Patrice Lumumba University of Russia: Ngome kuu ya majasusi wa KGB ya kufunza itikadi za Ujamaa kwa wanafunzi kutoka nchi masikini za Dunia ya Tatu

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Patrice Lumumba University of Russia: Ngome kuu ya majasusi wa KGB ya kufunza itikadi za Ujamaa kwa wanafunzi kutoka nchi masikini za Dunia ya Tatu.

IMG_20191111_092657_816.jpg

UTANGULIZI

Wakati wa kipindi cha vita baridi, People's Friendship (Patrice Lumumba) University of Russia (PLUR) kilitumiwa kama "Ngome" kuu ya idara ya ujasusi ya Soviet Union iliyojulikana kama KGB kwa kufunza damu changa ya vijana wenye nia ya ujamaa kutoka Afrika, Amerika Kusini, Asia ya Kusini-Mashariki na waarabu wa Mashariki ya Kati ambao wangefanywa baadaye kuwa viongozi wa nchi zao au wanamapinduzi.

Watu mashuhuri waliopata kusoma chuo hicho cha Patrice Lumumba ni pamoja na Osama Bin Laden, Mahmoud Abbas, Yasser Arafat, Fidel Castro, Che Guavara pamoja na Vladmir Putin.

Fidel Castro in his 1945 high school yearbook, left, and a 22-year-old Ernesto Guevara in 1951 while in Argentina


b2de255d276149c68d83f11daefd9388_18.jpg


CARLOS THE JACKAL
Ilich Ramírez Sánchez (Carlos the Jackal) ni mmoja wapo ya wanafunzi mashuhuri (Notable Alumni) wa chuo hicho. Baada ya Carlos kuwa trained na KGB aliondoka Russia na kwenda Lebanon kuungana na kikundi cha ukombozi cha PFLP (Popular Front for the Liberation of Palestine) ambapo central command ya PFLP iliyokuwa chini ya bwana Waddie Haddad ambaye pia ni product ya KGB ikampokea na kumpa Carlos mafunzo zaidi ya ujasusi.

Akiwa kijana mdogo kabisa Carlos aliteuliwa kuongoza kikundi cha vijana cha PFLP kupambana vita ya Black September. Bwana mdogo alibadili kabisa upepo wa vita hiyo, jeshi la Jordan liligaragazwa vibaya mno, Sanchez alichora mbinu za uvamizi zilizowachanganya maadui.

Alibuni magwanda ambayo yalifanana sana na yale ya jeshi la Jordan, akachora ramani ya kutengenga mitaro ya chini kwa chini (tunnels) kutoka walipoweka kambi hadi walipo jeshi la Jordan, walifika eneo la tukio usiku na kisha kujichanganya na wanajeshi wa Jordan. Baada ya hapo mashambulizi yanaanza.

Huyu ndiye Ilich Ramírez Sánchez (Carlos the Jackal)

images.jpg


Kiongozi mkuu wa PFLP Generali Wadie Haddad alifurahishwa na umakini wa Carlos hivyo kuamua kumpeleka Baghdad Iraq akapate mafunzo ya juu zaidi ya kijeshi. Mwaka uliofuata Carlos alienda mafunzoni Baghdad kisha akatumwa kikazi London na ndipo alianza matukio ya kigaidi.

Becoming a widely feared terrorist with his own small network of operatives, he allegedly worked during the 1970s and 80s for Muammar al-Qaddafi, Saddam Hussein, and Fidel Castro, for revolutionary groups, and for East European security agencies.

LIEUTENANT COLONEL VLADMIR PUTIN
Vladmir Putin kabla ya kuwa Rais wa Russia alikuwa ndiye boss wa kwanza wa KGB akiwa na cheo cha Lieutenant Colonel na haijawahi kutokea tena mpaka leo hii kwa maana Kwa kawaida idara ya ujasusi ya KGB ilikuwa ikiongozwa na wanajeshi wa vyeo vya Major Generals tu tangu kuanzishwa kwake.

IMG_20191110_120327_122.jpg


Baadae akaja akawa resident spy/station chief wa KGB huko jijini Dresden East German akiratibu shughuli (liaison officer) za idara ya usalama ya East German iliyokuwa inaitwa Staatssicherheit (Stasi) pamoja na zile za KGB.

YASSER ARAFAT
Wakati comrade Yasser Arafat alipotembelea Moscow mnamo mwaka wa 1968, Moscow ilianza kumuona kama vile ni mtu wao, na mwaka uliofuata Arafat akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa PLO (Palestinian Liberation Organisation). Mahusiano imara baina ya Soviets na watu wa Palestine ndio yakawa yameanzishwa.

images-15.jpg


Mpaka kufikia mwaka wa 1970, baada ya Soviets kupoteza ushawishi wake kwa Misri, mahusiano na wanamgambo wa kipalestina ulikuwa umeimarishwa zaidi na kuanzia hapo silaha pamoja na mafunzo ya kijeshi kutoka Soviet vilianza kupelekwa kwa makundi hayo ya wapalestine.

Ukweli ni kwamba, KGB ndio waliokuwa wanaamua kundi lipi linapaswa kupokea msaada wa kifedha pamoja na silaha na mpaka kufikia mwaka 1972 Soviets walikuwa wametamka ya kwamba harakati za wapalestina ni nguzo muhimu sana katika ukombozi wa waarab wote pale mashariki ya kati.

Ilipofika majira ya kiangazi mwaka 1974 ubalozi wa PLO ukafunguliwa rasmi huko jijini Moscow nchini Russia. Katika kipindi hiki Yasser Arafat akapewa mpaka nafasi ya kuhutubia Umoja wa Mataifa (UN) na punde tu PLO wakapewa hadhi ya kiti cha uangalizi (observer status) pale UN mnamo mwaka wa 1974.

Idadi kubwa ya wahadhiri (lecturers) katika Chuo Kikuu hicho walikuwa na background ya jeshi (wanajeshi wastaafu au walioacha kazi) au walikuwa kwenye payroll ya KGB.

BACK TO THE TOPIC

Mnamo mwaka 1983, KGB ilim-recruit Mahmoud Abbas, ambaye sasa ni Rais wa Mamlaka ya Wapalestina na mwenyekiti wa Shirika la Ukombozi la Palestina.

Mahmoud Abbas akiwa na Rais wa Russia ndugu Vladimir Putin.
IMG_20191110_120327_122.jpg


Katika hati zilizotajwa na watafiti, Abbas pia ameelezewa katika nakala ya wasifu ambayo inajumuisha kuzaliwa kwake huko Palestina iliyokuwa chini ya Uingereza mnamo 1935, uanachama wake katika kamati kuu ya Fatah, chama chake cha siasa , na PLO, ikifuatiwa na nukuu ya madai ya kuajiriwa na KGB huko Damascus Syria, ambapo alitumia muda mwingi wa utoto wake katika kujifunza siasa, na ambapo alikuwa amerejea kutoka sehemu zingine za uhamishoni katika Mashariki ya Kati mapema miaka ya 1980.

Uhusiano mkuu kati ya Waisraeli na Wapalestina leo ni Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi bwana Mikhail Bogdanov, ambaye alitumika mara mbili kama balozi wa Moscow kwenda Damascus, mwanzo wa kwanza mnamo 1983, mwaka ambao Abbas alidhaniwa alinyakuliwa na KGB.

Taarifa hii inaweza kuwa ya mashaka, imekuja wakati wa kipindi ambacho Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa akijaribu kuendeleza mazungumzo ya amani ya Israeli na Palestina huko Moscow, jukumu moja zaidi la kikanda ambalo Putin amelibeba kutoka kwa mbabe mwenzake ambaye ni Marekani.

KGB-and-Abass.gif


Wataalam wa Taasisi ya Truman katika Chuo Kikuu cha Kiebrania huko Yerusalemu waligundua jina la Abbas katika hati ya files iliyoandikwa kwa mikono ya miongo kadhaa iliyopita ya jalada la KGB, ambalo lilitoroshwa kutoka Soviet Union iliyovunjika mnamo 1991.

Mpaka Kufikia sasa, hakuna mtu aliyefanikiwa kukanusha taarifa hii.

Wanazuoni na maafisa wa ujasusi wa Magharibi wanaamini maelezo ya taarifa hizi yamewafanya kwa kiwango kikubwa kuangazia mapambo ya siri ya kambi ya Mashariki na kwa pamoja wanaunda yale ambayo FBI imeripoti kuwa "taarifa kamili na za kina kabisa za kijasusi ambazo haijawahi kupokea kutoka chanzo chochote"

Hata hivyo, maafisa wa Palestina wanasisitiza kwamba madai ya kwamba bosi wao aliwahi kufanya kazi katika Kituo cha Moscow ni ya kupuuzia.

"Kuna mbinu za wazi za kujaribu kumchafua Abu Mazen [Abbas]," mjumbe wa kamati kuu ya Fatah, Mohammed al-Madani, aliliambia gazeti la Israel la Haaretz. "Hii ni jaribio lingine la kumtukana na kuchafua taswira njema ya Abbas.

Viongozi wa PLO na Fatah wamebaini kuwa recruitment ya Abbas ingekuwa na kumbukumbu nzuri kama ingeandikwa vizuri kutokana na ushirika wa karibu kati ya serikali ya Soviet na taasisi kama hizi ambazo si za kidola.

Abbas pia aliongoza "taasisi ya urafiki" wa Palestina na Soviet, ambao ulimuweka vizuri ndani ya circle ya warusi.

Curriculum Vitae (CV) ya Abbas ni ndogo sana na inajikanganya mno.

Palestinian-Authority-leader-Mahmoud-Abbas-delivers-a-speech-about-the-new-U.S.-Mideast-peace-...jpg


Kwenye website yake, kwa mfano, Abbas anaandika ya kwamba mnamo 1982, "kabla ya uvamizi wa [Israeli] kwa Lebanon, nilijadili nadharia yangu ya PhD, inayoitwa 'Siri ya Urafiki kati ya Nazism na harakati ya Zionist,' huko Taasisi ya Mashariki ya Moscow...

ITAENDELEA WIKI IJAYO. JUST STAY TUNED!

ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO
 
Back
Top Bottom