Password ya kichawi ya nafsi ya mpenzi wako.

Password ya kichawi ya nafsi ya mpenzi wako.

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,977
Reaction score
37,879
JINSI YA KUFAHAMU PASSWORD YA NAFSI/ MOYO WA MPENZI WAKO

Baadhi ya wachawi wana dawa ambazo zinaweza kukufanya kujua anachokiwaza mpenzi wako kupitia ndoto au maono usiku.

Katika hali ya kawaida hauwezi kujua mtu fulani anawaza kitu gani kuhusu wewe. Lakini hakuna kisicho wezekana chini ya jua. Wapo wachawi na washirikina wenye dawa zinazo wapa uwezo wa kujua mtu au watu fulani wanawaza nini kuhusu yeye. Nadhani umewahi kusikia kuhusu uwepo wa dawa ambayo ukipakwa unakuwa na uwezo wa kuwaona uchawi usiku! Vivyo hivyo ili kufahamu mtu fulani anawaza kitu gani kuhusu wewe

Kwa mfano,
U
nataka kujua mke/mume wako, ama mpenzi wako, ama mchumba wako, huwa anaongea vitu gani kuhusu wewe, akiwa na wenzake

Unataka kujua mke/mume wako ama mpenzi wako huwa anaongea vitu gani kuhusu uwezo wako wa kitandani

Unataka kujua kama mke/mume wako, mpenzi wako anaongea na nani, anachati na nani, anapigiwa simu na nani, anawasiliana na nani, iwe ni kwa njia ya simu ama mtandao wa kijamii

Wachawi wanaweza kukupa dawa maalumu ya kunywa na kujipaka na kisha kunuiza kile kitu unacho taka kukisikia kuhusu mtu uliye mkusudia.

Kwa mfano, kwa mpenzi wako, kama unaishi naye, usiku wa siku hiyo, ataongea kwa nguvu kila kitu anacho kifanya ambacho wewe unakuwa umenuwia akiseme. Unacho takiwa kukifanya ni
1. Kujipaka mafuta hayo na kunywa dawa maalumu ya kichawi
2. Kunuiza kile unacho kitaka akiseme.
3. Kutumia mkono wako wa kushoto kumshika katika paji lake la uso, huku moyoni ukiwa unasema maneno maalumu ya kichawi

Kujipaka mafuta hayo, halafu unaamka saa saba na kusema maneno maalumu ya kichawi. ( Hakikisha wakati unatamka maneno hayo yeye anakuwa usingizini na wala hakusikii, endapo ataamka ukiwa unayasoma, basi dawa haitafanya kazi, ili kuepuka uwezekano wa yeye kuamka na kukuta ukiwa unasema maneno hayo ya kichawi na yenye nguvu ya ajabu, unashauriwa uende ukayatamke maneno hayo ukiwa chooni, kati ya saa sita na dakika moja usiku hadi saa saba na dakika moja usiku , isiwe baada ya muda huo. Itakuchukua kati ya dakika 3 mpaka 7 kuwa umemaliza kutamka maneno hayo. Hata huvyo unatakiwa kuwa makini sana wakati wa kutamka maneno hayo kwani endapo utakosea hata neno moja, mwanamke au mwanaume ambaye umemtamkia anaweza kufa akiwa usingizini

Baada ya kutimiza taratibu zote, basi alfajiri ya siku hiyo kuanzia saaa kumi hadi saa kumi na moja. Utaonyeshwa kila kitu ulicho kuwa ukikitaka kwa njia ya ndoto ambapo mtu uliyetaka aseme kitu fulani, atakujia katika ndoto na kuanza kusema maneno yote ambayo wewe ulitaka kuyafahamu.

Kama haujaelewa kuhusu hiyo ndoto, utafanya maombi maalumu kwa kuomba ndoto hiyo irudi tena,basi itafanyika kama unavyo taka wewe na inaweza kujirudia kwa kadri utakavyo

Shughuli hii huongozwa na kusimamiwa na PEPO LA UTAMBUZI. Pepo hili lina uwezo wa kufunua siri za mtu yoyote Yule na kuziwasilisha kwa mtu aliye omba kuzijua siri za mtu huyo. Kwa mfano unapo kwenda kwa mganga wa kienyeji, unacho kiwaza katika nafsi yako, kule katika ulimwengu wa kiroho unaongea kwa sauti kubwa sana, pepo huyu anacho fanya ni kuchukua yale unayo yawaza na kumpatia kiti wake, ambaye naye atakwambia jina lako, unapotoka na shida yako, wewe utadhani yeye amejua siri zako za ndani kumbe wewe mwenyewe ndio umemwambia bila kujijua. Kuna mamia kwa maelfu ya watu mbalimbali Dar Es salaam hii na katika miji mingine ya Tanzania na Afrika kwa ujumla,hufurika kwa waganga wa kienyeji ili kutafuta dawa hii kwa ajili ya kufahamu password za moyoni za wapenzi wao pamoja na watu wengine.

UTAJUAJE KUWA MTU FULANI ANAYAFUATILIA MAISHA YAKO KWA NJIA HII


Utakuwa unaota ukiwa uchi wa mnyama mara kwa mara. Na kama mambo yako ni mabaya au machafu basi utakuwa unao ta upo chooni umezungukwa na kinyesi . Ndoto hizi zitakuwa zinakujia mara kwa mara.


JINSI YA KUJIEPUSHA

Hakikisha unakuwa na uhusiano mzuri na Mungu wako.

MTU WA MUNGU ANAWEZA KUMUOMBA MUNGU AMPE PASSWORD YA MTU FULANI?

Ndio inawezekana kabisa, unacho takiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa Upo katika uhusiano mzuri na Mungu kwa sababu Mungu huwa hajibu sala za watu wenye dhambi

Jambo unaloliomba linapatana na Mungu. Kanuni ya kimungu ni “ EX TURPI CAUSA NON ORITOR ACTIO” Yaani, huweza kudai haki ya kisheria kama jambo ulilolifanya lipo kinyum na sheria. Kwa mfano, huweza kumshitaki mtu aliyekudhulumu pesa baada ya wewe kumuuzia bangi. So na kwa Mungu, huwezi kuomba akupe password ya girlfriend wako au boyfriend wako! Hiyo ni kufuru. Mtu anayeweza kuwa entitled hapa ni mke kuomba password ya mume wake au kinyume chake, ama mtu amekuja kukuchumbia basi unaomba password yake ili kujua siri zake za ndani.

" MIMI NI MUNGU NIKUFUNDISHAYE ILI UPATE FAIDA "...ISAIAH 48: 17.
 
JINSI
YA KUFAHAMU PASSWORD YA NAFSI/ MOYO WA MPENZI WAKO



Inatoka : ULIMWENGU
USIOONEKANA



[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align:
center"][/TD]
[/TR]

[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Picha ya mtu akiota. Baadhi
ya wachawi wana dawa ambazo zinaweza kukufanya kujua
anachokiwaza mpenzi wako kupitia ndoto au maono usiku.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Katika hali ya kawaida hauwezi kujua mtu fulani
anawaza kitu gani kuhusu wewe . Lakini hakuna kisicho wezekana
chini ya jua. Wapo wachawi na washirikina wenye dawa zinazo
wapa uwezo wa kujua mtu au watu fulani wanawaza nini kuhusu
yeye. Nadhani umewahi kusikia kuhusu uwepo wa dawa ambayo
ukipakwa unakuwa na uwezo wa kuwaona uchawi usiku! Vivyo hivyo
ili kufahamu mtu fulani anawaza kitu gani kuhusu wewe .


Kwa mfano,
· unataka kujua mke/mume
wako, ama mpenzi wako, ama mchumba wako, huwa anaongea vitu
gani kuhusu wewe, akiwa na

gorrrssshh.!!!
jukwaa gani hili nimringia.!?????
samahani mniwir radhi nilikuwa napita tu
byeee
 
Mkuu hiyo avatar yako na ulichokipost vinafanana!
 
Back
Top Bottom