Pasco unaijua nguvu ya Twitter?

Pasco unaijua nguvu ya Twitter?

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,333
Unakuwa Kama mtu mlugaluga au waluwalu asiyejua maana ya "Freedom of Speech " yaani unadhani Twitter ni sawa na magazeti yanayofungiwa na serikali wakati wowote?

Ukitaka kujua Twitter ni Mtandao wa aina gani, na wamiliki wake ni kina nani na nguvu yake ikoje chini ya jua basi Serikali ifuate Ushauri wako kisha waifungie Tanzania.

Yaani US Embassy iingie gizani, iache kuwasiliana na watu wake ambao huwa inawapata kirahisi mno kupitia Twitter, hapo ndo Pasco utaijua Twitter vizuri na ndo utajua kwanini viazi vitamu vinaitwa matobolwa vikikaushwa, na ndo utajua kwanini Trump anashinda Twitter.

Siyo kila jambo ni rahisi kufanyika hapa Duniani Kama unavyodhani,mengine ni ya kutazama na kuacha Kama yalivyo.
 
Daima mwanadamu ukianza kufikiria kwa kutumia tumbo na si akili, haijalishi ni msomi kiasi gani mawazo na fikra zako yanakuwa mithili ya kile kitokacho baada ya kuingia tumboni (kinyesi)

Njaa ya kuonekana na mtawala inadhalilisha hata wale waliokuwa na staha mbele ya jamii.

Kipindi hiki kuelekea uchaguzi tutaona na kusikia mengi. Ni swala la wakati tu atatokea mpuuzi mwingine kuomba hata haki ya kupumua igaiwe na serikali, yote ili aonekane na mtawala aambulie japo uDC.
 
Back
Top Bottom