Paramount Chief Thomas Marealle katika nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama 1950s

Uchaga ni pana sana ikiwa imetawaliwa na Ukristo hivyo siafiki kwamba ushawishi wa huyo sheikh Kirama ulimsaidia Thomas Mareale kushinda uchaguzi.

Ikumbukwe Mareale alikuwa mtu msomi jambo ambalo lilimjengea 'exposure' kwa watawala wa Kiingereza tofauti na Shangali. Ni wazi kwa wapiga kura wa kipindi hicho kuona faida ya kuwa na kiongozi mwenye elimu na ushawishi kwa Waingereza kama Mareale.

Ikumbukwe Mareale kushinda uchagani hajashida kwa kura za wamachame tu, Rombo pia ni uchagani.

IMG_2220.jpg

IMG_2222.jpg

Kilicho mpa Mareale ushindi dhidi ya Shangali ni ushawishi wake kwa Wachaga, sio kwa sababu alisaidiwa na Sheikh wa Nkuu.
 
Geza...
Mzee Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii ya Waislam wa Uchaggani katika sehemu zile ambazo walikuwapo Waislam.

Katika uchaguzi wowote kura hata moja ni muhimu kwa kuwa kura moja inaweza kuzaa kumi.
Mwanasiasa yeyote hapuuzi kura.

Thomas Marealle aliposhinda alikwenda Machame Nkuu kutoa shukurani zake kwa Mzee Rajabu.

Angalia picha hiyo hapo chini huyo aliyevaa kanzu na kilemba ndiye Mzee Rajabu Ibrahim Kirama na pembeni yake ni Mangi Mkuu Thomas Marealle.
View attachment 2120531
walikuwa wangapi? Kipindi hicho Kilimanjaro hata sasa waislam Uchaggani ni wachache ukiacha upande wa Upareni! Hata sasa nadhani ukristo tena Ulutheri ndo upo zaidi ukifuatiwa na Ukatoliki halafu makanisa chungu nzima ya Kilokole!
 
Who is shekhi Haruna?H

You have minimized your world kama chungu

Can’t even extend beyond your virtual wings
Janja...
Haruna ni Mwalimu wangu aliyonisomesha ilm ya kufanya mijadala na masomo mengine madogo madogo kama mantiki nk.

Hayo usemayo ya udogo wangu ndiyo niliyojaaliwa.
Nashukuru kwa hiki kidogo nilichopewa kwani wapo wadogo zaidi yangu.
 
Geza...
Mzee Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa na ushawishi mkubwa katika jamii ya Waislam wa Uchaggani katika sehemu zile ambazo walikuwapo Waislam.

Katika uchaguzi wowote kura hata moja ni muhimu kwa kuwa kura moja inaweza kuzaa kumi.
Mwanasiasa yeyote hapuuzi kura.

Thomas Marealle aliposhinda alikwenda Machame Nkuu kutoa shukurani zake kwa Mzee Rajabu.

Angalia picha hiyo hapo chini huyo aliyevaa kanzu na kilemba ndiye Mzee Rajabu Ibrahim Kirama na pembeni yake ni Mangi Mkuu Thomas Marealle.
View attachment 2120531
sawa ila influence huko Machame sidhani kama Uchaggani kotee yaani Marangu, old Moshi na Rombo! Mbona asiwepo kwenye Chagga Council kuna picha za Uongozi wote na Kabunge chao zimo humu JF mzee Kirama hayupo!
 
Uchaga ni pana sana ikiwa imetawaliwa na Ukristo hivyo siafiki kwamba ushawishi wa huyo sheikh Kirama ulimsaidia Thomas Mareale kushinda uchaguzi.

Ikumbukwe Mareale alikuwa mtu msomi jambo ambalo lilimjengea 'exposure' kwa watawala wa Kiingereza tofauti na Shangali. Ni wazi kwa wapiga kura wa kipindi hicho kuona faida ya kuwa na kiongozi mwenye elimu na ushawishi kwa Waingereza kama Mareale.

Ikumbukwe Mareale kushinda uchagani hajashida kwa kura za wamachame tu, Rombo pia ni uchagani.

View attachment 2120535

View attachment 2120536

Sikus
Kilicho mpa Mareale ushindi dhidi ya Shangali ni ushawishi wake kwa Wachaga, sio kwa sababu alisaidiwa na Sheikh wa Nkuu.
Under...
Sikusema kuwa Chief Marealle alishinda kwa kuungwa mkono na Mzee Rajabu.
Nimesema kuwa Mzee Rajabu alimuumga mkono Chief Marealle.
 
walikuwa wangapi? Kipindi hicho Kilimanjaro hata sasa waislam Uchaggani ni wachache ukiacha upande wa Upareni! Hata sasa nadhani ukristo tena Walutheri ndo ipo zaidi ikifuatiwa na Ukatoliki halafu makanisa chungu nzima ya Kilokole!
Geza...
Umesema kweli.
 
Under...
Sikusema kuwa Chief Marealle alishinda kuungwa mkono na Mzee Rajabu.
Nimesema kuwa Mzee Rajabu alimuumga mkono Chief Marealle.
Hapa nakuelewa na hata ukisema alimnadi kwa influence yake Machame nakuelewa ila sehemu nyingine sidhani kama Uislamu ulikuwa umejikita hivyo!
 
Hapa nakuelewa na hata ukisema alimnadi kwa influence yake Machame nakuelewa ila sehemu nyingine sidhani kama Uislamu ulikuwa umejikita hivyo!
Geza...
Hali ya Uislam miaka ya 1950 ilikuwa kama hivi:

''Maulid ya Mfungo Sita Moshi Uislam ulipopata nguvu Machame na vijiji vingine Kilimanjaro kwa kuleta walimu kutoka Zanzibar kuja kufundisha dini Usangi, Ugweno na sehemu nyingine za Upare, Maulid yalibadili sura ya mji wa Moshi.

Kuanzia asubuhi mabasi yaliyobeba Waislam yaliingia mjini kutoka milima ya Kilimanjaro na Upare yakiteremsha wake kwa waume na watoto wa madrasa waliokuja maulidini.

Hali hii ilifanya Uislam utawale Moshi mjini ambako ndipo Waislam walipojumuika kwanza katika zafa jioni wakizunguka mjini huku matari yakipigwa na kasida zikiimbwa barabara zikiwa zimejaa watu na mbele zikiwa zimetangulizwa bendera za rangi ya kijana zimeandikwa ‘’La Ilaha Ilallah,’’ yaani ‘’Hapana Mungu ila Allah.’’

Mji uligubikwa na hali ya furaha na misikiti miwili ya Moshi mjini, Msikiti wa Riadha na Misikiti wa Ijumaa ilijaa waumini kuhudhuria sala.''

(Kutoka kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama)
 
Geza...
Hali ya Uislam miaka ya 1950 ilikuwa kama hivi:

''Maulid ya Mfungo Sita Moshi Uislam ulipopata nguvu Machame na vijiji vingine Kilimanjaro kwa kuleta walimu kutoka Zanzibar kuja kufundisha dini Usangi, Ugweno na sehemu nyingine za Upare, Maulid yalibadili sura ya mji wa Moshi.

Kuanzia asubuhi mabasi yaliyobeba Waislam yaliingia mjini kutoka milima ya Kilimanjaro na Upare yakiteremsha wake kwa waume na watoto wa madrasa waliokuja maulidini.

Hali hii ilifanya Uislam utawale Moshi mjini ambako ndipo Waislam walipojumuika kwanza katika zafa jioni wakizunguka mjini huku matari yakipigwa na kasida zikiimbwa barabara zikiwa zimejaa watu na mbele zikiwa zimetangulizwa bendera za rangi ya kijana zimeandikwa ‘’La Ilaha Ilallah,’’ yaani ‘’Hapana Mungu ila Allah.’’

Mji uligubikwa na hali ya furaha na msikiti miwili ya Moshi mjini, Msikiti wa Riadha na Msikiti wa Ijumaa ilijaa waumini kuhudhuria sala.''

(Kutoka kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama)
Moshi mjini pia kuna Uislam muda ila kumbuka Moshi Town ni part of Old Moshi na density kubwa ya watu ipo nje ya Moshi town! Na pia Moshi town kama makao makuu ya mkoa ni mchanganyiko wa Makabila! Demographic ya Mkoa mzima una watu zaidi ya milioni mbili huku Moshi mjini ina less than 200,000.
 
Usipofanya hivyo jamii itakuhukumu, utashusha hadhi ya elimu unayoitoa kwasababu inaelemea upande fulani, utakuwa predictable na hadhira itakuchoka.
Mix...
Sijapata kuchokwa.
Kitabu changu cha kwanza cha Abdul Sykes (1998) kinakwenda chapa ya tano.

Hapa Jukwaa la Historia sema mwenyewe.
Naisomesha upya historia ya Mwalimu Nyerere na uhuru wa Tanganyika.

Vyombo vya habari electronic na print media vinapishana mlangoni pangu kutafuta mahojiano na mimi.

Hujui nimezumgumza vyuo vingapi Afrika, Ulaya na Marekani baada ya kutoka kitabu kile.
Hujui nimeandika vitabu vingapi na makala ngapi achilia research papers.

Nashukuru sana.
 
Moshi mjini pia kuna Uislam muda ila kumbuka Moshi Town ni part of Old Moshi na density kubwa ya watu ipo nje ya Moshi town! Na pia Moshi town kama makao makuu ya mkoa ni mchanganyiko wa Makabila! Demographic ya Mkoa mzima una watu zaidi ya milioni mbili huku Moshi mjini ina less than 200,000.
Geza...
Sitafuti ushindi ila naieleza mabadiliko yaliyotokea.
 
Mdukuzi,
Soma hapo chini niliyoandika katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama (2020):

''Historia ya Wachagga imeandikwa kwenye upeo wa hali ya juu na Wazungu kiasi cha kumstaajabisha msomaji inawezekanaje kwa Mzungu kutoka Ulaya mtu mgeni kuijua historia kwa undani wa kiasi kuweza kueleza mambo yaliyotokea miaka mingi sana iliyopita.

Mwandishi kama Mwingereza Charles Dundas ameandika historia ya Wachagga kwa kiwango cha kustaajabisha na kueleza Charles mengi ambayo mtu tabu hata kuyafikiri achilia mbali kuyajua hadi awe ameyasoma.

Wachagga wana hulka pale wanapompenda mgeni basi watampa lakabu inayoendana na heshima ya kabila lao.

Charles Dundas walimwita, Wasaoye-o-Wachagga, yaani Mzee wa Kichagga.

Historia ya Muro Mboyo aliyeishi Machame katika miaka ya katikati ya karne ya 19 imeishi katika simulizi za ukoo wake unaofahamika kama ukoo wa Nkya ikipokelewa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kwa miaka inayofikia 200 kama ilivyoelezwa.

Historia hii haikupata kuandikwa popote kwa nia ya kuwa historia hiyo inaandikwa ili ije kusomwa.

Hata hivyo mtoto wake, Kirama Mboyo ameacha utajiri mkubwa wa nyaraka zilizoandikwa kwa mkono na nyingine zimepigwa chapa zinozoeleza historia ya babu zake waliomtangulia kiasi cha miaka 100 nyuma na kueleza pia historia yake mwenyewe pale ilipoingia karne ya 20.

Baadhi ya nyaraka hizi ziko katika mfano wa barua, taarifa na maelezo ya kawaida zina tarehe na zipo nyingine hazina tarehe wala jina la mwandishi.

Muhimu ni kuwa kumbukumbu hizi zinaeleza historia muhimu sana ya takriban miaka 200 nyuma ya Wachagga wa Machame na sehemu nyingine za jirani ambao walikuja kuwa Waislam wa kwanza Uchaggani.''

Mimi si Mchagga na nimeandika historia ya Wachagga.
Charles Dundas Mzungu na kaandika historia ya Wachagga.

View attachment 2120511Uzinduzi wa kitabu cha Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama, Muslim University of Morogoro ''book signing.''
Hebu tuletee ile historia ya Muslim Welfare Society na jinsi ilivyopigwa vita na kufutiliwa mbali na Papa Pius XIX kabla hajafariki. Pia kwenye hilo usiwasahau wale Nshomile waislamu walivyodanganywa na marehemu Cardinal laurian Rugambwa.
 
ksk,
Hii ni mada nzito sana katika historia ya Waislam wa Tanganyika.

Watu wawili tu ndiyo waliofanya utafiti na kuandika kuhusu EAMWS - Dr. Mayanja Kiwanuka ‘'The Politics of Islam in Bukoba District’' (1973) na Mohamed Said '‘Islam and Politics in Tanzania’' (1989).

Bahati mbaya ni lugha ambayo umetumia.
Mathalan, ''kufutiliwa mbali,'' ''Nshomile.''

Hii mijadala ni mijadala inayohitaji utulivu wa akili na lugha zetu ili zivutie wasomaji makini na kupata michango ya maana.

Lete upya hili ombi lako katika lugha ya kistaarabu In Shaa Allah nitakujibu.
 
Mzee Mohamed Said aslmyaleikum nakupongeza kwa makala zako ni nzuri unatupa elimu kubwa tunashukuru Sana kwa Hilo,Lakini nakuomba utupe mchango wa Ukerewe na chifu wa wakerewe nadhani anaitwa Chief Gabriel Lukumbuzya kwenye harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.Nilishawai sikia huyu chifu alikua anatumiwa na Mwalimu Nyerere katika kuongoza Nchi.Tafadhali kama unajua naomba utusaidie na pia nasikia hadi Leo hii Kuna mambo alimwambia Mwalimu Nyerere ayazingatie kwenye kuongoza nchi na inavosemekana ni kwamba alikua kama mtabili kuhusu mambo ya kiutawala
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom