Paul Chizzi amuumbua Mwakyembe

Mbona anaye kanusha ana zungumzia TUMBONI...! aite press achambue hizo hayo madai sio mwandishi amfuate amuombe kuelezea!.... BIG UP MWAKYEMBE
Fuatilia vizuri we jamaa, hata kama ni gazeti la Kiingereza na shule za kata hazina walimu wa kutosha lakini ukweli ni kuwa Mwandishi wa habari kwa kuogopa kukurupuka kama magazeti yenu mengine alimfuata Chizi kujua ukweli na Chizi akatoa ukweli. Sasa wewe unaona dili na mahala alipozungumzia na sio fact aliyotoa. Ndio maana akina Mwakyembe ni mashujaa kwa kuwa wanajua jamii inayowazunguka inataka nini, yaani WAPE WATOTO NYAMA WANYAMAZE...
 

Other materials ndo iyo keep chenji Yao....yani kwa Lugha nyepesi "for tumbo street use only" a.k.a Vijisenti Kama vya Chenge.
inatisha...yani other materials imezidi hata bei ya kupachezi kilichowapeleka huko kwa kina Jack Chan? Mmh!

Mathematics Exercise:

50,000$ - 18,000$= 32,000$
Mmh! Yani other materials imenunuliwa kwa dola 32,000/=......duh! Huyu kweli Chizi.:confused2:
 
ndio sababu hata contracts za kimagumashi siku hizi wanapendelea kuchukua china...maana kule wanapewa bei poa wakija hapa TZ wanacheza dili na mahesabu....kwa kifupi chochote wanachofanya uchina kina faida kubwa sana kwenye wizi wao ukilinganisha na sehemu nyingine duniani....
 

Majina mengine uchuro. Hivi zile uniforma mmeziona zilivyo mavi matupu? Hizo nguo nafikiri angepewa mama Africa Sana kuanzia kudesign, kushona kudeliver hazifikia hata milioni hizo walizotuchapa.

Chizi apeleke uchizi wake nyumbani kwake, ma Pilot wafanye kazi.
 

Coment za mafisadi Hizi.......eti "kaeni pemben WATAALAM walumbane" mmmmh!
 
..... unafurahisha mjomba kama huyo jamaa ni msafi, kwanini assiite vyombo vya habari kutoa ufafanuzi badala yake waandishi wamtafute na wamuombe kuzungumzia madai hayo!
 
Ndugu Chizi maagent wako umu wanaweza tupa tafsiri ya other materials ambazo hutaki ata kuzitaja.Au labda ni nguo za ndani za hao Airhostess.
Alafu unaingia mkataba ata AG hajui kisa wewe umesomea mambo ya Anga,so unajua kila kitu on sheria na Anga?
Una bahati ni Tz nchi zingine usingepata ata mda wa kuhojiwa na magazeti.
Ni busara kukaa kimya bse huwezi rudi kwenye iyo post tena na malumbano hayafai bse taarifa alizosema Mwakyembe nyingi ziko featured kwenye vitabu vyenu ambavyo ungekuwa umeondoka navyo angalau ungekuwa umeficha ukweli
 
yaani nguo za wafanyakazi dola 18000 wakati ndege zenyewe hakuna sa hizo nguo wanazinunua wazitumie wapi?? hii nchi hii...sijawahi sikia uniform ya dola 18000
 


Kwani wazazi Wakimwita Mtoto wao "Chizi" ina maana inahitaji wataalamu wa kigeni Kugundua Mtu ni "Chizi" Kweli? Sasa ATCL WALIKUWA WAPI?
 
jiandaeni kulipa bil zingine na fidia juu kwa hawa madirector.......hivi zile za dowans bil 94 mlishalipa ee!!....
Hamnaaaaa ! Hawa tutawazungusha kama wale wa gongo la mboto !
 
Huyu ni "Chizi" mdogo, asiwasumbuwe !
 
Si ajabu anaitwa chizi....utatumiaje dola 18,000 kushona nguo ambazo zaweza shonwa kwa batiki za hapa hapa na hata Millioni 2 isifike.....

Jina lake linaeleza kila kitu sina la kuongeza zaidi mie ningepewa jina hilo nisingekurupuka ovyo kwenye media
 
Mkuu kama una nafasi nakuomba ukanunue gazeti la leo la Guardian ndio utaamini kuwa kumbe hata wale wenye Phd za ukweli wana matatizo.

Ndugu mimi nataka kuchangia hapa tu kwenye PHD, PHD au any certification yoyote hapa Tanzania does really stand for its credibility.

Yani hapa Tanzania ukisikia a doctor ukaja kumsikia akiongea (either kwenye mazungumzo au kujibu maswali) unaweza kuasikia wewe aibu. Kuongea i mean the way anavyotoa alivyo navyo kichwani ndo utajua hku africa kuna PHD za academics tu bt not more than that. (bt not all, most of them)

There is time nilikuwa nataka kujua kwanini waingereza na wamarekani wanatu demand tufanye TOEFL na ILETS knowing kabisa kwamba tunatumia english shuleni from form 1 to form six. NIkagundua maybe kwasbb wanajua shule tunakariri tu na tunabahatisha hence our results are questionable so they have to prove for themselves by having us sit for their tests.

Utamkuta mwanfunzi ana A kwenye somo au stright As, bt sit down with the student uone hw much he/she anajua kuhusu ilo somo au hayo masomo, u will be suprised.

but Marekani wanafunzi wanaopata 'A's kwenye masomo au Perfect scores kwenye SATs of ACTs huwa ni extraordinary kids, huwa ni little geniuses. Huwa wana IQ kubwa sana.
 

Je ungetegemea bwana Chizi asemeje?.
Basi audhibitishie umma kwamba tulipata wazabuni wazawa (orodha na gharama zao), lakini mali ya kichina ndo ikaonekana ni rahisi.
La sivyo hapa ni mbinu za kujitetea, tukizingatia kuwa wengi wa viongozi wa Tanzania wanaingia madarakani kwa lengo la kujinufaisha tu.
 

Ni vizuri kusoma na kuelewa thread kabla ya kuanza kuchangia. Fedha hizo ni za uniform za wafanyakazi wote wanaoruka na ndege na sio nguo moja tu!!Sasa ni juu yako kujua kuna Pilots na hostesses wangapi ATCL!!
 
huyu mzee ndo maana walimpa misumu afe ..maana anakurupukaga tu...yaleyale ya richmond hakuna cha maana zaidi ya mbwembwe na mikelele
 
Chizi awasilisha barua kwa Waziri Mkuu kupinga 'tuhuma' za Dkt. Mwakyembe dhidi yake - wavuti
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi ambaye hivi karibuni alitenguliwa katika cheo hicho na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wiki jana, amefikisha ramsi malalamiko yake kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Uchunguzi wa gazeti la Habari Leo umebaini kuwa Chizi amewasilisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu akipinga tuhuma zilizoelekezwa kwake na Waziri, Mwakyembe akidai si za kweli na kwamba zimelenga kumshushia hadhi kwa jamii.

Pamoja na barua hiyo, Chizi amewasilisha lundo la vielelezo vikifafanua tuhuma mbalimbali zilizotolewa na Dkt. Mwakyembe dhidi yake, ili kuthibitisha kutokubaliana na tuhuma hizo kwake. Kaimu Mkurugenzi huyo wa zamani wa ATCL alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo alikiri suala hilo kuwasilishwa ofisi ya Waziri Mkuu, ingawa hakuwa tayari kulizungumzia zaidi kwa madai kuwa liko kwenye mamlaka za juu sasa.

Tuhuma ya sare za milioni 80/-

Maelezo ya Chizi kwa Pinda, yanafafanua kwamba ATCL ilinunua loti 30 za vifaa mbalimbali vya wafanyakazi zikiwamo sare zilizotajwa na Dk Mwakyembe kwa thamani ya dola za Marekani 18, 920 na si dola za Marekani 50,000 kama alivyodai Waziri Mwakyembe, hatua ambayo ilifanya ATCL kuokoa zaidi ya Sh milioni 44 kama ingenunua sare hizo nchini kulingana na bei ya ununuzi iliyowasilishwa ATCL.

Tuhuma ya ukodishaji wa ndege

Anapinga pia kuhusishwa na ukodishaji wa ndege aina ya Airbus ambayo Waziri Mwakyembe alisema haikuwa na sababu ya kukodishwa, akisema ndege hiyo ilikodishwa mwaka 2007 na kufanya kazi hadi mwaka 2008, wakati yeye aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Agosti 2011. Dk Mwakyembe akizungumzia mkataba huo tata wa Airbus, alisema umeifanya nchi kudaiwa Sh bilioni 69 na kusisitiza kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yanayoendelea katika shirika hilo.

"Kuhusu ukodishaji wa ndege aina ya Boeing 737 – 500 kutoka Kampuni ya Aerovisto, utaratibu wa kawaida wa ukodishaji wa ndege kwa njia ya wetlease ulifanyika, taratibu zote kama zinavyotakiwa kisheria zilifuatwa.

"Ilikuwa ni suala la kushitua sana kwangu pale nilipopata maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu (Wizara ya Uchukuzi, Omar Chambo) kwamba taratibu hazikufuatwa, na hivyo ndege tuliyoikodi haikutakiwa kuruka kinyume na barua ya Waziri Mwakyembe mwenyewe ya Mei 12, akieleza kuridhishwa na hatua tulizochukua katika ukodishaji ndege na kuturuhusu kuendelea na mchakato," ilisema barua hiyo.

"Suala la kupeleka mkataba wa ACMI kwa AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) ambao si utaratibu wa kawaida, lilikuja wakati mchakato wa kuleta ndege uko katika hatua za juu kabisa. Hata hivyo, maagizo yalizingatiwa; mkataba ulikwenda kwa AG hata baada ya Waziri kutoa maoni yake kuwa ni mzuri. Waziri alitoa kauli kama hiyo pia kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Miundombinu kilipokaa Ofisi Ndogo za Bunge hivi karibuni," ilisema barua hiyo.

Tuhuma za fedha na akaunti

Barua hiyo kwa Waziri Mkuu ikifafanua kuhusu suala la sare za ATCL ilisema lilishafanyiwa uchunguzi baada ya Chambo kuunda Tume kuchunguza ubadhirifu huo ikiongozwa na DAP wa Sekretarieti ya Utumishi wa Umma Shekiondo Magesa na Tume kubaini hakukuwa na ubadhirifu wowote na kumpongeza Chizi kwa kuokoa fedha za Kampuni.

"Madai ya Waziri Mwakyembe kuhusu fedha za bima ni kwamba kampuni ya Alexander Forbes ilitoa taarifa, kuwa fedha za bima zingetumwa kwenye akaunti yetu wiki ya nne ya Mei 2012.

Menejimenti ya ATCL ilikaa na kutafakari agizo la Wizara kutaka fedha hizo zipelekwe CHC (Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma).

"Tulisubiri kupata akaunti ya CHC ili tutoe maagizo hayo. Hata hivyo, akaunti hiyo tulichelewa kuipata, ndipo tulipokwenda benki kutaka kupata njia mbadala ya kuhakikisha usalama wa fedha zetu. Mei 28 dola za Marekani milioni 3 zililipwa kwenye akaunti yetu ya Stanbic na Menejimenti ya ATCL ikaagiza benki ihamishe fedha hizo ili zishikiliwe kama dhamana ya ATCL kupata mtaji wa kujiendesha.

"Maagizo ya kuhamishwa pesa hiyo ili zihifadhiwe na benki yalitolewa kwa benki siku hiyo hiyo Mei 28. Asubuhi ya Mei 29 wakati mchakato wa kuzihifadhi haujakamilika, tulitaarifiwa kuwa dola milioni moja zimezuiwa na amri ya mahakama kutoka Kampuni ya Ultimate Security yenye thamani ya dola 993,000.

"Hapo hapo tulielekeza wanasheria wetu wazuie utekelezaji wa amri hiyo na jambo hilo lilifanyika na pesa hiyo ipo kwenye akaunti salama hadi leo, hakuna aliyelipwa kama alivyosema Waziri Mwakyembe. Shauri hilo litatolewa uamuzi Juni 18," ilisema barua hiyo.

Kulingana na vielelezo vilivyowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu, gazeti la Habari Leo limebaini kuwa wakati Wizara ya Uchukuzi ikiwasilisha barua ya maagizo ya fedha hizo za bima kuwekwa kwenye akaunti ya CHC, malipo hayo ya bima yalikuwa yamelipwa kupitia akaunti ya Stanbic na kampuni ya Alexander Forbes asubuhi siku hiyo.

Gazeti la Habari Leo lilipowasiliana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo jana, alithibitisha kupokewa kwa malalamiko hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa ATCL na kusema ofisi yake ilikuwa bado inayafanyia kazi ili kufahamu mwenendo mzima wa suala hilo kabla ya kulizungumzia.

Soma habari nzima katika tovuti ya gazeti la HabariLeo

Source: Previous Posts - wavuti
 
Kila mtu anapokuwa amebanwa lazima atafute utetezi hata kama ni wa uongo, hapo Chizi anatapatapa tu ukweli unabaki palepale, ATCL kulikuwa na ubadhirifu mkubwa saana, Miaka Ishirini iliyopita kulikuwa na ndege kubwa zaidi ya tano,Leo hii shirika hoi, Loh tumechoka kudanganywaa!!!
 
nafikiri ni kwa sababu wanapem\nda kufanya kazi kisiasa sana kuliko kutumia taaluma
na elimu yao ikiwadia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…