Part 3: TISS bado safari ngumu

Mbona kila linalofeli nchi hii lawama ni kwa TISS !?

TISS haiwezi kufanya kila kitu. Jambo la msingi ni kuboresha taasisi zetu nyingine zifanye kazi kwa ubora.

Hii kuitegemea TISS ifanye kila kitu ndio inaturudisha nyuma. Kukitokea rushwa lawama kwa TISS, mikataba mibovu lawama kwa TISS. Wakati huo huo kuna taasisi zinazohusika na hayo mambo.

Tukiachana na hayo, mimi ukiniuliza ni kwa nini tunapiga hatua za polepole kwenye maendeleo, ntakwambia tatizo ni elimu.

Elimu yetu imetengeneza lundo la wasomi ambao mchango wao kwenye taifa hili ni kiduchu sana. Sana sana taifa linaingia hasara ya kuwahudumia tu.
Mkuu Elimu yetu ina changamoto ndio lakini hii kusema tuna wasomi ila hawana tija sio sahihi.

Serikali haijaweka mazingira sahihi ya kumax potential za wasomi wetu

Mie binafsu nna mifano hai ya wasomi wawili wamebuni idea mbili kubwa sana moja ya app nyingine product.

Ila kupewa patent imekuwa changamoto, huyo wa product kaambiwa hawana standard ya kupimia ubora wa product yake coz ni mpya. Huyo wa App kanyimwa patent!!

Kwahyo shida hatuna mfumo, mmi nlisoma shule ya mfumo wa cambridge ilikua toka darasa la 3 wana monitor potential yako alafu wanawa classify. Mwishoni wanaweka nguvu kwenye potential yako unakua best.

Ndio maana kule unakuta mtu Kasomea nyoka tu ndio ajira yake kukamata majoka mijini!! Ssa Tz tuna mazingira wezeshi mtu aweze kujiajiri hilo eneo??

Shida sio wasomi ni mazingira wezeshihayajawekwa na serikali with TISS inclusive.
 
Mkuu kila kinachotokea kinaakisi malezi na makuzi ya watu wa jamii husika.
Nimekaa mahali katika shughuli inayonipa fursa ya kushuhudia vizazi tofauti katika nchi yetu jinsi vilivyo kitabia,perceptions,matumizi ya akili,etc.Amini ndugu zangu kama tutaendelea hivi,ipo shida kubwa inakuja mbele.
Kizazi cha watu wanaojua kuwaza,kuamua na kutenda kwa usahihi kilirithiwa na kizazi cha watu wanaowaza,kuamua na kutenda bila kutathmini kama ni sahihi au la,nacho sasa kinarithiwa na kizazi cha watu wasiowaza,wasioamua wala wasiotenda,no guts at all.
Tujiulize,tumefikaje hapo?
Sasa usije ukawalaumu Tiss ilhali wanaruhusiwa kurecruit maafisa toka jamii isiyofikiri wala isiyotaka responsibilities kabisa,na bado ndani ya jamii hiyo hiyo,kutokana na corruption na undugulization,tiss inarecruit mbegu mbovu zaidi ktk jamii mbovu!
10 years ago nilikuwa nainteract na vijana ambao ukimwambia kesho njoo ofisini twende mahali sikuhitaji kumfundisha dressing code,leo hii nainteract na vijana ambao hata chupi yake tu anaionyesha nje,sasa mtu huyu ambaye chupi tu kuificha ni shida,unategemea aingie tiss na kuwa na siri hata akilewa pombe?
Wapo vijana wa tiss nawajua,yaani hadi najiuliza where are we going as a nation?!Tunakosea wapi,the problem is so deep rooted.
Katika situation ya hivi,tiss ilipaswa kuwa makini sana ili kupata wenye unafuu toka jamii hii iliyochoka kichwani.Ilihitaji sana mkono wa wazee wetu kutumia busara zao kongwe kuandaa kizazi kipya kwa njia sahihi.You just trigger it,na wanaendeleza mengine wenyewe.
Wazee hawawezi kwenda na sayansi ya sasa,ila hawashindwi kuandaa kizazi chenye maadili ya kupambana na changamoto za sasa.
Zamani tulikuwa tunatumia nguvu nyingi kuelekeza vitu vidogo kwa watoto wadogo ndani ya nyumba,sasa hivi tunatumia nguvu kubwa kuelekeza vitu vidogo hata kwa vijana wakubwa wa chuo kikuu,tunakoelekea tujiandae kutumia nguvu kubwa kutiisha jamii hata katika level za wafanyabiashara,askari,hakimu etc.Tatizo linazidi kupanda kichwani and who knows,maybe kuna siku tutalazimika kumtiisha hadi Rais na makamu wake ikulu,huku watu wa kufanya hivyo wakiwa hawapo,maana jamii itajaa watu wasiowaza na kutenda!Sijui nani atatukomboa.
Shida inakuja kuwa wanaoajiriwa ndani ya taasis wanapelekwa kwa memo so hawaangalii tena talent na uwezo wa mtu wa akili na kuchanganua mambo.
pili taasis yenyewe imejiingiza kwenye siasa wakati haitakiwa kufunfamana na upande wowote.
Tatu ni kwamba taasis inatakiwa iboreshwa na ibadilushwee baadhi ya Sheria zake na department ziongezeke.
mfano ijengwe department ya economic intelligence iwe ni kukusanya taarifa na mbinu za kukuza uchumi na kukabiliana na vita ya biashara na majirani zetu pila intelligence techniques ziboreshwe zaid na sio kubaki na internal spying only tuwe na department ya exernal surveillance na economic surveillance pia tuje na strong and right selection ya team sio undugu
 
Ilikuwa 3June 2019 katika wilaya ya Ruangwa.
Gereza jela ilizinduliwa kwa ajili ya kuhifadhi wahalifu.
Kuna uwezekano wa kuwepo crime rate kubwa ktk wilaya hiyo na hivyo ilikuwa ni kipaumbele.
Tuache kulaumu ndugu zangu.

Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kila kinachotokea kinaakisi malezi na makuzi ya watu wa jamii husika.
Nimekaa mahali katika shughuli inayonipa fursa ya kushuhudia vizazi tofauti katika nchi yetu jinsi vilivyo kitabia,perceptions,matumizi ya akili,etc.Amini ndugu zangu kama tutaendelea hivi,ipo shida kubwa inakuja mbele.
Kizazi cha watu wanaojua kuwaza,kuamua na kutenda kwa usahihi kilirithiwa na kizazi cha watu wanaowaza,kuamua na kutenda bila kutathmini kama ni sahihi au la,nacho sasa kinarithiwa na kizazi cha watu wasiowaza,wasioamua wala wasiotenda,no guts at all.
Tujiulize,tumefikaje hapo?
Sasa usije ukawalaumu Tiss ilhali wanaruhusiwa kurecruit maafisa toka jamii isiyofikiri wala isiyotaka responsibilities kabisa,na bado ndani ya jamii hiyo hiyo,kutokana na corruption na undugulization,tiss inarecruit mbegu mbovu zaidi ktk jamii mbovu!
10 years ago nilikuwa nainteract na vijana ambao ukimwambia kesho njoo ofisini twende mahali sikuhitaji kumfundisha dressing code,leo hii nainteract na vijana ambao hata chupi yake tu anaionyesha nje,sasa mtu huyu ambaye chupi tu kuificha ni shida,unategemea aingie tiss na kuwa na siri hata akilewa pombe?
Wapo vijana wa tiss nawajua,yaani hadi najiuliza where are we going as a nation?!Tunakosea wapi,the problem is so deep rooted.
Katika situation ya hivi,tiss ilipaswa kuwa makini sana ili kupata wenye unafuu toka jamii hii iliyochoka kichwani.Ilihitaji sana mkono wa wazee wetu kutumia busara zao kongwe kuandaa kizazi kipya kwa njia sahihi.You just trigger it,na wanaendeleza mengine wenyewe.
Wazee hawawezi kwenda na sayansi ya sasa,ila hawashindwi kuandaa kizazi chenye maadili ya kupambana na changamoto za sasa.
Zamani tulikuwa tunatumia nguvu nyingi kuelekeza vitu vidogo kwa watoto wadogo ndani ya nyumba,sasa hivi tunatumia nguvu kubwa kuelekeza vitu vidogo hata kwa vijana wakubwa wa chuo kikuu,tunakoelekea tujiandae kutumia nguvu kubwa kutiisha jamii hata katika level za wafanyabiashara,askari,hakimu etc.Tatizo linazidi kupanda kichwani and who knows,maybe kuna siku tutalazimika kumtiisha hadi Rais na makamu wake ikulu,huku watu wa kufanya hivyo wakiwa hawapo,maana jamii itajaa watu wasiowaza na kutenda!Sijui nani atatukomboa.
Nimesoma hya mpaka nimekuwa disapointed.umeandika kwa uchungu sana.na huu ni ukwel
 
Vijana wa TISS siku hizi wala hawajifichi na hawajui kutunza siri. TISS anashinda baa halafu anajitambulisha kabisa akilewa. Na ukimfuatilia unagundua kweli huyu ni TISS. Hawajui kuwa ufanisi wa kazi yao unategemea usiri na kutojulikana kwao. Wanaume wa MOSAD na CIA hata mke wake hawezi kujua kama mumewe ni agent. Na ikitokea akajulikana basi anaacha kazi mara moja kwa sababu ni rahisi kuwa compromised akishajulikana. Sasa hawa UVCCM sijui hawajui maadili ya kazi zao. Mpaka kwa michepuko yao hawachelewi kuropoka kuwa wao ni TISS na wako juu ya sheria.

Binafsi nawadharau sana !!!

Na kujulikana maana yake haupo makini kwenye utendaji na majukumu yako ya kila siku. Na ukishajulikana unatakiwa kutoa Taarifa na kuondoka fasta hiyo sehemu.

Shida ya vijana wa siku hizi huwa TISS kwa connection za wazazi wazazi au kujuana juana.

Recruiting ya zamani ilikuwa very fascinating, yaani ilikuwa inaangalia Intelligence ya mtu , behavior interaction na jamii, skills mbalimbali ulizokuwa nazo.

Someone ambaye humjui anatoa Recommendation kuhusu wewe, unaanza kuwa spot for hata 5 years kukujua zaidi.....

Unashangaa tu wewe upo Town, unapigiwa simu na bibi yako kuwa kuna watu walikuja hapa kijijini wamejitambulisha wametokea utumishi wametuuliza uliza kuhusu wewe.

Unabaki upigwa na butwaa, miaka inapita, unasikia tena kuna watu walikuja kijijini leo hata hatuwajui.... wameuliza moja mbili Tatu .... wamesema wanatokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Unabaki kujiuliza nini kinaendelea. By the time unakuja ku realize ..... you are already there. Tofauti na siku hizi .

Siku moja wakati nimerudi TZ likizo nilikutana nae mmoja pale Coral Beach, alipack Gari vibaya na akanichuna, niliposhuka na yeye akashuka, nilipotizama ile Gari yake, nilipomuangalia na yeye... Nikamtambua. Out of the blue, anaanza ku fume ... mwisho wa siku naona anatoa identity yake, kitu ambacho ni kinyume na SOPs, nikaona hili luza.

Nilimvua his sun glasses nikamwambia https://jamii.app/JFUserGuide you, look at my face, ninakubabua na kesho Asubuhi nikukute kwa Msuya. Walinzi walipoona ooh, wakamwambia dogo ingia kwenye gari yako uondoke.

Na hili ni tatizo kwa sababu wakati mwingine unaona Rushwa kubwa zinapigwa na hakuna Taarifa za awali ilihali na TISS wapo , sasa ukichunguza unakuta na wao ni sehemu ya Rushwa yaani wanashiriki. Kama umeshiriki sasa utawezaje kutoa taarifa.

Kuna haja taasisi yetu ifanyiwe reform na iwe taasisi inayojitegemea badala ya kuendelea kubaki Idara.Atleast JPM anajitahidi sana kuboresha idara. Yule Mkwere ndio alikuwa kongoro kabisa.
 
TISS ndio nchi yenyewe kama hujui. Hata ungekuwa na elimu kiasi gani huwezi kufanya jambo lolote la maana kama TISS hawataki. Nakuhakikishia hata kama una uwezo wa kujenga kiwanda kikubwa kiasi gani, kilichopo eneo halali kabisa kama TISS hawataridhika na wewe huwezi! Wewe ni 'mgeni' kwenye utawala wa nchi. Nchi ina wenyewe, sisi wengine hata tungekuwa na cheo kikubwa kiasi gani kama TISS wakisema NO! Huwezi kwenda tofauti nao 'ukaishi'. Hata huyu mzee wetu vituko anavyofanya vya kuwaumiza wenzake ni kwamba TISS wameridhia. Wakisema hatutaki hiki lifanyike hana ubavu wa kukataa. Maan ukiwakatalia wanachokisema kwa maslahi ya nchi basi wewe utaondoka ili Taifa libaki salama. Kwa hiyo kwa ujumla TISS ndio mhimili wa nchi. Hakuna anayeweza 'kukohoa' mbele ya TISS kama wakisema hili hapana. Kwa hiyo hata Musiba TISS waliamua wamwache afanye atakavyo, lakini wangesema MUSIBA 'stop' misiba yako hatuitaki hangekuwa na jeuri ya kuendelea kufanya chochote. Hivyo ndugu yangu jua ya kwamba hakuna mwenye ubavu kuliko TISS ndani ya nchi yoyote duniani. TISS ikiwa dhaifu nchi itakuwa dhaifu tuuuu! Tunaiombea TISS ya nchi yetu iwe imara kwa Taifa imara.

Suala la Musiba ni Uhusika. Kila Mtendaji wa Idara ana uhusika wake. Ule ndio Uhusika wake.
 
Ukitaka kufanikiwa kimaisha, jifunze kwa watu waliofanikiwa, jenga urafiki na watu wenye mafanikio, jipendekeze kwao, jifanye mjinga siku ipite, kumbe lengo lako kuna kitu unachokitafuta.

Usijifanye mjuaji, kubali kukosolewa, pokea mawazo ya watu mbalimbali kisha uyachuje na kuchukua yale unayoona yanaweza kukusaidia, hiyo ndo siri ya mafanikio.

Idara yetu ya usalama wa taifa inatakiwa iige mafanikio ya idara zilizofanikiwa zaidi Duniani, MOSSAD, MI6,CIA,PSIA(Japan) huwezi kufanikiwa kwa kuendelea kuiga mifumo iliyoshindwa, na ndo maana kila kitu chetu hakiendi, tumebakia kuwa watu wa kulia lia kila siku na umaskini usio koma.

Sikushangaa kumwona waziri mkuu wetu akizindua Gereza, kuzindua Gereza ni mkosi, ni balaa, ni nuksi, ni laana, ni futureless.

Duniani pote ktk ufuatiliaji wangu wa habari za mataifa mbalimbali sijawahi kuona kiongozi mkuu wa serikali kwa level ya waziri mkuu akizindua Gereza, bali huwa nawaona wakizindua viwanda.

Kuzindua Gereza ni ishara ya kukata tamaa, unazindua ili nani akalale humo?

Wakati Uholanzi wanafunga magereza sisi tunazidi kuyajenga, 95% ya uhalifu inasababishwa na hali mbovu ya uchumi na si vinginevyo.

Ni idara ya usalama wa taifa pekee ndo yenye uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira ya utawala bora yanayopelekea uchumi imara kwa watu wake, hili Japan na Israel wamefanikiwa sana.

Kwa sasa Israel ina kiwango cha maisha bora mno kwa watu wake kuliko nchi nyingi tu za Ulaya.

Israel ni nchi ya 20 Duniani kwa kuwa na uchumi bora, na ni nchi ya pili Duniani baada ya Marekani kuwa na makampuni makubwa ya Technology na kampuni zingine kubwa kuzidi kuwekeza Israel na siyo China ambayo wengi wanaisifia, huu ni utundu uliotukuka wa vijana wa MOSSAD.

Mossad wanatumika kuhakikisha Israel iko salama kwa kitu, haki, Demokrasia, utu, uzalendo vimetamalaki Israel.

Sasa unawezaje kuwaiga Rwanda hao choka mbaya badala ya kutamani kuwa Kama Japan au Israel?

Binafsi huwa natamani kuwa na pesa nyingi na mafanikio Kama MO Dewji, sitamani kuwa maskini.

Huwa natamani sana kuiona Tanzania ikifanikiwa kiuchumi Kama Australia, ukiwa ktk nchi hii huhitaji maneno ya magazeti ya kisiasa kuwa eti nchi uchumi umekua, mandhali ya nchi na watu wake pekee yatosha kukujulisha kwamba hii ni nchi yenye uchumi mzuri.

Naporudi nyumbani Tanzania huwa nakaribishwa na mandhali iliyopauka kimaskini na nyuso za watu waliokata tamaa kwa ugumu wa maisha, Halafu nikienda kwenye kibanda cha magazeti nakutana na habari ya uchumi wa Tanzania kuzidi kupaa, naishia kucheka kwa huzuni.

Mtu mmoja alikuwa akitibiwa India eti kila siku gharama za matibabu ni sh mil 150, huyu naye mlishindwa kumdhibiti kwa wizi mkubwa wa kishamba hivi?

INAENDELEA

watanzania wakijua tu jina la taasisi basi wanaanza kuchambua uongo mtupu aisee jitathmini ufanye kazi achana na ujinga kama huu kwa vitu usivyo vijua
 
TISS wao wanachojua ni kuilinda CCM wabaki madarakani,Basi. Hawawazi zaidi ya hapo. Unapotaka wasimamie utawala bora, Kuna mkurugenzi gani wa TISS anaeweza kumwambia magu umekosea?
 
Na kujulikana maana yake haupo makini kwenye utendaji na majukumu yako ya kila siku. Na ukishajulikana unatakiwa kutoa Taarifa na kuondoka fasta hiyo sehemu.

Shida ya vijana wa siku hizi huwa TISS kwa connection za wazazi wazazi au kujuana juana.

Recruiting ya zamani ilikuwa very fascinating, yaani ilikuwa inaangalia Intelligence ya mtu , behavior interaction na jamii, skills mbalimbali ulizokuwa nazo.

Someone ambaye humjui anatoa Recommendation kuhusu wewe, unaanza kuwa spot for hata 5 years kukujua zaidi.....

Unashangaa tu wewe upo Town, unapigiwa simu na bibi yako kuwa kuna watu walikuja hapa kijijini wamejitambulisha wametokea utumishi wametuuliza uliza kuhusu wewe.

Unabaki upigwa na butwaa, miaka inapita, unasikia tena kuna watu walikuja kijijini leo hata hatuwajui.... wameuliza moja mbili Tatu .... wamesema wanatokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Unabaki kujiuliza nini kinaendelea. By the time unakuja ku realize ..... you are already there. Tofauti na siku hizi .

Siku moja wakati nimerudi TZ likizo nilikutana nae mmoja pale Coral Beach, alipack Gari vibaya na akanichuna, niliposhuka na yeye akashuka, nilipotizama ile Gari yake, nilipomuangalia na yeye... Nikamtambua. Out of the blue, anaanza ku fume ... mwisho wa siku naona anatoa identity yake, kitu ambacho ni kinyume na SOPs, nikaona hili luza.

Nilimvua his sun glasses nikamwambia **** you, look at my face, ninakubabua na kesho Asubuhi nikukute kwa Msuya. Walinzi walipoona ooh, wakamwambia dogo ingia kwenye gari yako uondoke.

Na hili ni tatizo kwa sababu wakati mwingine unaona Rushwa kubwa zinapigwa na hakuna Taarifa za awali ilihali na TISS wapo , sasa ukichunguza unakuta na wao ni sehemu ya Rushwa yaani wanashiriki. Kama umeshiriki sasa utawezaje kutoa taarifa.

Kuna haja taasisi yetu ifanyiwe reform na iwe taasisi inayojitegemea badala ya kuendelea kubaki Idara.Atleast JPM anajitahidi sana kuboresha idara. Yule Mkwere ndio alikuwa kongoro kabisa.
Umeongea kweli tupu vijana wengi ambao wako recruited na TISS kwa miaka ya hivi karibuni hawakupaswa kuwa huko wengi wao wanaona sifa kuji exposed ambapo ni kosa kubwa mno kujulikana maana una risk maisha yako pia ku risk siri za nchi. Vijana wengi waliopo huko wamekuwa ni walevi na hawaogopi kumwaga siri zao kwa machungudoa ambapo pia madada poa hao wapo kazini wakitumiwa na nchi jirani kukusanya taarifa.

Recruitement team ijitathimini kwa hili pia na vijana waliopata nafasi ya kuitumikia nchi katika nafasi hizo wajifunze kuwa wasiri kuna vijana ukikutana nao na mazungumzo yao unaona kabisa hawakufaa kuingia taasisi hiyo nyeti.
 
TISS wao wanachojua ni kuilinda CCM wabaki madarakani,Basi. Hawawazi zaidi ya hapo. Unapotaka wasimamie utawala bora, Kuna mkurugenzi gani wa TISS anaeweza kumwambia magu umekosea?

Hili Pia ni Tatizo. Ikiwa Mkurugenzi wa Idara akianza kuwa kinyume na Boss wake ambae ni Amir Jeshi, Jamaa fasta anamuondoa kwenye nafasi hiyo na kumuweka kitimoto.

Ni ngumu sana Tanzania Intelligence and Security Services kufanya kazi kwa matakwa yake; yaani lazima ifanye kazi chini ya mawazo ya Amir Jeshi.

Kimsingi Tanzania Intelligence itamshauri Rais na Kutoa mapendekezo juu ya jambo fulani, lakini utekelezaji wake ni lazima Amir Jeshi atoe go ahead. Idara inatakiwa kuwa full authority yaani independent entity kwa kila jambo ikiwa ni pamoja na kuchunguza mienendo ya Rais alie madarakani.

Baadhi ya marais huwa ni vibaraka kwa manufaa yao na hujihusisha na Rushwa kubwa kubwa au kufanya mambo kwa kupendelea maeneo ya kwao.

Mkuu wa Idara anatakiwa Kutoa tahadhari na maonyo kwa Mkuu wa nchi kwa mienendo ya aina hiyo . Kwa Mfano; ilipoonekana Trump anatumika, CIA na vyombo vyote vya ulinzi USA wakapika jungu la kumuweka huyu jamaa kando na kuvua power zake zote na moja ya njia iliyotumiwa kumuondoa ni Hizo ballot paper kwa njia ya Posta.( Postal Ballots).

Utaona ni kiasi gani Security Services ya USA ilivotumia akili kumuondoa Jamaa kwa njia ya amani na kuaminisha raia kwamba it was fair and okay.

Hiyo ndio kazi ya chombo chenye kujitegemea. Hapo TZ, Jamaa kwenye mikutano yake anaweza kukutaja; TISS yupo wapi , njoo hapa mbele .., au anaweza kusema huyu nimemteua lakini alikuwa ni TISS na amefanya sana kazi zetu, haya ni matunda ya chombo kutojitegemea.

All in all Tanzania Intelligence inafanya kazi vyema kwa level ya Third world countries.

Tunachombo makini sana kulinganisha na nchi za EAC na baadhi ya Africa Magharibi.
 
Back
Top Bottom