Nilikuwa napitia posts hapa JF na nikakutana na hii statement aliyoitoa Pasco (rangi nyekundu hapa chini)....I was shocked !.
" Moja ya makosa makubwa sana Hitler aliyoyafanya, na kuwabakiza baadhi ya hawa jamaa!, walipaswa wote kabisa wawe wiped kwenye uso wa dunia ndipo asamani ya kudumu ingepatikana enero la Mashariki ya Kati "
Pasco wewe hapa JF, kwa watu wengi unajulikana ni mtu mwenye upeo mkubwa na vile vile kama sijakosea ni mwandishi wa habari. Kama mtu kama wewe ambaye kwa uelewa wako, utakuwa unajua genocides zote huwa zinaanza na propaganda za chuki na hatimaye zinawaingia watu mpaka wanakuwa kama wanyama na kuanza kuua watu wengine kwa sababu tu ya race zao, unawezaje kusema maneno kama haya !!!????
Miaka kama kumi hivi iliyopita, kuna wakati fulani, nilispend kama week nzima kusoma history ya vita kuu ya pili na niliposoma mauaji aliyokuwa anayafanya Hitler ya kuchukua watu na kuwaingiza kwenye gas chambers na kuua mamilioni ya watu kwa njia hiyo, nikajaribu kujiuliza, Hitler aliwezaje kuwashawishi na kuwafanya wajerumani wakubali kuwa wanyama kiasi hiki !. Lakini leo nilipoona statement yako hii, nikawaza, kama mtu kama Pasco anaweza akatamka maneno kama hayo, then kitu kama hiki kikianza kutokea duniani atakisupport na kama mtu wa uelewa wako Pasco atasupport kitu kama hiki, mbona ni rahisi kwa wengine wenye uelewa mdogo kukitekeleza....Probably hata wewe unaweza ukajikuta uko mstari wa mbele kutekeleza.....Ndio maana kwa wajerumani sasa hivi, manano kama hayo uliyoyasema yangekupeleka selo ! Wanajua problem ya statement za chuki kwani wame-experience first hand, na mpaka sasa hivi, wengi wao bado wana wakati mgumu kui-face history yao kama taifa !
Hakuna mtu anayezaliwa mnyama, tunabadilika na kuwa kama wanyama kwa kudharau vitu vidogo kama hivi na kutojifunza kutokana na history ! Baada ya hitler, bado genocides zimeendelea kutokea duniani (mojawapo ni kwa majirani zetu Rwanda) na kwa mtindo kama wa kwako Pasco ninalazimaka kwa masikitiko makubwa kuamini kwamba zitatokea tena na tena na tena.....
Wakati wewe, unafurahia kwamba Hitler alijitahidi kuangamiza race fulani hapa duniani, na wakati huo huo kusikitika kwamba alishindwa kumaliza kazi, Wajerumani, ambao Hitler alikuwa kiongozi wao, wameweka sheria kwamba kumshabikia hitler ni kosa kubwa kwa mujibu wa sheria zao !
Kwa kweli leo nimeamini usemi huu maarufu : "We learn from history that we never learn anything from history".