tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 25,995
- 25,392
Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia nilizopenyezewa na raia wema ni kwamba genge hatarishi la Panya Road limefanya uhalifu usiku huu katika maeneo ya Chamazi (Jimbo la Mbagala) na sasa wamekusanyika karibu na eneo la chuo cha afya cha Muhimbili lililopo Chamazi, wakilenga kuendelea na uhalifu wao kama kawaida. Hivi sasa wananchi wako roho juu wakihimizana kufunga milango ya nyumba zao na kuepuka kutoka nje ili kujilinda na uhalifu wa genge hili la kimafia linalozidi kutikisa jiji la Dar es Salaam siku hadi siku.
Nimeuweka uzi huu hapa kwa makusudi. Panya Road wametufikisha hapa baada ya kushindwa kudhibitiwa kikamilifu na vyombo vya ulinzi.
Tutapeana taarifa baadaye kadri ninavyozipata kutoka eneo la tukio. Wananchi wanaishi kwa hofu kubwa kufuatia kundi hili linalojibadilisha kila kukicha kutoka genge la wahalifu na kuwa kundi la kigaidi. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwalinda raia na mali zao na ikibidi wananchi wamilikishwe silaha nzito kwa ajili ya kujilinda wao wenyewe na mali zao. Kuna haja ya kuanzisha mafunzo ya lazima ya kijeshi kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kujilinda.