Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo, Februari 3, 2023 Kwenye Bunge la 10, Kikao cha 4
Serikali yasema Vijana 1,732,509 hawana ajira
Akizungumza Bungeni, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Paschal Katambi amesema:
“Utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa Mwaka 2021 unaonesha kuwa vijana wenye umri wa miaka 15-35 ambao wanaukosefu wa ajira ni 1,732,509 sawa na 12% ya nguvu kazi ya vijana wenye umri huo ambao hawana ulemavu unaowazuia kufanya kazi.
“Katika kuhakikisha vijana wanaendelezwa ili kushindana katika soko la ajira ndani na Nje ya Nchi, Serikali imeweka mkakati wa kitaifa wa kukuza ujuzi wa miaka 10 ambapo imefanya maboresho ya mitaala katika elimu ya juu na ya kati kwa mafunz ya stadi ya ufundi.
Pia kuna maboresho kwa vijana walio nje ya mafunzo rasmi kama uanagenzi, mafunzo ya uzoefu kazini (internship) na mafunzo ya kilimo cha kisasa.
MBUNGE APENDEKEZA MAWAZIRI WAPATIKANE KWA KUOMBA KAZI
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akiwa Bungeni amehoji “Kwanini Serikali isiache utaratibu wa ajira kwa njia ya uteuzi ili kupata watu wenye uwezo ambao hawatiliwi mashaka, ajira ipatikane kwa njia ya ushindani iwe kwa viongozi, watendaji, Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na watendaji wengine Serikalini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Paschal Katambi akajibu “Kwa sasa Katiba yetu ya Mwaka 1977 inaeleza mfumo wa uendeshaji wa Serikali na inatambua mifumo ya uteuzi na ushindani kulingana na nafasi zinazohitajika.”