Pascal Mayalla nakuomba uanzishe Kipindi Cha Kitimoto

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Posts
2,782
Reaction score
877
Wakati wa Mkapa Nakumbuka PASCAL MAYALLA alianzisha Kipindi Cha KITIMOTO ambapo watendaji kadhaa na viongozi wa serikali walihojiwa kuhusiana na mambo mbali mbali sasa tunaelekea katika uchaguzi 2015 na kuna watu wengi sana wanataka madaraka lakini umma hauwafahamu. Pia kuna mambo mengi sana yanafanyika serikalini kiasi cha kutuhumiana wao kwa wao huku wakilindwa ili chama kiendelee kutawala Kwa Mfano:
1.Suala la Ukawa linayumbisha umma na serikali kiasi kwamba inaonekana kama Ukawa wana makosa huku CCM wakimbilia kwa wananchi na Pinda naye anaweweseka sasa hili linaweza kutatuliwa kwa kuweka kiti moto kitakacho rushwa live , na kuhusisha makundi ya Ukawa na hao CCM . Kwa Sasa Bunge la Katiba halina maana kwa kuwa hakuna katiba itakayopatikana hapo lakini kipindi hiki kinaweza kuepusha matumizi mabaya ya Bunge la katiba na kuleta mwelekeo.
Mtu yoyote anayefahamu mambo ya siasa anaweza kung'amua kuwa Uchaguzi 2015 lazima ufanyike kwa kutumia katiba ya zamani hivyo kuna umuhimu wa kuunda tume huru ya uchanguzi yenye sura ya Tume ya warioba bila hivyo huko mbele kuna machafuko makubwa

2.Viongozi wa dini wenye mvuto wa kisiasa na nguvu ya umma wanaweza kutoa mwelekeo wa nini kifanyike kwenye mdahalo huo ili kuwaandaa watu na mabadiliko ya kukosa katiba mpya.
Ni jambo la ajabu sana kuwa watu walikuwa na matumaini na katiba mpya na pesa nyingi zimetumika lakini hakuna katiba mpya na CCM wanasingizia kuwa Ukawa ndo wamevuruga Katiba mpya wakati ukweli unafahamika


3. CCM wanakiri kwamba kuna mawaziri mizigo na wamewataja kwa majina , watu hao ni mzigo kwa Taifa na si kwa CCM hivyo wanatakiwa kuhojiwa na KITIMOTO na si kamati kuu ya CCM

4. Wizi wa Escrow na matusi ya akina MUHONGO, MASWI na WEREMA walipaswa wahojiwe na KITIMOTO ili kufahamu kuwa aliyewateua alifanya hivyo kwa kuwa ni watukanaji wakubwa??

NB Kute Kenya wanataka NATIONAL DIALOGY sasa sisi hapa tukianzisha KITIMOTO tutawajua wagombea kabla ya wao kuiba kura na kuingia kwa nguvu ya dola


UP date
Tumaini Makene



​
TAARIFA KWA UMMA


KUHUSU


MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA YANAYOENDELEA BUNGE MAALUM LA KATIBA


Ndugu wanahabari


Sote tunaelewa kuwa kwa matakwa ya CCM, Bunge Maalum la Katiba (BMK) limeendelea kufanya vikao vyake mjini Dodoma kuanzia Agosti 5 mwaka huu, kinyume kabisa na matarajio ya Watanzania, ambao kupitia fursa mbalimbali wamepaza sauti zao wakisisitiza maridhiano na mwafaka wa kitaifa kutangulizwa mbele badala ya maslahi ya watawala.

Tukiwa viongozi wa kisiasa ambao ni sehemu ya uongozi ndani ya jamii, wenye wajibu wa kuwa na maono chanya na muhimu kwa taifa letu, tumeendelea kufuatilia kwa karibu namna mchakato wa Katiba Mpya unavyoendelea kunajisiwa kupitia vikao hivyo vya BMK linaloendelea mjini Dodoma, likitumia rasilimali za taifa, zikiwemo kodi za Watanzania wanyonge, kujadili vitu visivyotokana na wananchi.


Mtu yeyote makini ataweza kubaini kuwa kwa namna mchakato wa Katiba Mpya unavyopelekwa au unavyokwenda kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa uongozi wa kisiasa kwa Chama kinachoongoza Serikali, CCM.


Kuna ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa katika jambo hili. Ni kama vile mchakato unajiendea tu wenyewe bila mwongozo wowote kutoka kwa watu walioko madarakani ambao wananchi walitarajia wangetumia mamlaka yao ya dhamana ya uongozi ili taifa lipite salama katika wakati huu mgumu na tupate Katiba Mpya na bora.


Vipo viashiria vingi tu vinavyoweka wazi hali hiyo ya ombwe la uongozi wa kisiasa katika mchakato huu wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kauli kinzani za viongozi wa Serikali na CCM yenyewe.

Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza kama vile kunahitajika mazungumzo zaidi na kwamba suala la muundo wa serikali lilipaswa kupigiwa kura kabla, Mwenyekiti wa BMK anaendelea kuongoza bunge kama vile mchakato ni mali binafsi ya CCM na walioko madarakani.

Wakati baadhi ya viongozi wa Serikali ya CCM wakitoa kauli za kuhitaji kuwa makini na taratibu za kuendesha mchakato huu chama chao kinatoa kauli za kuzidi kuharamisha na kutia najisi mchakato mzima. Mchakato unakwama, nchi inayumba, Watanzania wako katika sintofahamu kwa sababu tu tumekosa uongozi wa kisiasa katika jambo hili.


Kiashiria kingine cha pengo hilo la uongozi wa kisiasa ambacho kwa kweli kwetu sisi kimetusikitisha zaidi kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuendelea na ‘hamsini zake' kama vile nchi haina tatizo lolote.


Yaani wakati nchi na wananchi wako katika sintofahamu ya hatma ya Katiba Mpya itakayoweka misingi ya wao kujitawala na kuongozwa watakavyo, makundi mbalimbali yakipaza sauti zao, mataifa mengine yakituangalia kwa makini na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wakifuatilia mchakato, Rais Kikwete anapata muda wa kutembelea ranch ya Rais Mstaafu wa Marekani George Bush!


Wakati Rais Kikwete akiendelea kutalii dunia, wenzake wako mjini Dodoma wakichukua posho kwa kazi ambayo wananchi hawajui wanaifanya kwa maslahi ya nani!


Kwa ujumla mambo yote yanayoendelea sasa katika mchakato huu ni matokeo ya ombwe hilo kama tulivyosema.


Inaonesha kuwa CCM wamelewa madaraka na viongozi wanaona dhamana ya uongozi iko juu ya wananchi hivyo hawajali umuhimu na nafasi ya mamlaka ya wananchi katika kuamua mstakabali wa taifa lao kwa ajili ya kizazi cha sasa na kuweka msingi wa vizazi vingi vijavyo.

Hivyo leo tungependa kuzungumza tena kuhusu Rasimu ya Katiba na mchakato wenyewe hapa ulipokwama;

Tunapenda kusema wazi kuwa tumeshangazwa sana na kitendo cha CCM na Serikali yake kulazimisha kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba Mpya, tena kwa mtindo ule ule wa kunajisi na kupuuza maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya kama yalivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.


Wamefanya hivyo pasi na kujali kilio cha wananchi kinachopazwa kutoka kila kona ya nchi, ambapo Watanzania mmoja mmoja na katika makundi mbalimbali wametaka maoni yao yazingatiwe kwa kujadiliwa, kuboreshwa na kisha kupitishwa na Bunge Maalum la Katiba kabla wao hawajayapigia kura ya maoni kwa ajili ya kuipitisha au kuikataa Rasimu ya Katiba Mpya.


Wajumbe wanaotokana na CCM pamoja na makada wengine wapatao 166 wa chama hicho ambao waliteuliwa kuingia kwenye bunge hilo kusimamia maslahi ya CCM kupitia kundi la wajumbe 201, wameamua bila haya mbele ya umma si tu kupuuza rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi bali sasa wameamua kuingiza mambo yao waliyodhamiria tangu mwanzo kwa kadri ya maamuzi na maelekezo ya vikao vya chama hicho vikiongozwa na Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete.


Bila kujali wala kuguswa na miito ya Watanzania mbalimbali wanaotaka jambo hili liongozwe na maridhiano kwa ajili ya mwafaka wa kitaifa badala ya kuweka matamanio ya watawala mbele, CCM na mawakala wao katika mchakato huu wameendelea pia kufuja na kutumia vibaya fedha za wananchi kupitia Bunge Maalum la Katiba kwa kujadili na kuingiza vitu visivyokuwemo au visiyotakiwa kuwa sehemu ya rasimu hii iliyopo sasa.


Hali hiyo imefanyika kwa namna kadhaa ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria inayosimamia mchakato mzima, kubadili kanuni za uendeshaji wa BMK hasa katika taratibu za kujadili na kupitisha ibara na kubwa zaidi kuingiza masuala ya Tanganyika kwenye Rasimu ya Katiba ya Muungano.


Kimsingi masuala wanayoyajadili na kuyachomeka kinyemela kwenye Rasimu ya Pili ya Warioba, mathalan masuala ya Ardhi, Elimu, Maji, Kilimo, Uvuvi, Mifugo, Serikali za Mitaa nk ni masuala yanayopaswa kuandikwa kwa kina ndani ya Katiba ya Tanganyika na siyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Ni vyema kukumbuka kuwa Zanzibar walijadili wenyewe mambo Yao ya Ndani na kutengeneza Katiba yao na hatuoni mantiki ya kuruhusu Wajumbe toka Zanzibar kujadili na kuamua mambo ya Tanganyika. BMK haina Sifa ya kujadili yasiyo ya Muungano.


Hivyo tofauti na wanavyotaka kujionesha katika jamii, CCM kupitia BMK wameamua kupindua kabisa rasimu nzima na kuweka maazimio ya vikao vyao kuwa ndiyo Katiba ya Tanzania. Jambo hili haliwezi kukubalika.


Kutokana na uchakachuaji huo wa Katiba Mpya unaoendelea kufanywa na CCM kupitia BMK, UKAWA tumefikia maamuzi yafuatayo;


· Tunamtaka Rais Jakaya Kikwete asitishe shughuli za BMK mara moja lisiendelee kuvuruga
na kuharibu mchakato wa Katiba Mpya na kuiweka nchi katika sintofahamu juu ya jambo hili
nyeti;

· Tunamtaka Rais Kikwete asitishe BMK ili lisiendelee kufuja fedha za Watanzania maskini
wanaopigania Katiba Mpya iwapatie matumaini ya kuongozwa na kujitawala wanavyotaka.


· Tunamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum
kwenye matumizi ya fedha za BMK ambayo kuanzia Bunge la Bajeti lililopita tumebainisha
wazi kuwa yana uvundo mkubwa wa ufisadi na hayana maelezo sahihi.


· Iwapo Rais Kikwete atashindwa kutumia mamlaka yake kusitisha BMK na hivyo likaendelea
kinyume cha matakwa na maslahi ya wananchi kama lilivyofanya awali na linavyofanya sasa,
UKAWA tutawaongoza Watanzania kupaza sauti zaidi kupinga najisi inayotiwa kwenye maoni
yao, kupitia maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima.



Asanteni kwa kutusikiliza.


Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti CUF


Freeman Aikaeli Mbowe
Mwenyekiti CHADEMA


James Francis Mbatia
Mwenyekiti NCCR Mageuzi


Wilbrod Peter Slaa
Kny Makatibu Wakuu, UKAWA.

WAKUU WA NCHI WANA NDIMI MBILI
1.UKAWA wameunga Mkono hoja ya Tume ya Jaji Warioba wa CCM.
2.Jaji Warioba aliteuliwa na Kikwete(Mwenyekiti wa CCM) kukusanya maoni kwa Muujibu wa Sheria
3.Baada ya Kukusanya maoni Warioba alimufuata Kikwete Ikulu na kumupa ripoti na Kikwete akasoma na kusema ni nzuri na akaamua kusaini na kuendelea na mchakato
Jibu Maswali haya:
1.Hoja ya Tanganyika ni Maoni ya Wananchi na waliokusanya na Kuhakiki ni CCM . Je Kikwete na CCM ni wachochezi??
2.Kwa nini Kikwete kama ana uelewa alisaini Ripoti ya Tume ya Warioba wakati anajua ina Msimamo wa Serikali tautu na Tanganyika??
3.Watendaji wa serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu walikuwa na msimamo wa Serikali tatu je, Ikulu imemeguka lini??
4.Nilini Serikali ya CCM na Ikulu ya Kikwete wameanza kupinga kupinga serikali tatu? Kumbuka Zaidi asilimia 70% ya Wajumbe wa Tume ya Warioba ni CCM???
5.Ni kwa nini Kikwete alikubali ripoti ya Tume ya Warioba Ikulu wakati inawakilishwa lakini ghafla anakuja kupinga Bungeni??

KIKWETE ANAPOKEA RIPOTI YA WARIOBA KWA FURAHA IKULU NA KUISANI , LAKINI ANAMSHAMBULIA BUNGENI



​
 
kama Muhongo alikataa tu mahojiano na DW kuhusu kashfa inayowakabili na kusema kwamba haoni umuhimu wa kushiriki
mahojiano hayo wakati ana mambo mengi ya kufanya kiofisi.... sasa sipati picha wala negative huyo mayyalla kama si kumvua nguo kabisa...'MUONGO' ni janga la taifa..!!
 
Watu kama Muhongo, Maswi na Werema wanatakiwa kuhojiwa katika KITI MOTO hii inaweza kuua tabia ya baadhi ya wanasiasa kununua waandishi wasio waaminifu !!
Watu kama akina Ridhiwani Kikwete wataacha kutukana media wataheshimu watu na sio media!!
Sasa hivi mtu anaweza kununua waandishi na wakampamba wakati hana kitu !!
CCM wanatabia ya kuhodhi TBC ndo maana walimfukuza Tido aliyeanzisha mdahalo wa kuwahoji wagombea kwa kuwa CCM mara zote walichemka!!

Sasa mimi naamini TIDO anaweza kufanya vizuri katika kusimamia midahalo na hata huyo Pascal Mayalla sasa hakuna shinikizo la kitu hicho kuanzishwa kwa kuwa watawala wanalindana!!
Hiki ndicho chanzo cha uzembe serikalini , kuna double standard , wapo mawaziri ni watendaji wazuri kwenye serikali hiyo hiyo kuna wavivu wakubwa na wana achwa!!
 
...na kama ikitokea akafanikiwa kanzisha iwe thru tv au radio, basi ajue 'RUNGU' la kizandiki kutoka TCRA na serikali yake litamuhusu!!! na kuitwa mchochezi, mvuruga amani na misamiati yote ya 'sirikali' ya si si emu!!
 
huu ndio ukiritimba wa watanzania, yaani mtu ni pascal mayala tu wa enzi hizo wakati wengine hata hatukumbuki kama alifanya kitu, mbona hamumpi heshima yake mtanzania mwenzenu yule mama wa Mdahalo pamoja na sasa kila mtu anajidai anafanya midahalo? Hivi mchakato majimboni uitufunugua kuliko midahalo ya Tanzania tunayoitaka? mpeni mama wa watu haki yake mpaka leo bila hiki kipindi mngewahi kumjua slaa, Lipumba, tanesco na data za wakina Januari na Zito kabwe ama Itikadi za vyama? acheni ubaguzi jamani au kwa kuwa anaonekana hana u CCM? Hivi leo si kweli kwamba watu wakisikia mdahalo wake wanajua kumekucha? mimi simjui personally lakini nimemjua kuhusu kazi yake huyu wa leo mla jana kala nini?
 

Cha kuchemsha ama kyrost
 
Do you think we need to waste time kuwabembeleza hao watu kwa njia hio? We need to act yaani siku moja tunaamka tu na kulianzisha, basi ndio adabu itawafika
 
Hapana Pascal Mayalla hakuanzisha hicho kipindi, si ukweli.

Kuna mtu anaitwa Alioki, ushawahi kumsikia? Muulize Pascal atakueleza. Kuna Meb pia, muulize na yeye pia utajuwa ukweli.

Pascal siku hizo bado sana.

Aisee, unaogopa nini wewe?

Kwani Si mnsema Allah aliumba kila kitu. Khaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…