PAROKO KIRUMBA MWANZA KANISIKITISHA.

PAROKO KIRUMBA MWANZA KANISIKITISHA.

Katika hali ya kushangaza, misa ya jumatano ya majivu, Paroko katika matangazo yake akasema anatoa fursa ya kubatiza vichaa, mazezeta na mataira, tena akiongea kwa sauti isiyo na staha. Binafsi nilishangaa ni vipi mtu kama huyu alishindwa kuchagua maneno yenye staha kwa watu kama hawa? Alishindwa vipi kuwaita watu wenye changamoto ya akili, walemavu wa akili? Kwa nafasi yake alistahili kuwapa faraja, binafsi nilipata mashaka makubwa na wito wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatupendi ukweli wabongo ndo shida.
Kichaa asemwe kama ni kichaa kabla ya kuokolewa wala kufarijiwa.

Wewe ulitaka atumie jina gani? Aseme wako na afya ilihali sio kweli??

Unafiki utatufikisha pabaya

Shida haijirudii
 
Hatupendi ukweli wabongo ndo shida.
Kichaa asemwe kama ni kichaa kabla ya kuokolewa wala kufarijiwa.

Wewe ulitaka atumie jina gani? Aseme wako na afya ilihali sio kweli??

Unafiki utatufikisha pabaya

Shida haijirudii
Mkuu hujaelewa muktadha wa hoja yangu, je mtu hata kama ni taahira unaweza kumwambia wewe ni taahira huku ukicheka? Namna alivyokuwa akiwaita pia inatia mashaka, ni namna isiyo na staha hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom