Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,088
- 865
Mahali ulikopachoka na unawaza kuacha kazi kwa notisi ya saa 24, mwingine ndio anaomba Mungu amsikie apate hapo kazi ya ndoto zake. Mpenzi unayemfanyia vituko ukitafuta kila sababu ya kuwa mbali naye msionane, mwingine hapati usingizi akimsihi Mungu ajibu maombi yake.
Unapambana kutokula kwa makusudi, unavusha milo upunguze uzito wakati mwingine kula milo miwili kwake ndio kipimo cha mafanikio. Unalalamika unalipwa mshahara mdogo na huna marupurupu wakati kuna mtu anafunga na kuomba apate robo ya mshahara wako. Unalalamika watu hawakutembelei wakati wengine wanaupambania huo uhuru ulio nao wewe wa kuamua ukamtembelee nani muda unaoutaka wewe.
Una msongo wa kutafuta mtoto wa jinsia fulani kiasi cha kugombana na mwenzi wako wakati mwenzio ndoto ya kuwa mtoto haijatimia. Una mgogoro na mzazi wako na hutaki hata kupokea simu zake, wakati mwingine anatamani angekuwa na bahati hata ya kuwa na mzazi asiyevumilika.
Tunatamani tusichonacho tunadharau tulichonacho. Ugumu tunaoupitia wakati mwingine ndio ndoto kubwa ya mtu mwingine. Unachofikiria kinakuumiza, kwa mwingine huenda kingekuwa faraja. Pamoja na kuwaza mambo makubwa, tusiache kukosa shukrani kwa hatua tuliyonayo ambayo, ukiangalia kwa jicho la unyenyekevu, kuna wakati iliwahi kuwa ndoto inayotunyima usingizi.