Paramount Chief Thomas Marealle katika nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama 1950s

Home-cooked garbage.
Schmidt,
Mimi nimesoma elimu ya mnakasha, yaani mijadala kwa Sheikh Haruna.
Huyu alikuwa mwalimu wa madrasa ambayo wewe umeiandika kwa dharau na kejeli.

Kanifunza mengi na mojawapo ni adabu.
Adabu akikusudia kuwa watu hawatukanani katika kujadili masomo ya kielm.

Sheikh Haruna alikuwa anasema ukiona mtu anakimbilia matusi jua ameshindwa na hapana haja ya kuendelea na yeye katika mjadala kwani matusi hayajibiwi.
 
Quit the BS, Mzee MS. Only fools would believe any of your tales , spins and half-truths.
Schmidt,
Hapana huu uwanja uko huru kwa yeyote kuchangia fikra zake.
Sasa wewe kunifukuza kuwa nisiwepo hapa barzani si haki.

Anaetakiwa kujiondoa hapa ni wewe si mie.
Wewe ndiyo hupendezewi na kalamu yangu.

Huna haja ya kujiumiza bure na ukawa unatukana.
Unachotakiwa kufanya ni kuacha kunisoma.

Ikiwa wewe huamini haya niandikayo hapana ugomvi wako wanaoelemika na kalamu yangu.
 
Schmidt,
Hapana huu uwanja uko huru kwa yeyote kuchangia fikra zake.
Sasa wewe kunifukuza kuwa nisiwepo hapa barzani si haki.

Anaetakiwa kujiondoa hapa ni wewe si mie.
Wewe ndiyo hupendezewi na kalamu yangu.

Huna haja ya kujiumiza bure na ukawa unatukana.
Uachotakiwa kufanya ni kuacha kunisoma.

Ikiwa wewe huamini haya niandikayo hapana ugomvi wako wanaoelemika na kalamu yangu.
Let’s agree on one simple thing: You’re a fake historian, Mzee MS. You can never be taken seriously in anything you write. You’re a fraudster. A pretender.
 
Let’s agree on one simple thing: You’re a fake historian, Mzee MS. You can never be taken seriously in anything you write. You’re a fraudster. A pretender.
Schmidt,
Mimi sina tatizo na unavyoniona.
Pokea zawadi hii ndogo hapo chini kutoka kwangu:

1644943441128.png


Hii ni baraza ya nyumba ya marehemu Ali Msham.
Nyumba hii iko Mtaa wa Jaribu na Uweje, Magomeni Mapipa.

Kwenye baraza hii ukiangalia vizuri utaona kuna meza zimepinduliwa.
Nyakati za mchana hapo panapigwa pasi nguo.

Nyumba hii ilikuwa moja ya matawi ya TANU na tawi hili alifungua mwenyewe mwenye nyumba Ali Msham mwaka wa 1954.

Ali Msham katika nyumba hii alimfungulia Mama Maria Nyerere duka la kuuza mafuta ya taa.

Wakati huu Mwalimu Nyerere alikuwa anaishi Magomeni Maduka Sita.

Kwenye baraza hii walikaa masheikh kufanya dua wakati Mwalimu Nyerere anakwenda UNO safari ya kwanza mwezi Februari 1955.

Kuzunguka nyumba hii siku hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuja kushiriki katika dua hii.

1644944181786.png
Ali Mshama ni huyo aliyesimama kushoto mwenye shati jeusi akiwa na wanachama wa TANU katika mkutano wa ndani uani nyumbani kwake.
 
Schmidt,
Mimi sina tatizo na unavyoniona.
Sawa Mzee MS. Kubali kwa umri wako wewe ni sawa na chawa tu wa akina Sykes. Upo kichawa zaidi Mzee wangu, kwa hiyo familia. Huna lolote la maana unaloandika zaidi ya kuwasifia Sykes na kuendekeza udini.
 
Lokonga,
Katika maajabu niliyokutananayo ni hii historia ya Sykes.

Kila utakaemkuta katika historia ya Tanganyika yumo katika nyaraka zao.

Ajabu kubwa sana.
Unadhani nafanya utani?

Nimesoma barua za Chief Thomas Marealle katika nyaraka hizo.

Wanaelezana mambo makubwa ya hali ya baadae ya Tanganyika.

Bahati mbaya siwezi kueleza hayo kwa kuwa yalikuwa mazungumzo binafsi sana.

Unaumia kuwa kuna watu Allah aliwanyanyua kupita wengine.

Tungefahamu vipi historia ya Nyerere kama si nyaraka hizi za Sykes?

Nilialikwa Northwestern University Evanston Chicago kufanya mhadhara juu ya Abdul Sykes.

Hiki chuo ndiyo kinaongoza ulimwenguni katika African History.

Sikutegemea hata kwa mbali kama haya mambo yatakuwa makubwa kiasi hiki.

Yuko publisher aliposoma mswada wa kitabu cha Abdul Sykes aliniambia kuwa mswada wangu ni mgodi wa dhahabu.

Lakini aliogopa kuchapa kitabu changu.

Miaka hiyo mimi kijana kiasi miaka 30.

Samahani sana kama unatabishwa na kalamu yangu.

Kitabu kinakwenda toleo la tano.

View attachment 2119388

View attachment 2119390
Hizi liberal inclined colleges and universities in the US huwa wanawaalika trending individuals kwenye fields mbalimbali toka dunia nzima wenye mitazamo mbadala ya ile iliyo rasmi kwenye seminars and lectures kwa manufaa ya wanafunzi wao, lakini haimaanishi wewe kualikwa huko North Western University kunakufanya uwe World Class Scholar. Hao Wanafunzi bado inabidi wachambue mbivu na mbichi. Hilo ndilo lengo lao hao Wazungu kukualika huko.
 
Hizi liberal inclined colleges and universities in the US huwa wanawaalika trending individuals kwenye fields mbalimbali toka dunia nzima wenye mitazamo mbadala ya ile iliyo rasmi kwenye seminars and lectures kwa manufaa ya wanafunzi wao, lakini haimaanishi wewe kualikwa huko North Western University kunakufanya uwe World Class Scholar. Hao Wanafunzi bado inabidi wachambue mbivu na mbichi. Hilo ndilo lengo lao hao Wazungu kukualika huko.
Schmidt,
Hapana tatizo ndugu yangu.
 
Historia ya wachaga itaandikwa na wachaga wenyeww na historia ya waswahili itaandikwa na waswahili wenyewe kila mtu aandike historia yake
 
Sawa Mzee MS. Kubali kwa umri wako wewe ni sawa na chawa tu wa akina Sykes. Upo kichawa zaidi Mzee wangu, kwa hiyo familia. Huna lolote la maana unaloandika zaidi ya kuwasifia Sykes na kuendekeza udini.
Schmidt,
Hakuna tatizo.
Umekasirika sana.

Mwaka wa 1988 niliandika makala ''In Praise of Ancestors,'' katika jarida moja likiitwa Africa Events (AE) likichapwa London.

Katika makala ile nilimtaja Abdul na Ally Sykes katika historia ya TANU.
Nikaitaja TAA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Toleo zima la gazeti hili likakusanywa.
Makala chache sana ziliweza kupenywa na kusomwa.

Toleo lililofuatia Dr. Mayanja Kiwanuka kutoka Makao Makuu ya CCM, Dodoma akatoa jibu la makala yangu akiwa kahamaki kweli kweli.

Dr. Kiwanuka alinitukana akaniita mbilikimo.
Leo wewe umeniita, ''chawa.''

Mwalimu wangu Sheikh Haruna kanifunza anasema ukitukanwa hurudishi tusi unanyamaza.
Historia ya wachaga itaandikwa na wachaga wenyeww na historia ya waswahili itaandikwa na waswahili wenyewe kila mtu aandike historia yake

1644950034289.png
 
Historia ya wachaga itaandikwa na wachaga wenyeww na historia ya waswahili itaandikwa na waswahili wenyewe kila mtu aandike historia yake
Mdukuzi,
Soma hapo chini niliyoandika katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama (2020):

''Historia ya Wachagga imeandikwa kwenye upeo wa hali ya juu na Wazungu kiasi cha kumstaajabisha msomaji inawezekanaje kwa Mzungu kutoka Ulaya mtu mgeni kuijua historia kwa undani wa kiasi kuweza kueleza mambo yaliyotokea miaka mingi sana iliyopita.

Mwandishi kama Mwingereza Charles Dundas ameandika historia ya Wachagga kwa kiwango cha kustaajabisha na kueleza mengi ambayo mtu tabu hata kuyafikiri achilia mbali kuyajua hadi awe ameyasoma.

Wachagga wana hulka pale wanapompenda mgeni basi watampa lakabu inayoendana na heshima ya kabila lao.

Charles Dundas walimwita, Wasaoye-o-Wachagga, yaani Mzee wa Kichagga.

Historia ya Muro Mboyo aliyeishi Machame katika miaka ya katikati ya karne ya 19 imeishi katika simulizi za ukoo wake unaofahamika kama ukoo wa Nkya ikipokelewa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kwa miaka inayofikia 200 kama ilivyoelezwa.

Historia hii haikupata kuandikwa popote kwa nia ya kuwa historia hiyo inaandikwa ili ije kusomwa.

Hata hivyo mtoto wake, Kirama Mboyo ameacha utajiri mkubwa wa nyaraka zilizoandikwa kwa mkono na nyingine zimepigwa chapa zinozoeleza historia ya babu zake waliomtangulia kiasi cha miaka 100 nyuma na kueleza pia historia yake mwenyewe pale ilipoingia karne ya 20.

Baadhi ya nyaraka hizi ziko katika mfano wa barua, taarifa na maelezo ya kawaida zina tarehe na zipo nyingine hazina tarehe wala jina la mwandishi.

Muhimu ni kuwa kumbukumbu hizi zinaeleza historia muhimu sana ya takriban miaka 200 nyuma ya Wachagga wa Machame na sehemu nyingine za jirani ambao walikuja kuwa Waislam wa kwanza Uchaggani.''

Mimi si Mchagga na nimeandika historia ya Wachagga.
Charles Dundas Mzungu na kaandika historia ya Wachagga.

1644954735600.png
Uzinduzi wa kitabu cha Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama, Muslim University of Morogoro ''book signing.''
 
KUMBUKUMBU KIFO CHA MANGI MKUU THOMAS MAREALLE 14 FEBRUARY 2007: PARAMOUNT CHIEF THOMAS MAREALLE KATIKA NYARAKA ZA RAJABU IBRAHIM KIRAMA WA MACHAME NKUU

Mara yangu ya kwanza kusoma historia ya Mangi Mkuu Thomas Marealle ilikuwa ndani ya Nyaraka za Sykes wakati natafiti kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Kwa bahati mbaya sikuweza kutumia yale niliyosoma katika kitabu nilichokuja kuandika kwa kuwa mengi katika yale niliyosoma yaikuwa mambo binafsi zaidi kuliko historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ingawa jina la Nyerere lilikuwa likijitokeza.

Nimekuja kukutana tena na Mangi Mkuu Thomas Marealle baada ya kiasi cha miaka 30 kupita katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha ya Mzee Rajabu wa Machame Nkuu.

Napenda kama kumbukumbu ya kifo cha Mangi Mkuu nieleze machache katika yale ambayo nimejifunza katika kusoma barua walizokuwa wakiandikiana watu hawa wawili kutoka Kilimanjaro kila mmoja akiwa na nafasi muhimu katika jamii ya kabila la Wachagga.

Thomas Marealle akiwa kwanza Mangi wa Marangu kisha Mangi Mkuu wa Wachagga, Rajabu Kirama yeye akiwa kiongozi wa Waislam na mtu aliyeueneza Uislam Uchaggani akianzia harakati zake kijijini kwake Machame Nkuu katika miaka ya 1930.

Harakati hizi zilileta uadui mkubwa kati yake na Chief Shangali.

Mwishoni wa miaka ya 1800 Wajerumani baada ya kuchoshwa na vita visivyokwisha baina ya Wachagga wenyewe kwa wenyewe waliamua kuwakamata takriban mangi wote isipokuwa Shangali na Marealle.

Jumla ya mangi 19 walinyongwa hadharani isipokuwa Chief Marealle na Chief Shangali.

Haya ndiyo madhila yaliyowakumba Wachagga chini ya utawala wa Wajerumani.

Watoto wa machifu hawa wawili hata hivyo walikuja kupata nguvu kubwa sana katika utawala wa Waingereza.

Katika utawala wa Waingereza na katika hali ya amani na utawala Wachagga waliunda chama - Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) (Umoja wa Raia wa Kilimanjaro).

Petro Njau akiwa kiongozi wa chama hiki alipewa jukumu la kusimamia maslahi ya Wachagga kama taifa.

Katika kanuni za KCCU kanuni hizi zinawataja Wachagga kama watu waliozaliwa huru na wenye haki ya kulinda uhuru wao.

Petro Njau alikinadi chama hiki kuwa ni ‘’chama cha siasa cha kikabila.’’

Nilipokuwa nasoma Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama nilishangaa sana kusoma kuwa Wachagga kwa asili waliichukulia Kilimanjaro yote kuwa ni nchi.

Nyaraka za KCCU zimejaa maneno ya itikadi ya: ‘’nchi,’’ ‘’taifa,’’ ‘’raia,’’ ‘’uchaguzi,’’ ‘’kura,’’ na ‘’utawala.’’

Petro Njau Rajabu na Ibrahim Kirama walikuwa wanaunganishwa na kukubaliana katika jambo moja kubwa na muhimu sana katika utawala wa Wachagga nalo ni kuwa Mangi walikuwa na nguvu zilizopea wakati raia wao hawakuwa na sauti yoyote.

Kwa ajili hii basi wanastahili kuondolewa wote na awekwe kiongozi mmoja tu atakaetawala Kilimanjaro yote na Wachagga wote.

Petro Njau alikuwa mwandishi wa Mzee Rajabu na pia mwandishi wa Chief Thomas Marealle pale Kilimanjaro ilipokuwa katika siasa za uchaguzi kutafuta Mangi Mkuu atakaekuwa juu ya Mangi wote, yaani Paramount Chief.

Rajabu Kirama alisimama bega kwa bega na Petro Njau katika fikra hii.

Thomas Marealle na Abdiel Shangali ndiyo walikuwa wanagombea nafasi ya Mangi Mkuu na bahati mbaya sana kwa Abdiel Shangali ni kuwa alikuwa na uadui mkubwa na Rajabu Ibrahim Kirama.

Rajabu Kirama akasimama kumsaidia Chief Marealle awe kiongozi wa Wachagga wote.

Hivi ndivyo Thomas Marealle alivyokuja kuchaguliwa kuwa Paramount Chief, yaani Mangi Mkuu.

Picha: Mzee Rajabu Ibrahim Kirama, Mangi Mkuu Thomas Marealle wa Marangu na Chief Abdiel Shangali wa Machame.

View attachment 2119338
Kwahiyo unataka kusema hakupewa support na mamangi wengine maana juzi kutawazwa Samia Kilimanjaro tumeonyeshwa mamangi wengi Uchaggani! Sidhani kama mzee Kirama alikuwa na influence Uchaggani kote mbali na Machame! Na hata kama walikuwa wamenyongwa na Wajerumani ikumbukwe Wajerumani walikuwa Tanganyika mpaka 1918 tu na Waingereza walirudisha Umangi kupitia Chieftancy! BTW Wajerumani walinyonga Wamangi wote Uchaggani na around Tanganyika watemi na machifu!
 
Huyo chifu mpaka sasa amefanya wakibosho na wamachame hawaivani hata kuoleana,na suo hilo tuu hata nyumba mkibosho akijenga ni marufuku kugeuzia mlango usawa wa machame..
Nje ya mada;niliwahi ambiwa na mzee wangu kuwa huyu mariale haikuwa ukoo wake bali ni neno lilitokana na kupishana kauli baina ya mtu aliekuwa anamuulizia huyu mangi alikuwa amelala sasa akaja mzung kumtembelea sasa yule msaidizi wa chifu akamjibu (mangi nale))yaani kwa kichaga ni mangi kalala)sasa yule jamaa akasindwa kutamka lile neno akasemaa marialeee marialeeee ndio likawa chimbuko la kijiita jina hilo mariale mariale hadi likazoeleka.ila ukoo kabisa aliokuwa akitumia ni (mushi)

Sent using Jamii Forums mobile app

Uongo.
 
Schmidt,
Mimi nimesoma elimu ya mnakasha, yaani mijadala kwa Sheikh Haruna.
Huyu alikuwa mwalimu wa madrasa ambayo wewe umeiandika kwa dharau na kejeli.

Kanifunza mengi na mojawapo ni adabu.
Adabu akikusudia kuwa watu hawatukanani katika kujadili masomo ya kielm.

Sheikh Haruna alikuwa anasema ukiona mtu anakimbilia matusi jua ameshindwa na hapana haja ya kuendelea na yeye katika mjadala kwani matusi hayajibiwi.
Who is shekhi Haruna?

You have minimized your world kama chungu

Can’t even extend beyond your virtual wings
 
kwahiyo unataka kusema hakupewa support na mamangi wengine maana juzi kutawazwa Samia Kilimanjaro tumeonyeshwa mamangi wengi Uchaggani! Sidhani kama mzee Kirama alikuwa na influence Uchaggani kote!
Geza...
Mzee Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii ya Waislam wa Uchaggani katika sehemu zile ambazo walikuwapo Waislam.

Katika uchaguzi wowote kura hata moja ni muhimu kwa kuwa kura moja inaweza kuzaa kumi.
Mwanasiasa yeyote hapuuzi kura.

Thomas Marealle aliposhinda alikwenda Machame Nkuu kutoa shukurani zake kwa Mzee Rajabu.

Angalia picha hiyo hapo chini huyo aliyevaa kanzu na kilemba ndiye Mzee Rajabu Ibrahim Kirama na pembeni yake ni Mangi Mkuu Thomas Marealle.
1644955519696.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom