Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
JE UMEANZA KUMCHOKA MKEO AU MSICHANA WAKO ULIYEISHI NAE MUDA MREFU?
Waswahili wanasema ndoa nyingi ni Tamu sana mwanzoni lakini zinapoendelea hufikia Uchungu uliopitiliza. Katika uchunguzi wangu nimebaini sababu kadhaa zinazo sababisha mapenzi ya ndoa kupoteza ladha.
Sababu hizo ni:
1.Unadhifu/Urembo wa awali kipindi cha uchumba hupotea.
2.Majina ya kuonyesha upendo kama vile Mpenzi, Sweetheart , Dear na kadhalika huwa adimu na wakati mwingine hupotea kabisa.
3.Kujali na kuthamini kimapenzi kunafifia: Kwa mfano enzi za uchumba mwanaume alikuwa tayari kumfungulia mkewe Mlango wa Gari lakini siku zinavyozidi kwenda haoni tena tabia kama hizo. Inafifiza mapenzi ya ndoa na kupelekea kuchokana..
4.Kumtoa out mkeo/Mmeo mara kwa mara kipindi cha uchumba havionekani mkiwa ndani ya nyumba.
Hizo ni baadhi ya visababishi ya upotevu wa ladha ya ndoa....
Siku moja mzee mmoja alinimbia Huwezi kula mahindi kila siku. Hii kauli haifai katika maisha ya Ndoa.
Ulisha apa kuwa utamlinda, utamheshimu, utakuwa nae hadi kifo kiwatenganishe. Mahidi yanaweza kutumika kama Makande, Ugali au Uji.
DAWA NI HII
Yanayokupasa kutenda ilikudumisha ndoa yenye furaha na Amani ni haya yafuatayo:
1.Kuwa nadhifu/Mrembo zaidi.
2.Mwite majina ya upendo kwa mfano: My lovely wife nk
3.Endelea kumjali na Kumthamini zaidi ya mtu/watu wengine wa kawaida. Na aone jinsi unavyo mthamini
4.Mtoe out mara kwa mara kwenda mbuga za wanyama, Baharini, kwenye Hotel za kifahari na kadhalika.
5. Onyesha furaha unapokuwa nae katika mazungumzo yafamilia na kawaida. Mkiwa njiani onyesha tabasamu kubwa kuonyesha kufurahishwa kutembea na mkeo/mmeo.
6. Leta mada zenye utani usio na mauzi ili kuleta vicheko muda wote ndani ya nyumba.
7. Kuwa mwepesi kusamehe na kusahau makosa ya mpenzi wako..
Kumbuka:
Mkeo/Mmeo ni Bora hivyo Mpende na Umjali kwa dhati.
UKIYAFUATILIA HAYA, FURAHA KATIKA NDOA YAKO ITADUMU DAIMA HADI KIFO.