Paramount Chief Thomas Marealle katika nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama 1950s

Mzee Mohamed Said aslmyaleikum nakupongeza kwa makala zako ni nzuri unatupa elimu kubwa tunashukuru Sana kwa Hilo,Lakini nakuomba utupe mchango wa Ukerewe na chifu wa wakerewe nadhani anaitwa Chief Gabriel Lukumbuzya kwenye harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.Nilishawai sikia huyu chifu alikua anatumiwa na Mwalimu Nyerere katika kuongoza Nchi.Tafadhali kama unajua naomba utusaidie na pia nasikia hadi Leo hii Kuna mambo alimwambia Mwalimu Nyerere ayazingatie kwenye kuongoza nchi na inavosemekana ni kwamba alikua kama mtabili kuhusu mambo ya kiutawala
Babe...
Simjui Chief Michael Lukumbuzya kwa kiwango hicho unachotaka nimzungumze.

Namjua Chief Lukumbuzya kidogo kama kupita njia jinsi nilivyokutananae katika utafiti wakati naandika maisha ya Abdu Sykes ili kueleza harakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Haya ninavyokueleza kanihadithia Mama Daisy mke wa Abdul Sykes.

Abdul Sykes na mkewe walikuwa wanakwenda Nansio, Ukerewe kumtembelea Hamza Mwapachu.

Ilikuwa mwaka wa 1951.

Mwaka wa 1950 lilimwagika vumbi kubwa ofisi za TAA New Street kwa uongozi wa TAA kuchanguliwa na Gavana Edward Francis Twining na kutupwa majimboni kwa sababu ya memorandum ya Mapendekezo ya Katiba waliyowasilisha serikalini.

Katika mapendekezo hayo pamoja na mdai mengine TAA ilidai uchaguzi na baada ya miaka 13 Waingereza waondoke Tanganyika.

Haya mapendekezo yaliandikwa na TAA Political Subcommittee ambayo wajumbe wake walikuwa Abdul Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Hii ndiyo ikawa sababu ya viongozi hawa wa TAA waliokuwa waajiriwa wa serikali kuondolewa Dar es Salaam na kupelekwa majimboni.

Hamza Mwapachu akajikuta yuko kisiwani Nansio.

Abdul Sykes na mkewe wakawa wamepanda meli Mwanza wanakwenda Nansio kwa Hamza Mwapachu na sababu ya safari hii ni kwenda kupata ushauri wa Mwapachu nini kifanyike kuendeleza mapambano dhidi ya Waingereza.

Katika meli ile alikuwako Michael Lukumbuzya akitokea Makerere College anakwenda likizo Nansio.

Lukumbuzya alipigwa na bumbuazi walipofika bndarini Nansio kwani alikuta ngoma zinapigwa kumpokea Abdul Sykes na Mwapachu yuko bandarini kumlaki mgeni wake na mkewe.

Lukumbuzya akataka kujua huyu mtu anaepewa mapokezi yale ni nani?

Hamza Mwapachu akamfahamisha kuwa ni Abdul Sykes kiongozi wa TAA kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam.

Inaelekea kuwa kufikia miaka ile ya mwanzoni 1950s Chief Lukubuzya alikuwa bado hayuko katika siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kuwa hakuwa hata anamjua Abdul Sykes ni nani.

Haya machache ndiyo ninayoyafahamu kuhusu Chief Michael Lukumbuzya wa Ukerewe.

Screenshot_20220220-175321_Facebook.jpg
 
Babe...
Simjui Chief Michael Lukumbuzya kwa kiwango hicho unachotaka nimzungumze.

Najua Chief Lukumbuzya kidogo kama kupita njia jinsi nilivyokutananae katika utafiti wakati naandika maisha ya Abdu Sykes ili kueleza harakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Haya ninavyokueleza kanihadithia Mama Daisy mke wa Abdul Sykes.

Abdul Sykes na mkewe walikuwa wanakwenda Nansio, Ukerewe kumtembelea Hamza Mwapachu.

Ilikuwa mwaka wa 1951.

Mwaka wa 1950 lilimwagika vumbi kubwa ofisi za TAA New Street kwa uongozi wa TAA kuchanguliwa na Havana Edward Francis Twining na kutupwa majimboni kwa sababu ya memorandum ya mapendekezo ya katiba waliyowasilisha serikalini.

Katika mapendekezo hayo TAA ilidai uchaguzi na baada ya miaka 13 Waingereza waondoke Tanganyika.

Haya mapendekezo yaliandikwa na TAA Political Subcommittee ambayo wajumbe wake walikuwa Abdu Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Hii ndiyo ikawa sababu ya viongozi hawa wa TAA waliokuwa waajiriwa wa serikali kuondolewa Dar es Salaam na kupelekwa majimboni.

Hamza Mwapachu akajikuta yuko kisiwani Nansio.

Abdul Sykes wakawa wamepanda meli Mwanza wanakwenda Nansio kwa Hamza Mwapachu na sababu ya safari hii ni kwenda kupata ushauri wa Mwapachu nini kifanyike kuendeleza mapambano dhidi ya Waingereza.

Katika meli ile alikuwako Michael Lukumbuzya akitokea Makerere College anakwenda likizo Nansio.

Lukumbuzya alipigwa na bumbuazi walipofika Nansio kwani alikuta ngoma zinapigwa kumpokea Abdul Sykes na Mwapachu yuko bandarini kumlaki mgeni wake na mkewe.

Lukumbuzya akataka kujua huyu mtu anaepewa mapokezi yale ni nani?

Hamza Mwapachu akamfahamisha kuwa ni Abdul Sykes kiongozi wa TAA kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam.

Haya machache ndiyo ninayoyafahamu kuhusu Chief Michael Lukumbuzya wa Ukerewe.
Nashukulu sana
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom