na kwa gharama za aina yoyote ile,kwa sababu wenye kuguswa maslahi yao hawawezi kufurahi wanapoona akiendelea kuwapambania wananchi. hivyo watampiga mishale ya Majungu,fitina,uzushi,uongo na kila aina ya mishale ya maneno ili kutaka kumdhoofisha na kumrudisha nyuma katika juhudi zake za kuwatetea wanyonge. Watataka wafanye kila liwezekanalo ili kumchongea uongo kwa Mheshimiwa Mwenyekiti wetu.

Taifa letu na katika nchi za kiafrika ni muhimu sana na kwa gharama zozote zile kuwalinda kwa nguvu zote viongozi aina ya Mwamba Paul Makonda.hasa ikizingatiwa ukweli kuwa wengi wetu wa Afrika tukiwa mezani tunakula hatusemi mpaka tumalize chakula.ndio maana leo unaweza kuta mtu alikuwa ni kiongozi mkubwa kama waziri au mkuu wa wilaya au mkoa au mkurugenzi au katibu ndani ya chama au serikali ,alikuwa kimya muda wote lakini anapotolewa katika uongozi anaanza kutoa maneno ya chuki na uzushi kwa serikali na chama na kwa baaadhi ya watu walio uongozini kwa sababu tu hayupo uongozini Au madarakani.

Lakini ukimuangalia na kumfuatilia Mwamba na komandoo Paul Makonda unaona Namna yeye alivyo mtu wa tofauti sana.yeye ni mtu ambaye muda wote na wakati wote anajikita kutatua kero na kuwasikiliza wanyonge. Makonda hata leo hii ukimpa uenyekiti wa kitongoji basi ni lazima kitongoji hicho kitafahamika Tanzania nzima na hata nje ya nchi.kwa sababu Makonda ni mtu mbunifu sana na kiongozi mchapa kazi sana.

Jiulize kabla ya Paul Makonda hajawa DC kila mtu aliona kama nafasi ya kawaida lakini alipoingia na kupewa Ukuu wa wilaya kila mmoja akajuwa kumbe mkuu wa wilaya anaweza fanya mambo makubwa katika wilaya kusaidia wananchi? Hata alipokuja kupewa ukuu wa mkoa napo watu ndipo wakaja kutambua nguvu ya mkuu wa mkoa na mamlaka makubwa aliyo nayo mkuu wa mkoa.mpaka kuamsha wengine kutoka usingizini. Haya yote ni kutokana na ubunifu, uchapakazi,ujasiri,uzalendo na moyo wa kujitoa alio nao Paul Makonda.

Leo amepewa ukatibu wa itikadi, uenezi na mafunzo ya chama cha Mapinduzi Taifa kila mtu anaona namna mchaka mchaka unavyopigwa mitaani.namna moto unavyowaka na kuwashwa ,namna watu walivyoamka na kutambua nguvu ya chama katika kuisimamia serikali iliyotokana na CCM.kila mtu anaona namna mikutano yake ilivyogeuka kuwa kimbilio la wanyonge .jiulize ni kwanini? Jiulize je hakuna viongozi katika maeneo hayo anayopitia?

Jiulize kwanini wananchi hawapeleki kero huko na badala yake wanaona Makonda kama tumaini jipya katikati ya giza na kukata Tamaa? Wapi tumekwama? Viongozi ngazi za mikoa na wilaya wanajisikiaje wanapoona hali hiyo? Hawaoni kuna mahali wameshindwa kutimiza majukumu yao? Hawaoni wananchi wamekosa msaada kutoka kwao? Hawaoni wanapaswa kuwa wanyenyekevu na wasikivu kwa wananchi na kujenga mazingira ya kufikika na kuaminika na watu?

Makonda ni kama kiraka tu ambaye popote utakapo mpeleka na kumpachika lazima akupatie matokeo makubwa na Chanya. Shida yetu wa Afrika unakuta mwingeni badala ya kumsaidia na kumuunga mkono anaanza kuona wivu ,chuki na kuwa na kinyongo kuona Makonda anasifiwa na kukimbiliwa na watu wenye shida.swali ni kuwa wewe unayeona wivu ni nani anayekuzuia kuzuia kufanya kama Makonda kuwasikiliza watu? Nani amekuzuia wewe kuchapa kazi kama Makonda?

Mliopewa uongozi sehemu yoyote ile acheni kufanya kazi kwa mazoea, acheni Umungu mtu,acheni Majungu, uzushi, fitina, uchawi na uzembe.kuweni wanyenyekevu, waungwana, wapole, wasikivu, wenye utu,wacha Mungu, watenda haki na wazalendo wa kweli.jueni uongozi ni dhamana tu. Acheni viburi na roho mbaya. Mtu unafanya ofisi ya umma kama mali yako? Unamzungusha mtu anayetaka msaada ofisi ya ofisi ya umma mpaka mtu anatokwa machozi halafu wewe huna habari.

Hongera sana sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Dr Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kutuletea Paul Makonda. Nafikiri unaona na unafuatilia kila kinachojili katika ziara zake. Unaona malalamiko ya wananchi, unaona na kusikia kero za wananchi. Unapata taswira nzuri ya kazi ya watendaji na viongozi mbalimbali uliowateua huko ngazi za mikoa mpaka chini huko.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
KERO Anazo tatua zimetokea,zimetokana na chama Gani Cha upinzani!?
 
Kwa hakika Mheshimiwa Paul Makonda anahitaji kuungwa mkono na sisi watanzania wazalendo zidi ya wacheche wanaoweza taka kumkwamisha kiongozi wetu huyu aliyeamua kujitolea kwa ujasiri mkubwa kuwatetea na kuwasemea watanzania wanyonge.
Sidhani kama unajua sifa za uongozi.
Anachofanya makonda ni usanii na sio uongozi!
 
Hii nchi inapiga marktime sababu watu wenye akili wamewaacha watu kama nyie mfanye mtakavyo kwenye siasa!
 
Marekani hao hao na unafiki wao ndio walisema Saddamu Husseni anamiliki silaha za maangamizi.lakini mwisho wa siku hawakuionyesha Dunia hizo silaha. Ni hao hao ndio walioshiriki kumuua Gadaffi kwa uonezi na kwa maslahi yao tu.
Wewe ni jinga, umechangia umaskini wa taifa hili shetani mkubwa wewe na mawazo mfu kama haya.
 
Style ya uongozi wa makonda ilishapitwa na wakati uwezi kuwatisha watendaji wa nchi kwa kelele na mikwara aliyafanya sana mwendazake ila haikusaidia sana sanasana iliumiza watu na familia zao.

Watendaji wanapaswa kuimizwa kufuata utaratibu na miongozo ya kazi zao katika kutumikia wananchi watendaji waelemishwe bila kuchoka majukumu yao na yeyeto atayeenda kinyume sheria zifuate mkondo wake bila kupapasa papasa..

Issue ya maadili na nidhamu kwa hii nchi sasa ni bidhaa hadimu sana kwa hawa viongozi wetu. Tujisahihishe.
Kwani unafikiri mtu wa chini au wakawaida asie na mtetezi huko juu atatetewa na nani? Kwa mfano utakapokwenda wanakwangalia waone kama unaweza kuwatikisa kama uko loose hata haki yako hupati. Ndo imetoka ....
Tunahitaji vijana wajasiri wala usikatae mku
 
Sidhani kama unajua sifa za uongozi.
Anachofanya makonda ni usanii na sio uongozi!
Unaanzia wapi kusema ni usanii wakati unaona namna watu wanavyopata majibu katika kero zilizokuwa zikiwatesa? Huoni akiwa kimbilio la wanyonge wanaofurika kupata tumaini jipya kwa mwamba mwenyewe Paul makonda. Huoni namna maelekezo yanatolewa na kufanyiwa kazi?
 
Naona umeishia kutukana tu kama mlevi aliyezidiwa gongo kichwani aliyobugia na njaa tumboni.
Mimi ni mlevi mwenye busara,kuliko wewe mchungaji,Shehe usiejua kutofautisha rangi ya KANIKI & KAKI.😂😂😂😂😂😂😂.Bay the way,sijatukana,ila umejikuta unajikuta humohumo.
 
Hivi Mh Makonda anajisikiaje akiona matokeo ya form four wenzake wamepata div 1 wakati yeye alishindwa kupata hata four ikabidi aibe vyeti?
 
Back
Top Bottom