Pastor wa EAGT akutwa na mwanamke machakani.

Pastor wa EAGT akutwa na mwanamke machakani.

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
236
Katika kuufungua mwaka mpya 2014 Mchungaji wa kanisa la EAGT lililoko katika kata ya Bulige, Msalala, Kahama alikutwa na binti wa kilokole ambaye ni mshirika wa kanisa lake wakiwa zero distance katika kichaka kimoja kilicho umbali wa km 1 toka lilipo kanisa la pastor huyo. Siri ya Pastor huyo zilianza kuvuja tar 31.12.2013 na baada ya uchunguzi wa kina tar 01.01.2014 barua iliyoandikwa na mchungaji huyo kwenda kwa binti ilinaswa na intelejensia waliopo kanisani humo, ambayo ilikuwa inamtaka binti akutane na Mchungaji huyo ktk eneo muda wa saa 1:30 usiku.
Baada kukamata barua hiyo intelijensia hao waliweka ulinzi katika eneo husika ili kumdaka pastor huyo anayechunga kondoo wa Bwana; tar mosi binti alifika eneo akasubiri lakini pastor hakutokea na baada ya kusubiri sana binti aliamua kuondoka na mara Pastor naye akafika kakuta binti kaondoka eneo hilo. Kesho yake yaani tar pili kama kawaida walinzi walikwenda eneo hilo tena kujificha wasionekane na mara binti akafika na muda si muda naye Pastor akafika na kuanza tomasatomasa na mambo mengine kama kawaida, ndipo walinzi waliposogelea eneo lao na wao kuanza kutimua mbio lakini binti alikamatwa huku mchungaji akijitahidi kutimua mbio na kushinda marathoni. Baada ya kesi pastor alikubali kosa na kuwaomba wazee wa kanisa wamsamehe kwani wakimsema kwa wakubwa atafukuzwa kazi na kumfanya aishi maisha ya taabu kwani kwasasa anaishi kwa msaada wa kanisa lake la EAGT. Wazee wamemsamehe lakini kanisa limegawanyika kwa kuwa wengine wanasema anastahili kutengwa na wengine ambao wengi wao ni ndugu, jamaa na rafiki zake wanamuunga mkono kuwa aendelee kula kondoo wa bwana kwa kuwa ni halali yake.

Ndo hayo jamani ya ufunguzi wa mwaka mpya 2014.

UPDATES

Jamani Upastor ni mtamu...! Huyo pastor baada ya kupambana na kesi ya kuwala kondoo wa Bwana Yesu, alifukuzwa upastor. Lakini mpaka naleta kwenu taarifa hii ni kwamba kwa kutumia kundi lake jamaa anapigana kufa na kupona ili arudi kazini ingawa tabia yake ya kuwala kondoo bado anaendelea nayo na kwa sasa ana wanawake watatu ndani ya kanisa hilo la kilokole la hapo Bulige. Leo hii tayari Maaskofu wawili toka jimboni Kahama wamefika kanisani hapo kwa lengo la kuona namna ya kumrudisha Pastor huyo mla kondoo wa kundi lake. Naendelea kufuatilia sakata hilo na habari zaidi mtazipata hapahapa.
 
Kila mbuzi hula urefu wa kamba yake
 
Mchungaji alikutwa na mwanamke au binti? Be specific
 
We ni muongo nasema muongo kama si muongo weka picha si mliandaa mpango weka tuamini
 
We ni muongo nasema muongo kama si muongo weka picha si mliandaa mpango weka tuamini

Mkuu bahati mbaya picha zilizopigwa zina giza tu na waliokamatwa hawaonekani vizuri. Lakini ushahidi 100% upo hapo kanisani na barua ipo.
 
Back
Top Bottom